JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

  Report Post
  Page 5 of 26 FirstFirst ... 34567 15 ... LastLast
  Results 81 to 100 of 518
  1. Zero One Two's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th September 2007
   Posts : 9,399
   Rep Power : 16999
   Likes Received
   2955
   Likes Given
   11111

   Default Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

   Wandugu, salam za mida hii.

   Natafuta hotuba ya "SABABU TUNAYO, NIA TUNAYO NA UWEZO TUNAO."


   Nataka kusikia hizo "sababu tunazo" na hoja ya Rais ya kwenda vitani kwa mapana na urefu, badala ya kumbukumbu ya mstari mmoja tuliyokaririshwa toka udogoni.


   Nitangulize ahsante.


  2. Mtanganyika's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th July 2007
   Location : US
   Posts : 1,693
   Rep Power : 127196814
   Likes Received
   505
   Likes Given
   173

   Default re: Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

   Quote By Nazjaz View Post
   Nyerere kweli anfgekubali kuwa nyuma ya maslah ya wamerekani na waingereza?
   Sidhani? Je tulikuwa na haja ya kumwacha nduli aichukue kagera yetu?
   But Nyerere was a sweetheart of the West. Nyerere alipewa press conference Rose Garden na JFK. Jimmy Carter called him " African Statesman". He welcome him in his office not for one day, but two days in 1977. So, i don't buy that west didn't like Mwalim. Mwalim was a darling of the west.
   Attached Thumbnails Attached Thumbnails Click image for larger version. 

Name:	Nyerere.jpg 
Views:	34 
Size:	29.5 KB 
ID:	21687  
   If a free society cannot help the many who are poor, it cannot save the few who are rich.

  3. Jumakidogo's Avatar
   R I P Array
   Join Date : 16th July 2009
   Location : DOM & DAR
   Posts : 1,868
   Rep Power : 1308
   Likes Received
   393
   Likes Given
   42

   Default Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Baada ya vita ile kali kati ya Uganda na Tanzania. Ukabaki utata mkubwa, wengine wakisema IDD AMIIN ndiye alikuwa mchokozi. Wengine wakisema Nyerere ndiye msababishaji. Wanaojua zaidi wanaweza kuiweka sawa simulizi ya mtu mmoja hapa chini ambaye alishiriki kwa karibu mtiti huo akiwa upande wa Uganda.

   Inaaminika kuwa rais mwana mapinduzi IDD AMIN DADA Alichafuliwa jina lake na sifa kutokana na sababu za kisiasa. Mchezo uliokuwa unafanywa na Rais wa Tanzania enzi hizo hayati Mwl Nyerere na rafiki yake mkubwa aliyefurushwa madarakani na IDD AMIN, MILTON OBOTE. Askari mpiganaji wa chini kwa chini wa kilichokuwa kikosi maalumu cha askari wa AMIN kilichojulikana kwa jina la MARILE TROOPS bwana Hezron Kagwa anakumbuka machache kuhusu mzozo huo.

   Mwaka 1971 IDD AMIN aliipindua serikali ya Uganda iliyokuwa ikiongozwa na OBOTE na kusababisha rais huyo aishi uhamishoni huku akifadhiriwa na rafiki yake mkubwa mwalimu JK NYERERE. Kitendo hicho kilijenga chuki kubwa kati ya Nyerere na Amin, ndipo zilipoanza propaganda za kumchafua Amin kwa kumwita Dikteta pamoja na sifa zote chafu. Hali ambayo ilifanya kiongozi huyo wa mapinduzi Uganda kuchukiwa na wananchi wa Tanzania na kuonekana adui mkubwa.

   Nduli, fashisti, joka kuu haya ni baadhi ya majina yaliyokuwa yakitamba na kujulikana sana aliyokuwa akiitwa IDD AMIN. Wakati huo kilianzishwa kikosi cha wanamgambo ambacho kiliundwa na vijana wa Uganda waliokuwa wakiishi Tanzania. Baadae kikosi hicho kilijulikana kwa jina la FRONANSA ambacho kilikuwa chini ya uongozi wa mtu aliyejulikana kwa jina la YOWERI MUSEVEN.

