JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

  Report Post
  Page 39 of 76 FirstFirst ... 293738394041 49 ... LastLast
  Results 761 to 780 of 1509
  1. Field Marshall ES's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2006
   Posts : 13,876
   Rep Power : 196824
   Likes Received
   722
   Likes Given
   225

   Default


   _________________

   Mwalimu (RIP)Baba Wa Taifa Hili, na Mkewe Mama Maria

   Wakuu Wote Jamii Forums, Heshima mbele!

   Katika hiki kipindi cha mapumziko nimeona sio vibaya tukijikumbusha historia yetu ya taifa katika picha, ninawaomba wakuu wote wenye picha interesting kisiasa kwa taifa letu, tuziweke hapa ili tujikumbushe na kuelemishana kidogo kuhusu taifa letu lilikotoka, unajua wananchi wasiojua walikotoka hawawezi kujua wanakokwenda.

   Ahsante wakuu.


  2. Kichuguu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th October 2006
   Location : Popote Porini
   Posts : 8,015
   Rep Power : 9270302
   Likes Received
   2691
   Likes Given
   1707

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Jasusi View Post
   Safarilands.org

   To this day in Majita there is a place called Iramba. Kitundu and Magembe are Bajita names.
   Rev. Kishoka upo hapo?
   There are more of us who came from Burundi than we realize.
   Jasusi unaniangusha aisee, Wajita hawasemi Iramba; wanasema KWIRAMBA.
   Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

  3. Shedafa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st May 2008
   Location : White Hart Lane
   Posts : 784
   Rep Power : 946
   Likes Received
   139
   Likes Given
   60

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Jasusi View Post
   Wakati nikiwa Tambaza kila alhamisi mchana British Airways lilikuwa linatua wakati huo ikiitwa BOAC kutoka London. Schedule yake ni kama ilikuwa imepandikizwa kichwani.
   Du! hii itakuwa zamani sana, mwaka gani huo?. Mimi British Airways ninayoikumbuka ni ile ilikuwa na kofia ya malkia, halafu ilikuwa Boing 747. Ilikuwa inafika saa 12 alfajiri, ikiwa inatua ilikuwa na madoido ya jinsi yake hivi tofauti na ndege nyingine. Ilikuwa raha kweli kiitazama, nakumbuka siku nilipopata bahati ya kuipanda ilikuwa kama nimeokota nyota ya jaha vile, kila mtu alinihusudu.

  4. Rev. Kishoka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th March 2006
   Posts : 4,514
   Rep Power : 12370
   Likes Received
   879
   Likes Given
   737

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Jasusi View Post
   The reason the Nyiramba migrated out of the ancestral lake zone area is because they were a peaceful people and not a warlike people. They were driven out by the warlike Kurias who migrated from the the North of Lake Victoria to the Eastern part of the Lake due to their wars with the Maasai. Until today the Kuria tribe and the Nyiramba's call one another "Jokey" , i.e. Watani because they fought a war between them long ago.

   Rev. Kishoka upo hapo?
   There are more of us who came from Burundi than we realize.
   Ahhh sasa Jasusi mbona unaleta Utani mbele ya hadhara bwana? Unataka Mpaka Mwalimu Kichuguu naye ajue kuwa ni "mujukuu" wetu?

   By the way alieandika ni Baba Mdogo!
   Amani Iwe Nanyi,

   Camerlengo

   Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

   "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

   'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"

  5. Rev. Kishoka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th March 2006
   Posts : 4,514
   Rep Power : 12370
   Likes Received
   879
   Likes Given
   737

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By kafara View Post
   msondo kulikuwa ndio maskani ya wababe. nakumbuka mtu ukiingia unaweza ulizwa "kijana umekuja mupweke au na mukaka yako?" kisha mtu unajibu "na mukaka wangu" halafu unapandisha t-shirt yako kidogo kumuonyesha muuliza swali nanga/kisu ulichobeba lol
   Kafara,

   Hii ya "Mukaka Yako" ni kali nilikuwa sijawahi kuisikia, sishangai Gurumo alipokuwa Sikinde alirushiwa mavi na jamaa wa Msondo!
   Amani Iwe Nanyi,

