Jana kuna MwanaJF alianzisha thread akilalamika kuwa mbunge wake wa Arumeru Mashariki ni mgonjwa sana na hivyo hawana mwakilishi jimboni kwao. Alitaka kujua serikali inaonaje kama Wana-Arumeru wakifanya uchaguzi mwingine ili wapate muwakilishi mwingine. Kwenye ile thread wapo waliosema kuwa “wakati mwingine tuweke utu mbele, thamani ya mtu ni utu, ubinaadamu ndio unatangulia na mengine yote yanafuatia..” Wengine wakasema kuwa “suala sio kubeza ugonjwa wa mbunge bali ni uwakilishi wa wanajimbo la Arumeru Mashariki full stop.”
Pia jana hiyo hiyo, Faiza Foxy alipewa ban ya miaka miwili kwa kwa kutenda “kosa dhidi ya UTU” ikiwa na maana ya “Kukejeli na kubeza marehemu na sababu zilizopelekea kifo chake ni kosa tena kukosa Heshima.”
Swali langu ni nini hasa maana ya utu? Ni utu kuendelea kumwacha madarakani kiongozi ambaye ni mgongwa sana to the extent kuwa hawezi hata kuwawakilisha tena waliomchagua? Je, mtu unaweza kula ban hapa JF kwa kutokuwa na utu? Ni vigezo gani tunavyotumia kujua kama mtu hana utu au amefanya jambo ambalo halina utu?
Nim-quote Gaijin: “Utu ndio kitu gani? Utu unau define vipi? Kwa standards za nani? Tunaweza kusemaje nani ana utu zaidi kuliko mwingine kwa kufanya vitendo gani?”
“Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.
Nadhani ni vigumu kusema sheria kazi yake kulinda utu iwapo hatuwezi hata kuueleza utu ni nini. Kwa sababu tunaposhindwa kufasiri utu basi na sheria lazima itashindwa kuulinda
Chukua kesi ya FaizaFoxy kwa mfano; alichokifanya si makosa kisheria licha ya kuwa ameonekana kukosa utu.
Ukiangalia kwenye bandiko langu la kwanza hapo juu nimejaribu tu kidogo kutoa mtazamo wa "utu" wetu ni kitu gani....
Utu unaweza ukaandikwa kwenye katiba (kwa maana jamii yetu inatafsiri vipi utu na inaweka mambo gani kama kigezo cha utu) lakini zaidi msingi wake ni katika "utashi" wetu wa kibinadamu, kwa yale ambayo tutayatafsiri kama "utu" au "kukosa utu"
Zaidi ya yote kwa ufahamu wangu mdogo wa basic law, sheria zipo (plus sheria mama yaani katiba) ili kuhakikisha utu wa mtu unazingatiwa katika uendeshaji wa shughuli za binadamu, either by state machinery au kati ya watu wenyewe kwa wenyewe. Inasaidia kutoa tafsiri ya ni wapi mtu kavunjiwa utu wake na ni nini remedy (kwa aliyevunjiwa utu) na punishment (kwa alievunja utu). Kwa mfano anagalia sheria zote unazozifahamu kuanzia biashara, mikataba, ardhi, jinsia au ndoa n.k utagundua zinachokusudia ni kuweka usawa na kuhakikisha kila mtu anastahili kile anachostahili (kwa tafsiri ile niliyotoa kwenye bandiko langu la kwaza).....Tatizo ni wale waliokabidhiwa jukumu la utungaji na utekelezaji wake kuna mahali wanaharibu.
Hili ndilo MLK Jr anasema "Law and order exist for the purpose of establishing justice and when they fail in this purpose they become the dangerously structured dams that block the flow of social progress"
All in all, cha msingi na cha kuelewa ni kuwa "Utu" sio lazima uwe kwenye maandishi kwa kile kinachoitwa "sheria" au "katiba", utu lazima uwe kwenye MOYO na UTASHI wa mwanadamu kwani hata kama utakuwa uko kwenye maandishi na hauko kwenye MIOYO na UTASHI wa watu, bado hauwezi kuonekana kwenye JAMII husika........DIGNITY IS A HUMAN "EMBLEM", a totality of our vibrancy as human race
Last edited by Cathode Rays; 15th November 2011 at 12:12.
Hizo taratibu zimezingatia utu kwa mujibu wa nani? Kwangu mimi kwa mfano utu wangu ningeona nimpe mwaka mmoja kama hajapona uchaguzi ufanyike achaguliwe mwengine; wakati taratibu zimekuwa labda niseme na utu mwingi kuliko mie na kutoweka kikomo cha muda wa ugonjwa unaokubalika kisheria.
