| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
#51
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Wanawane mwanishangaza,hayo matunda kuyasifia
Ukweli daima hamtoweza,kunishawishi kuyatumia Daima kwangu la kwanza,Embe dodo ninalitumia Mimi wa Usukumani,embe dodo namba wani Embe dodo lapatikana,kila mkoa wa Tanzania Zabibu ni adimu sana,wachache ndo lawafikia Dafu ni ngumu sana,mnazini kukwea kulifikia Mimi wa Usukumani,embe dodo namba wani Utamu wa ndizi jamani,kwa embe dodo cha mtoto Nikiweka ndizi tumboni,navimbiwa kama Mpoto Ewe Suki mwanawani,jaribu dodo si la msoto Mimi wa Usukumani,embe dodo namba wani Maamuma na Mwanakijiji,wa bure ushauri nawapa Tunda zuri kama mwahitaji,Embe dodo ndio supa Ukila shushia ya baridi maji,ya mtungini si ya chupa Mimi wa Usukumani,embe dodo namba wani Embe dodo Usukumani,baada ya chakula laliwa Daima walikuta mezani,kwa vipande limekatwa Vyakula vya Usukumani,mtindi,viazi-matovolwa Mimi wa Usukumani,embe dodo namba wani Embe dodo tunda letu,daima twalila tutakavyo Twakata vipande vyetu,na kuvila itakiwavyo Pia kulinyonya ndo zetu,kama mtoto anyonyavyo Mimi wa Usukumani,embe dodo namba wani Litaendelea…. Na; Balantanda Masalakulangwa(Sauti ya Gamboshi)
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||