JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Neno "shikamoo"

  Report Post
  Page 1 of 3 123 LastLast
  Results 1 to 20 of 47
  1. MwanaFalsafa1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Posts : 5,599
   Rep Power : 9983
   Likes Received
   717
   Likes Given
   504

   Default Neno "shikamoo"

   Kwa nilivyo sikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako. Pia nime sikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa lina tumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao. Kuna baadhi ya watu nawajua hawa pendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawa jibu marahaba. Je kama hili neno ni la kitumwa kwa nini sisi tuendelee kuli tumia kama neno linalo ashiria heshima? Kama lili tumika kuwa kandamiza mababu zetu kwa nini na sisi tulipe nafasi? Au tuna litumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lili tumika kudharau mababu zao na kuli fanya la kwetu sasa?


  2. Kaka Mkubwa's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 10th October 2008
   Posts : 155
   Rep Power : 647
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: neno "shikamoo"

   Shikamoo mwanafalsafa!
   "Don't walk as if you rule the word, walk as you don't care who rules the word" That is called attitude.

  3. Mkaa Mweupe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th June 2007
   Posts : 595
   Rep Power : 802
   Likes Received
   82
   Likes Given
   5

   Default Re: neno "shikamoo"

   Hapo umechukua uhalisia wa neno, lakini katika kiswahili neno hili linatumika kama salamu, tazama mfano mwingine:

   mambo: haina maana ya salamu lakini watu wanatumia kama salamu.

   upo hapo?
   The best way to get out of dificulty is through it

  4. Babuyao's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th June 2009
   Posts : 1,721
   Rep Power : 925
   Likes Received
   193
   Likes Given
   148

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By MwanaFalsafa1 View Post
   Kwa nilivyo sikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako. Pia nime sikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa lina tumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao. Kuna baadhi ya watu nawajua hawa pendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawa jibu marahaba. Je kama hili neno ni la kitumwa kwa nini sisi tuendelee kuli tumia kama neno linalo ashiria heshima? Kama lili tumika kuwa kandamiza mababu zetu kwa nini na sisi tulipe nafasi? Au tuna litumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lili tumika kudharau mababu zao na kuli fanya la kwetu sasa?
   Kwa asili neno hilo kweli lilimaanisha hicho ulichosema. Lakini ujue lugha inazaliwa, inakua na kubadilika kadiri jamii inavyobadilika kufuatana na wakati. Kumbe katika lugha nyingi - si Kiswahili tu - misamiati imenyumbuka, kubadilika na hata kuwa na maana tofauti na ile ya mwanzo. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa etymology ya neno au msamiati. Kwa hiyo neno "shikamoo" lenye asili ya Kiarabu lilimaanisha kujidunisha chini ya bwana. Lakini kadiri muda ulivopita, na hasa neno lilivoingia katika lugha ya Kiswahili, lilibadilika maana yake badala ya ile kitumwa likamaanisha Heshima ya mdogo kwa mkubwa wake. Kumbe likawa na maana chanya badala ya ile hasi.
   Kumbe wanaokataa kupokea "shikamoo" hawajui tu. Waelimishwe wajue kwamba kwa leo tena kwa Kiswahili lina maana nzuri tu japo kiasili likuwa na maana hasi ya kudhalilisha.
   Jayonepey and kimui like this.

  5. shiumiti's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2009
   Posts : 435
   Rep Power : 669
   Likes Received
   15
   Likes Given
   0

   Default Re: neno "shikamoo"

   Ndio maana linatumika kumsalimia mtu aliyekuzidi umri, kwa ajili ya heshima uliyonayo kwake.......

  6. shiumiti's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2009
   Posts : 435
   Rep Power : 669
   Likes Received
   15
   Likes Given
   0

   Default Re: neno "shikamoo"

   Ndio maana mtoto hawezi kumsalimia mtoto mwenzake "Shikamoo" au watu wenye umri unaolingana hawasalimiani shikamoo.....
   SALAMU YA SHIKAMOO NI KWA AJILI YA KUMSALIMIA MTU ALIYEKUZIDI UMRI TUU.............

  7. kosamfe's Avatar
   Member Array
   Join Date : 14th April 2009
   Posts : 71
   Rep Power : 603
   Likes Received
   2
   Likes Given
   1

   Default Re: neno "shikamoo"

   Nafikiri matumizi yake kwa sasa ni tofauti na zamani. Kama ndiyo hivyo hata maana yake pia itakuwa imebadirika na kuchukuliwa kama linavyotumika kwa sasa yaani salamu za mdogo kwenda kwa mkubwa.