   Kikosi hicho baada ya kupata mafunzo maalumu ya kijeshi kikapelekwa huko Kagera mpakani mwa Tanzania na Uganda kwa lengo la kufanya chokochoko na uchokozi katika eneo ambalo lilikuwa linajulikana kama KAGERA SALIENT.

   IDD AMIN alikuwa akilalamikia sana vitendo vya kihuni vya askari hao ambao walikuwa wakivuka mpaka na kwenda kufanya vitendo vya kihuni nchini Uganda ikiwemo ubakaji. Lakini malalamiko yake yalikuwa yanapuuzwa na jumuia za mataifa. Ndipo IDD AMIN alipotuma vikosi vyake maalumu MARILE TROOPS ambavyo vilivamia ndani ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la kuwasaka wanamgambo hao.

   Kitendo kilichosababisha vikosi hivyo kukamata ardhi ya Tanzania kwa umbali wa km 80 huku vikisababisha mauaji na uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwepo daraja kuu la mto Kagera. Vikosi vya MARILE TROOPS vilikuwa chini ya gen OYITE.

   Hapo ndipo Nyerere alipopata sababu ya kuingia vitani kwa lengo la kumtoa IDD AMIN ili Rafiki yake OBOTE arudi madarakani. Vita ambayo inatajwa kusababisha uchumi wa Tanzani kuyumba kwa kishindo. Vinginevyo baada ya majeshi ya Tanzania kuvifukuza vikosi vya Uganda kutoka Kagera kulikuwa hakuna sababu ya kusonga mbele mpaka kumtoa IDD AMIN madarakani.

   Hata hivyo raia wa Uganda waliopata bahati ya kuwepo wakati wa utawala wa IDD AMIN wanaamini kuwa rais huyo ndiye aliyekuwa bora zaidi kuwahi kutokea katika nchi hiyo kutokana na kuukuza uchumi wa nchi hiyo kwa kasi kubwa.

   Hata hivyo historia bado inachanganya kwani watanzania wengi wanaamini kuwa AMIN ndiye aliyekuwa mchokozi katika vita ile....Swali la kujiuliza, kama AMIN hakuwa na sababu ya msingi ya kuvamia Tanzania. Kwa nini hakuvamia nchi nyingine za jirani? Kama ni kweli Nyere ndiye aliyekuwa mchokozi.

   Basi historia ya vita hiyo si ya kujivunia hata kidogo.
   Last edited by Jumakidogo; 14th December 2011 at 04:50.

  4. RUTARE's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 10th December 2011
   Posts : 149
   Rep Power : 537
   Likes Received
   31
   Likes Given
   108

   Default Re: VITA VYA KAGERA; Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho. Hii si historia ya kujivunia.

   Hiyo inajulikana sana nyerere alimwomba obote amuuzie ugomvi/vita.

  5. Smarty's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2011
   Posts : 649
   Rep Power : 678
   Likes Received
   187
   Likes Given
   84

   Default Re: VITA VYA KAGERA; Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho. Hii si historia ya kujivunia.

   nyerere hakuwa raisi..namsifu tu kuondoa ukabila yaliyobaki yoote alikuwa mchemkaji tu. Kwanza naskia kisa cha kuwachukia wahaya ni kwa sababu walikuwa wanamtania maana alidisco masomo ya udaktari huko uganda akaamua kukimbilia masomo ya historia hivo wale wemzake wahaya aliokuwa anasoma nao wakaanza kumsema kuwa nchi hii inaongozwa na kilaza..

  6. #85
   FIFA's Avatar
   Member Array
   Join Date : 7th December 2011
   Posts : 71
   Rep Power : 522
   Likes Received
   14
   Likes Given
   90

   Default Re: VITA VYA KAGERA; Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho. Hii si historia ya kujivunia.

   100% true.kuanzia hapo JK akatuambia miezi 18 tufunge mikanda hali ya uchumi ni mbaya mno, cha ajabu hadi leo mikanda imekataa kufunguka.


  7. Ndahani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2008
   Location : Somewhere
   Posts : 11,270
   Rep Power : 4473
   Likes Received
   3569
   Likes Given
   6900

   Default Re: VITA VYA KAGERA; Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho. Hii si historia ya kujivunia.