   Camerlengo

   Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

   "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

   'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"

  6. Rev. Kishoka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th March 2006
   Posts : 4,514
   Rep Power : 12370
   Likes Received
   879
   Likes Given
   737

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By mchongoma View Post
   ...cha ajabu basi, wakati huo zilikuwa zinakuja ndege za mashirika makubwa kama PAN AM ya marekani, SABENA ya ubelgiji, AEROFLOT ya mrusi, ALITALIA ya muitaliani, LUFTHANSA ya mjerumani, hata AIRFRANCE ya mfaransa! ...Jumatatu mpaka jumapili kwa ratiba nilijua saa ngapi na siku gani ndege gani ingekuja pale Dar Airport, terminal 1
   Mchongoma,

   Si kujua ratiba tuu, mpaka sauti za ndge tulikuwa tunajua ni ndege gani ikipita kabla hujaangalia angani. Zilizokuwa rahisi kabisa ni yale Ma-Tupolev ya Aeroflot, yalikuwa na mlio mono, huku Boeing, McDonnel na Lockheed zikiwa stereo na bado tulikuwa tunajua ni shirika gani kwa sauti kila siku;)
   Amani Iwe Nanyi,

   Camerlengo

   Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

   "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

   'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"


  7. Kichuguu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th October 2006
   Location : Popote Porini
   Posts : 8,015
   Rep Power : 9270302
   Likes Received
   2691
   Likes Given
   1707

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Rev. Kishoka View Post
   Ahhh sasa Jasusi mbona unaleta Utani mbele ya hadhara bwana? Unataka Mpaka Mwalimu Kichuguu naye ajue kuwa ni "mujukuu" wetu?

   By the way alieandika ni Baba Mdogo!
   Dah!!!, unajua wakati mwingine historia humbua watu sana. Kwa hiyo naona tusiulize maswali kabisa kuhusu uanachamwa wa Rwanda na Burundi kwenye EAC.
   Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

  8. #767
   Jasusi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th May 2006
   Posts : 12,055
   Rep Power : 173664483
   Likes Received
   4953
   Likes Given
   15529

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By shedafa View Post
   Du! hii itakuwa zamani sana, mwaka gani huo?. Mimi British Airways ninayoikumbuka ni ile ilikuwa na kofia ya malkia, halafu ilikuwa Boing 747. Ilikuwa inafika saa 12 alfajiri, ikiwa inatua ilikuwa na madoido ya jinsi yake hivi tofauti na ndege nyingine. Ilikuwa raha kweli kiitazama, nakumbuka siku nilipopata bahati ya kuipanda ilikuwa kama nimeokota nyota ya jaha vile, kila mtu alinihusudu.
   Hii ilikuwa kabla ya Boeing 747. Walikuwa na ndege zinaitwa Viscount (Super VC-10) nadhani ilikuwa haina spidi kama Boeing. Ilikuwa inaingia Dar saa sita mchana au saba kasorobo.

  9. Phillemon Mikael's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 5th November 2006
   Location : mwanza,/uk/santa clara
   Posts : 7,173
   Rep Power : 1198335
   Likes Received
   2642
   Likes Given
   50

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By mchongoma View Post
   ...ha ha ha... hillarious! :D

   Zamani undava/Utemi ilikuwa ndio desturi eeh!?... nakumbuka kipindi fulani madogo walisumbuliwa sana na yanki mmoja mitaa ya ilala/uwanja wa karume aliyekuwa anajiita eti Mtemi Sigasiga!

   Mndava huyo kwanza alikuwa na tabia ya kuacha signature yale kutani kila anakopita mfano wa Graffiti, Sigasiga kapita hapa,... halafu madogo wakikutwa na raba mtoni lazima wamuachie,... :D

   Tabia ya ubabe zilikuja rithiwa mpaka mashuleni, 'Vita' baina ya shule za Tambaza na Kinondoni katika mechi za Mpira hususan pale Uwanja wa shule ya Muhimbili, enzi hizo kina Athumani China, Amasha, etc
   ...ubabe wa tambaza ulifutwa badaye baada ya wanafunzi kuhamishwa karibu wote na shule kubadilishwa kuwa ya mchanganyiko kama sikosei...kufuatia ugomvi mkubwa uliopelekea kijana mbabe PUZZA wa tambaza kuuliwa...

