JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

  Report Post
  Results 1 to 11 of 11
  1. nngu007's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd August 2010
   Posts : 15,932
   Rep Power : 840916
   Likes Received
   5660
   Likes Given
   614

   Default Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza   MWAKA 1848, Mmishenari wa Kijerumani Dk Johan Ludwig Krapf, alitembelea kijiji cha Magila kilichopo Muheza mkoani Tanga akiwa katika safari zake za Afrika Mashariki.
   Magila kuna mlima ulio katika safu za milima ya Usambara ukipakana na mlima wa Magoroto ambao ndio chanzo cha maji ya mto Mkurumuzi unaoelekea Muheza.

   Historia inaonyesha eneo la mlima Magila wenye miamba na mawe mengi, zamani kabla ya kuja wageni lilitumika kuwatenga wagonjwa wa ukoma na magonjwa mengine yasiyotibika, kwa lengo la kuwazuia wasiwaambukize wengine.

   Dk Krapf alipofika na kuwaona wagonjwa hao waliokuwa wakiishi kwa madhila makubwa, alichonga msalaba katika mti wa mkuyu kwa imani kuwa Mwenyezi Mungu angewaponya wagonjwa hao.

   Eneo hilo ndilo lililokuja kujengwa shule ya kwanza na Waingereza mwaka 1886. Alama ya msalaba huo ipo hadi na sasa na ndipo ilipo Shule ya Sekondari Hegongo.

   Hadi leo mahali hapo panaitwa Magila Msalabani. Kwa sasa Magila ni kata yenye vijiji vya vya Magila, Mikwamba, Misongeni na Mafleta.

   Nilifika katika eneo hilo nilipokuwa wilayani Muheza hivi karibuni ili kuchunguza historia ya eneo hilo.

   Hapo nikutana na Luteni Kanali mstaafu John Mhina ambaye amekamilisha kuandika kitabu kuhusu historia ya Magila Msalabani, kinachoeleza historia ya kijiji hicho na ujio wa wazungu walioanzisha shule ya kwanza Tanganyika na kanisa.

   Luteni Kanali Mhina aliyelitumikia Taifa kwa muda mrefu kama mwanajeshi ,na baadaye kuwa Mbunge wa Muheza kutoka mwaka 1990 hadi 1995, anasema harakati za kuanzisha shule katika kijiji hicho zilitokana na Wamishenari waliokuja Afrika Mashariki kutoka Ulaya kwaajili ya kueneza dini ya kikristo tangu miaka ya 1770.

   Anawataja baadhi ya Wamishenari hao kuwa ni pamoja na David Livingstone, Charles Mackenzie, William Tozer na Edward Steer.

   Anasema harakati hizo zilianzia tangu visiwa vya Zanzibar mwaka 1863 ambako pia walikomesha biashara ya utumwa na kuanza ujenzi wa kanisa la Anglikana la Mkunazini Zanzibar kwa miaka 10 tangu mwaka 1873.

   Anasema wakati huo kulikuwa na shule iliyoanzishwa Zanzibar maeneo ya Kiungani na Kiinua mguu na Askofu William Tozer mwaka 1869. Hata hivyo, anasema shule hiyo haikuwa rasmi na ilikuwa ikifundisha elimu ya dini kwa watumwa waliokombolewa.


   Uamuzi wa kujenga shule Bara
   “Mnamo Agosti 13, 1967 Askofu Tozer alimtuma Padri CA Alington aende Vuga (Lushoto) kwa Chifu Kimweri ili apate kibali cha kujenga kituo cha misheni kwenye maeneo ya Bara,’’anasimulia Luteni Kanali Mhina na kuongeza:


   “ Padri Alington alimchukua Vincent Mkono aliyekuwa mwanafunzi wake wa Kiungani na mwingine Mwinyi Khatib aliyekuwa mkalimali. Msafara huo ulipata baraka za Sultan Majid aliyekuwa akitawala Zanzibar.”


   Anaeleza kuwa baada ya msafara wao kufika Vuga, Chifu Kimweri aliwasikiliza, lakini akaomba apewe muda wa kutafakari kwanza.


   Baadaye Januari 20, 1868, Padri Alington alirudi Vuga na kuruhusiwa na Chifu Kimweri kujenga sehemu yoyote katika maeneo ya Pwani.


   Anasema Padri Alington aliamua kuchagua eneo la Magila ambalo lilikwishajulikana kutokana na alama ya msalaba uliowekwa na Dk Krapf.


   “ Jumbe Kifungiwe aliyekuwa akiongoza Magila wakati huo chini ya baraza la ‘wamaka’ (Baraza la Wazee wa Kibondei), walimpa mlima wote wa Magila wakidhani kuwa atashindwa kujenga kwa sababu ya kuwa na mawe mengi….kwa mshangao aliporudi aliyatumia mawe hayo kujengea.” anaeleza.


