Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia
Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.
LOVE is a flower, and YOU,its only seed Mjukuu Mtiifu, 2012.
Fidel ebu mwache binti wa watu mbona unamkosesha raha jamani? MJ1 endelea kujifariji bwana achana na kaka zako bwana, 'haweshi' mambo ati!
Huyu analipenda limtu lisilo mpenda na kumjali sasa mm nampenda yeye hanipendi umeona sasa ni vice versa mtu umpendae yeye hakupendi na unae mpenda nae hakupendi.
**^^+..Ukiuza Utumbo usiogope nzi..+^^**
Chuda Raha
Email: [email protected]
Huyu analipenda limtu lisilo mpenda na kumjali sasa mm nampenda yeye hanipendi umeona sasa ni vice versa mtu umpendae yeye hakupendi na unae mpenda nae hakupendi.
Au mpwa nijaribu bahati yangu? Huwezi jua mipango ya Mungu bana.
Atulie kivipi mamii, anahitaji kuchangamshwa, si kuachwa. Ebo!
Ni kweli anahitaji kuchangamshwa ila haya mambo ya kumwambia sijui nani amsarandie bado ni mapema ujue bado ana maumivu,cha muhimu tuwe naye karibu,tumtie moyo.
Ni kweli anahitaji kuchangamshwa ila haya mambo ya kumwambia sijui nani amsarandie bado ni mapema ujue bado ana maumivu,cha muhimu tuwe naye karibu,tumtie moyo.
Kusarandiwa ni sehemu ya kuchangamshwa mamii. Msindima acha kumwekea mpwa wangu kauzibe.
Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia
Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.
Pole dada pole, pole mwana jamii
mapenzi polepole, ndani ya yetu jamii
ulianza hisi polepole, ukadhani huumii
sasa yamegonga kole, watutangazia jamii
nimekusoma kwa kitambo, kwenye forum ya jamii
unalalama kimtindo, ewe mwanajamii
wengi tuliona kombo, kama wana jamii
tukasema mweke kando, akuumizaye mwanajamii
Vera na nyamayao, walikupa zao bidii
wote jinsia yao, walijituma kwa bidii
vidume ni kama zao, wakaanza kwa bidii
wakakaa kimkao, wakusherehe kibidii
lakini hadi sasa, ewe mwana jamii
sipati hata msasa, na kuelewa hii jamii
ni vipi twatakasa, tena kwa zetu bidii
kutoa ndoa takasa, ya Muumba kwa bidii?
Last edited by TIMING; 13th October 2009 at 13:39.
Reason: sed
Follow Us Here