  10. #769
   Majita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th January 2008
   Posts : 560
   Rep Power : 823
   Likes Received
   88
   Likes Given
   27

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   To this day in Majita there is a place called Iramba. Kitundu and Magembe are Bajita names.
   Rev. Kishoka upo hapo?
   There are more of us who came from Burundi than we realize.[/QUOTE]

   Historia inasema kuwa,hapo zamani za kale,kuna watu walikuwa wanaishi Mara,as wajita wakurya nk.Baadae ikatokea njaa miongoni mwa wajita,baasi wajita hao wakapangana jinsi ya kwenda kutafuta chakula.likaanza kundi la kwanza la wajita hao wakachukua Punda zao wakazunguka huko na huko Wakarudi Mara.Hao ndo wajita wa sasa wa Majita.Likaenda kundi la pili la wajita,nao kama kawaida wakachukua punda wakazunguka huko na huko.Lakini hawakupata chakula na njaa ikawauma SANA.Hivyo hawakuwa na jinsi ikabidi wachinje Punda wakala.Baada ya kula punda hao wakaogopa kurudi Mara kwani wangeulizwa punda na wangeadhibiwa kwa kuwala punda ho.KWA HIYO IKABIDI WAENDELEE NA SAFARI HADI WAKAFIKA SINGIDA wakatia nanga.baada ya kufika Singida Wajita hao waliokuwa wametokea majita sehemu za Kwiramba wakaa sehemu moja na wakaiita IRAMBA nao wakajiita Wanyiramba.hiyo ndo maana kuna kufanana kwa majina kati ya Iramba,kwiramba,magembe,nk.

   Haya wanyiramba nawapa changamoto rudini kwenu Majita hatutawadai punda wetu tena.Tulishawasamehe manake sasa tunajua ukali wa njaa.Hahahahaha

  11. Challenger's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th September 2007
   Location : Mafinga
   Posts : 53
   Rep Power : 740
   Likes Received
   19
   Likes Given
   8

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By kafara View Post
   mkuu heshima mbele kwa kumbukumbu kali.

   ongezea stc/biashara jazz band

   nakumbuka marijani rajabu (RIP) baada ya kutoka olympio primary ambako alikuwa nyanda/golkipa mzuri tuu na mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule
   alikwenda bendi ijulikanayo kama stc jazz band na baada ya hapo ndipo akaanzisha safari trippers.

   nawakumbuka pia familia ya akina kapinga (george, amato na abraham) ambao wote walikuwa katika timu ya waanzilishi wa bendi ya the barkeys.

   kweli tumetoka mbali
   Mkuu nashukuru kwa list nzuri ambayo nafikiri vijana wa zamani inatufikisha mbali saaaaaana!. Naomba kwenye list tuongeze Kyauli Voice au wenyewe walikuwa wanajiita mwendo wa jongoo na vumbi Nyuma, Bila kuwasahau Orchestra Toma Toma ya Tom, pia Uda Jazz, Bima Lee, Ushirika Jazz, Chamwino, Unajua enzi hizo bendi za mashirika zilikuwa nyingi sielewi iwapo zilikuwa na mlengo wa kisiasa, burudani au kuhamasisha shirika au kampuni husika

   Kisondella

  12. #771
   Mahoo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 25th August 2008
   Posts : 42
   Rep Power : 687
   Likes Received
   5
   Likes Given
   12

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Asante sana umenikumbusha mbali

  13. Son of Alaska's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd June 2008
   Location : london
   Posts : 2,828
   Rep Power : 1256
   Likes Received
   844
   Likes Given
   337

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   jamani,tusisahau kwamba katika historia tulikuwa na wafanya biashara kama akina BATENGA,ambao kibiashara walivuma sana dar.sifa yake kubwa ilikuwa ile motto yake ya "win at all costs"

  14. WildCard's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd April 2008
   Posts : 7,430
   Rep Power : 2306
   Likes Received
   2201
   Likes Given
   79

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Inaonekana miaka 20 ya Mzee Mwinyi na Mkapa ni kama vile historia ya Taifa letu ilisimama kidogo. Hakuna muziki wa maana uliopigwa wakati huo, hakuna mpira wa maana uliochezwa, hakuna Chuo KIkuu kilichojengwa mbali na kubadili majengo kuwa vyuo vikuu, hakuna kiwanda cha maana kilichojengwa.