  8. Oxlade-Chamberlain's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th May 2009
   Location : dodoma
   Posts : 7,627
   Rep Power : 4498
   Likes Received
   796
   Likes Given
   750

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By MwanaFalsafa1 View Post
   Kwa nilivyo sikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako. Pia nime sikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa lina tumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao. Kuna baadhi ya watu nawajua hawa pendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawa jibu marahaba. Je kama hili neno ni la kitumwa kwa nini sisi tuendelee kuli tumia kama neno linalo ashiria heshima? Kama lili tumika kuwa kandamiza mababu zetu kwa nini na sisi tulipe nafasi? Au tuna litumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lili tumika kudharau mababu zao na kuli fanya la kwetu sasa?
   kila kitu ulichoandika hapo juu umepatia.ni neno la kitumwa kweli lakini ndio hivyo mababu zetu kwa kupenda umwinyi wakaliendeleza tu.mara nyingi mimi huwa nalikuwepa neno hilo kwa kutumia "asalam aleykum".
   "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

  9. Peterlyimo's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 25th February 2009
   Posts : 1
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: neno "shikamoo"

   Sawa ni salamu ya mdogo kwa mkubwa lakini inakuwaje pale inapotokea unashindwa kukadiria kwa haraka umri wa unayemsalimia na umri wako? Unapompa mtu shikamoo kumbe ulitakiwa wewe kupewa hiyo shikamoo, hapa huwa haileti picha nzuri kwakweli

  10. LazyDog's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2008
   Posts : 2,302
   Rep Power : 21119
   Likes Received
   69
   Likes Given
   1447

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By Peterlyimo View Post
   Sawa ni salamu ya mdogo kwa mkubwa lakini inakuwaje pale inapotokea unashindwa kukadiria kwa haraka umri wa unayemsalimia na umri wako? Unapompa mtu shikamoo kumbe ulitakiwa wewe kupewa hiyo shikamoo, hapa huwa haileti picha nzuri kwakweli

   Nawapa shikamoo walionizidi miaka mitano au zaidi. Sio rahisi nikaenda fyongo
   A person who won't read has no advantage over one who can't read. -Mark Twain

  11. Mzizi wa Mbuyu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th May 2009
   Posts : 4,190
   Rep Power : 1543
   Likes Received
   816
   Likes Given
   611

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By Arsene Wenger View Post
   kila kitu ulichoandika hapo juu umepatia.ni neno la kitumwa kweli lakini ndio hivyo mababu zetu kwa kupenda umwinyi wakaliendeleza tu.mara nyingi mimi huwa nalikuwepa neno hilo kwa kutumia "asalam aleykum" .
   Mzee Wenger vipi bwana? hata hiyo pia siyo asilia tumekopi mahali!
   Labda ungekuwa unasema "habari za saa hizi, za leo, za siku nk"

   Au uwe unasalimia kilugha, huwa hakina ukubwa au udogo;
   Solowenyo.......inajibiwa solowenyo
   Mihanyenye ....... Misaha
   Wabonaki........Nabonakantu
   Ulmphola...........
   Nazinginezo... zinasidia sana kuikwepa shikamoo, upo?
   kimui likes this.
   Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.

  12. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964199
   Likes Received
   762
   Likes Given
   721

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By shiumiti View Post
   Ndio maana linatumika kumsalimia mtu aliyekuzidi umri, kwa ajili ya heshima uliyonayo kwake.......
   Hili neno hata mimi huwa linanipa maswali nikifikiria historia.Kwani TUK - Taasis ya Uchunguzi wa Kiswahili katika tafiti zao mbalimbali hawajaweza kupata neno lingine kutoka makabila yaliyopo Tanzania kama mbadala wake? Kwenye kabila langu kwa mfano hakuna neno linalofanana na shikamoo! Zipo salamu za kila wakati zenye kuonyesha heshima kwa waliokuzidi umri.Naamini hata makabila mengine wanayo.

   Ila inavyoonekana SHIKAMOO IS HERE TO STAY!
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  13. StaffordKibona's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st April 2008
   Location : Tabora
   Posts : 673
   Rep Power : 774
   Likes Received
   34
   Likes Given
   2

   Default Re: neno "shikamoo"

   Mimi huwa inanikera kumsalimia shiakamoo mtu ninayemzidi umri at. kwa sababu ni shemeji yako Mkubwa yaani dada mkubwa wa mke au mama mdogo wa mke amabye labda unamzidi miaka 10. mambo ya uswahilini utakuta wanaidai kabisa. Kwangu shikamoo siyo salaam mbaya kwa anayekuzidi umri zaidi ya miaka 5

  14. MwanaFalsafa1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Posts : 5,599
   Rep Power : 9983
   Likes Received
   717
   Likes Given
   504

   Default Re: neno "shikamoo"

   Bado ukweli uko pale pale kwamba hili neno lilikuepo kukandamizwa watumwa(haswa sisi weusi), iweje tuli chukue na kulifanya letu? Kama WoS alivyo sema kwani hamna neno mbadala? Iweje kumuambia mtu nipo chini ya miguu yako iwe heshima? Kwani lazima tuige kila kitu? Au sasa ni sisi tunaendeleza utumwa wa kimawazo bila pingu na kengele? Nawashukuru wachangiaji wote hata wale ambao tuna mawazo tofauti.
   Last edited by MwanaFalsafa1; 9th June 2009 at 17:14.

