Napatwa utata pale mtu anapoulizwa jina lake au kuagizwa aandike jina lake, kisha anajibu au kuandika, mimi ni fulani fulani fulani ( John Alfa Mohamedi).
Ni sahihi mtu kujibu au kuandika majina matatu wakati kaulizwa JINA lake?
Ukipenda kuepukana na maswali mengi nenda Kenya. Pale sawa ukiingia mahali na kuita tu "Lete taska baridi" - utaipata. Ukiomba bia Kenya uko hatarini kufukuzwa baa maana hawapendi waombaomba.
Lakini si vibaya kuongea kidogo, kwa mawazo yangu ni njia ya kujenga utu na heshima. Sioni hasara yoyote kuendelea na njia ya kibongo. Faida yake nyingine: ukiomba "bilauri" pamoja na bia yako utaipata ila Kenya utamwona mara nyingi mhudumu asiyeelewa kitu.
Hata kwa Kiingereza wanasema “what is your name?”. Hawasemi “what are your names?” Na jibu ni "my name is Augustine Moshi", na sio "my names are Augustine Moshi". Lugha za kikabila vile vile zinatambua Augustine Moshi kama jina langu, na sio majina yangu.
Nirudi tena kwenye Maandiko: Mungu alimwambia Musa kwamba jina lake ni “I AM”. Hilo ni jina la Mungu, na sio majina ya Mungu.

IKO kazi.
Wataalamu toka BAKITA mko wapi?
Nani anipe mawasilano na BAKITA?
The Following 2 Users Say Thank You to Exaud J. Makyao For This Useful Post:
Emma M. (6th December 2009), Idda (9th December 2009)