| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 1101
|
||||||||||||
|
#2
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Mzee mwanakijiji,
Usichoke kujihoji, Ahidi tanipa taji, Jibu nikikupatia. Ndege asotuliaga, Nirahisi kumtega, Na kisha ukamfuga, Kibandani kutulia. Hutegwa kwa tundu bovu, Wala si kwa ndizimbivu, Fanya kama mpumbavu, Mkononi tamtia. Exaud J. Makyao |
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Hategeki kwa urimbo, Wala kipande cha bati
Huyu mtungie wimbo, atalala katikati Tena usitie fumbo, la mti wa katikati Ndege asiyetulia, hutulizwa kwa gitaa! Ni wimbo namna gani, wauliza asilani Si wa lugha ya kigeni, aya zake teni teni Muimbishe kinyumbani, ataingia kimyani Ndenge asiyetulia, hutulizwa kwa gitaa! Matejoo wa Kwetu |
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Huyo ni ndege mjanja, hunaswa na tundu bovu,
Kama walivyo wajanja, hukwama mali pabovu, Hutegeshwa kwa ujanja, si kwa mbinu mbovumbovu. Ndege asiye tulia, hunaswa na tundu bovu. Na tundu bovu hunaswa, ndege asiye tulia Umakini haswa haswa, na akili lo tulia, Na ujipange ki haswa, ndipo atapotulia, Ndege asiyetulia, hunaswa na tundu bovu. Kwa ndani ya tundu bovu, ulipakae ulimbo, Lonekane bovu bovu, na sio lenye urembo, Lisijulishe ni bovu, na kumbe ni limtambo, Ndege asiyetulia, hunaswa na tundu bovu. Wewe tulia kwa mbali, watajileta mwenyewe, Wa aina mbalimbali, watasogea wenyewe, Na kutokea kwa mbali, utamuona mwenyewe, Ndege asiye tulia, hunaswa na tundu bovu. Tamati nimefikia, hapa ninamalizia, Mtegoni kafikia, ndege kajimalizia, Mwanakijiji sikia, usije jimalizia, Ndege asiye tulia, hunaswa na tundu bovu. By Pasco |
|
#5
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Kandege!.gif |
|
#6
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Mzee mwanakijiji,
Hoja uliianika, Kwa moyo ukatuhoji, Msaada ukitaka, NDEGE AMESHATEGEKA? Ndege ulimuhitaji, Kutulia hakutaka, Hukujua utegaji, Ushauri ukataka, NDEGE AMESHATEGEKA? MATEJOO msomaji, Alijibu kwa hakika, Kisha PASCO mtungaji, Pembeni hakujiweka, NDEGE AMESHATEGEKA? SURA yule mchoraji, Picha akaibandika, MAKIYAO msemaji, Sikuacha kuandika, NDEGE AMESHATEGEKA? |
|
#7
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Ndege niliyemtaka
Huyo ameshanasika Mtego nilioweka, Mwenyewe kajitundika! Ndege nikamtambua Si kwale wala si hua Ni tetere nikajua Hamu ikanizingua! Kisu kikalamba shingo, Nikamweka kwenye ungo Kanyonyolewa kwa mpango, Huku nikiweza tungo. Ndipo nikamuandaa, Na macho nimeyatoaa Mate nikidururizaa Na tumbo likingurumaa! Ndipo nikambanika Limao nimemfunika Na chumvi ya kutosheka Ndege wangu kaungika! Nikamla! Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" |
|
#8
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Furaha imenijia,
Mwanakijiji sikia, Ndege uliyelilia, Mkononi kumtia. Mbona huja tukumbuka, Meza ulipoandika, Walau tuje kucheka, Huku tukiserebuka? E. J. M |
|
#9
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Mtanionea gele,
Na mate yatoke tele Kwa huyo wangu tetere Mwisho mnizidi mbele!
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" |
|
#10
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Wala hatungekuonea gele,wako tetere ukila
Kwani tungekupigia vigelegele,muda huo ukimla Wala hisingekua kelele, wakti wa kulala Hongera mwanakijiji, kwa kumnasa huyo tetere
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 11:02 AM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||