   Haahaa! Pilipili usiyoila inakuwashia nini? Do we know Amin that well? Au ndio hadithi za gahawa gahawa? Nimeanza kuamini kabisa, in Africa, there are so many confused people. They just wake up everyday without knowing the purpose of being alive and the meaning to work for. They are driven by whatever that would come on their way....tuna safari ndefu sana ya kwenda.
   We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
   Ralph Waldo Emerson

  8. #87
   Ritz's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st January 2011
   Location : Republic of Nauru
   Posts : 38,440
   Rep Power : 95730680
   Likes Received
   18913
   Likes Given
   2216

   Default Re: VITA VYA KAGERA; Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho. Hii si historia ya kujivunia.

   Nyerere alikuwa msanii namsifia kitu kimoja kuongea kiswahili

  9. mdoe mchaina's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 1st December 2011
   Posts : 138
   Rep Power : 536
   Likes Received
   22
   Likes Given
   0

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Ndio siasa zenyewe ipo siku watanzania walio enda kupigana kule uganda wataweka kila kitu hadhrani .

  10. KakaKiiza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th February 2010
   Location : Here Where you see me!!
   Posts : 8,634
   Rep Power : 88721937
   Likes Received
   4016
   Likes Given
   2246

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Zote porojo!Amin alikuwa mwehu!Wewe hujui historia ya vita!Ila kama wewe ni mganda tafuta ukweli kwa asikali waliokuwa wakilinda huko mpakani mwa mbalala!!
   Maisha ya Mtanzania magumu kuliko aliyepo jela.

  11. Ngongo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th September 2008
   Location : Mlima Meru
   Posts : 9,605
   Rep Power : 244522929
   Likes Received
   6590
   Likes Given
   7152

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   [1] Nyerere alianzisha vita ya Uganda !.

   [2] Nyerere kawasahau Wazee wetu wa Gerezani waliopigania uhuru wa Tanganyika !.

   [3] Nyerere si mtanzania !.

   [4] Nyerere muhasisi wa mfumo kristo !.

   [5] Nyerere aliwakandamiza waIslamu (Usisahau aliachia madaraka miaka 26 iliyopita)

   [6] Nyerere mbaya sana !.

   [7] Nyerere hafai kabisa !.

   [8] Nyerere Nyerere Nyerere bado tunasubiri story nyingine ahaaa aaaa hadi raha ngoja nikope msemo wa Dada FF wanchekesha.

  12. Dingswayo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th May 2009
   Posts : 3,969
   Rep Power : 172213111
   Likes Received
   2817
   Likes Given
   9187

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Aidha unaaandika haya kwa makusudi kwa kuitikia wito wa campaign ya kumchafua Mwl. J.K. Nyerere, au haya ni matokeo ya mfumo wa elimu duni.
   Batallamos hasta la victoria, siempre!

  13. Mabagala's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th November 2009
   Location : Nansio, Ukerewe
   Posts : 1,407
   Rep Power : 895
   Likes Received
   265
   Likes Given
   281

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   kastory kanaelekea elekea kwenye ukweli lakini
   Promises are comfort to a fool

  14. Ndahani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2008
   Location : Somewhere
   Posts : 11,270
   Rep Power : 4473
   Likes Received
   3569
   Likes Given
   6900

   Default Re: VITA VYA KAGERA; Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho. Hii si historia ya kujivunia.

   Quote By ritz View Post
   Nyerere alikuwa msanii namsifia kitu kimoja kuongea kiswahili
   Lakini hajamfikia huyu msanii wa sasa. Na hata kiswahili pia amepigwa bao maana kile cha kule katikati ya magomeni Nyerere hakuweza kukijua.
   We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
   Ralph Waldo Emerson

  15. Ndahani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd June 2008
   Location : Somewhere
   Posts : 11,270
   Rep Power : 4473
   Likes Received
   3569
   Likes Given
   6900

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Quote By Ngongo View Post
   [1] Nyerere alianzisha vita ya Uganda !.

   [2] Nyerere kawasahau Wazee wetu wa Gerezani waliopigania uhuru wa Tanganyika !.

   [3] Nyerere si mtanzania !.

   [4] Nyerere muhasisi wa mfumo kristo !.

   [5] Nyerere aliwakandamiza waIslamu (Usisahau aliachia madaraka miaka 26 iliyopita)

   [6] Nyerere mbaya sana !.

   [7] Nyerere hafai kabisa !.

