tuseme karibia watu wote wa Tz wanazungumza kiswahili , je ni sahihi kuwaita wote waswahili ? ama waswahili ni wale tu ambao wana asili ya mrima / mwambao ? naomba ufafanuzi ....
tuseme karibia watu wote wa Tz wanazungumza kiswahili , je ni sahihi kuwaita wote waswahili ? ama waswahili ni wale tu ambao wana asili ya mrima / mwambao ? naomba ufafanuzi ....
mswahili ni mtu mwenye asili ya uswahili....
lakini maana inabadilika kulingana na matumizi....
wakati mwingine maana yake ni mtu mweusi...
au mtu masikini
au mtu wa pwani ya africa mashariki
au mtu mbabaishaji
au mtu wa africa mashariki...n.k
Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!
Mswahili ni yule anaetumia maji kujisafishia baada ya kwenda haja kubwa.
Waswahili wanaishi sehemu za mwambao wa Afrika mashariki.Pia kiswahili ndio lugha yao ya uzawa.
waswahili ni watu wanaoishi pwani ya africa mashariki pamoja na visiwani... ni kweli nonda allivosema hapo juu waswahili wana ustaarabu wao pamoja na kutumia maji wanapomaliza haja kubwa! waswahili wakiongea kiswahili basi hutopenda amalize nenda kamsekilize muunguja an mdigo wa kule tanga pamoja na mombasa.. wanaongea lugha moja tamu sana ,... kuliko wale wa kutoka nyanda za juu "bara" wasukuma na wengineo ..
“Not only am I better looking….I’m just plain better.”Arsenal My heart Juventus My soul
Bwana Nonda!!
Nafikiri umetoa majibu mepesi.
Hebu fikiria haya maswali hapa chini yaliyotokana na majibu yako:
"mwambao wa pwani" ni eneo la umbali gani kutoka baharini? 2km, 10km, 200km, 1000km? Je waluguru (about 200km from indian ocean) ni waswahili iwapo wanatumia maji baada ya kwenda haja kubwa?
Je nikiwa nimehamia na wazazi wangu kutoka Lubumbashi zaire, na sasa tunaishi Mwananyamala na tunatumia maji kutawaza, tunaongea kiswahili vizuri lakini bado tunaongea na kilingala chetu, je sisi ni waswahilli?
Je nikiwa mhamiaji kutoka Pakistani au Misri na ninaishi Mombasa au Lamu, na nitawaza kwa maji na ninaongea na kuandika na kusoma kiswahili vizuri, je mimi mimi ni mswahili?
Ndugu Nanren.
Uswahili ni kama kabila.
Wenye uasili wa uswahili ni kama nilivyoeleza.(wengi ni kizazi cha mchanganyiko wa makabila na races tofauti)
Kuna "gray areas" kama ulizozitaja au ulizoziuliza.
Katika makabila mengi, mtu wa nje ya kabila huweza kukubalika kuwa ni mmoja wao kwa kupata,kufanyiwa "initiation", kufinyangwa, kubatizwa au "naturalisation".
Kama mtu akitimiza vigezo hivyo vya kuwa mswahili na wenyewe waswahili wa asili wakimkubali basi atakuwa ni mmoja wao.
Nakumbuka zamani kulikuwa na mwalimu, mzungu , UDSM, aliandika vitabu, alijiita "baba malaika". Alioa mtanzania na alipata watoto..lakini baba malaika anajinadi kuwa ni mtanzania.
Watoto wa Dr. Remmy ni kabila gani? je ni watanzania?
Natumai nimeongeza ugumu wa kumtambua nani mswahili!
Ni kweli umeongeza ugumu.
Katika kuishi kwangu na kutembelea pwani ya tanzania bara, mimi sijawahi kukutana na mtu anayejitambulisha kabila kama "mswahili". Nimekutana na wazaramo, wakwere, wang'indo, makonde, wazigua, wabondei, wakutu, wadigo. Hata watu ambao kwa muonekano wanaonekana kuwa ni mchanganyiko wa mweusi na watu wa asia, bado wanajitambulisha kwa makabila mengine, na aghalabu kuna wanaojinadi kuwa ni wangazija, waarabu, nk. Waswahili kwa kabila sijawahi kukutana nao.
Na tukirudi kwenye kigezo cha umwambao, hivi mtu mwenye asili ya mwambao akihamia Tabora na kuendelea kuishi huko, "uswahili" wake unapotea?
Nafikiri kuna haja ya kuki-define "kiswahili" kwanza. Mtazamo wa watu wengi wa mwambao, ni kuwa hiyo ni lugha na fahari yao. Hii haina ubaya. Ila nafikiri, in their subconscious mind, wanajaribu kuihodhi na kuifanya yao exclusively, na kuona kwamba watu makabila mengine hayana chao katika kiswahili (kumbuka kuna over 50% kibantu). Mimi naona tukubali historia kuwa kiswahili ASILI YAKE ni MWAMBAO wa afrika Mashariki. Lakini haina maana kwa sasa kufikiri kuwa watu walioko mashariki ya DRC hawaongei kiswahili. Ni kiswahili tu, hata kama sio sawa na tunachokijua. Huwa kuna dialects na accent katika lugha zote. Ndio maana waingereza pamoja na kujua kuwa kiingereza kama lugha kimetokea kwao, bado wanatambua kuwa kiingereza cha Australia, India, America bado ni kiingereza tu.
