Wakubwa woote Shikamooni na niliowazidi umri Marhabaa!
Wana jukwaa hili ninawaomba, tena kwa heshima zote! Mnifahamishe maana ya hili neno; "Kafiri" jee! ni tusi! au ukimuita mtu Kafiri unamvunjia heshima?
Shukrani!
Wakubwa woote Shikamooni na niliowazidi umri Marhabaa!
Wana jukwaa hili ninawaomba, tena kwa heshima zote! Mnifahamishe maana ya hili neno; "Kafiri" jee! ni tusi! au ukimuita mtu Kafiri unamvunjia heshima?
Shukrani!
Last edited by Userne; 5th May 2012 at 14:49.
Userne
Kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI
kafiri* nm ma- [a-/wa-] infidel, unbeliever, atheist, pagan. (Kar)
Dduhsi itnuhn kose kiri itda ---> 뜻이 있는 곳에 길이 있다
.......
"NAJUA kwamba mimi ni mwerevu na mwenye akili,kwa sababu nafahamu kwamba HAKUNA NINACHOFAHAMU" socrates
Rose1980....na huyu pia ni kafiri eeeh......
Life is too short to waste time hating anyone.........
Neno lolote linaweza kuwa tusi au sifa. Inategemea utapolitumia.
"Yule kijana mkafiri kweli kwa kupiga kitale", hiyo ni sifa nzuri tu.
"Kafiri mkubwa wee" ni sifa lakini sio sifa njema.
Neno "kafiri" linatokana na neno la Kiarabu (kama ilivyo kwa maneno mengi ya Kiswahili) "kafir", Kafir kwa kiarabu ni mwenye kukufuru, haijalishi ni wa dini ipi, hata Muislaam anapokwenda kinyume na Uislaam wake basi huyo anakuwa amekufuru "kafir".
Kuna wale ambao Waislaam huwaona kuwa wame "declare" kabisa kwenda kinyume na Mwenyeezi Mungu kwa kuabudu, binaadam wenzao, kuabudu wanyama, kuabudu masanamu, hao wote ni makafiri mpaka watakapojitoa katika kuamini hayo.
Last edited by zomba; 8th May 2012 at 14:31.
Kwa hapa kwetu bongo ni neno tu ambalo waislamu tunalitumia kuwakera wakristo. Halina tofauti na wao wanavyotuita shehe ubwabwa kwa kuwa tunapenda sunna ya wali a.k.a ubeche
Kwa lugha si neno baya. Ni sawa na kusema mtu asiye na dini. Kuwa baya au zuri ni tafsiri. Kwa mfano, tafsiri ya mtu MSHENZI ni mtu asiye na dini, yaani mpagani. Lkn unaweza kuona kwamba namna neno mshenzi litakavyotamkwa linaweza likamfanya mpagani ahi kutukanwa badala ya kuwa fairly addressed.
.
Haya Preta yule mjusi anaitwa Red headed rock Agama ... Mjusi Kafiri ana tabia ya kukaa kwenye jiwe na/au kupigapiga kichwa chake juu na chini .. Ila to be honest sijui ni kwanini huyu mjusi aliwakosea nini binadamu mpaka akaitwa Jina hilo.
Dduhsi itnuhn kose kiri itda ---> 뜻이 있는 곳에 길이 있다
asante sana mkuu Dotworld.....je sasa na huyu hapa anaitwaje kwa kiswahili.....?
Life is too short to waste time hating anyone.........
.
Asante mkuu Preta
Nimekuelewa vizuri tu ... sasa unajua katika Kiswahili nafikiri huwa tunawaita tu mijusi alafu inaishia hapo ni mara chache ukakuta watu wanasema huyu ni mjusi wa aina gani.
Hata hivyo hii picha ni ya mjusi ambae kwa kingereza anaitwa House Gecko ingawa ukim-define zaidi anaitwa Flat-tailed House Gecko. Ambapo mara nyingi huitwa Common House Gecko ambapo huwa wanafupishwa na kuitwa Gecko
Kwa Kiswahili (Huyo mjusi wako hapo juu)
Common House Gecko = Gecko = Mjusi Kafiri
Sasa kwa nini Yule mwingine hapo juu ambae kwa kawaida watu humuita mjusi kafiri mimi sijui
Ingawa pia kuna aina nyingine ya mijusi ambayo ina majina ya kiswahili:
Mfano:
Goromwe ni (kind of tree lizard)
Guruguru ni (large burrowing lizard)
.
Back to the point,
Huyo mjusi wako hapo juu Common House Gecko = Gecko = anaitwa Mjusi Kafiri
.
Dduhsi itnuhn kose kiri itda ---> 뜻이 있는 곳에 길이 있다
Kiislamu Binadamu wamegawanyika katika aina mbili:
Muumini (Muislamu) na Kafiri, hakuna aina ya tatu.Hivyo kila asiye Muislamu ni Kafiri.
Na muovu zaidi na mbaya wa makafiri wote ni mnafiki, huyu naye ni kafiri ila huficha kufuru yake hali akidhihirisha Uumini.
Na wanafiki kuna aina mbili:
Mnafiki wa asili na mnafiki asiye wa asili.
Mnafiki wa asili:
Huyu ni yule ambaye hajawahi kusilimu au kuingia katika Uislamu, lakini hujifanya ni Muislamu.
Mnafiki asiye wa asili:
Huyu ni yule ambaye aliwahi kuwa Muislamu, halafu akauacha Uislamu na kuwa si Muislamu lakini hujidhihirisha kuwa ni Muislamu.
Muislaam ambae haabudu Mwenyeezi Mungu Mmoja, au anaenda kinyume na maamrisho ya Mwenyeezi Mungu (anamkufuru) unaweza kumuita kafir, kama Muislaam ana abudu Mwenyeezi Mungu mmoja na haendi kinyume na Maamrishi ya Mwenyeezi Mungu, ukimuita kafir, inakuwa humtendei haki, kwani mwenye kukufuru ni yule niliyemuelezea huko juu.
Naona tuko darsa leo.....nachukia sana hili neno 'KAFIR' silipendiiiii aaarrrgggghhhh
God can heal a broken heart but you have to give him all the pieces.
Follow Us Here