  15. Kitoto Akisa's Avatar
   Member Array
   Join Date : 23rd April 2009
   Posts : 52
   Rep Power : 598
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: neno "shikamoo"

   Ni kweli shikamoo lina asili ya utumwa, lakini kama walivyotanabaisha wachangiaji wengine lugha hukua na sehemu moja wapo ya ukuaji wa lugha ni kama haya mabadiliko tunayoyaona kwenye neno shikamoo. Na sio neno hili pekee ambalo limekuwa "adopted" katika kiswahili kwa maana nzuri tu japo mwanzo yalikuwa na asili fulani ya uduni hivi, mfano neno 'rabeka' ni neno ambalo lilitumika na mwanamke kumuitikia mume wake, na lina asili ya kiarabu pia, na kwa jinsi ilivyokuwa wanawake kwa waarabu walikuwa hawathamini sana, lakini sasa linatumika kama heshima ya mwanamke kumuitikia mumewe hasa katika ukanda wa pwani, neno jingine ni ' naam' ni neno lilikuwa linatumika kukubali kitu au jambo, lakini kwa sasa kwenye kiswahili linatumika kama kiitikio cha heshima kwa mtoto wa kiume aitwapo. Yapo maneno mengi tu kama mem sahib, sasa linatumika kama mamsapu nk

  16. Dingswayo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th May 2009
   Posts : 3,696
   Rep Power : 86311930
   Likes Received
   2462
   Likes Given
   6598

   Default Re: neno "shikamoo"

   Shikamoo: shika moyo wangu

  17. MwanaFalsafa1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Posts : 5,599
   Rep Power : 9983
   Likes Received
   717
   Likes Given
   504

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By KAKA MKUBWA View Post
   Shikamoo mwanafalsafa!
   Dah huu uchokozi kaka mkubwa hahaha.

  18. Sasha Fierce's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th February 2009
   Posts : 357
   Rep Power : 670
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: neno "shikamoo"

   Ok inajulikana kuwa shikamoo ni salaam unayompa mtu aliyekujizi umri (sifahamu kama kuna age limit) Ila Kuna wababa wengine especially binti wa kike akimwambia shikamoo humjibu "salama tuu binti hujambo".And why is that?.
   I am sasha fierce.

  19. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964199
   Likes Received
   762
   Likes Given
   721

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By Sasha Fierce View Post
   Ok inajulikana kuwa shikamoo ni salaam unayompa mtu aliyekujizi umri (sifahamu kama kuna age limit) Ila Kuna wababa wengine especially binti wa kike akimwambia shikamoo humjibu "salama tuu binti hujambo".And why is that?.
   SF,
   Hii inatokana na kwamba - unapotanguliza shikamoo ni kama umeweka kizuizi cha heshima.Anapokataa kuitika inavyotakiwa ni kwamba alikuwa ana mpango mwingine na wewe na anashangaa barrier ya nini tena?
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  20. Raia Fulani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th March 2009
   Posts : 9,905
   Rep Power : 2828
   Likes Received
   1501
   Likes Given
   962

   Default Re: neno "shikamoo"

   Quote By MwanaFalsafa1 View Post
   Bado ukweli uko pale pale kwamba hili neno lilikuepo kukandamizwa watumwa(haswa sisi weusi), iweje tuli chukue na kulifanya letu? Kama WoS alivyo sema kwani hamna neno mbadala? Iweje kumuambia mtu nipo chini ya miguu yako iwe heshima? Kwani lazima tuige kila kitu? Au sasa ni sisi tunaendeleza utumwa wa kimawazo bila pingu na kengele? Nawashukuru wachangiaji wote hata wale ambao tuna mawazo tofauti.
   tafuta kwanza hicho chanzo kinachosema hivyo ndio tuendelee na mada
   Beware of a sucker punch


  Page 1 of 3 123 LastLast

  Similar Topics

  1. Replies: 5
   Last Post: 8th November 2013, 14:43
  2. "Shikamoo" baina ya wanandoa: Je kuna umuhimu?
   By Pretty in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
   Replies: 66
   Last Post: 6th October 2012, 10:06
  3. Replies: 0
   Last Post: 12th September 2011, 01:11
  4. Eti soko la """kitimoto ""kuanza kupungua kuanzia kesho""
   By Pdidy in forum Celebrities Forum
   Replies: 2
   Last Post: 11th August 2010, 12:27

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...