  15. Field Marshall ES's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2006
   Posts : 13,876
   Rep Power : 196824
   Likes Received
   722
   Likes Given
   225

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Kuna Jamhuri Jazz ambao ndio chimbuko la Simba wa Nyika au Arusha Jazz, na Atomic Jazz. Nyimbo zao kama "Kipande cha Papa " = Jamhuri pamoja na "Joyce" = Atomic kwa kweli zilivuma sana miaka ile.
   Ni kweli kabisa mkuu, Jamhuri Jazz ndio waliokuwa chanzo cha Simba Wanyika, hata wakulu George Peter na Wilson Peter, kina Luza mpiga sax, na kina Tom Malanda, walianzia Jamhuri na baadye walikuwa kuwa Simba Wa Nyika's big na Les Wanyika.

   Sawa sawa.

  16. #775
   Chief's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th June 2006
   Posts : 1,248
   Rep Power : 1044
   Likes Received
   192
   Likes Given
   367

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Field Marshall ES View Post
   Ni kweli kabisa mkuu, Jamhuri Jazz ndio waliokuwa chanzo cha Simba Wanyika, hata wakulu George Peter na Wilson Peter, kina Luza mpiga sax, na kina Tom Malanda, walianzia Jamhuri na baadye walikuwa kuwa Simba Wa Nyika's big na Les Wanyika.

   Sawa sawa.
   Nadhani Simba wa Nyika ilikuwa jina la kutokea la Arusha Jazz, kwani baada ya Jamhuri Jazz kuvunjika, hawa 3 Peters ( George, Wilson and William)walihamia Arusha na kuunda hiyo Arusha Jazz. Jina la Simba wa Nyika nadhani origin yake ni ule wimbo wa Jamhuri Jazz wa "Mganga No 3" (kama sijakosea) ambao chorus yake ya instrumental ilitumika sana miaka ile kama kianzishio cha kipindi cha Jioni Njema cha RTD. Huo wimbo ulikuwa na sauti ya simba akinguruma.

   Walipohamia Kenya ndipo walipoanza kutumia Les Wanyika.


  17. mgirima's Avatar
   Member Array
   Join Date : 24th May 2008
   Posts : 82
   Rep Power : 708
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Field Marshall ES View Post
   Mkuu Mgirima,

   Unajua binafsi nilikuwa ninamuona Dede kuwa ni very rough, unajua sometimes jamaa huachia midevu na huvaa rafu rafu sana, halafu ni mkorofi sana akilewa masanga, kwa hiyo sikua mpenzi sana wa nyimbo zake, nilikuwa ninazimia tu na wimbo wake alioutoa akiwa Bima Lee yaani ule wa "Samaki Baharini Huishi Vipi", halafu siku zote nilidhani kuwa Bitchuka, alikuwa akimu over promote mno as opposed na kipaji chake hasa, ingawa sio siri kwua jamaa alikuwa maarufu sana, au?


   Ni kweli Dede ni mkorofi kwa tabia. Kuna wakati Hussein Jumbe alipokuwa Sikinde waliwahi kuzipiga ukumbini. Kinachompa chati ni uwezo wake wa kutunga nyimbo zenye hisia kali na ukorofi wake unasaidia kujenga nidhamu kwenye bendi. Hata Sikinde, huwa anakuwa kiongozi baada ya muda wanamtoa kisha kumrudisha tena. Ni mtoto wa Kariakoo!

