jamani wapedwa kuna utata umejitokeza chit-chat kuhusu utofauti wa hayo maneno hapo juu.naomba ufanunuzi please!
jamani wapedwa kuna utata umejitokeza chit-chat kuhusu utofauti wa hayo maneno hapo juu.naomba ufanunuzi please!
ASIYEUMBA HAUMBUI
kumbe siko peke yangu watu ishiri walioview hakuna hata aliyepapasa ka jibu,kiswahili ki gumu jamani
ASIYEUMBA HAUMBUI
Ngoja nijaribu, kimsingi maneno hayo hayana tofauti ni kama ni moja ni mbadala wa lingine, maana kwa kiingereza yote yanafasiriwa kama Mixes breed au Half caste! lakini hili Shombe limedadavuliwa zaidi kwa kuonesha ni mchanganyiko wa damu hasa ya mwarabu na watu wa jamii nyingine, wakati Chotara ni " coloured" na haijalishi amechanganya vipi damu! nawasilisha
kilebwe asante kwa kunipa mwaga hafifu ngoja tuwasubiri na wengeni.............
ASIYEUMBA HAUMBUI
ummu kulthum kwa Mujimu wa Kamusi ya TUKI
shombe nm ma- [a-/wa-] halfcaste person, mulatto, mixed blood, coloured.
chotara nm [a-/wa-]
1. chotara = half caste, mulatto.
2. chotara = mixed breed, crossbreed (of seeds or animals):
- Kuzaa watoto chotara = miscegenation;
- Mbwa chotara = mongrel/mutt;
- chotara wa Kiberiberi na Kiarabu = Moor.
miscegenation n uchotara, usuriama; kuzaa watoto chotara.
.
Life was Simple When Apples and Blackberries were Just Fruits
Mimi naona maana ni moja
Blessed are hearts that bend but shall never broken
jamani wapedwa kuna utata umejitokeza chit-chat kuhusu utofauti wa hayo maneno hapo juu.naomba ufanunuzi please![/QUOTE]
Kwa mtazamo wangu ni vyema kwanza kujua maana ya Chotara na shombeshombe
Chotara naamini na mchanganyiko wa damu au asili ya mataifa mawili tofauti kwa level ya mabara na mchanganyiko wa asili ya mabala tofauti kwa maana hiyo naamini hata mchanganyiko wa makabila mawili unazalisha Chotara
Shombeshombe ni mchanyiko wa wabantu na watu wenyeasili ya uarabu huo ni mtazamo wangu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Follow Us Here