JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw

  Report Post
  Results 1 to 4 of 4
  1. The Quonquerer's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2009
   Posts : 788
   Rep Power : 1204
   Likes Received
   106
   Likes Given
   121

   Default Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw

   Katika Mkoa wa Kagera wenye Halmashauri za Wilaya (8) jumla ya wanafunzi 49,804 waliandikishwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (Darasa la VII) mwaka 2010, kati ya hao walioandikishwa wanafunzi waliotahiniwa na kufanya mtihani wa darasa la saba ni 48,893 ambazo ni asilimia (98.2%) ya wanafunzi wote walioandikishwa kufanya mtihani mwaka 2010, wanafunzi 911 ambao ni asilimia (1.8%) hawakufanya mtihani wa darasa la saba
   Wanafunzi waliofaulu ni 29,385 asilimia (60.1%) kati ya wanafunzi 48,893 waliofanya mtihani. Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2011 ni 27,258 asilimia (92.8%) kati ya wanafunzi 29,385 waliofaulu, na wanafunzi 2,127 asilimia (7.2%) wamebaki kutoka idadi ya wanafunzi 29,385 waliofaulu mwaka huu 2010.
   Aidha kiwango cha ufaulu Mkoa wa Kagera kimepanda kwa asilimia (4.51%) ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana (2009) ambapo kiwango cha ufaulu kilikuwa ni asilimia (55.59%) lakini kwa mwaka huu (2010) kiwango cha ufaulu ni asilimia (60.10%).
   Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imeendelea kuongoza Mkoa wa Kagera kwa asilimia (76.3%) na kushika nafasi ya Kwanza, Wilaya ya Biharamuro imeshika nafasi ya pili kwa asilimia (72.5%) kutoka nafasi ya nne iliyoshika mwaka jana 2009. Manispaa ya Bukoba imeshika nafasi ya tatu kwa asilimia (71.9%) na mwaka jana ilishika nafasi ya tatu. Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi imeporoka nafasi mbili kutoka nafasi ya pili iliyoshika mwaka jana (2009) na kushika nafasi ya nne kwa asilimia (65.0%).
   Halmashauri za Wilaya nyingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyopanda nafasi moja tokay a mwaka jana (2009) na kushika nafasi ya tano kwa asilimia (61.5%). Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imeshuka nafasi moja kutoka nafasi ya tano (2009) na kushika nafasi ya sita kwa asilimia (56.4%). Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imeendelea kushika nafasi ya pili kutoka mwisho kama mwaka 2009, lakini mwaka huu 2010 kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia (4.35%), kutoka aslilimia (50.55%) za mwaka 2009 mpaka asilimia (54.9%). Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imeendelea kushika nafasi ya Mwisho Kimkoa japo kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka aslimia (33.99%) za mwaka 2009 mpaka aslimia (50.4%).
   H/WILAYA

   MWAKA 2010
   NAFASIMWAKA2009

   NAFASI

   NGARA
   76.3%

   1
   73.04%
   1

   BIHARAMULO
   72.5%

   2
   63.45%
   4

   BUKOBA MANISPAA
   71.9%

   3
   66.27%
   3

   MISSENYI
   65.0%

   4
   67.90%
   2

   CHATO
   61.5%

   5
   55.65%
   6

   MULEBA
   56.4%

   6
   58.24%
   5

   KARAGWE
   54.9%

   7
   50.55%
   7

   BUKOBA VIJIJINI
   50.4%

   8
   33.99%
   8
   JEDWALI HAPA JUU NI VIWANGO VYA KUFAULU KIWILAYAPicha ya Afisa Elimu Mkoa Kagera Bw. Florian Kimolo
   Aidha kiwango wanafunzi waliofaulu walichaguliwa kwa kiwango cha alama ya juu ambayo ni 230 kw awavulana na wasichana alama 228, lakini kiwango cha alama ya mwisho kuchagua ni alama 100 kwa wasichana na wavulana kwa mwaka 2010.
   Shule ilyoishika nafasi ya kwanza Kimkoa ni Shule ya Msingi Kaizilege kutoka Manispaa ya Bukoba . Mwanafunzi aliyeongoza Kimkoa, Kiwilaya na Kishule ni Ligobert Linus Kutoka Shule ya St. Peter Claver iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe . Aidha, Machumi John Nyarukubara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ameshika nafasi ya mwisho kwa kupata alama 6 tu kati ya shule 967 zilizofanya mtihani.
   Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera akielezea sababu za Halmashauri ya Wilaya za Bukoba na Karagwe kendelea kushika nafasi mbili za mwisho alisema pamoja na sababu nyingine maandalizi hafifu kwa baadhi ya shule, hali mbovu ya miundombinu, upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia na baadhi ya walimu kutomudu kufundisha masomo ya Hisabati na Kiingereza na hivyo kusababisha wanafunzi wengi kushindwa masomo hayo.


  2. Matango's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th January 2011
   Posts : 512
   Rep Power : 657
   Likes Received
   84
   Likes Given
   120

   Default Re: Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw

   Je naweza kupata matokeo hayo kwa ukamilifu, majina ya shule na wanafunzi nchi nzima ? Kuna mtu amewahi kuyasoma mahala ?

  3. #3
   jafora's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 1st November 2011
   Posts : 4
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1
   Likes Given
   1

   Default Re: Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw

   Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana kutangaza idadi ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ilhali majina yenyewe na shule wandazo kutofahamika,wuika wangejipanga wakamilishe yote

  4. KENET's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th July 2012
   Posts : 253
   Rep Power : 528
   Likes Received
   58
   Likes Given
   89

   Default Re: Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw

   Quote By jafora View Post
   Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana kutangaza idadi ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ilhali majina yenyewe na shule wandazo kutofahamika,wuika wangejipanga wakamilishe yote
   .Serikali inachofanya siku hizi inaangalia shule zile za Private ambazo wanafunzi wamefaulu vizuri na wana GRADE A wanawapangia kwenye shule mojawapo ya kata darasa Zima kwa makusudi kabisa wakijua wazi kabisa kwamba hawa hawatakwenda au wazazi wao hawatakubali mtoto mwenye A masomo yote akasome pale kwa hiyo nafasi zinabaki nyingi wanapeleka hao ambao wametangaza kuwa wamefaulu bila ya kuwapangia shule. Je hii ni halali?


  Similar Topics

  1. Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano 2011
   By Chona in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 12
   Last Post: 2nd April 2012, 01:14
  2. waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2011
   By dedam in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 0
   Last Post: 16th March 2011, 22:24
  3. Majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano mwaka huu 2011 yanatoka lini?
   By Bizzly in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 1
   Last Post: 8th March 2011, 15:08
  4. Matokeo kidato cha nne ni standardization ya matokeo halisi baada ya wanafunzi kufeli
   By Nicazius in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 16
   Last Post: 6th February 2011, 12:12

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...