  18. #777
   Gottee's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th September 2008
   Posts : 176
   Rep Power : 717
   Likes Received
   1
   Likes Given
   5

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Wimbo wa kwanza wa Remmy ulikuwa ni 'Siku ya Kufa'

  19. #778
   Gottee's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th September 2008
   Posts : 176
   Rep Power : 717
   Likes Received
   1
   Likes Given
   5

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Wengi hawafahamu kuwa mwanamuziki aliyekuwa akiongoza mapinduzi kuanzia Juwata na hatimaye Sikinde ni Marehemu Abel Baltazar. Huyu ndiye alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa bendi ya Mlimani Park Orchestra! Na ni huyu huyu ndiye aliyeongoza 'mapinduzi' ya kuwahamisha wanamuziki sita wa Sikinde kwenda OSS na kuanzisha mtindo wa Ndekule na inasemekana ni yeye ndiye aliyewapeleka Mwanyiro, Dede na Mulenga Bima Lee. Pamoja na nguvu zote alizokuwa nazo Baltazar hakuwa na tamaa ya madaraka na ndio maana baada ya kuanzishwa 'Nginde' alimwachia Maalim Gurumo uongozi wa Bendi na ndivyo ilivyokuwa huko Ndekule.

   Wakati wanamuziki wa Juwata wanahama na kaunzisha Sikinde wakishirikiana na wanamuziki wengine waliotoka Dar International kama Cosmas Thobias Chidumule Bitchuka hakuwemo alibakia Juwata na kuanzisha mtindo wa 'magoma kitakita' Utakubaliana nami kuwa katika zile nyimbo za kwanza za Sikinde sauti ya Bitchuka haikuwemo. Nyimbo kama Selina, Barua kutoka kwa Mama sehemu ya kwanza, Kassim Namba moja sauti ya Bitchuka haimo. Sauti zinazosikika mle ni za Gurumo, Marehemu Khamis Juma (Maalim Kinyasi), Cosmas Thobias Chidumule. Sauti ya Bitchuka utaisikia katika mkupuo wa pili wa kurekodi wa Sikinde. Nyimbo kama Kassim namba mbili unaweza kusikia sauti ya Bitchuka. Wakati Bitchuka anaondoka Msondo Shabaan Dede alikuwa ameshajiunga na ndio akawa akiongoza safu ya Uimbaji. Utakumbuka nyimbo kama Zuleka. Shabaan Dede Kamchape alitokea Dodoma International. Miaka ya Mwanzo ya 80 Msondo walijiimarisha kwa kumchua Moshi William kutoka bendi ya Polisi. Sauti ya Moshi akiwa Polisi Jazz utaisikia katika wimbo ule maarufu wa "Mwaka wa Watoto" ndani ya wimbo ule sauti ya Moshi inasikika ikilalamika... 'Unalewa bila kipimo hata watoto huwakumbuki'

   Baadaye Dede alijiunga na Sikinde akitokea Msondo. Pamoja na kwamba Sikinde ilishawahi kuchukua wanamuziki kutoka Msondo tena wengi kwa mkupuo na labda maarufu kushinda Dede. Kuhama kwa Dede kulizua mtafaruku mkubwa sana! Siku moja pale Klabu ya Simba Dede alikuwa amesimama kwenye kituo cha basi, wapenzi wa msondo walimvamia na kumvua 'nguo za msondo' Kumbuka siku zile bendi zilikuwa zikitoa 'yunifomu' na ilikuwa ruksa 'kutoka' nazo mitaani au hata harusini.

   Kuvuliwa nguo hadharani ndiko kulikopelekea Dede atunge wimbo wa 'Talaka Rejea' pale Msondo 'walipomwangukia' ili arudi kundini. Dede aliendelea kuwaimba msondo 'kama hana akili nzuri'. Kuna ule wimbo wenye maneno 'watoto wamekimbia nyumbani umebaki na wajukuu pia watasambaa' lilikuwa ni dongo la Said Mabera ambaye hajawahi kuhama Msondo tangu mwaka 1968 alipojiunga nayo.

   Wakati Msondo ikipita kwenye kipindi kigumu baada ya kuondoka Dede, ndipo walipomnyakuwa mwanamuziki 'kinda' wakati huo kutoka Dar International. Naye si mwingine ni Fresh Jumbe Mkuu. Kwa taarifa yenu huyu ni miongoni mwa wanamuziki wachache ambao Jabali la muziki liliwapa nafasi ya kuimbisha. Wengi wa wanamuziki wa Marijan Rajabu walikuwa ni waitikiaji. Utakubaliana nami utakapousikiliza ule wimbo wa 'Masudi Jambazi' na 'Nyota Njema'.

