Toka enzi za kuuzana utumwani hili suala la usaliti miongoni mwa Waafrika, kama lilivyo suala la uzalendo, halipingiki - ni suala la kihistoria na mpaka leo linaendelea hasa kwenye nyanja ya 'vijisenti'. Historia ya Waafrika kutoka Cairo mpaka Cape na kutoka Dar-es-Salaam hadi Dakar imegubikwa na ujasiri wa wazalendo na woga wa wasaliti. Ifuatayo ni dondoo kutoka kwenye kitabu cha ' A Modern History of Tanganyika' kuhusu sakata la Mangi Sina na Mangi Meli pamoja Mangi wengine wa Uchagga - kwa maelezo zaidi inabidi tujisomee ukurasa 100 -102 wa Kitabu hicho kilichotungwa na Profesa John Illife:
"When Wissmann's column [A German General's Army Expedition] reached Kilimanjaro it entered an even more complicated web of intrigue. Rindi of Moshi had welcome his first German visitors and even sent emissaries to Berlin in 1889 to present a huge elephant tusk to the Kaiser. Appropriate presents [i.e. arms] were returned...Rindi needed the cannon. Sina of Kibosho had defeated him a few months earlier. Both were fighting to install their candidates in the Machame chiefdom. The first German embassy reached Sina in August 1890: 'I hear that Sin is troubling Ngameni [In Machame] and sending his warriors against him...What business have Kibosho's warriors in Machame?' 'Ngameni has attacked me. I am defending myself.' 'But Ngameni is now my friend.' 'If Ngameni is your friend', Sina replied, 'Shangali is mine''...A month later Sina attacked Ngameni again. Inflamed by Rindi, German relations with Sina deteriorated until his destruction was the main object of Wissmann's expedition. With some 300 soldiers and 400 auxiliaries provided by Rindi, Wissmann entered Kibosho on 12 February 1891...He shelled and stormed it [i.e. Sina's stone fort], losing control of his troops, who slaughtered every living thing inside. Sina escaped and harried the German withdrawal...Threatened with deposition, Sina submitted. He saved his throne, other Chagga chiefs hurriedly declared loyalty, Rindi gained several thousand cattle, and Sina killed every man in Kibosho who had hesitated to support him. 'In my twelve years' experience in Africa', Wissmann concluded, 'never have I met negroes [sic] so brave as Sina's men...Rindi's death in November 1891 opened the way for a new German ally, Marealle ('the Indefatigable') of Marangu, the most brilliant of all the chiefs who manipulated the Germans, Marealle was Sina's nominee for the Marangu chieftainship and a pawn in the struggle between Kibosho and Moshi until, appreciating European power, he befriended European travellers and joined Wissmann's expedition against Sina...Early in 1892 an askari was killed in a private quarrel in a chiefdom subordinate to Meli of Moshi, Rindi's young son. Probably incited by Marealle, the German commander panicked and marched into Moshi, brushing aside Meli's peace overtures...While Marealle tried to deceive the other chiefs that German troops still held Marangu, Meli demanded their submission. But the chiefs had no love for Rindi's son [i.e. Meli] and welcomed the Germans who re-occupied Marangu three months later. Sina offered to 'lead Meli to [the Germans] by the hand like a child' if supplied with ammunitition... Meli negotiated half-heartedly, fearing German revenge and knowing that his people opposed capitulation. In August 1893 the governor led 366 Askaris into Moshi and captured Meli's fortress. He kept his throne but lost the overlordship of Uru to Sina and of Kirua and Kilema to Marealle...Sina died in 1897, allegedly poisoned on Marealle's orders...Captain Johannes, Marealle's friend, took Chagga warriors to devastate Meru and Arusha; then, on regaining Moshi, he arrested Meli, Molelia of Kibosho, and seventeen other notables and hanged them from a tree outside the military station. Marealle became the most powerful ruler Kilimanjaro had ever known..."
Hii ndio historia yetu, pale ambapo chumvi imeongezwa na wanahistoria tunaweza kuipunguza. Na pale ambapo kuna kauongo hatuna budi kuiandika historia upya kwa uadilifu. Ila hatuwezi kuubadili ukweli wa Kihistoria. Shuleni tulisoma Kitabu cha 'Mashujaa wa Tanzania' ambacho kwa bahati mbaya leo nakala yake iko mbali kidogo na hapa nilipo ila nakumbuka kuwa kilikuwa kinaeleza ukweli bayana kuhusu usaliti wa baadhi ya machifu wetu. Kama anavyosema mwanafalsafa maarufu wa historia, George Santayana, wale wanaosahau yaliyopita - yaani historia yao - wanajihukumu kuirudia historia hiyo. Jukumu letu kama mtu binafsi na kama jamii/Taifa ni kuhakikisha kuwa haturudii kulea usaliti huu ambao ndio ulipelekea tuuze ndugu zetu utumwani na tutawaliwe na wakoloni. Hatuna budi kupambana na usaliti wa aina hii ambao leo hii ndio chanzo kikubwa cha ufisadi nchini!
Follow Us Here