Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Historia ya Noti ya Tanzania

    Report Post
    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 21 to 40 of 77
    1. #1
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,836
      Rep Power : 3272
      Likes Received
      1316
      Likes Given
      919

      Default Historia ya Noti ya Tanzania

      Wiki chache zilizopita niliwaletea historia ya fedha ya sarafu hapa nchini kwetu nikaahidi kumalizia na historia ya noti. Kwa bahati mbaya majukumu yamenizidi nikashindwa kupata nafasi ya kuiandika ingawa nilikuwa nimeshaifanyia utafiti wa kutosha. Leo hii nimeamua kulivalia njuga ili niikamilishe, samahani sana kwa wanachama kwa vile historia hii ni ndefu kidogo kuliko ile ya sarafu kwa vile noti zilipitia mabadiliko mengi sana kuliko sarafu.

      Kwa muda mrefu fedha zilizotumia katika nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatsi zilianza kutumiaka mwaka 1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo zilitolweka katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na sikufanikiwa kupata picha yake

      Rupie 5

      Rupie 10

      Rupie 50

      Rupie 100

      Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu niliyofanikiwa kupata.

      5 Zanzibari rupee




      Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake

      1 Rupie

      5 Rupien

      10 Rupien

      20 Rupien


      50 Rupien


      Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.



      Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa inaitwa "Tabora Pound."


      .....INAENDELEA
      Last edited by Kichuguu; 4th September 2007 at 02:32.
      Tuyuku, Mr. Teacher and mosagane like this.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    2. Miaka 50

    3. #21
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default

      Excellent piece of research Bravo Prof...

    4. #22
      Kakalende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 2,919
      Rep Power : 1230
      Likes Received
      384
      Likes Given
      376

      Default

      Mzee Kichuguu, chukua 5 shule nzito hiyo mkuu!

    5. #23
      Mwendapole Old's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th December 2006
      Posts : 655
      Rep Power : 769
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Hiyo noti ya bluu ya Tsha elfu kumi ya kipindi cha Mkapa ina matumaini ya kuishi...pengine ilikuwa na nguvu, au ni mvuto tu..

    6. #24
      Mpaka Kieleweke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2007
      Posts : 2,690
      Rep Power : 1172
      Likes Received
      692
      Likes Given
      7

      Default

      Nikupe Tano Mkuu.

      Nawezaje Kuziweka Kwenye E-mail Yangu.?

    7. #25
      Kasheshe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Location : Bububu
      Posts : 3,547
      Rep Power : 1331
      Likes Received
      165
      Likes Given
      279

      Default

      Du! haya nisemeje bwana, kichuguu, umesaidia kuweka mambo wazi yasijepotea, amini usiamini watasoma watu wengi kuhusu post hii, sasa na vizazi vijavyo!!!

      Hongera sana! These were our expectations when we decided to register with JF, "learning" and little of "mipasho" kind of words as, if we needed them then we could buy those udaku papers


    8. #26
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,523
      Rep Power : 46715
      Likes Received
      16439
      Likes Given
      8471

      Default

      Mwalimu, nimefurahia darasa! Hizo picha za mwisho za fweza yetu zimenikumbusha filamu ya "Coming to America" ambapo wanaonesha fedha za mwana wa Mfalme wa Zemunda! Ila zinapendeza hasa hiyo yenye picha ya Simba!!
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    9. #27
      The Invincible's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2006
      Location : Online
      Posts : 1,947
      Rep Power : 1058
      Likes Received
      170
      Likes Given
      0

      Default

      Asante mwalimu kwa somo hilo. Sifahamu utaratibu wa utunzaji wa posts zetu hapa ukumbini. Ila mimi napendekeza hii post itunzwe vizuri na iwe rahisi kuifikia wakati ujao...Hii ni kati ya historia adimu.
      Watanzania mbumbumbu wamemchagua raisi dhaifu ajenge taifa la watu wasiojiamini, 2010/2015 - Tafakari

    10. #28
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,523
      Rep Power : 46715
      Likes Received
      16439
      Likes Given
      8471

      Default

      Naomba ruhusa yako nijeiweka kwenye Pdf jinsi ilivyo... kama una la kuongezea ongezea.. by the end of the week nitajaribu kuanza kuiweka kwenye pdf na kuiwekea ripoti "Historia ya Fedha Yetu". Je unayo historia ya sarafu (coins)?
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    11. #29
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,670
      Rep Power : 21816
      Likes Received
      736
      Likes Given
      3195

      Default

      MKJJ

      Mbona historia ya sarafu Prof Kichuguu alishaiweka ngoja niitafute nikuwekee link........good suggestion!!

    12. #30
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,670
      Rep Power : 21816
      Likes Received
      736
      Likes Given
      3195

      Default

      MKJJ

      nafikiri link ni hi hapa chini ya kuhusu sarafu
      http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4756

      kila la kheri...tuwekee kumbukumbu

    13. #31
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,836
      Rep Power : 3272
      Likes Received
      1316
      Likes Given
      919

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Naomba ruhusa yako nijeiweka kwenye Pdf jinsi ilivyo... kama una la kuongezea ongezea.. by the end of the week nitajaribu kuanza kuiweka kwenye pdf na kuiwekea ripoti "Historia ya Fedha Yetu". Je unayo historia ya sarafu (coins)?
      MKJJ,

      Picha na posts zote hizi hazina copyright protection yoyote ingawa acknowldegement ya jamboforums itakuwa appreciated. Unaweza kuzitumia kwa njia yoyote bila kuhitaji ruhusa ya mtu yeyote yule.

