Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nizinusheni wakuu wa luhga

    Report Post
    Results 1 to 6 of 6
    1. #1
      WANGU MTENZI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th June 2012
      Location : MTWAPA-KENYA
      Posts : 20
      Rep Power : 356
      Likes Received
      5
      Likes Given
      33

      Default Nizinusheni wakuu wa luhga

      Lahaja ya Kiunguja ndiyo ilo sanifishwa kuunnda Kiswahili kulingana na historia yake.Kulikuwepo na lahaja nyingine nyingi ikiwemo;Kimvita,Kijomvu,Kimtan gata n.k.Ni sababu zipi hasa zilizochangia kupendekezwa kwa Kiunguja?
      Dotworld likes this.

    2. #2
      Dotworld's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 2,740
      Rep Power : 1152
      Likes Received
      1541
      Likes Given
      1941

      Default Re: Nizinusheni wakuu wa luhga

      lahaja = dialect.

      Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia. Lahaja za lugha moja zatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati.

      Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi na siyo lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.

      Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:

      vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)
      vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika (k.m. lahaja maarufu)
      vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)
      vipengele vya eneo (kitarafa)

      Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingerezana lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine.

      Tena, lahaja za Kiswahili hutofautishwa kulingana na maeneo yake kama Kiamu (kisiwani kwa Lamu), Kimvita (mjini kwa Mombasa), Kiunguja (kisiwani kwa Zanzibar, Kingazija (visiwani kwa Komoro) na kadhalika

      ==

      Lahaja za Kiswahili

      Kiswahili kimepatikana kwa namna au lahaja mbalimbali. Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.

      Kati ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:

      Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.
      Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
      Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
      Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
      Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.
      Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
      Kingwana: Kiswahili cha Kongo
      Shikomor: Kiswahili cha Komoro
      Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
      Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
      Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
      Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba
      Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia

      Sheng
      : Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya

      ==

      Kurudi kwenye swali la mleta mada WANGU MTENZI

      Swali:
      Ni sababu zipi hasa zilizochangia kupendekezwa kwa Kiunguja?

      Jibu:
      kuhusu sababu sijui .... ila nachofahamu ni kuwa Wakati wa ukoloni wa Uingereza AZIMIO lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar

      Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda..

      Dduhsi itnuhn kose kiri itda ---> 뜻이 있는 곳에 길이 있다

    3. #3
      mtemiwaWandamba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2011
      Location : MTONI RUIPA
      Posts : 429
      Rep Power : 497
      Likes Received
      76
      Likes Given
      66

      Default Re: Nizinusheni wakuu wa luhga

      [QUOTE=Dotworld;4216660]lahaja = dialect.

      [/QUO

      Ahsante mkuu, nimepata mengi hapa.
      swali la nyongeza: Na hii Lahaja ya Kimtangata ni ya maeneo gani hii?
      au inaingiliana na Kimvita?
      WANGU MTENZI likes this.
      Maajabu ya Kenge; anakimbia Mvua anaingia Mtoni.

    4. #4
      Dotworld's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 2,740
      Rep Power : 1152
      Likes Received
      1541
      Likes Given
      1941

      Default Re: Nizinusheni wakuu wa luhga

      Quote By mtemiwaWandamba View Post

      Ahsante mkuu, nimepata mengi hapa.
      swali la nyongeza: Na hii Lahaja ya Kimtangata ni ya maeneo gani hii?
      au inaingiliana na Kimvita?
      mtemiwaWandamba
      ... Kimtangata ... ni cha mwambao wa Tanga
      Dduhsi itnuhn kose kiri itda ---> 뜻이 있는 곳에 길이 있다

    5. #5
      mtemiwaWandamba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2011
      Location : MTONI RUIPA
      Posts : 429
      Rep Power : 497
      Likes Received
      76
      Likes Given
      66

      Default Re: Nizinusheni wakuu wa luhga

      Quote By Dotworld View Post
      mtemiwaWandamba
      ... Kimtangata ... ni cha mwambao wa Tanga
      Ahsante mkuu.
      Dotworld likes this.
      Maajabu ya Kenge; anakimbia Mvua anaingia Mtoni.

    6. #6
      li sheng's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th September 2008
      Location : Tanzania.
      Posts : 47
      Rep Power : 558
      Likes Received
      12
      Likes Given
      8

      Default Re: Nizinusheni wakuu wa luhga

      Quote By WANGU MTENZI View Post
      Lahaja ya Kiunguja ndiyo ilo sanifishwa kuunnda Kiswahili kulingana na historia yake.Kulikuwepo na lahaja nyingine nyingi ikiwemo;Kimvita,Kijomvu,Kimtan gata n.k.Ni sababu zipi hasa zilizochangia kupendekezwa kwa Kiunguja?
      Asante, Mim binafsi nahisi labda kwanza niongezee Unguja mjini, mana akisema Mdonge au mkojani au Mmakunduchi utaondokea patupu.
      Sababu
      !. Kiunguja lugha yake haina lafdhi (TONE) iko mshazari (Straight) mfano haina ma re re re au le lele au kuimba kama watanga
      2.Kuinguja kimechanganya maneno mengi ya kujaliza kama kiiengereza Baskeli=Bicycle, kiarabu halwa =Haluwa , kihindi paisa = pesa etc ni lugha rafiki inakubalika
      3. Ina madaha au mayaaghani mfano, "Mmh yakhee unajua kama leo Ijumaa kuna harusi!", maneno ya mkato mfano twende zetu = twenzetu, etc
      4. Makao makuu ya utawala na kituo kikuu cha biashara au uchumi kilikuwa Unguja watu wengi walikuja Unguja hivyo kuongea kiunguja ni rahisi kuongea na waswahili wote.
      Natumai sijui utakuwa umeridhika?
      WANGU MTENZI likes this.

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...