Hapa ndipo tunapokabiliana na uwanja mpana wa tafsiri kulingana na matukio na nani mwenye ku-impose tafsiri ya utu kwenye tukio husika
Kwenye blue, mkuu dont complicate issues, utu ni kwa mujibu wa sisi binadamu kwa yale tuanayoyafanya na tunayofanyiwa na yakakubalika na jamii, utu ni nature huitaji kuwa na source mkuu, ninapo umwa kwa hali ya kawaida nategemewa kupona, hivyo kuna grace period ya kusubiria au daktari athibitishe vinginevyo kuwa huwezi tena kuendelea na position hiyo, sasa ukiumwa malaria kesho na mwingine anaweza kuja na hoja kama zako akaona wewe kuumwa wiki moja ni nyingi na akataka uchaguzi uitishwe kama wewe ulivoona mwaka ni mwingi.
Issue hapa sio muda tu, muda ni debatable nakubali lakini utu hapa ni kutambua chances yake ya ku recover, na mleta mada kiukweli aliileta kishabiki zaidi ndio maana zikaja tuhuma za utu.
Niuzungumzie “utu” kama ambavyo wenzetu wanauita “dignity”
Mkuu nimeipenda post yako yote but I am interested hapo ulipo-translate utu kama "dignity". Hapo nyumba Mkuu Paulss ali-translate utu kama "humanity" Sasa ili ku-clear any doubt, which is which? Au "dignity" na "humanity" is the same thing?
“Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.
Mkuu nimeipenda post yako yote but I am interested hapo ulipo-translate utu kama "dignity". Hapo nyumba Mkuu Paulss ali-translate utu kama "humanity" Sasa ili ku-clear any doubt, which is which? Au "dignity" na "humanity" is the same thing?
Teh teh teeeh
Yaani wewe umekaapembeni unatupambanisha tu mkuu,
Lakini natumai umepata mwanga utu ni nini
Mkuu Gaijin, naomba nisikujibu moja kwa moja ila niulize swali ili litujengee uelewa mpana zaidi
Kwa nini sheria zipo? Je si ili kulinda "utu" wa wananchi/wanajamii wa nchi/jamii husika?
hebu tusaidiane mtazamo hapo kwanza ndiyo tuone tunachukua njia gani katika kuamini hili
At the same time, kuna watu kama Kant on "Morality and Dignity" ana-define kazi kubwa ya morality kama ku-foster dignity. Kama "dignity" ni utu kama ulivyo-translate, does it also mean that morality inasaidia kulinda utu? Najua Gaijin ataniuliza na morality ni nini? lol.
“Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.
At the same time, kuna watu kama Kant on "Morality and Dignity" ana-define kazi kubwa ya morality kama ku-foster dignity. Kama "dignity" ni utu kama ulivyo-translate, does it also mean that morality inasaidia kulinda utu? Najua Gaijin ataniuliza na morality ni nini? lol.
You got that one right......who defines morals? lolz
Ibara ya 9 ya Katiba juu ya kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inasema kuwa "....Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha- (a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;.." Kwa hiyo utu unaweza ukawa ni haki?
Pia ibara ya 12 (2) inachohusu usawa wa binadamu inasema "Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake." Hakuna definition ya utu kwenye hicho kkifungu na katiba nzima
Lakini Ibara ya 25(1) iinaelezea wajibu wa kushiriki kazini kwa kusema "Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu." Kwa hiyo wajibu wa kushiriki kazini ni kipimo cha utu? Kwa maana wale ambao hawatimizi huo wajibu hawana utu au kama hushirikishwi kazi then utakuwa unanyimwa wajibu wako?
“Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.
Mkuu nimeipenda post yako yote but I am interested hapo ulipo-translate utu kama "dignity". Hapo nyumba Mkuu Paulss ali-translate utu kama "humanity" Sasa ili ku-clear any doubt, which is which? Au "dignity" na "humanity" is the same thing?
