Re: Zabibu!
Tunda zabibu silifagilii
Utamu wake haunivutii
Hata ufanye bidii
Kunishawishi sintokutii
Tunda nilipendalo asilani
Ni Embe dodo la kijijini
Lina utamu uso kifani
Hasa likiivia mtini
Zuri likiivia mtini
Zabibu haioni ndani
Saba mara sabini
Daima lawa namba wani
Wewe Mzee wa kijijini
Kula zabibu umeanza lini
Waachie watu wa mjini
Zabibu iwe mwao akilini
Embe dodo la thamani
Likianguka toka mtini
Linalala mchangani
Kisha najiokotea kiualini
Ninalimenya kwa mbwembwe
Mithili ya Mwanamazingaombwe
Daima nalila kwa mbwembwe
Na umakini kama Zitto Kabwe
__________________
Amantium irae amoris integratio est
10th March 2009, 12:32 AM
Binti Maringo
Thinking!
JF Senior Expert Member
Join Date: Wed Jul 2007
Posts: 2,625
Thanks: 48
Thanked 172 Times in 132 Posts
Rep Power:
28
Re: Zabibu!
Quote:
Wewe Mzee wa kijijini
Kula zabibu umeanza lini
Waachie watu wa mjini
Zabibu iwe mwao akilini
Balantanda usimzalau mzee wa kijijini ooh! shauri yako
anyways i am otu for the day!....see you all manyana...i got go cook for my cupcake.you know how it is inabidi na mimi nipalilie shamba langu maana mimi ni tunda uwii!...
xoxo
__________________
Nothing shall delay my miracles!...
10th March 2009, 12:40 AM
Balantanda
Arsenal damu
JF Senior Expert Member
Join Date: Sun Jul 2008
Location: Kusadikika
Posts: 2,467
Thanks: 744
Thanked 1,083 Times in 624 Posts
Rep Power:
27
Re: Zabibu!
Quote:
Balantanda usimzalau mzee wa kijijini ooh! shauri yako
anyways i am otu for the day!....see you all manyana...i got go cook for my cupcake.you know how it is inabidi na mimi nipalilie shamba langu maana mimi ni tunda uwii!...
xoxo
Yeah,always bradha awe first bwana...Thank God he found you 'embe dodo'
__________________
Amantium irae amoris integratio est
10th March 2009, 03:45 AM
Suki
is lickin' the lackin' luck...
Senior Member
Join Date: Tue Nov 2007
Posts: 218
Thanks: 0
Thanked 20 Times in 13 Posts
Rep Power:
23
Re: Zabibu!
Quote:
I know... didn't I say I'm a first learner too?
Zabibu ukijapewa
Hilo utalichukuwa
La bure ukimegewa
Utalila kama muwa?
Vipi kama bado bichi,
Tena kijani kibichi,
Utatusa kuwa mbichi
Au hata hivyo huliachi?
Vipi ukilingishiwa,
Kinywani kupitishiwa
Ulimini kuonyeshwa
Kisha likaondolewa?
Langu mie si zabibu
Nasema bila aibu
Ndizi iso mahasibu
Sebenzwayo taratibu
Lako katu sitamani
Hata kwa kisu shingoni
Tunda hilo la ugoni
Halifiki kisogoni
__________________
Lester Brown...wtf!!!
10th March 2009, 06:05 AM
Ogah
is Omnipotent
JF Premium Member
Join Date: Fri Mar 2006
Posts: 3,374
Thanks: 1,363
Thanked 375 Times in 206 Posts
Rep Power:
2031
Re: Zabibu!
kwi kwi kwi kwi kwi............JF is soooo funny.... I Love JF wallah
10th March 2009, 09:36 AM
Mundu
is fighting for survival
JF Senior Expert Member
Join Date: Fri Sep 2008
Posts: 444
Thanks: 35
Thanked 114 Times in 72 Posts
Rep Power:
22
Re: Zabibu!
jamani tunda nanasi
kula uwe na nafasi
unapojaa ukwasi
hautajifaidia
kwa chakula cha mchana
mezani kimejazana
juisi yake mwanana
hakika utasifia
nanasi liwe shinani
wachuma kiulaini
hakuna purukushani
mkononi wachukua
Embe dodo kule juu
hadi lidondoke puu!
kweli kwa mtaji huu
hupaswi kulisifia
jamani hizo zabibu
hasa alolima babu
sana sana kwa ulabu
kama wataka kulewa
nakukaribisha kwangu
leo maulidi yangu
ule nanasi mwanangu
ni tamu tena murua
10th March 2009, 03:48 PM
Suki
is lickin' the lackin' luck...
Senior Member
Join Date: Tue Nov 2007
Posts: 218
Thanks: 0
Thanked 20 Times in 13 Posts
Rep Power:
23
Re: Zabibu!