   Sikinde waliendelea kuishambulia Msondo kwa kumnyakua Fresh Jumbe baada ya Dede kwenda Bima Lee na Chidumule kuhamia Kurugenzi ya Arusha.

   Msondo nao kwa kujiimarisha walimchukua Mwanamuziki kipofu kutoka Kenya aliyekuwa na Bendi ya Les Cuban ya Morogoro, Nico Zenge Kala na 'tunda' jingine la Marehemu Marijani, Marehemu Augustino Masenge au kama alivyokuwa akijulikana kama Tino Masinge. Wengi watakumbuka Nico ndiye mwanamuziki mtunzi wa wimbo wa Solemba ambao ndio ulikuja kuzaa maneno ya 'kuachwa solemba' Kuna wakati wanamuziki wa Les Cuban walishawahi kumtorosha Nico na kumrudisha Morogoro. Inasemekana Nico alisusa kula na kudai hatakula hadi amuone Said Mabera. Ilibidi arudishwe.

   Kifo cha Nico hadi leo kwa wapenzi wa msondo wanaamini 'mbaya' alikuwa ni Shabaan Dede ambaye naye alisharudi Juwata baada ya kutoka Bima Lee. 'Mashambulizi' yalipomzidi Dede alijiengua msondo na kurudi Sikinde tena. Dede alianza kufanya visa na kisa cha mwisho alichofukuzwa Msondo yeye aliamua kwenda mpirani kuangalia mechi ya Simba na Coastal Union wakati wenzake walikuwa wanaporomosha muziki Amana. Watu walio karibu na Dede wanasema kinachomponza Dede kutopendwa na wenzake ni 'uwazi' alionao. Kama nyimbo zake zilivyo na 'madongo' na kauli zake ziko hivyo hivyo kwa maana nyingine wenzake hawapendi. Pamoja na yote ukweli utabakia kuwa Dede ni mtunzi mzuri wa nyimbo na ametunga nyimbo nyingi kuliko wanamuziki wengine wa Tanzania ukimwondoa TX Moshi William waliovuma kuanzia miaka ya mwisho ya sabini. Sina kumbukumbu nzuri za kina Mbaraka Mwishehe na Salum Abdalla. Naambiwa Mbaraka alikuwa akitungiwa nyimbo na 'ubabe' wake anasema katunga yeye.

   Tuendelee. Msukosuko mkubwa ambao sitausahau ulikuwa ni wa Sikinde kupoteza wanamuziki saba kwa mkupuo waliohamia OSS. Suala hapa halikuwa idadi kubwa ya ya wanamuziki bali ni umuhimu wa wanamuziki hao. Majina ambayo bado nayakumbuka hapa walikuwemo, Maalim Gurumo, Hassan Bitchuka, Fresh Jumbe, Benno Villa Anthony, Khamis Kinyasi, (waimbaji) Marehemu Kassim Rashid (Solo) na Charles John Ngosha (Bass) Ukiangalia hapo safu ya waimbaji waliobaki Sikinde walikuwa ni Marehemu Francis (Nasri) Lubua na Maximillian Bushoke.

   Ilibidi uongozi wa DDC chini ya Marehemu Mohamed Mpocho, (Meneja Mkuu DDC) Marehemu Hezron Mwampulo (Meneja wa Bendi) wahahe hadi usiku wa manane na kufanikiwa kumrudisha Benno Villa Anthony. Na wakati huo huo kufanya na mawasiliano na Chidumule aliyekuwa Kurugenzi Arusha. Na kwa haraka haraka kuwachukua Marehemu Mohamed Mwinyikondo (sina hakika nadhani alitoka Lola Africa ya Buguruni) na Hussein Jumbe kutoka Urafiki.

