Nimekuwa nasikia maneno haya lakini yananichanganya kujua matumizi yake sahihi.
Vukiza au fukiza?
Vundika au vumbika?
Compyuta?
Mtandao
ila
ingawa
msanii
puchu
mkwara
mwake
chuna
mbongo
Ninayo maneno lukuki lakini nashindwa kuyaainisha yote hapa. Naomba wataalam wa lugha hii adhimu mnisaidie nitoke niliko walau hatua moja mbele katika kujifunza Kiswahili.
Ahsanteni
__________________ Welcome to JF Phase II...
Contact me:
Mobile: +255713444649
Email: maxence@maxence.co.tz
Pls DO NOT send me Job applications... Read adverts carefully!
Samahani, Zomba, ninavyojua mimi "munkari" ni kisawe cha "kitu kibaya, kitendo haramu, jambo ovu". Lakini watu kadhaa hutumia "munkali" kama kisawe cha "hasira", tazama hapa: Mzee Cheche alisema kwa ghadhabu,kitendo kile kilimpandisha hasira Mode na kujikuta akimvaa Jose,ambaye hakukubali wakaanza kupigana. Ilibidi mzee Cheche awe mpole ili kupunguza munkali wa Mode
"Mode ninyi wote ni wapenzi wangu usiwe na hofu utapata kile ulichokikosa"http://maisha.co.tz/kurasa.php?soma=...abariNamba=641
Unaonaje?
Mwishowe, uliandika "... hiyo inachafuwa...". Je, ulitaka kuandika "inachafua"?
Asante sana.
Bila samahani, kwani kiswahili ni lugha inayokuwa kwa haraka sana kwa uchanga wake na kusambaa kwake, inawezekana neno "munkali" lipo nami silijuwi. Nilijuwalo mimi ni munkar(i).
Lakini bado hoja ya kuwa wengi hubadili "r" ikawa "l" ipo pale pale, inawezekana pia hiyo "munkali" ni katika huko kubadili hizo "r" lakini hapo likawa ni neno linaloleta maana nyingine kama ulivyofafanuwa (wala sikusudii fafanua).
kuhusu "inachafuwa" au "inachafua", ni makusudio yangu kutumia "inachafuwa" na wala sikuwa na kusudio la kutumia "inachafua"
Bwana mmoja hapa kasema eti thread ni utepe lakini la thread ni Uzi na utepe ni 'Tape', n kwa issue ya thread kama hizi za JF naonelea ziitwe 'nyuzi' kama ingewezekana. na mimi naulizaje Matongo kwa Kiingereza yaitwaje.....wanugu ebu niambieni....KTY (kwa taarifa yenu) nchi jirani kenya Nugu ni aina ya sokwe....lol
__________________
LOVE IS BLIND BUT MARRIAGE IS AN EYE OPENNER
Bwana mmoja hapa kasema eti thread ni utepe lakini la thread ni Uzi na utepe ni 'Tape', n kwa issue ya thread kama hizi za JF naonelea ziitwe 'nyuzi' kama ingewezekana. na mimi naulizaje Matongo kwa Kiingereza yaitwaje.....wanugu ebu niambieni....KTY (kwa taarifa yenu) nchi jirani kenya Nugu ni aina ya sokwe....lol
Wakuu naomba kuwasilisha.Kutegema na kama uko Uropa ama Marekani neno matongo huitwa Goop,Crud au Rheum (medical terminology). Wengine huita matongo Crystals...wamarekani hawa!
__________________
'Belief in myths allows the comfort of opinions without the discomfort of thought.' - JFK