JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Matokeo kidato cha nne 2009

  Report Post
  Page 2 of 8 FirstFirst 1234 ... LastLast
  Results 21 to 40 of 143
  1. Tripo9's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th September 2009
   Posts : 2,106
   Rep Power : 1046
   Likes Received
   398
   Likes Given
   722

   Default Matokeo kidato cha nne 2009

   Source: Muhtasari wa habari TBC1 saa 10jioni.   Ufaulu wapungua.

   Mzimu wa somo la Hisabati waendelea kuumiza vichwa vya wadogo zetu.
   Last edited by Invisible; 6th February 2010 at 21:55. Reason: Link included
   "Smile though your heart is aching"...Me says


  2. Shy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2006
   Posts : 4,896
   Rep Power : 0
   Likes Received
   120
   Likes Given
   0

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Au tembelea www.naombakazi.com

  3. #22
   Tiba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th July 2008
   Posts : 4,470
   Rep Power : 204554487
   Likes Received
   2833
   Likes Given
   1533

   Default Re: Matokeo kidato cha nne yametoka.

   Quote By vitendo View Post
   http://www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm

   Tafuta huko yako pia matokeo ni kwenye website ya wizara.
   Mkuu Vitendo,

   Asante sana huku kwenye website ya wizara matokeo yako nje nje tena bila hata uficho, ni centre na majina ya wanafunzi yako wazi against matokeo.

   Shukrani.

   Tiba

  4. Katoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 11th March 2008
   Posts : 138
   Rep Power : 731
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   kweli kiwango kimeshuka, hata St. Francis hamna point 7?

  5. Katoma's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 11th March 2008
   Posts : 138
   Rep Power : 731
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   s0248 marian girls secondary school


   div-i = 79 div-ii = 5 div-iii = 0 div-iv = 0 fld = 0

   examination centre ranking
   examination centre region; pwani
   total passed candidates: 84
   examination centre gpa: 1.5292
   centre category: centre with 35 candidates or more
   centre position in its category(regionwise): 1/66
   centre position in its category(nationwise): 1/2259

  6. PingPong's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2008
   Posts : 758
   Rep Power : 814
   Likes Received
   49
   Likes Given
   45

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   jamani wadau hii inakuaje baadhi ya shule zinafunguka vzr wakati nyingine zinagoma?


  7. Ilumine's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 27th December 2008
   Location : hapa na pale
   Posts : 196
   Rep Power : 701
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Bado, nashindwa kufungua, sijui ni tatizo la website, au mtandao wangu. Kuna yeyote aliyefaulu kufungua na kuyaona hadi muda huu?
   "Never allow Failure to be an Option"

  8. PingPong's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2008
   Posts : 758
   Rep Power : 814
   Likes Received
   49
   Likes Given
   45

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By Ilumine View Post
   Bado, nashindwa kufungua, sijui ni tatizo la website, au mtandao wangu. Kuna yeyote aliyefaulu kufungua na kuyaona hadi muda huu?
   mkuu mi nimefanikiwa gonga hiyo link iliyotolewa na muanzilishi wa thread utaenda moja kwa moja kwenye site yenyewe ila tatizo nalopata hapa ni kuwa baadhi y shule zinagoma kufunguka, sijui y!

  9. Baba Mkubwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : LAPPEENRANTA
   Posts : 770
   Rep Power : 826
   Likes Received
   20
   Likes Given
   8

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Jamani sasa yapata masaa mawili nahangaika kufungua....tafadhari wakuu mwenye uwezo wa kufungua, naomba msaada wa linki ya moja kwa moja ya matokeo ya shule ya makongolosi.................

  10. rmashauri's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Location : Ng'wanza Sukuma
   Posts : 3,041
   Rep Power : 1368
   Likes Received
   409
   Likes Given
   995

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By Katoma View Post
   s0248 marian girls secondary school


   div-i = 79 div-ii = 5 div-iii = 0 div-iv = 0 fld = 0

   examination centre ranking
   examination centre region; pwani
   total passed candidates: 84
   examination centre gpa: 1.5292
   centre category: centre with 35 candidates or more
   centre position in its category(regionwise): 1/66
   centre position in its category(nationwise): 1/2259
   Hongera zao!
   Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote (Mithali 14:34)

  11. rmashauri's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Location : Ng'wanza Sukuma
   Posts : 3,041
   Rep Power : 1368
   Likes Received
   409
   Likes Given
   995

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By Baba Mkubwa View Post
   Jamani sasa yapata masaa mawili nahangaika kufungua....tafadhari wakuu mwenye uwezo wa kufungua, naomba msaada wa linki ya moja kwa moja ya matokeo ya shule ya makongolosi.................
   Mimi pia najaribu hapa imefunguka shule moja tu zingine zinanipa blank page.
   Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote (Mithali 14:34)

  12. epigenetics's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th May 2008
   Posts : 234
   Rep Power : 739
   Likes Received
   40
   Likes Given
   100

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   ukifungua page ikagoma, click "Reload" au "Refresh" icon kwenye browser, itakubali the 2nd or 3rd trial... Website za bongo, kweli balaa

  13. Papizo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Location : What for??
   Posts : 3,991
   Rep Power : 243308
   Likes Received
   589
   Likes Given
   3088

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Mimi mpaka dakika ya sasa sijafanikiwa kufungua kabisa,imenigomea kabisa sasa sielewi tatizo zaidi ni nini!!