   [8] Nyerere Nyerere Nyerere bado tunasubiri story nyingine ahaaa aaaa hadi raha ngoja nikope msemo wa Dada FF wanchekesha.
   This new obsession about Nyerere is quite amazing....people are wasting their time. The guy has gone!!
   We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
   Ralph Waldo Emerson

  16. Ndebile's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th September 2011
   Posts : 2,123
   Rep Power : 2429832
   Likes Received
   523
   Likes Given
   787

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   kunanukia harufu ya ukweli,nimekuwa kila mara najaribu kuunganisha dots ili nipate jibu la Museveni kuishi Muhutwe,Karagwe,kusoma Ihungo,n.k na vita vya Kagera....ngoja niendelee kufuatilia uzi huu!

  17. timbilimu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd September 2010
   Location : DSM
   Posts : 4,536
   Rep Power : 1481
   Likes Received
   1279
   Likes Given
   426

   Default

   Quote By Dingswayo View Post
   Aidha unaaandika haya kwa makusudi kwa kuitikia wito wa campaign ya kumchafua Mwl. J.K. Nyerere, au haya ni matokeo ya mfumo wa elimu duni.
   Mkuu Dingswayo haya ni matokeo ya mfumo mbovu wa elimu na Watanzania kutokuwa na mazoea ya kujisomea vitabu,majarida na magazeti badala yake wako busy kusoma udaku na kusikiliza ujinga ktk FM radio stations ambako watangazaji wake wengi ni wenye elimu duni! Imenisikitisha sana kwa baadhi ya michango kama hawa ni Great Thinkers!

  18. Jumakidogo's Avatar
   R I P Array
   Join Date : 16th July 2009
   Location : DOM & DAR
   Posts : 1,868
   Rep Power : 1308
   Likes Received
   393
   Likes Given
   42

   Default

   Quote By timbilimu View Post
   Mkuu Dingswayo haya ni matokeo ya mfumo mbovu wa elimu na Watanzania kutokuwa na mazoea ya kujisomea vitabu,majarida na magazeti badala yake wako busy kusoma udaku na kusikiliza ujinga ktk FM radio stations ambako watangazaji wake wengi ni wenye elimu duni! Imenisikitisha sana kwa baadhi ya michango kama hawa ni Great Thinkers!
   Tunaendelea kuusaka ukweli, lisemwalo lipo, Amin hakuwa chizi wa kukurupuka na kuvamia bila sababu, mbona hakuvamia Zaire, Sudani, au Kenya?

  19. Jumakidogo's Avatar
   R I P Array
   Join Date : 16th July 2009
   Location : DOM & DAR
   Posts : 1,868
   Rep Power : 1308
   Likes Received
   393
   Likes Given
   42

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Mi naomba kitu kimoja kutoka kwa wanaopingana na hili, tuambieni sababu mnayoijua ya AMIN kuvamia Tanzania.

  20. Mwakalinga Y. R's Avatar
   JF Tanzanite Member Array
   Join Date : 22nd October 2008
   Location : UVUNGUNI
   Posts : 2,731
   Rep Power : 17310777
   Likes Received
   1349
   Likes Given
   3987

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   Yupo prof mmoja wa uchumi nchini uganda nilipata nafasi ya kubadilishana naye mawazo,analaani sana kitendo cha uvamizi wa Nyerere nchini Uganda..Anasem Nyerer ndie aliyesababisha nchi ya Tanzania na Uganda kuwa na Uchumi duni zikiachwa mbali na Kenya.Anasema "Nyerere alitupa shida sana na amesababisha uchumi wetu kuwa dhaifu sana,nasikia wana mpango wa kumsimika kama mwenye heri.Tunakoelekea ukweli utakuja julikana kuhusu Nyerere" mwisho wa kunukuu.

  21. Jumakidogo's Avatar
   R I P Array
   Join Date : 16th July 2009
   Location : DOM & DAR
   Posts : 1,868
   Rep Power : 1308
   Likes Received
   393
   Likes Given
   42

   Default re: Vita vya Kagera: Nyerere na Obote Walitupiga changa la macho, hii si historia ya kujivunia!

   kutoka dira yangu


   Sunday, July 26, 2009


   NANI ALIANZISHA VITA YA KAGERA?