   Anasema pamoja na kazi ya kueneza dini Wamishenari hao walijipa jukumu la kuwatunza wagonjwa wa ukoma na kuanzisha shule.


   “Shule ya sokoni ilikuwa kwanza kujengwa maeneo hayo mwezi Aprili 1869 chini ya Padri Fraser na wanafunzi wake walikuwa ni pamoja na Jumbe Kifungiwe na ndugu yake Sagosago na vijana wengine. Palikuwa na soko dogo na mti mkubwa wa Mzindanguuwe, watu wazima walipenda kukaa hapo ili walione jambo hilo geni,” anaongeza kusema.


   Sekondari ya Hegongo
   Hivi sasa eneo hilo kuna shule iitwayo Hegongo. Mkuu wa shule hiyo, Wilfred Mdimu anasisitiza kuwa eneo hilo ndipo palipojengwa shule ya kwanza Tanzania ambapo mpaka sasa kuna mabaki ya darasa la kwanza lililojengwa na Wamisheni.


   Hivi sasa anasema darasa hilo linatumiwa kama ofisi ya walimu wa shule ya sekondari ya kata Magila.


   “Hili ndilo darasa la kwanza lililojengwa mwaka 1869 na Waingereza. Awali lilikuwa ghorofa lakini likabadilishwa. Inasemekana shule nyingine ilijengwa Bagamoyo na baadaye Minaki,” anasema Mdimu na kuongeza,


   “Walijenga pia kanisa baada ya lile la Mkunazini Zanzibar. Lakini lilipochakaa ndipo wakajenga kanisa jingine mwaka 1886 kama lile la Mkunazini na ndiyo linatumika hadi sasa.”


   Akizungumzia uchaguzi wa eneo hilo, Mdimu anasema awali wazungu walitaka kujenga shule maeneo ya Muhenza Mkumbi na Mkanyageni, lakini wakaathiriwa na malaria, ndipo wakahamia katika mlima wa Magila.


   Kuhusu shule hiyo, Mdimu anasema kuwa awali ililenga kuwaandaa Waafrika ili wawasaidie wamisheni katika kazi zao. Waliwafundisha kusoma, kuandika na kuhesabu.


   Baadaye elimu ikapanuka baada ya shule za St. Marys na St Martin kujengwa zikiongeza masomo na wanafunzi.


   Anaongeza kuwa shule hizo hazikudumu muda mrefu, bali zilibadilishwa na kuwa Sekondari ya wasichana ambayo nayo ilikuja kuhamishiwa wilayani Korogwe ilipo shule ya wasichana maarufu kwa jina la Korogwe girls.


   Baada ya kuhamisha shule hiyo, matumizi yakabadilishwa na kikaanzisha chuo cha ualimu kwa wanawake tu. Hata hivyo, anasema chuo hicho nacho kilihamishiwa tena Korogwe kilipo chuo cha ualimu hadi leo.


   “ Mwaka 1974 hadi 75, majengo hayo yakafanywa kuwa mahali pa kujifungulia wanawake na ndipo ilipoanzia hospitali teule ya Muheza. Lakini ikahamishiwa eneo ilipo sasa na majengo haya yakabaki matupu,” anasema Mdimu.


   Kuanzishwa kwa Hegongo sekondari
   Mwalimu Mdimu anasema baada ya majengo kubaki matupu, mwaka 1976 wenyeji wa Magila walimwomba Askofu wa kanisa hilo dayosisi ya kaskazini John Ramadhani, ili waanzishe shule ya sekondari hasa kwenye majengo ulipo msalaba wa Dk Krapf, naye akawakubalia.


   “Februari 24, 1977 shule ya Hegongo ilianzishwa ikiwa chini ya wenyeji wa Magila ili kuwapa elimu watoto wa wilaya hiyo,” anasema.


   Hata hivyo anasema shule hiyo haikuwa na maendeleo mazuri kwa muda mrefu. Isitoshe, wasimamizi wa shule hiyo walishindwa kuiendesha kutokana na madeni makubwa ya umeme, mishahara ya watumishi na mafao yao.


   Hegongo ya sasa
   Anasema hadi mwaka 2000 wasimamizi wa shule hii walishindwa kabisa kuiendesha wakairudisha kwa kanisa.


   “Tangu wakati huo uongozi wa kanisa umeamua kuiendesha kwa kwa kulipa madeni makubwa yaliyokuwepo na kuimarisha hali ya elimu,” anasema na kuongeza:


   “Kwa sasa tunaboresha majengo, tumejenga maabara, maktaba ya kisasa na tutaongeza nyingine. Askofu wa sasa ameamua kuwachukua mapadri 10 waliomaliza kidato cha sita na kuwapeleka vyuo vikuu ili wasomee ualimu kwa ajili ya shule hii.’’