Haiba yake machoni
Furaha tele moyoni
Toka ganda hadi ndani
Livutie utamani
Hizo ndogo mdomoni
Zaishilia kooni
Hilo nalo na shinani
Sitamani muwashani
Langu laja kwa mafungu
Uchaguzi ni wa kwangu
Nabeba wote mkungu
Hadi kunako uvungu
Sijali zielemee
Siziachi zilegee
Watu,ndege hata mee
Siwachi wakodolee
...kimya kimya...
__________________
Lester Brown...wtf!!!
Last edited by Suki; 10th March 2009 at 04:21 PM ..
10th March 2009, 04:22 PM
Mzee Mwanakijiji
anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,334
Thanks: 8,121
Thanked 4,393 Times in 1,232 Posts
Rep Power:
44
Re: Zabibu!
Quote:
Haiba yake machoni
Furaha tele moyoni
Toka ganda hadi ndani
Livutie utamani
Hizo ndogo mdomoni
Zaishilia kooni
Hilo nalo na shinani
Sitamani muwashani
Langu laja kwa mafungu
Uchaguzi ni wa kwangu
Nabeba wote mkungu
Hadi kunako uvungu
Sijali zielemee
Siziachi zilegee
Watu,ndege hata mee
Siwachi wasodolee
...kimya kimya...
Wewe kula hizo ndizi,
Wengine wala andazi,
Hata ule tangawizi,
Zabibu tunda la kazi!
Hadi umenye maganda,
yale yalogandaganda,
Ndiyo ule lako tunda,
Hilo unalolipenda.
Uzuri wake zabibu,
Kula kwake siyo tabu,
Mdomoni taratibu,
Nafyonza kama tabibu.
Ndizi ina ukakasi,
Ulimini kama pasi,
Zabibu ladha halisi,
Mwenyewe najinafasi!
Mundu kasema nanasi,
Kwangu halina nafasi,
Zabibu siwezi asi,
Nisije jipa mkosi!
Zabibu ninalo hamu,
Mengine siyo matamu,
Nitalila kitaalamu,
Kama nilivyo mwalimu!
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
10th March 2009, 04:53 PM
Balantanda
Arsenal damu
JF Senior Expert Member
Join Date: Sun Jul 2008
Location: Kusadikika
Posts: 2,467
Thanks: 744
Thanked 1,083 Times in 624 Posts
Rep Power:
27
Re: Zabibu!
Quote:
jamani tunda nanasi
kula uwe na nafasi
unapojaa ukwasi
hautajifaidia
kwa chakula cha mchana
mezani kimejazana
juisi yake mwanana
hakika utasifia
nanasi liwe shinani
wachuma kiulaini
hakuna purukushani
mkononi wachukua
Embe dodo kule juu
hadi lidondoke puu!
kweli kwa mtaji huu
hupaswi kulisifia
jamani hizo zabibu
hasa alolima babu
sana sana kwa ulabu
kama wataka kulewa
nakukaribisha kwangu
leo maulidi yangu
ule nanasi mwanangu
ni tamu tena murua
Taja matunda yako yote
Yapatikanayo kotekote
Nanasi na mengine yote
Dodo tamu kuliko yote
Nanasi lina ukakasi
Kulila lataka nafasi
Nikila nina wasiwasi
Meno kupata ukakasi
Embe dodo nalipenda
Siliachi hata ukiponda
Mjini kijijini ukienda
Watu wengi walipenda
Hakika Dodo namba wani
Kuliko hata dafu la Pwani
Ukija kwangu ewe mgeni
Dodo daima lipo mezani.
Litaendelea……
__________________
Amantium irae amoris integratio est
10th March 2009, 04:54 PM
Suki
is lickin' the lackin' luck...
Senior Member
Join Date: Tue Nov 2007
Posts: 218
Thanks: 0
Thanked 20 Times in 13 Posts
Rep Power:
23
Re: Zabibu!
Quote:
Wewe kula hizo ndizi,
Wengine wala andazi,
Hata ule tangawizi,
Zabibu tunda la kazi!
Hadi umenye maganda,
yale yalogandaganda,
Ndiyo ule lako tunda,
Hilo unalolipenda.
Uzuri wake zabibu,
Kula kwake siyo tabu,
Mdomoni taratibu,
Nafyonza kama tabibu.
Ndizi ina ukakasi,
Ulimini kama pasi,
Zabibu ladha halisi,
Mwenyewe najinafasi!
Mundu kasema nanasi,
Kwangu halina nafasi,
Zabibu siwezi asi,
Nisije jipa mkosi!
Zabibu ninalo hamu,
Mengine siyo matamu,
Nitalila kitaalamu,
Kama nilivyo mwalimu!
Njoo uje huku kwa energy needs bana.
Tusiishie tunda tunda...huku mabazazi wanakata mti.
__________________
Lester Brown...wtf!!!
Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
Thread Tools
Display Modes
Linear Mode
Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts
HTML code is Off
Similar Threads
Thread
Thread Starter
Forum
Replies
Last Post
Vitabu vitakatifu vimezuia POMBE?
Maxence Melo
Habari na Hoja mchanganyiko
240
21st January 2010 07:23 AM
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako !
All times are GMT +3. The time now is 02:10 AM .
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com