   Je ni Iddi Amini au Tanzania?

   Jana nchi ya Tanzania ilikuwa inasherehekea miaka 30 ya kumbukumbu ya mashujaa wa vita ya Kagera. Ni tukio linalokumbushia juu ya ushiriki wa nchi ya Tanzania katika vita pekee kubwa iliyiighar imu nchi yetu hasa. Hapa naleta mtizamo wa nje ya Tanzania juu ya chanzo cha vita ile:

   Miaka thelathini iliyopita, serikali ya kijeshi ya Uganda ikiongozwa na Iddi Amin ilipinduliwa na muungano wa majeshi ya wakombozi ambao walikuwa ni waasi waliokuwa wakiishi nchini Kenya na Tanzania katika miaka ya sabini wakisaidiwa na jeshi la Uganda. Kupinduliwa kwa serikali ya Iddi Amini kulileta hatima ya uongozi wa mtu ambaye ni miongoni mwa madikteta waliowahi kutokea katika historia ya Afrika. Makala hii inataka kuchokonoa kutoka kwa wanakumbuka kama kweli vita hii ilisababishwa na Iddi Amini ama kuna sababu zingine za msingi?

   Swali la kujiuliza juu ya vita ya Kagera ya mwaka 1978 – 79 ama Tanzania na Uganda ni je vita hii ilisababishwa na nini? Hisia na imani za watu wengi kuanzia kwenye vitabu, majarida na magazeti, na hata wavuti mbalimbali duniani ni kuwa Iddi Amini ndiye alikuwa mtu mbaya ambaye aliamua kutuma majeshi yake kuivamia Tanzania bila sababu yeyote, na ndipo Tanzania ikajibiza mashambulizi. Kuna imani nyingine kuwa hapo tarehe 19/04/1978 ilitokea ajali ya gari ambayo ilimuua Makamu wa Raisi wa Amini, ndugu Mustapha Adrisi; kutokana na ajali hiyo watu waliamini kuwa ajali hiyo ilipangwa na ilileta hali ya wasiwasi mkubwa katika jeshi la Uganda. Hali hii ilimfanya Amini aamue kuivamia Tanzania ili kuhamisha mawazo ya maafisa wa jeshi na hata akili za wananchi wa Uganda. Hili linathibitishwa na taarifa iliyowahi kutolewa na Raisi Milton Obote ambaye alipinduliwa na Iddi Amin ambaye alisema kuwa: “Kuna ushahidi wa kutosha kuwa uvamizi wa Amini dhidi ya Tanzania ulikuwa ni hatua za makusudi za Amini kujinasua kutokana na kushindwa kwa Amini kulidhibiti jeshi lake”.


   Tatizo moja kubwa ambalo limejitokeza kila tunapojaribu kuelezea kuhusu historia ya Uganda wakati wa utawala wa Iddi Amini ni ile kukosekana kwa mtizamo wenye usawa na kuachana na mitizamo iliyojaa uzandiki (stereotyping) juu ya Iddi Amini. Ni wazi kizazi cha leo kinamjua Iddi Amini kama mtawala dhalimu kabisa na hili limeachiwa likaenea dunia nzima bila utafiti wa kina. Na ili tuweze kujua nini hasa ni ukweli wa hali halisi wa vita ya Kagera, ni lazima tuitizame hali ya Uganda kati ya mwaka 1977 na 1978 kabla ya vita kutokea.

   Kwa mujibu wa Compton Encyclopedia Yearbook, 1979, inasema kuwa mwaka 1977 Uganda ilipata mafanikio makubwa kiuchumi hasa kutokana na bei kubwa ya zao la kahawa kwenye soko la Dunia. Hali hiyo iliifanya Uganda kupata nakisi ya bajeti kubwa kuwahi kutokea tangu uhuru. Ukiacha mafanikio hayo, kitabu hicho kinaendelea kusema kuwa mafanikio hayo kiuchumi yaliambatana na kuundwa kwa vikundi vya waasi nje na ndani ya nchi vyote vikitaka kumpindua Iddi Amini ambaye naye aliponea chupuchupu kuuawa mara nne. Kuponea huku kuuawa kulisababishwa na uimara ulioambatana na unyama wa wanausalama wa Iddi Amini na pia heshima kwa amiri jeshi mkuu. Kutokana uongozi wa Amini kuwa wa kibabe hasa ikizingatiwa alikuwa tayari ana maadui wengi, vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa havina uhusiano mzuri na Iddi Amini hasa ikizingatiwa ugonjwa wa kutu ya kahawa (frost) kule Brazili uliwezesha mauzo ya kahawa ya Uganda kuleta nakisi katika uchumi hivyo hakujali sana nchi za magharibi.