   Onyesho la kwanza la 'Nginde' baada ya kuondoka kina Gurumo lilifanyika pale DDC Magomeni. Ukumbi ulijaa kuangalia Sikinde itaimba bila 'mastaa' wake. Ukweli ni kwamba mapengo yote yalizibwa. Pengo la Gurumo lilizibwa na Meddy Mwinyikondo, la Bitchuka lilizibwa na Francis Lubua (Mbuyu wa Sikinde) na kina Cosmas na Bushoke waliimarisha sauti ya pili, bila kumsahau Benno. Baadaye sikinde walimchukua Tino Masinge kutoka msondo kuja kuziba pengo la Fresh Jumbe.

   Kuna habari zinasema SIkinde kabla ya kuchukuliwa na DDC ilikuwa inamilikiwa na na UwT na ndio maana Volvo nyingi zilikuwa zinajaa pale DDC Mlimani Park. Inaaminika kuwa 'tyuni' ya sikinde haijawahi kubadilika kwa sababu ya kuwepo mwanamuziki marehemu Michael Enock ambaye ndiye alikuwa 'afisa ufundi' mkuu wa kuchanganya sauti. Watanzania hatuna tabia ya kuwaenzi wanamuziki wetu lakini miongoni mwa majina hayatasahaulika ni jina la TX Moshi William au Shaban Muhoja. Huyu jamaa atabakia kuwa ni mwanamuziki wa kihistoria ukiondoa akina Mbaraka labda na Maneti.

   Senti zangu hamsini.

  20. BabaDesi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th June 2007
   Posts : 2,787
   Rep Power : 1296
   Likes Received
   446
   Likes Given
   2382

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By kichuguu View Post
   Asante sana mzee FMES kwa kutufahamisha mengi kuhusu huyu mwanamuziki mahiri tuliyewahi kuwa naye. Kuna mengi yaliyokuwa yanatokea Dar siyafahamu hasa kwa vile wakati huo mimi nilikuwa naishi huko Tabora, na nilikuwa nafika Dar kwa msimu tu kutumia treni inayosafiri siku mbili njiani usiku na mchana. Hata hivyo, naona ugumu sana kukubaliana nawe kuwa mtindo wa Koka Koka ulianza mwaka 1976, kwa vile mimi niliandika T-Shirt yangu neno Kokakoka mwaka 1975 nikiwa nalihusisha na Vijana Jazz. Inawezekana huo mtindo wa Kamata Sukuma ulitumika mwanzoni mwa mwaka 1974 na haukuvuma kabisa kwa vile mtindo wa kwanza kujulikana ulikuwa huu wa Koka Koka.

   Turudi nyuma tena; kumbuka kuwa kati ya mwaka 1975 na 1976 Vijana Jazz walikuwa wanarekodi nyimbo zao kwa kutumia Label za Moto Moto na kama hii hapa.


   Partial listing ya Catalogue ya Moto Moto inaoinyesha santuri zao kwa utaratibu ufuatao:


   MOTO 7-907 : Sabina/Niliruka Ukuta - Vijana Jazz Band , 1975
   MOTO 7-918 : Magdalina No 2/Miaka Mingi - Vijana Jazz Band , 1975
   MOTO 7-922 : Koka Koka No 1/Ujirani Mwema - Vijana Jazz Band , 1975
   MOTO 7-923 : Shangazi/Gwe Manetu Fii - Vijana Jazz Band, 1975
   MOTO 7-928 : Pili Nihurumie/Zuhura Naondoka - Vijana Jazz Band, 1976
   MOTO 7-930 : Unakufa Kiofisa/Wajue Vijana Jazz - Vijana Jazz Band, 1976


   Unaona kuwa hata ule wimbo KokaKoka Namba 1 ulipigwa mwaka 1975, mwaka ambao wimbo wa Niliruka Ukuta ulipotolewa pia. Nina imani kuwa Zuhura Naondoka uliopigwa mwaka 1976 bado ulikuwa kwenye mtindo wa Koka Koka. Inawezekana nyimbo nyingine hazikuwekwa kwenye santuri, ila zilirekodiwa RTD tu. Unajua kuwa baada ya kuvunjika kwa EAC (1977,) kuna wakati mpaka wetu na Kenya ulikuwa umefungwa, na hivyo wanamuziki wengi wa Tanzania wakawa hawarekodi nyimbo zao huko Kenya tena; ndipo wakawa wanarekodia RTD kwa ajili ya kupiga redioni tu, wala hakukuwa na santuri tena. Nadhani hiyo ilipunguza sana mapato yao na hivyo kudororesha maendeleo ya Muziki kwa vile studio zote za kurekodi santuri zilikuwa Kenya.


