__________________ Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Mashkuura yaa jamiiya. Nimefurahi sana huu usanifu wa lugha.
Dr Hamza. (Barubaru)
Mwalimu, duh nimefurahi kutambua kwamba upo. Natumaini na familia nzima wote wazima. Tunakukaribisha tena na tena. Usipotee hivyo ndugu yangu.
M.M.
__________________ Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Wakulu, nadhani hizi beti zinanoga zaidi mchana....wakati wa jua kali na unenge ukiwa uko kwao.
Kwa maana nyingine waote mlikua amnanja............
__________________ God inspired me,Do not seek any perfect trust of the people and do not depend on them for they will perish you.......'' Bahaeddin al Balkh (Maarif I/360)
Sasa narudi tena,kwa usongo na kiburi
Ugali chema chafana,Njaa unasitiri
Wafaa liwa mchana,Chokapo kazi tiririri
Ugali ni kitu chema, kimenikuza nakiri
Napenda tonge mawili,yalonasana kikweli
Kwa kisu na pilipili,na tunda la stafeli
Mboga iwe tumbili,Au kuku wa da' pendaeli
Ugali ni kitu chema,Kimenikuza nakiri
Nasema tena na nena,Unafaa kwa shughuli
Hasa ukiwa kijana,mwenye nguvu na rijali
Mke hamtokosana,'Wazungu' hawatofeli
Ugali ni kitu chema,kimenikuza nakiri.
Nyie kuleni tu wali,mkiibiwa shughuli
Ugali ngoma hailali,Kibada -Gonja Betheli.
Jaribu kula ugali,uvute sigara kkali
Hutapata ile hali,wapatayo wala wali
Ugali ni kitu chema,kimenikuza nakiri
Wageuzwa wapikwa wali,Aku, kamwe mi sili
Ageuzwe perege a-ghali,huyu tamla kwa ugali
Wali harufuye kali,Hakika nasema sili
Ugali ni kitu chema,kimenikuza nakiri
Kadi tamati wa tama,kama malenga wa zama
Nimetoa nlosema,Chumbani kwangu nazama
Nahavacheni wote jama,Ugali kama Obama
Ugali ni kitu chema,Kimenikuza nakiri
Amani...
__________________ He who wants to keep his garden tidy doesn't reserve a plot for weeds
Wote nimewashangaa, mlosifia ugali,
Mmefanya ukang’aa, kwa sifa zisizo kweli,
Wengine mwagaagaa, kushangilia ugali,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?
Kila palipo ugali, hapakosi kitoweo,
Kumeza tonge muhali, bila chake kimezeo,
Na huo ndio ukweli, mawio hadi machweo,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?
Mnasifia ugali, pembeni mwataja mboga,
Hebu semeni ukweli, mboga ndio inanoga,
Acheni kututapeli, kutugeuza mizoga,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?
Mzee Mwanakijiji, ndugu yangu wa daima,
Ugali si kama uji, bila mboga utatema,
Bora wali wa Ujiji, usiokuwa na nyama,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?
Yametajwa matembele, mlenda pia kisamvu,
Pweza, dagaa mchele, kachumbari na mnavu,
Nyama nayo vilevile, ya mchuzi ama kavu,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?
Ugali huli mkavu, kama ubwabwa wa Kyela,
Yatakuvimba mashavu, tonge huwezi kulila,
Yataka uwe shupavu, vinginevyo ni madhila,
Utamu si wa ugali, bali chake kitoweo!
Msinione mbishi, bali ni yangu maoni,
Wala msinishawishi, niyakubali ya nani,
Maswali siyajalishi, kuweni uhuru moyoni,
Utamu si wa ugali, bali chake kitoweo!