   Tarehe 28/07/2006, kupitia kituo cha redio cha STAR FM, mtangazaji Semwanga Kisolo alikumbusha wasikilizaji kuwa kipindi cha Iddi Amini alihakikisha mishahara ya wafanyakazi wa umma ilikuwa inalipwa si zaidi ya tarehe ishirini na tano na kama ingelichelewa Iddi Amini mwenyewe alikuwa akitoa karipio kali kwa wanaohusika. Anaeleza kuwa Amini alikuwa mtu anayejali muda kuwahi kazini na katika matukio muhimu ya kitaifa na alisisitiza wafanyakazi pia wajaliwe ili waweze kuwahi na kutimiza majukumu yao. Anasema kuwa wakati wa serikali ya Iddi Amini, majeshi yote, polisi, magereza, jeshi la anga, na usalama wa Taifa na hata maafisa wa kati katika utumishi wa umma waliishi maisha ya kujitosheleza (comfortable): kama kumudu kusomesha watoto katika shule nzuri, kuendesha magari mapya katika idara mbalimbali za serikali. Magari hayo yalikuwa kama Fiat Mirafiori, Honda Civic, na Honda Accord. Kwa ufupi kipindi cha utawala wa Iddi Amini sarafu ya Uganda ilibadilishwa kwa kati ya shilingi 7 na 7.50 kuanzia mwaka 1971 – 1979. Mfumuko wa bei ulikuwa ni chini kwa kipindi chote cha utawala wa Iddi Amini.

   Hadi Iddi Amini anapinduliwa mwaka 1979, hospitali kuu ya Mulago pamoja na hospitali zote za serikali Uganda zilikuwa na magodoro, mashuka na mito na mablanketi na hakuna mgonjwa aliyelala chini kama ilivyo leo hii. Pia kila chumba cha binafsi hospitalini hapo kilikuwa na televisioni ya rangi. Matibabu yote kwa waganda yalikuwa ni bure. Kwa ujumla kiuchumi Uganda ilikuwa haijafikia hali mbaya hata kidogo na ndio maana baada ya Iddi Amini kuingia madarakani jumuiya ya kimataifa iliiwekea vikwazo vya kiuchumi Uganda lakini Uganda iliweza kumudu hali hiyo bila matatizo.

   Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, Uganda iliunda Shirika la Ndege (Uganda Airlines) na shirika la reli kutokana na masalia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; hii yote ilikuwa ni katika kuimarisha “Hadhi ya Taifa” National Pride. Tatizo kubwa kwa Iddi Amini lilikuwa ni vikundi vya waasi waliokuwa katika nchi za jirani wakipata misaada mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakijipanga kuivamia Uganda na kumng’oa Iddi Amini wakati wowote. Ikumbukwe tu kuwa vikundi vya waasi vilikuwa vikiongozwa na watu kama Yoweri Museveni ambaye kwa sasa ni raisi wa Uganda.


   Hadi hapa ni wazi kuwa Iddi Amini ambaye anaelezwa kama mtu katili na aliyechukiwa sana nchini Uganda anaonekana kama alikuwa ni kiongozi mwenye mafanikio ya kiuchumi. Je ni kwa nini alichukiwa; ama ni kwanini utawala wake usababishe watu kuunda vikundi vya waasi? Ni wazi watu kama Milton Obote, ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Julius Nyerere ndiye aliyehusika sana kumpaka matope Iddi Amini akieleza kuwa vita ya mwaka 1978 -79 ilisababishwa na Iddi Amini. Ni wazi kunahitajika uchambuzi zaidi wa kina na usio na upendeleo wa aina yeyote (objective) na si hizi hekaya za akina Obote na Museveni kwani hazina uzani sawasawa.