   Kwa wale ambao wanasikia jina la wimbo Niliruka Ukuta bila kuufahamu, nimefanikiwa kuupata online: Gonga hapa uusikilize na kuuangusha (download MP3) kwenye computer yako ukiependa.

   FMES, mimi na wewe tunakwenda sambamba vizuri kuhusu Maneti na VijanaJazz lakini hapa naomba kuungana na Mkuu Kichuguu kuhusu Koka Koka. Naomba nikiri tu kwamba mwaka 1974 mimi nilikuwa form One pale Musoma Alliance na kwa maana hiyo nyimbo nyingi nilikuwa nikizisikia zaidi pale nilipokuwa likizo ukiacha mara chacegh bendi zilipokuja Jumba la Maendeleo Musoma na sisi Wanafunzi kutoroka usiku kwenda kuchungulia madirishani (sio kuingia!). Lakini kubwa ambalo nina hakika nalo ni kwamba wimbo wa Kuruka Ukuta ulianza kusikika mwishoni mwa mwaka 1974 na nakumbuka kabisa watangazaji wengi wa radio wa wakati huo walikuwa wanataja kuwa ulikuwa umepigwa katika mtindo wa Koka Koka, unless they were all wrong!

   Mkuu kichuguu, baadaye hata kabla mpaka wa Tz na Kenya kufungwa baadhi ya Bendi zetu zilishaanza kushitukia kwenda kurekodi Nairobi kwa sababu nyimbo zilikuwa zinatoka ndivyo sivyo tofauti na zilivyokuwa kwenye Master-Tape ya RTD. Angalia wimbo wa Marijani Rajab wa Hanifa kwa mfano, ulikuwa miongoni mwa nyimbo zilizopendwa sana mwaka 1975 na kuendelea lakini ulipokwenda kurekodiwa Nairobi mwaka 1976 si wengi waliinunua rekodi yake kutokana na recording yake kuwa ya kiwango cha chini mno. Tunaendelea....!

  21. BabaDesi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th June 2007
   Posts : 2,787
   Rep Power : 1296
   Likes Received
   446
   Likes Given
   2382

   Default Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

   Quote By Chief View Post
   Nadhani Simba wa Nyika ilikuwa jina la kutokea la Arusha Jazz, kwani baada ya Jamhuri Jazz kuvunjika, hawa 3 Peters ( George, Wilson and William)walihamia Arusha na kuunda hiyo Arusha Jazz. Jina la Simba wa Nyika nadhani origin yake ni ule wimbo wa Jamhuri Jazz wa "Mganga No 3" (kama sijakosea) ambao chorus yake ya instrumental ilitumika sana miaka ile kama kianzishio cha kipindi cha Jioni Njema cha RTD. Huo wimbo ulikuwa na sauti ya simba akinguruma.

   Walipohamia Kenya ndipo walipoanza kutumia Les Wanyika.
   Chief, heshima yako mkuu! Nadhani hapa umekosea kidoooogo. Jina walilolitumia walipoingia Nairobi na kupata sifa nalo lilikuwa ni Simba wa Nyika baadaye migongano ikaanza ndani ya bendi ndipo yakazuka makundi ya Les Wanyika, Jobiso na kadhalika!


  Page 39 of 76 FirstFirst ... 293738394041 49 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Replies: 2
   Last Post: 23rd September 2011, 18:30
  2. TANZANIA: Historia ya Taifa Letu na Sheikh Yahya (RIP!)
   By W. J. Malecela in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 108
   Last Post: 7th June 2011, 09:18
  3. Replies: 5
   Last Post: 2nd May 2011, 14:36
  4. Replies: 7
   Last Post: 20th November 2010, 15:20
  5. Dhana Ya Uwekezaji Katika Taifa Letu Ina Maana Ipi?
   By Mr EWA in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 0
   Last Post: 31st July 2007, 15:54

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...