Tukisha kubali kuwa kiswahili kama lugha haimilikiwi na watu, hapo tunaweza kujaribu ku-define mswahili ni nani.
duu! kama hutumii maji kuchambia nadhani mpododo wako utakuwa unanuka kimavi full time labda mpaka utakapooga! we unadhani kutumia toilet paper pekee ndo mpango mzima? toilet paper inatumika kupunguza' makali' ya mabaki ya mavi kwenye mpododo then ndo unamalizia na maji, au mkuu bado hujaona kwenye vyoo vya kisasa kunakuwa na pipe inatoa water jet kwa pressure kwa ajili ya kujiswafi kunako sehemu? pole sana kwa kutembea na mabaki ya kinyesi mpododoni kila siku, ushauri wa bure huo na kwa wengine ambao hawajastaarabika kama wewe, mwenyewe umeulamba uko zako down town kwenye michakaliko kumbe una chembechembe za kinyesi matakoni!
Ndugu Nanren,
Kwanza isome thread ilipoanzia.Mwanzisha thread ametaka kujuanani mswahili na asili yake.
Mswahili ni mtu wa mwambao wa Afrika mashariki ambaye lugha yake ya uzawa ni kiswahili.
Bila shaka kuna wazungumzaji wengi wa kiswahili lakini sio kila mzungumzaji wa kiswahili ni mswahili.
katika dhana ya kileo ya "duality", je mswahili pia anaweza kuwa mchaga? mmakonde? .Hili linazungumzika nadhani.
Hili la lahaja za kiswahili halina ubishi,lahaja zipo njingi.
Umeshasema mlingala anazungumza kilingala,kama kilingala kitaalamu,ikiisimu inakubalika ni lahaja ya kiswahili basi atakuwa ni mzungumzaji wa kiswahili lakini si mswahili.
Mswahili si lugha tu,ni utamaduni wake na vikorombwezo,vipambio vyengine.
Kikawaida "aliyemo hatoki na asiyekuwemo haingii" lakini wenyewe wakikubali kumuingiza na kumkubali kama mmoja wao nani hapo atakuwa na haki ya kupinga?
Waswahili wengi wanajaribu kukimbia kujiita waswahili kutoka na tafsiri potofu, mbaya inayonasibishwa na matumizi ya neno "mswahili".
Angalia post#2.
Last edited by Nonda; 16th May 2011 at 22:59.
Basi mimi najivunia sana kuwa Mswahili Kindaki ndaki.
“I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”
'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.
(¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)
Waswahili ni wabantu hususani wenyeji wa pwani ya Afrika mashariki na kaskazini mwa msumbiji,ni wenye kufanana utamaduni na hutumia kiswahili kama lugha mama.na ukitazama neno swahili ambalo kwa upeo wangu naamini ndio limezaa waswahili,na neno swahili asili yake ni neno la kiaarabu 'sawahil' likiwa na maana wenyeji wa pwani.na kadiri kiswahili kinavyozidi kupanuka na waswahili nao wanaongezeka.
Na pia ipo ingawa sio rasmi wakati mwingine ipo hali inayo pelekea mtu kuitwa mswahili,ukiwa ni mtu wa kila utakachoambiwa basi wewe lazima ulete nahau kugeuzageuza maneno ndio ukubali utaitwa mswahili, au ukiambiwa njoo saa nne unakuja saa tano unaitwa mswahili.
Bwana Nonda. Nakushukuru kwa majibu.
Next, ningependa tusaidiane, maana ya PWANI. Ni umbali gani kutoka baharini? Hivi ukichukua kisiwa kama Madagascar, kwa mfano, je chote kinakuwa ni sehemu ya pwani? au ni umbali kadhaa kutoka baharini? Na visiwa vya zanzibar? Ukiwa Zanzibar kwenye nchi kavu, unakuwa ndani ya pwani? au kunakuwa na kaeneo fulani kutoka baharini kanakoitwa pwani (within Zanzibar). Sitoki nje ya mada, nahitaji tu-define pwani maana yake nini, halafu tujue watu wa pwani ni watu gani, ili tuzidi kuelewa zaidi kuhusu mswahili.
Maana ya pwani. Bofya hapa Search Results for 'coast' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'coast' | The Kamusi Project
Coast - Wikipedia, the free encyclopedia
Kimasafa sina utaalamu nalo kuwa ukomo uwe kilomita ngapi kutoka makutano ya bahari na ardhi. Lakini kwa visiwa vidogo kimantiki yaweza kutumika ni eneo la pwani.
Lakini hapa tusichanganye mgawanyo wa kijografia na utawala,kama mkoa wa Pwani au mikoa ya pwani. Lililo hakika ni kuwa Ukerewe si pwani.Mafia, Zanzibar vina mwambao wa pwani.
Kwa hiyo watu wa pwani ni watu walio karibu na bahari.
Rafiki zao ni samaki wa maji chumvi.
Kisiwa kama UK au Madagascar vimezungukwa na bahari, zina mwambao lakini kwa ukubwa wake kuna bara na mwambao. Hata Australia imezungukwa na bahari..lakini linaitwa sub-continent lakini ina miambao katika pande zake zote. aka sehemu za pwani.
Ndugu Namren..mimi Nonda si mtaalamu wa lolote, JF ndio shule yangu.Ninajifunza mengi humu.
Natumai watajitokeza wataalamu wa jiografia na kutusaidia hili la masafa.
Swahili people - Wikipedia, the free encyclopedia
YouTube - Utamaduni wa mswahili
Waswahili ni wale wenye kulijua beni (au waweza ita mbwa kachoka ukipenda), kidumbak, kibao kata, taarab, sumsumia,
Wale wenye kula wali wa asumini, vipopoo, bokoboko, mbatata za urojo, kaimati,
Wale wenye kuujua kuutumia udi, halawa, liwa, singo,....
ebana weee....bora niishie hapa kwa sasa
Follow Us Here