   Swali la msingi: Ni je ni nini hasa chanzo cha vita hii?
   Tuanze na harakati za awali katika eneo la mpakani – Mtukula - kati ya Tanzania na Uganda mwaka 1978. Kwa mujibu wa Generali Yusuf Himidi akinukuliwa na gazeti la Standard la Tanzania toleo la tarehe 3/07/1978. Generali Himidi aliyekuwa ni kamanda wa Brigadi ya Magharibi, alisema kuwa Uganda inajihusisha na matendo ambayo yanaweza kusababisha mapambano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili. Matendo yaliyokuwa yanalalamikiwa na Generali Himidi inasemekana yalikuwa yametokea na kuelekezwa kwa raia wa Tanzania kutoka kwa watu ambao kiasili walikuwa waganda ambao inaaminika walitokea upande wa Tanzania. Hii inaonesha kuwa uchokozi wa mwanzo kabisa ulitokea Tanzania, kwani Iddi Amini aliwahi kulalamika kuwa Tanzania inatumia eneo la Mutukula kuwapenyeza waasi wa Uganda ambapo aliweka kikosi maalumu kujaribu kuzuia shambulizi lolote ambalo alilitarajia.

   Je waganda ambao walitokea Tanzania ni akina nani? Na kama walikuwepo, ni wazi Iddi Amin alikuwa sahihi ama alikuwa anaongopa? Ingawa hakuna uhakika sana, lakini kama mtu atarejea katika kitabu kiitwacho: “Sowing the Mustard Seed: The Struggle for Freedom and Democracy in Uganda” ambacho kimeandikwa na mwanamapinduzi wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, tunaweza kuona uhalali wa madai ya Amin. Katika ukurasa wa 62, ni kuwa katika kipindi hicho, yeye alikuwa ni mpigananji wa msituni akiongoza kikundi cha wakombozi wa Uganda waliokuwa wakiendesha harakati zao katika eneo la Kagera, sehemu iitwayo “Kagera Salient”. Kikundi cha akina Museveni kilijulikana kama FRONASA, je, si inawezekana ndio waliokuwa wakiendesha mauaji dhidi ya raia wa Uganda mpakani Mutukula mwaka 1978 ambapo waliwaua wakazi wanne wa kiganda waliokuwa wakinywa pombe ya kienyeji “MALWA” mpakani? Mauaji hayo ndiyo yaliyomchagiza Amin kuamua kuiona Tanzania kama mchokozi. Na inawezekana kabisa, FRONASA ilikuwa inagombanisha nchi mbili hizi ziingie vitani huku wakijua watafaidika na vita hiyo.

   Kwa mfano, inasemekana Iddi Amini aliunda kikosi maalum kuweka usalama eneo la Mutukula “Malire Troops” baada ya mauaji ya raia wa Uganda na watu wenye asili ya Uganda ambao waliingia kutokea Tanzania na baada ya mauaji, walikimbilia nchini Tanzania. Chanzo cha uvamizi wa Tanzania inasemekana ilikuwa katika kujibu mapigo baada ya jeshi la Uganda, kupitia kikosi cha Malire Troops kuingia Kagera kuwasaka wauaji wa raia mmoja wa Uganda aliyeuawa. Raia huyo alikuwa ni shemeji wa Kamanda Mkuu wa Malire Troops, Luteni Kanali Juma Ali. Malire Troops waliingia Kagera hadi kilomita 80 ndani ya Kagera. Kwa mujibu wa gazeti la Weekly News, toleo la tarehe 5/11/1978, Majeshi ya Tanzania yaliivamia Uganda kuanzia tarehe 10 – 31, 1978 na kuteka maili 400 za mraba sehemu ya Uganda ambapo mapambano makali yalifanyika katika kilima cha Minziro.


  Page 5 of 26 FirstFirst ... 34567 15 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Video za Vita vya Kagera
   By MaxShimba in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 3
   Last Post: 19th September 2011, 02:23
  2. Vita vya Kagera tulipigana na Libya (Gadafi)
   By Mwana wa Mungu in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 123
   Last Post: 22nd March 2011, 09:22
  3. Mashujaa wetu wa vita vya Kagera
   By MaxShimba in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 1
   Last Post: 27th July 2009, 03:22
  4. Miaka 30 Ya Vita Vya Kagera
   By X-PASTER in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 1
   Last Post: 2nd November 2008, 02:36

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...