      Nadhani kuna typos kadhaa kadhaa. Itakuwa vizuri kama utaweza kuidentify typos na kuniambia kusudi nizirekebisha kabla hujaweka kwenye PDF yako. Hii post ilikuwa ni extension ya historia ya sarafu ambayo nilipost wiki chache zilizopita kama alivyoonyesha Ogah. Nilikuwa motivated na efforts zinazoendelea kwa Afrika Mashariki kutumia sarafu moja.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    14. #32
      YournameisMINE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2007
      Location : Peramiho
      Posts : 3,794
      Rep Power : 1155
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default

      Kichuguu,
      Research yako ya kina ni ya kupendeza......suala hili la fedha ya nchi yetu /EA na historia yake ili kuwa preserved vizuri, appreciated na kufanya wengi waelewe.....inaweza kuwa researched further na labda kutafutiwa kaupenyo kwenye mtaala wa historia ktk shule zetu aidha msingi au sekondari. Mie kama mtu anayependa kujifunza ninge-enjoy na kuwa proud ku-score good grades kama topic hii ingefundishwa mashuleni!!!!!. Kichuguu hongera sana........hii si tu kwamba ni Fantastic research bali pia ni cocastic......two BIG thumbs up!!!.

    15. #33
      Brutus's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Rome
      Posts : 212
      Rep Power : 649
      Likes Received
      18
      Likes Given
      91

      Default

      Mkuu Kichuguu!
      Asante sana kwa kutupa somo la Historia
      Hizi sarafu za Olympic zilishawahi kutumika?
      Et tu, Brute?

    16. #34
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,836
      Rep Power : 3272
      Likes Received
      1316
      Likes Given
      919

      Default

      Quote By Brutus
      Mkuu Kichuguu!
      Asante sana kwa kutupa somo la Historia
      Hizi sarafu za Olympic zilishawahi kutumika?
      Zilitumika kwa muda mfupi sana. Ni wachache walioziona, na nadhani ziliishia pale Dar tu; mimi nilikuwa na bahati ya kuona mojawapo ya sarafu hizo.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    17. #35
      mvumilivu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st June 2007
      Posts : 75
      Rep Power : 625
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Tunashukuru kwa hili somo,na mimi nitajaribu kuiweka kwenye PDF file kama nikipata tatizo nitaomba msaada.

    18. #36
      Brutus's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Rome
      Posts : 212
      Rep Power : 649
      Likes Received
      18
      Likes Given
      91

      Default

      Waheshimiwa.. kama mtafanikiwa kuiweka kwenye pdf. basi tunaomba mtuwekee attachment hapa ili tuweze ku-download. Maana hii historia si mchezo!
      Et tu, Brute?

    19. #37
      Samvulachole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd October 2006
      Posts : 744
      Rep Power : 792
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default

      Naona Wazanzirabi Walisahauliwa Kabisa Kwenye Hizo Pesa

      Picha Ya Nyerere Imekuwa Ya Kudumu Lakini Maalim Abein Amani Karume Haimo Sasa Haya Ndiyo Mamabo Yanayopelekea Muungano Kuonekana Ni Wabara Tuuuu


      Nichukieni Sasa Kwa Kusema Hilo

    20. #38
      Steve Dii's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2007
      Location : Kihesa - Iringa
      Posts : 6,795
      Rep Power : 3279
      Likes Received
      924
      Likes Given
      2800

      Default

      Quote By samvulachole
      Naona Wazanzirabi Walisahauliwa Kabisa Kwenye Hizo Pesa

      Picha Ya Nyerere Imekuwa Ya Kudumu Lakini Maalim Abein Amani Karume Haimo Sasa Haya Ndiyo Mamabo Yanayopelekea Muungano Kuonekana Ni Wabara Tuuuu


      Nichukieni Sasa Kwa Kusema Hilo
      Mimi sito kuchukia kwa hili, nadhani ni hoja iliyo kamilika kabisa... ila ndiyo sina jibu la kukupatia. Ahsante.

      SteveD.



      Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi. SD1-09.

      Fikra ni nyenzo endelezi au potofu. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SD6-07Rev.2-09.



    21. #39
      Samvulachole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd October 2006
      Posts : 744
      Rep Power : 792
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By SteveD
      Mimi sito kuchukia kwa hili, nadhani ni hoja iliyo kamilika kabisa... ila ndiyo sina jibu la kukupatia. Ahsante.

      SteveD.

      KAMA PICHA YA NYERERE NI YA KUDUMU KWA NINI ISIWEPO NA YAKARUME?

      au KARUME HAKUWA RAIS?

    22. Dua
      #40
      Dua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2006
      Posts : 3,534
      Rep Power : 1365
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By samvulachole
      Naona Wazanzirabi Walisahauliwa Kabisa Kwenye Hizo Pesa

      Picha Ya Nyerere Imekuwa Ya Kudumu Lakini Maalim Abein Amani Karume Haimo Sasa Haya Ndiyo Mamabo Yanayopelekea Muungano Kuonekana Ni Wabara Tuuuu


      Nichukieni Sasa Kwa Kusema Hilo
      Karume hakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
      Dua la kuku halimpati mwewe

    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    Similar Topics

    1. Historia ya Tanzania: Dr Kleruu
      By GM in forum Jukwaa la Historia
      Replies: 179
      Last Post: 1st April 2013, 01:05
    2. Historia ya muziki wa Tanzania
      By ngalikikinakiki in forum Entertainment
      Replies: 1
      Last Post: 29th March 2011, 17:26
    3. Replies: 27
      Last Post: 17th December 2010, 18:10
    4. I noti nyingi za shilingi 1000 na 2000 za tanzania zina nini ?
      By MAHENDEKA in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 7
      Last Post: 28th November 2010, 10:58

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...