Mkuu naamini na Paulss hatujatofautiana ila ku-supplement kujazia vema....sijui ni mapungufu ya maneno kwa lugha yangu au la ndiyo maana nilipenda kuleta upande wa pili wa neno la kingereza linalotumika kama "utu" hapa kwetu
Ila ukisoma definition niliyotumia ya Mette Lebech inatumia maneno yote mawili, naomba niirudie hapa
Mette Lebech anaesema Dignity is the quality of worth (status/values) and honour (respect) intrinsic to every person which establishes the basic boundaries of humanity
Kwa hiyo ili kwenda kwa undani naomba nikupe tafsiri mbili mbili kutoka kwa watu wengine wanavyotafsiri haya maneno mawili then utapata mwanga wa kuelewa kwa undani
Humanity NIkimsoma Simon Rees kwa undani ananiambia kuwa humanity ina-describe abilities and characteristics of human beings in whole which defines our civil rights and social causes - yaani akiwa na maana ya how one is to be treated by or to treat others
Kwa tafsiri hii naweza kusema kuwa humanity, in its totallity, are those chemistry which makes us "humans"
Kwa upande wa Dignity
Dignity:
Social Care Institute for Excellence wanasema Dignity is a state, quality or manner worthy of esteem or respect; and (by extension) self respect……….. it is a kind of system or setting which supports and promotes, and does not undermine a person's self respect regardless of any difference.
Royal College of Nursing wanasema Dignity is concerned with how people feel, think and behave/act in relation to the worth or value of themselves and others. To treat someone with dignity is to treat them as being of worth, in a way that is respectful of them as individuals
Labda itasaidia kutupa mwongozo wa kuchanganua haya maneno mawili
But in my personal opinion naweza kusema kuwa Humanity has to do with "our whole being" and Dignity has to do with "how that whole being is treated by your own self or others"........ i stand to be corrected
Ibara ya 9 ya Katiba juu ya kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inasema kuwa "....Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha- (a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;.." Kwa hiyo utu unaweza ukawa ni haki?
Absolutely mkuu, hili halina ubishi....tena sio tu kuwa ni haki, bali ndilo linalopaswa kuwa mstari wa mbele......if not for that, everyone will treat you they way he/she want
Pia ibara ya 12 (2) inachohusu usawa wa binadamu inasema "Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake." Hakuna definition ya utu kwenye hicho kkifungu na katiba nzima
Hahaaa,hapo sasa........... hope wapitia Katiba watakuwa wamekupata vema hapa na watalichukua kwa umaanani
Lakini Ibara ya 25(1) iinaelezea wajibu wa kushiriki kazini kwa kusema "Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu." Kwa hiyo wajibu wa kushiriki kazini ni kipimo cha utu? Kwa maana wale ambao hawatimizi huo wajibu hawana utu au kama hushirikishwi kazi then utakuwa unanyimwa wajibu wako?
Mkuu kazi ndiyo heshima, ndiyo thamani ya utu wako japo katika definition ya utu tunasema mtu habaguliwi kwa msingi wowote (hata kama hana kazi) but if we are back in relality, (KA MFANO RAHISI TU) HUNA KAZI, HUNA KIPATO THEN HUNA FEDHA YA KUNUNUA NGUO NA UTATEMBEA HUKO BARABARANI KALIO WAZI....Umedhalilisha ule utu wako
Ibara ya 9 ya Katiba juu ya kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inasema kuwa "....Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha- (a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;.." Kwa hiyo utu unaweza ukawa ni haki?
Kwa mujibu wa katiba, haki na utu kwa pamoja zinahitaji kulindwa na dola na sio utu pekee
By EMT
Pia ibara ya 12 (2) inachohusu usawa wa binadamu inasema "Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake." Hakuna definition ya utu kwenye hicho kkifungu na katiba nzima
Lakini Ibara ya 25(1) iinaelezea wajibu wa kushiriki kazini kwa kusema "Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu." Kwa hiyo wajibu wa kushiriki kazini ni kipimo cha utu? Kwa maana wale ambao hawatimizi huo wajibu hawana utu au kama hushirikishwi kazi then utakuwa unanyimwa wajibu wako?
Kwa hiyo ukitaka kumtizama mtu ana utu kiasi gani utizame anafanya kazi kiasi gani? lol
Sheria inayozuwia ndoa za watu wa jinsia moja inalinda utu wa nani? ....
Wewe. Usitake hii thread ifungwe kwa mara ya pili. lolz
"Naye Katibu wa Baraza la Maaskofu nchini (TEC), Padri Antony Makunde, alisema "....Uingereza wasitumie umaskini wa Waafrika kulazimisha suala hilo. Wakitaka kutupa msaada watupe, lakini si kwa masharti hayo ya kuunyanyasa utu wetu wa Afrika ili tukubaliane na utamaduni wao.” Alisema ni heri Waafrika wakaendelea kuwa maskini na kulinda utu na heshima waliyonayo lakini si kutaka kudhalilishwa kwa ajili ya misaada iliyojaa laana ya ushoga na usagaji.
