Wapendwa natafuta kitabu cha hadithi kinachoitwa 'Mambo ya Ajabu Yaliyompata Allan Quatermain na Wenzake' tafsiri ya Kiswahili. Je, kuna sehemu yoyote ndani ya Tanzania nitakipata hiki kitabu?
Wapendwa natafuta kitabu cha hadithi kinachoitwa 'Mambo ya Ajabu Yaliyompata Allan Quatermain na Wenzake' tafsiri ya Kiswahili. Je, kuna sehemu yoyote ndani ya Tanzania nitakipata hiki kitabu?
du zamani tulikuwa stori hizo tulikuwa tunazikariri vichwani, nangoja kusikia vinakopatikana
Umenikumbusha Umsolopogas "Mwana wa Mfalme Chaka", Sir Henry Curtis, Nyleptha, Solais kwenye nchi ya Wazuvendi
Hahahaaa, nimekumbushwa mbali. Na ile shoka iliitwaje?Inkosikazi au?
Je, naweza kupata wapi kile cha 'Mlima kolelo' na 'Mashimo ya Mfalme Suleiman'?
...Kinaitwa ' Hadithi ya/za Allan Quarterman'. Jaribu pale duka la Vitabu mtaa wa Samora karibu na Extelcomms. Unaweza kukipata japokuwa kitakuwa toleo la kisasa na sio lile tulilosoma sisi mwaka 47
Sema Kwa Sauti, Mimi Ni Mweusi Na Najivunia Kuwa Hivyo!
Nilisoma story ya umsolopagas,kumbe was a true man,tafuta around samora Ave, unaweza ukapata mkuu!
Nenda katika duka la TPH mitaa ya Posta. Nilivikuta nkanunua hadi nkaviacha.
Musia Mkuu, wasialiana na X-PASTER pia tembelea uzi wake huu: Riwaya za Zamani, Hadithi ya Allan Quatermain
"JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"
pia sio mbaya ukitafuta movie hii
'THE LEAGUE OF EXTRA ORDINARY MEN'
NI MOVIE ILIYOTENGENEZWA NA HISTORIA YA ALAN
Follow Us Here