Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hebu kumbuka tulikotoka, bongo fleva ni mtoto wa jana

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      galagaja mtoto's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Posts : 84
      Rep Power : 368
      Likes Received
      15
      Likes Given
      26

      Default Hebu kumbuka tulikotoka, bongo fleva ni mtoto wa jana

      TUNDA

      Sheria na mila zetu, utokapo utotoni watambulika na watu, waingizwa ukubwani, waitwa mzima mtu, kisa ndevu kidevuni, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Kundi kubwa kijijini, wengi wao ni vijana, pinde ziko mkononi, visu tulinoa jana, twaelekea porini, kwenda kusaka amana, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Safari imekolea, mikono watupungia dua wanatuombea wengine watulilia, msitu twauendea, kijiji twakiachia, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Safari hii hakika uvumilivu yataka, inagharimu miaka na miongo kukatika, Huusisha kinakaka , na wadada kadhalika, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Sekunde dakika siku, miezi kufika mwaka, mchana hadi usiku, amana tunaisaka, zunguka huku na huku wengine wameshachoka, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Kila tunakopitia, mengi tunajionea, wengine wanabakia vizuri kijibebea, wachache tumebakia safari kuendelea, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Ilifika siku moja nilibakia mwenyewe, zaidi ya mia moja walishaweka vijiwe, nikaona tunda moja lisilo na mfanowe, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Kwa hakika tunda hili limependeza mtini, hajaliona tumbili lisingedumu mtini, napiga hatua mbili nasogelea mtini, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Wenzangu walio nyuma wamejenga na vibanda, kwa bahati ya karima familia wameunda pekee nimesimama, nalitaka lile tunda, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Nachukua mawe yangu nilishushe lile tunda, na mimi dhamira yangu kusimamisha kibanda, kama wlivyo wenzangu , familia kuiunda, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Mojamoja natupia jiwe kwenye tunda lile, na tena nalisifia, tunda lapendeza lile, tena limejiivia nalipenda ili nile, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Mwili wote umechoka tunda ninalililia, ni mitano sasa miaka mawe ninalitupia, nami pia kwa hakika moyoni nimelitia, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Si chungwa wala si embe sio epo sio dafu, nikiufanya uzembe, naweza geuka mfu, lafanana na kiumbe mwenye baba mtukufu, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Jamani nakaa chini pekee nimebakia, panatisha msituni, lakini ninayo nia, njia nyiongine nipeni nipate kulitungua, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa.

    2. Miaka 50

    3. #2
      mizambwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2008
      Posts : 1,436
      Rep Power : 974
      Likes Received
      367
      Likes Given
      1805

      Default Re: Hebu kumbuka tulikotoka, bongo fleva ni mtoto wa jana

      Quote By galagaja mtoto
      TUNDA

      Jamani nakaa chini pekee nimebakia,
      panatisha msituni,
      lakini ninayo nia, njia nyingine nipeni
      nipate kulitungua, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa.

      Pole sana ndugu yangu, kwa uchovu ulopata,
      Kweli yatia uchungu, kwa tunda kutolipata
      Yote mkabidhi Mungu, neema ataileta
      Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

      Kwa tunda lilio zuri, shida sana kulipata,
      Walifungia safari, Ubungo hadi Msata,
      Kwani ni tamu na zuri, gharamia hutosita,
      Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

      Ongeza yako juhudi, na tamaa kutokata,
      Itafikia kipindi, hilo tunda utapata,
      Unahitaji ufundi, ili upate livuta
      Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

      Pindi ukirusha jiwe, pia jaribu kuita,
      Lahitaji lisifiwe, kwa maneno yenye nta,
      Na ulimi utumiwe, ili kuweza livuta,
      Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

      Na bado nasisitiza, kwa tama kutokata,
      Lala kesha ukiwaza, mbinu mpya utapata,
      Tabasamu liwe kwanza, hakika utalipata
      Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

      ============================== ===========


      MIZAMBWA
      INANIUMA SANA!!!
      Last edited by mizambwa; 19th June 2012 at 16:19.
      SASA NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!!, TUANDAE KABURI LA KUIZIKA MWAKA 2015

    4. FemaTV & Radio

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...