Mwingine anasema: “Inaonekana kama vile Uingereza na nchi nyingine tajiri bado zinaamini kwamba nchi za Kiafrika ni nchi zinazoongozwa na watu ambao uroho na tamaa yao ya misaada vinaweza kuwafanya wakubali lolote lile hata likiwa baya kwa mila, desturi, imani, utamaduni na utu wa watu wao……Umaskini hauimanishi maskini kukubali kuuza roho, utu na imani yake kwa ajili ya kupewa misaada.”
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Dk. Kitima, "..ushoga ni vitendo vya uovu na ukinuiwa na Serikali ni kuwaudhi wananchi wake, na kwamba kauli ya Waziri Cameron wa Uingereza ni sawa na kauli ya kutaka kuua utu wa watu…. Ushoga unaharibu utu wa mtu. Kukubali ushoga ni sawa na kuua vizazi vijavyo…”
Pia Bakwata imeahidi kuendelea kuunga mkono Serikali kwa misimamo yake ya kukataa kusaidiwa kwa masharti yasiyojali wala kuheshimu utu na thamani ya Mtanzania, kwa sababu ina lengo zuri la kuutetea utaifa.
Akizungumza katika Baraza la Idd el Hajj katika Msikiti wa Masjid Al Farouq, Kinondoni, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema, heri kuwa tayari kufa kwa njaa kutokana na umasikini, kuliko kupewa misaada ya maendeleo kwa masharti ya kudhalilishwa utu.
Ukisoma huko kwenye red inalinda kutonyanyasika kwa "utu wetu wa Afrika", kutokuuliwa au kutoharibiwa kwa utu wa watu, kuheshimu utu, kutokudhalilishwa, nk. Do the above shed some lights? lol. kazi ipo.
“Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.
Ukisoma huko kwenye red inalinda kutonyanyasika kwa "utu wetu wa Afrika", kutokuuliwa au kutoharibiwa kwa utu wa watu, kuheshimu utu, kutokudhalilishwa, nk. Do the above shed some lights? lol. kazi ipo.
EMT Pal thank you for this Insightful and USEFUL thread na kunishtua pia… It has Great Discussions in it.
Nimesoma Commets za humu ndani of which most are really really IMPRESSIVE!! Nimependa the fact kua as much as woote mmeongelea the same thing “Utu” imefanya kila mmoja aelezee toka angle yake… which kind of makes it really really interesting and Entertaining to an interested Mind. And prove as a fact kua “Utu” is a broad term, which must be understood from the context of what one is defining and from which community/society drawn.
The definition of “Utu” I would say differs from Society to Society… Sometimes it would even from members of the same society for it is such a conceptual term. Mara nyingi Utu unazungumziwa in the same lines as “Ubinadamu” na ubinadam consist of the facts and acts considered as humane in ones eye or society Or oneself…..
Kwa kutolea Mfano ambao upo so Valid na una many Schools of thoughts and various debates…. Ni hili suala zima la Ushoga. Hawa Westerners miaka sio Mingi saana hapo nyuma a gay person was considered as kutokua na “Utu” dhidi yake mwenyewe na jamii kwa kuenda kinyume cha Maumbile wakati wa faragha (kuenda nyuma ya maumbile is another discussion/debate pia as in what determines kua ni nyuma ya Maumbile) BUT tunaona with time the situation has evolved sasa hivi mpaka wanatetewa by all means kua they have the right to be gay na ni kwamba it is acceptable and has to be acceptable!
Where as tunaona jamii yetu ya hapa Tanzania ilivomaka kuhusiana na suala zima la Ushoga… Alternatively known as u-Cameroon sasa. Inaonekana kabisa hicho kitendo sio “utu” na hao watu kama wamelaniwa vile.
Hivo basi I would say “Utu” lies in the lines of defining what is right and what is wrong in close relation with what is considered as one’s right in a certain or particular context as subjected with one(s) around...
You got that one right......who defines morals? lolz
What is your thoughts on "Might makes right"?
Nafikiri tuna-define morality kulingana na experiences and beliefs zetu. Hizo experiences na beliefs zinakuwa shaped au influenced na jamii tunayoishi, our religious and/or spiritual path, nk. Lakini at the end of the day, we all define our own morals. Of course, wapo watakaosema kuwa Mungu/Allah ndiye anaye-define morality, lakini this may ignore the fact that those who argue such have chosen their own faith and therefore have chosen to accept God's definition of what is moral.
