Wakubwa woote Shikamooni na niliowazidi umri Marhabaa!
Wana jukwaa hili ninawaomba, tena kwa heshima zote! Mnifahamishe maana ya hili neno; "Kafiri" jee! ni tusi! au ukimuita mtu Kafiri unamvunjia heshima?
Shukrani!
Wakubwa woote Shikamooni na niliowazidi umri Marhabaa!
Wana jukwaa hili ninawaomba, tena kwa heshima zote! Mnifahamishe maana ya hili neno; "Kafiri" jee! ni tusi! au ukimuita mtu Kafiri unamvunjia heshima?
Shukrani!
Last edited by Userne; 5th May 2012 at 14:49.
Kafiri ni mtyu yeyote anayepinga imani fulani...
Mfano wewe ukisema Yesu ni mwana wa Mungu, mtu mwingine akapinga basi, huyo mtu ni Kafiri.....
Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.
Kafiri ni mtyu yeyote anayepinga imani fulani...
Mfano wewe ukisema Yesu ni mwana wa Mungu, mtu mwingine akapinga basi, huyo mtu ni Kafiri.....
Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.
Kafiri pia inaamaanisha mtu mweusi South Africa na unaweza kushitakiwa ukilitumia hili neno.
Ni tusi kwa sababu ya watu wanavyolitumia kama tusi ila technically maana yake ni sawa na Atheist ambalo watu hawalioni kuwa ni tusi.
“Society is like a stew. If you don't stir it up every once in a while then a layer of scum floats to the top.”
Mimi nadhani kwa tafsiri ya kiislam ambayo imetokana na kiarabu ambacho ndiyo chimbuko la neno husika, kafir ni mtu yeyote asiyefuata kikamilifu mafundisho ya mtume Mohammed SWA. Kwa hiyo kwa tafsiri ya kiislamu wakristu, wahindu, wabudha nk wote ni makafiri.
TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO KAMA AKINA EL, JK, EC na RA
Hii kauli huwa inanikera sana sijawahi kumsikia mkristo yeyote anamwita mtu yeyote ambaye si mkristo kafiri, lakini wiki iliyopita nilikuwa napita Kiwalani kulikuwa na mabishano kati ya waislamu na wakristo, wale waislamu walisema mtu yeyote ambaye si mwislamu ni kafiri.Lakini kuna tafsiri inayosema kafiri ni sawa na mpagani lakini maana halisi ya neno kafiri ni mtu yeyote asiye muislamu ni kafir.
Katika dunia ya leo iliyoelimika na kustaarabika (kustaafrika?) kumuita mtu mwingine kafiri ndio ukafiri wenyewe.
Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.
Tungekuwa sote tunaoishi eneo moja mathalani tanzania ni waislamu (ndio dini inayotumia neno hilo) basi kuwaita wasiokuwa waislam kafir inaweza kueleweka, lakini kuwaita wenzako kafiri katika mchanganyiko wa dini kama hapa kwetu na wakaona kwao ni tusi,basi ni sawa kusema hilo neno ni tusi.
Kwa kumbukumbu bungeni wamekataza kutumia neno "kukazana"
Kwenye Quraan yeyote ambae haamini kitabu hicho basi ni KAAFIR , na wamegawanyika pia, kuna Kafiri anaeupinga Uislamu na KAFIRI ambae haupingi Uislamu. na wana HUKMU TOFAUTI. so kama Muislamu atamwita asie Muislamu Kafir basi sidhani kama kosa kwa sababu ndio kitabu kinavomuelekeza, Sijui kuhusu Injiil imesema vipi.
Wapo sahihi ikiwa tu watatumia kwa yoyote yule isipokuwa Muislamu.Hakuna Muislamu ambaye haabudu Mwenyezi Mungu mmojaBy UserneSi sahihi kumuita kafir kwa sababu madhambi hata makubwa hayamtoi muislamu automatically kwenye Usilamu, huyu unaweza kumuita faasiq (Mfanyaji ufuska), dhaalim (dhalimu),muovu n.k lakini si kaafir.By UserneInakubalika na Muislamu ambaye hakubali kum declare kaafir ambaye Allah mwenyewe amem declare kuwa kaafir kwenye Quran,basi huyo Muislamu mwenyewe anakuwa kaafir kwa sababu atakuwa ameikanusha Quran.By Userne
*Baada ya yote haya yaliyosemwa hapa sielewi ni kwa nini mtu ambaye si Muislamu anajiona kuwa ametukanwa kwa kuitwa Kafiri!
Napita kimya kimya tu
nadhanisuali hili linatakiwa kujibiwa kiiman zaidi,kwani neno kafiri matumizi yake yapo katika dini na si matumizi ya kawaida, mfano unaweza kumuita mtu wewe shetani,je shetani ni kiumbe au sifa?jibu shetani ni sifa ya kiumbe mtenda maovu,awe binadamu au jini(malaika hayumo),Ibilisi ndio jina halisi la yule aliyeasi amri ya Mungu kumsujudia adamu(kwa waisalmu)wakristo aliyemshawishi kuliwa kwa tunda.
nikirudi kwenye suali la msingi Kafiri si tusi,bali ni jina lilobeba sifa,utambulisho,hivyo kuna muislamu na kafir(kwa mujibu wa imaan ya uislamu)na kuitwa kafir maana yake aliyekataa yale aliyokuja nayo mtume Muhmmad(rehma na amani ziwe juu yake)hivyo mkristo hawezi kumuita muislamu kafir kwani kapinga kipi? injili,taourat,zaburi vyote muislamu anavikubali,hivyo hawezi kuwa kafiri.
Follow Us Here