   Kwa upande mwingine, majengo ya zilizokuwa shule za St. Mary’s na St. Martin sasa zimechukuliwa na Serikali, huku mojawapo ikitumika kama shule ya sekondari ya kata ya Magila na nyingine kama shule ya msingi.


   Mwananchi
   Last edited by nngu007; 13th December 2012 at 00:03.


  2. #2
   mkupuo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Posts : 593
   Rep Power : 609
   Likes Received
   152
   Likes Given
   60

   Default re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   mkuu ahsante sana kwa kuipost humu jamvini hii thread.Yaani nilipoiona picha ya kanisa na jengo la karibu yake limenikumbusha miaka ya 1993 wakati nilipokuwa maeneo hayo kama mwalimu wa kujitolea Hegongo sec.Mimi nilikaa ktk jengo hilo kwa miezi 6.Big up!

  3. Capt Tamar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th December 2011
   Posts : 4,247
   Rep Power : 13984
   Likes Received
   1494
   Likes Given
   531

   Default re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Historia nzuri!! Ahsante

  4. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,951
   Rep Power : 77628742
   Likes Received
   14701
   Likes Given
   2693

   Default re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Ina maana ma Kungwi wote hawakuwahi kujenga shule kabla ya Krapf?
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  5. Zakumi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2008
   Location : Mtoni
   Posts : 4,609
   Rep Power : 1604
   Likes Received
   1657
   Likes Given
   477

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Quote By Kiranga View Post
   Ina maana ma Kungwi wote hawakuwahi kujenga shule kabla ya Krapf?
   Si unajua kwa nchi yetu shule ni majengo. Ndio maana tunaridhika kukaa kwenye madarasa yasio na waalimu.
   If we permit feathers to be freely borrowed, who is to tell the peacock from the crow?


  6. zumbemkuu's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 11th September 2010
   Location : street dweller
   Posts : 8,633
   Rep Power : 355221031
   Likes Received
   4045
   Likes Given
   13802

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   ''Overcome the devils with a thing called love'' bob marley

  7. Elli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th March 2008
   Location : Kijito-Upele
   Posts : 19,804
   Rep Power : 429501091
   Likes Received
   9055
   Likes Given
   7694

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Quote By zumbemkuu View Post
   hahahahaaa napakumbuka sana HEGONGO sec, ilikua shule yenye vituko vya kila aina, sijui kama bado ipo hadi leo ila nakumbuka iliwahi kufungwa kutokana na umakaya na bangi wanazovuta wanafunzi......oioooohhh home sweet home. Ngoja keshokutwa naelekea huko Kicheba ntapitia huko
   "The Lord will fight my case and I shall hold my peace".Exodus 14:14

  8. MANI's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 22nd February 2010
   Location : CHINI YA MBUYU
   Posts : 5,083
   Rep Power : 429498046
   Likes Received
   2457
   Likes Given
   4882

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Quote By Elli View Post
   hahahahaaa napakumbuka sana HEGONGO sec, ilikua shule yenye vituko vya kila aina, sijui kama bado ipo hadi leo ila nakumbuka iliwahi kufungwa kutokana na umakaya na bangi wanazovuta wanafunzi......oioooohhh home sweet home. Ngoja keshokutwa naelekea huko Kicheba ntapitia huko
   Mkuu miaka ya mwisho ya 70 Hegongo ilikuwa inatisha !cc zumbemkuu
   " TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"

  9. cheichei2010's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th September 2010
   Posts : 907
   Rep Power : 752
   Likes Received
   338
   Likes Given
   74

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Ni historia nzuri sana,nimeipenda.hiyo inabidi iwe sehemu pia ya makumbusho na utalii,sema sisi tumelala.Nimepata mshangao kwamba elimu ilianzia maeneo ya pwani ,lakini watu wa huko waliipa kisogo,na leo hii ndio wanaolalamika kuonewa.

  10. Siri Sirini's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th March 2012
   Posts : 547
   Rep Power : 1473
   Likes Received
   190
   Likes Given
   78

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Mic u Hegongo Holly Cross Secondary School

  11. authentic's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th March 2013
   Posts : 635
   Rep Power : 568
   Likes Received
   145
   Likes Given
   17

   Default Re: Picha: Shule ya kwanza Tanzania ilijengwa Muheza

   Quote By Elli View Post
   hahahahaaa napakumbuka sana HEGONGO sec, ilikua shule yenye vituko vya kila aina, sijui kama bado ipo hadi leo ila nakumbuka iliwahi kufungwa kutokana na umakaya na bangi wanazovuta wanafunzi......oioooohhh home sweet home. Ngoja keshokutwa naelekea huko Kicheba ntapitia huko
   mzee shule ipo kwa mujibu wa mleta mada.


  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...