  14. PingPong's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2008
   Posts : 758
   Rep Power : 814
   Likes Received
   49
   Likes Given
   45

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By Papizo View Post
   Mimi mpaka dakika ya sasa sijafanikiwa kufungua kabisa,imenigomea kabisa sasa sielewi tatizo zaidi ni nini!!
   For now naona zote zinafunguka, kama bado hauwezi kufungua kuna uwezekano wa tatizo kuwepo hapo kwako.

  15. TanzActive's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th November 2007
   Location : DSM
   Posts : 351
   Rep Power : 790
   Likes Received
   60
   Likes Given
   3

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Mimi nimeshangaa zile shule nyingi za english ambazo zina majengo bora ,wazazi wanalipa mamilioni na usafiri wa shule upo lakini wafanya vibaya kuliko hata shule za serikali

  16. PingPong's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2008
   Posts : 758
   Rep Power : 814
   Likes Received
   49
   Likes Given
   45

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By TanzActive View Post
   Mimi nimeshangaa zile shule nyingi za english ambazo zina majengo bora ,wazazi wanalipa mamilioni na usafiri wa shule upo lakini wafanya vibaya kuliko hata shule za serikali
   kweli inashangaza na kutia uchungu kwa wazazi husika , mahela yote waliotoa ni sawa na wametupa shimoni, kibaya zaidi matokeo yakitoka ndio yametoka hata ufanye nini.

  17. Vitendo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2009
   Posts : 599
   Rep Power : 747
   Likes Received
   58
   Likes Given
   61

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   MATOKEO ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne kwa mwaka 2009 yametangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) huku yakionyesha shule za serikali zikiendelea kufanya vibaya kwa kushindwa kuwemo kwenye shule 10 bora huku kiwango cha ufaulu kikizidi kupungua.

   Aidha, matokeo ya mtihani huo uliofanyika Oktoba mwaka jana yanaonyesha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa asilimia 11.2 kwani mwaka 2008 kilikuwa asilimia 83.69 wakati mwaka huu kikishuka hadi kufikia asilimia 72.51

   Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es salam kwenye ofisi za baraza hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako, alisema watahiniwa 351,152 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, kati yao wasichana ni 167,591 sawa na asilimia 47.73 na wavulana 183,561 sawa na asilimia 52.27 wakati mwaka 2008 watahiniwa 241,472 walisajiliwa.

   Alibainisha kuwa watahiniwa 42,672 sawa na asilimia 17.85 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ambapo wasichana ni 13,788 sawa na asilimia 12.47 na wavulana 28,884 sawa na asilimia 22.48.

   Alisema, watahiniwa waliopata daraja la nne ni 130,651 sawa na na asilimia 54.66 wakati waliopata sifuri ni 65,708 sawa na asilimi 27.49 idadi inayoonekana kuongezeka tofauti na mwaka jana.

   Akizungumzia hilo, Joyce alisema kati ya shule 10 bora hakuna shule ya serikali hata moja na kueleza kwamba shule zinazoongoza ni zile za seminari na nyingine zinazomilikiwa na watu binafsi.

   Katibu huyo alizitaja shule 10 bora zenye watahiniwa zaidi ya 35 kuwa ni Shule ya Wasichana Marian na St. Mary’s Junior Seminary, zote za Bagamoyo; St. James Seminary, Uru Seminary, Anwarite Girls, Maua Seminary na St. Mary Goreti, zote za Kilimanjaro; nyingine ni Don Bosco Seminary ya Iringa; St. Francis Girls ya Mbeya; na Feza Boys ya Dar es Salaam.

   Aidha, alizitaja shule 10 bora zenye wanafunzi chini ya 35 kuwa ni Feza Girls; Thomas More Machrina na Hellen’s za Dar es Salaam; Mafinga Seminary na Bethelsabs Girls za Iringa; na St. Joseph-Kilocha seminary ya Kilimanjaro.

   Nyingine ni Queen of Apostles Ushirombo ya Shinyanga; Dungunyi Seminary ya Singida; Rubya Seminary ya mkoani Kagera; na Sengerema Seminary ya Mwanza.

   Alisema nafasi ya kwanza kwa mtahiniwa aliyefanya vizuri imekwenda kwa msichana Imaculate Mosha kutoka Marian Girls wakati mvulana bora ni Gwamaka Njobelo wa Shule ya Sekondari Mzumbe.

   Hata hivyo alizitaja shule zilizoshika mkia zenye wanafunzi zaidi ya 35 kuwa ni Sekondari ya Busi na Jangalo za Dodoma; Sekondari ya Misima, Chekelei na Potwe za Tanga; Sekondari ya Milola na Mandawa za Lindi; Sekondari ya Kiwere ya Tabora; Sekondari ya Msata ya Pwani; na Sekondari ya Masanze ya Morogoro.