But kama kuna mgongano kati ya morals za watu wawili, who gets to decide who "wins"? If, by adhering to your moral code, you violate someone else's right to live their life as they see fit, have you overstepped your bounds?
“Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.
Gaijin
Utu wa binadamu, kuwa its against the nature Kumbuka si kila sheria inalinda utu na si kila utu unatamkwa na sheria
Well said mkuu....tumeshakuwa hadi na sheria za kunyonga (which i declare it is against humanity) mpaka ilipofika mahali kelele za watu kupigania "utu"/"ubindamu na haki ya binadamu kuishi, ndipo inafahamika kuwa ni kosa na sheria hizo sasa zinafutwa
Nimependa pale uliposema utu hauna reference/source na ndiyo maana nikasema Utu "is human emblem", that totality of who we are na haya mengine kama sheria ni kupigania kuhakikisha hakuna mtu mwingine anaathiri utu wa mtu mwingine na pia mtu haathiri utu wake na ndiyo maana ukitaka kujinyonga leo utashtakiwa na Jamhuri (hahaaaa, hapa itakuwa ngumu "kumesa")
Nafikiri tuna-define morality kulingana na experiences and beliefs zetu. Hizo experiences na beliefs zinakuwa shaped au influenced na jamii tunayoishi, our religious and/or spiritual path, nk. Lakini at the end of the day, we all define our own morals. Of course, wapo watakaosema kuwa Mungu/Allah ndiye anaye-define morality, lakini this may ignore the fact that those who argue such have chosen their own faith and therefore have chosen to accept God's definition of what is moral.
But kama kuna mgongano kati ya morals za watu wawili, who gets to decide who "wins"? If, by adhering to your moral code, you violate someone else's right to live their life as they see fit, have you overstepped your bounds?
Kimsingi wenye nguvu ndio wanao define morals za jamii husika
Tukiangalia kwenye suala hilo la ushoga kwa mfano au suala la malezi ya watoto. Waafrika tunajinsi yetu ya kulea watoto, lakini Westerners kwa vile wana nguvu wanakuwa na haki ya kutufasiria morals za malez ni zipi na ndipo tunapoanza kubadili namna ya ulezi wetu.
Well said mkuu....tumeshakuwa hadi na sheria za kunyonga (which i declare it is against humanity) mpaka ilipofika mahali kelele za watu kupigania "utu"/"ubindamu na haki ya binadamu kuishi, ndipo inafahamika kuwa ni kosa na sheria hizo sasa zinafutwa
Kwa hiyo hapa mkuu unataka kusema zamani tulipotnga hizo sheria utu wetu ulikuwa chini, na sasa tumenyanyua viwango vya utu wetu na tumeamua kujirekebisha?
Before long tutasema tulipozuwia ndoa za jinsia moja ilikuwa ni kinyume na humanity kwa sabau wale pia wana haki ya kutambulika kisheria kama binaadamu wengine wanavyotambulika.
utu ni jambo liko binded na vitu mbali mbali katika jamii
jamii zina tamaduni zake na zinaweza kutofautiana . wagogo wana tofauti na wahehe
jamiii zina dini a nyingine hazina
Jamii zina miiko na madili
Hayo na mengine mengine ndio yana shape utu wa mtu kuwa defined na yanatofautiana
Mtikilia aliwahi kunukuliwa kuwa mzoga wa mwalimu nyerere uligharimu taifa pesa nyingi. Ni weli kitu kilichokufa kintwa mzoga lakini hapo inawezekana alikosa utu kwakuchagua hilo neno sio tu kwa nyerere bali binadamu yeyote.
Waafrika sehemu mbali mbali walikuwa na tamaduni kuwakeketa wanawake lakini waafrika hao hao tamaduni nyingi hazitambui ushoga na ndoa za jinsia moja. Lakini ukenda sweeden na ulaya bado ni utu kwa mwanaume kuwa shoga na si utu wa mwanamke kukeketwa.
Kuna dini zina miiko aina ya chakula. kwa hiyo kipimo cha utu kwa kigezo cha dini au imani inaweza kuonekana kwa mtu fulani hana utu n wingine akajiona haimundolei utu kwa kula mjusi, chura etc.
Kazi ipo kwenye kutafuta universal definition ya utu.
Follow Us Here