Ndugu Wahitimu kidato cha Sita na kidato cha nne 2012 ambao matokeo yao wametoka kuanzia tarehe. 30.05.2013,

Nimepata taarifa hivi punde tu toka Wizarani Makao Makuu Idara ya Elimu ya Ualimu kuwa muda wowote kuanzia wiki ijayo Wizara ya Elimu kupitia website yake itatangaza nafasi za masomo ngazi ya Ualimu (Vyuo vya serikali) kwa wahitimu wa kidato cha sita (Diploma ) na kidato cha nne (certificate - ambao watakuwa wamefikisha points 27 baada ya matokeo ya juzi kutangazwa).

Hivyo basi kuanzia jumanne ya tarehe 4 june, mnatakiwa kutembelea mara kwa mara katika website ya wizara ya Elimu.