   Sekondari nyingine zilizofanya vibaya zenye wanafunzi chini ya 35 ni Kizara ya Tanga; na Mingumbi, Nahukahuka, Marambo, Ruponda na Mpunyule zote za Lindi. Nyingine ni Songolo ya Dodoma; Dole ya Zanzibar; Ruruma ya Singida; na Viziwi Njombe ya Iringa.

   Pamoja na hayo alisema jumla ya watahiniwa 410 wamefutiwa matokeo yao chini ya kifungu namba 52 cha kanuni za mitihani baada ya kubainika kwamba walifanya udanganyifu.

   Aliongeza kuwa watahiniwa 184 walibainika kuwa na makaratasi yenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika mtihani wa somo; watahiniwa 141 walikamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa makaratasi yanayohisiwa kuwa na majibu ya somo husika.

   Alisema kuwa watahiniwa 64 walibainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu jambo ambalo si rahisi kwa wanafunzi wenye uwezo wa kufikiri tofauti.

   “Jamani nawaomba wanafunzi wajitahidi kusoma kwani wakikaa kufikiri mtihani utavuja au watapewa majibu kuna hatari kubwa ya kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao au kukamatwa iwapo wataingia na majibu katika vyumba vya mitihani,” alisema Dk. Ndalichako

   Aidha, alisema mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari ya Kadoto, aliandika matusi mazito katika mtihani wa Biolojia 1 kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5 (13) cha kanuni za mitihani.

   Alisema, matokeo ya watahiniwa 7,242 yamesitishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipa ada hasa kwa shule za serikali.

   Alisema matokeo ya wanafunzi hao yatatolewa pindi mwanafunzi atakapolipa ada ya mtihani na iwapo katika kipindi cha miaka miwili wahusika watakuwa hawajalipa Baraza la Mitihani la Taifa litafuta matokeo yao.

   Hata hivyo, alisema baraza hilo limetoa onyo kali kwa vituo mbalimbali vilivyobainika kufanya udanganyifu na kuvifutia usajili vituo viwili ambavyo ni Sinza Iteba na Dar es Salaam Prime kwa kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani kwa kuwa na wanafunzi wengi kuliko uwezo wake.

  18. Baba Mkubwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : LAPPEENRANTA
   Posts : 770
   Rep Power : 826
   Likes Received
   20
   Likes Given
   8

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By PingPong View Post
   For now naona zote zinafunguka, kama bado hauwezi kufungua kuna uwezekano wa tatizo kuwepo hapo kwako.
   Mkuu mpaka sasa mimi hakieleweki kabisa, kama vipi naomba mtu mwenye kuweza kufungua anipositie link ya matokeo ya shule ya makongolosi.

   Kama ni network basi yangu ni kimeo!!!!

  19. Binti Sayuni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2009
   Location : MWILINI
   Posts : 341
   Rep Power : 721
   Likes Received
   32
   Likes Given
   80

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By Baba Mkubwa View Post
   Mkuu mpaka sasa mimi hakieleweki kabisa, kama vipi naomba mtu mwenye kuweza kufungua anipositie link ya matokeo ya shule ya makongolosi.

   Kama ni network basi yangu ni kimeo!!!!
   Mkuu hata mimi ni hivyo hivyo shule ninayotafuta haifunguki.

  20. Baba Mkubwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : LAPPEENRANTA
   Posts : 770
   Rep Power : 826
   Likes Received
   20
   Likes Given
   8

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   Quote By Binti Sayuni View Post
   Mkuu hata mimi ni hivyo hivyo shule ninayotafuta haifunguki.
   Binti jalibu hapa

   http://www.necta.go.tz/publishedresults/csee.php?v=2

   Kwenye makongolosi, weka jina la shule uitafutayo

  21. Samora Lyakurwa's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 7th February 2010
   Posts : 2
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Matokeo kidato cha nne 2009 yametoka!

   wadau ebu nipeni msaada, nimejaribu kutumia broswers zote lakini nimeshindwa kufungua matokeo ya kidato cha nne, msaasa tutani


  Page 2 of 8 FirstFirst 1234 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Matokeo ya kidato cha nne 2006
   By Invisible in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 24
   Last Post: 12th March 2014, 16:25
  2. Matokeo kidato cha nne
   By Jumakidogo in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 3
   Last Post: 22nd February 2011, 13:36
  3. Matokeo kidato cha nne ni standardization ya matokeo halisi baada ya wanafunzi kufeli
   By Nicazius in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 16
   Last Post: 6th February 2011, 12:12
  4. Matokeo Kidato cha Sita 2009
   By epigenetics in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 43
   Last Post: 2nd May 2009, 22:52
  5. Kidato cha Tano 2009: Majina ya waliochaguliwa
   By SMU in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 0
   Last Post: 2nd April 2009, 09:24

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...