JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

  Report Post
  Page 2 of 2 FirstFirst 12
  Results 21 to 28 of 28
  1. Dancani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th April 2012
   Posts : 801
   Rep Power : 711
   Likes Received
   365
   Likes Given
   375

   Default Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetaja shule 24 za sekondari ambazo zitatoa wanafunzi 5,000 waliomaliza kidato cha sita watakaojiunga na jeshi hilo. Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Mahuga alisema katika taarifa yake jana kuwa wanafunzi hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo ifikapo Machi 2, mwaka huu.

   Shule hizo za sekondari ni Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza.Shule nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos. Nyingine ni Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.

   Taarifa hiyo ilisema maofisa wa JKT watakwenda kwenye shule hizo kuanzia Januari 9, mwaka huu kwa ajili ya kutoa utaratibu wa mafunzo na kambi ambazo watakwenda.“Mkuu wa JKT kwa mamlaka aliyopewa kisheria ya mwaka 1964 na kufanyiwa mapitio mwaka 2002, chini ya kifungu cha sheria namba 5,” ilisema taarifa hiyo. Iliongeza kuwa “Anawaita vijana watakaohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ifikapo terehe 2, Machi 2013.” Utaratibu wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ulisimamishwa tangu mwaka 1994.

   Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Julai mwaka jana, Waziri wake, Shamshi Vuai Nahodha alisema kambi zilizopo za JKT zina uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka huu wataanza kwa majaribio na vijana 5,000.


   Alisema wanafunzi 41,348 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika mwaka 2013 na kwamba vilikuwa vikiandaliwa vigezo ili kuwapata vijana 5,000 ili kujiunga na JKT.

   Kwa mujibu wa jarida la JKT, mafunzo hayo yatakuwa ya miezi sita katika Kambi za JKT Bulombora na Kanembwa mkoani Kigoma.
   Nyingine ni Mlale (Ruvuma), Mafinga (Iringa), Msange (Tabora) na Oljoro(Arusha).

   source Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu - Kitaifa - mwananchi.co.tz

   Hoja: Kwanini huo mujibu wa sheria uwe kwa baadhi ya wanafunzi na kwanini wamelenga kuchukua wanafunzi kutoka shule nyingi za serikali kama sio zote na isiwe zile za watu binafsi?


  2. Nguchiro's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd November 2009
   Location : Musoma, Mara
   Posts : 363
   Rep Power : 687
   Likes Received
   27
   Likes Given
   0

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   hakuna nchi inayoongozwa kisanii na kifala kama Tanzania, anayebisha abishe tu

  3. zuberi's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 27th June 2009
   Posts : 160
   Rep Power : 668
   Likes Received
   7
   Likes Given
   0

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   huna akili acha upuuzi wako tafakari kabla ya kuzungumza

  4. bruda's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th September 2012
   Posts : 28
   Rep Power : 472
   Likes Received
   1
   Likes Given
   13

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   Nawaonea huruma sana watakao enda bulombora na mafinga iringa kuna shuruba ya kufa mtu.....

  5. omujubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2011
   Location : Bumbire Island
   Posts : 4,087
   Rep Power : 31861
   Likes Received
   1936
   Likes Given
   4378

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   Quote By bruda View Post
   Nawaonea huruma sana watakao enda bulombora na mafinga iringa kuna shuruba ya kufa mtu.....
   we unadhani jkt ya sasa inaweza kuwa kama ya enzi hizo?? Sasa hivi mambo yote ni dot.com na sidhani kama watawanyimaq uwezekano wa kutumia laptops zao angalau hata saa moja kwa siku na hapo ni mbali na kuwa na simu zenye full internet!
   Ukitafakari hapo ndipo unapata jibu kwamba hili zoezi na sawa na kumfundisha mbwa mzee mbinu za kisasa za uwindaji

   Tusiruhusu wasiotaka mabadiliko kuamua juu ya mustakabali wa mabadiliko - Onyesha ushirikiano!

  6. Nzowa Godat's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th June 2011
   Posts : 2,337
   Rep Power : 1000
   Likes Received
   530
   Likes Given
   16

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   Mimi nawaasa maafande wetu to adhere to the moral ethics hasa kwa hawa mabinti zetu. Ni vyema kutambua kwamba hiki kizazi cha dot com ni cha chips MAYAYI pia waiunge mkono dunia kuepusha maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI chonde chonde.


  7. Ze Heby's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th May 2012
   Location : Upanga
   Posts : 1,166
   Rep Power : 718
   Likes Received
   226
   Likes Given
   8

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   Wakuu nimechaguliwa kambi ya Bulombora Kigoma.Kwa yoyote anayejua hali ilivyo huko anijuze tafadhali.Shukran

  8. #27
   bily's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th April 2012
   Location : SCANDINAVIA.
   Posts : 5,656
   Rep Power : 29883658
   Likes Received
   1232
   Likes Given
   268

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   Quote By wa katikati View Post
   jangwani?, zanaki?, kisutu?- au makamanda hawataki kuburudika?.

   kua basi nani kakuambia kua hao makamanda nao wana akili kama ya kwako

  9. lukindo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th March 2010
   Posts : 3,746
   Rep Power : 1347
   Likes Received
   1530
   Likes Given
   2078

   Default Re: Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

   Quote By Ze Heby View Post
   Wakuu nimechaguliwa kambi ya Bulombora Kigoma.Kwa yoyote anayejua hali ilivyo huko anijuze tafadhali.Shukran
   tafuta mawe ya kutosha ya kuzuia sumu za nyoka maana huko cobra ni kama mijusi tu kwa jinsi walivyo wengi
   Mobutu answered (1990s) about corruption in Congo: If you want to steal, steal a little in a nice way. But if you steal too much to become rich overnight, you'll be caught.


  Page 2 of 2 FirstFirst 12

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...