Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

    Report Post
    Results 1 to 5 of 5
    1. #1
      Ngongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th September 2008
      Location : Mlima Meru
      Posts : 4,972
      Rep Power : 6859
      Likes Received
      2414
      Likes Given
      3175

      Default Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

      CHUO kikuu Huria Tanzania kimebadili mfumo wa utoaji majaribio kutoka mara tano kwa mwaka hadi mara mbili, ili kuongeza ufanisi na ubora wa kukuza uwezo wa wanafunzi katika kufaulu mitihani.

      Akizungumza katika mkutano wa Wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho, Makamu Mkuu wa chuo Tolly Mbwette, alisema mfumo huo mpya utawawezesha wanafunzi kupata muda na nafasi ya kujiandaa na mitihani ya majaribio.

      "Hatua ambayo chuo imechukua ni nzuri, kwa sababu njia hii itamsaidia mwanafunzi kukuza uelewa wake badala ya kutegemea kufanyiwa majaribio na mwenzake", alisema.

      Mbwette alifafanua kwamba, wanafunzi waliowengi wamekuwa wakifanyiwa mazoezi na wanafunzi wengine kwasababu ya kuwa na kazi nyingi ambazo zinawafanya washindwe kumudu kufanya majaribio yanayotolewa na chuo.

      " Hatua hii itasaidia kwani walimu waliowengi hawasahihishi mitihani kwa muda mwafaka, baadhi yao wanasaisha mitihani mingi bila kujali ubora kwa ajili ya kulipwa fedha nyingi" alisema Mbwette.

      Hata hivyo, alifafanua kwamba bajeti ya fedha iliyotolewa na serikali mwaka huu ni ndogo haiwezi kukidhi mahitaji yote ya chuo hivyo bado wanaendelea kufanya jitihada za kuweza kupata fedha za kutosha ili kuboresha elimu ya juu katika chuo hicho.

      "Tunaishukuru serikali kwa kukubali kutuongezea wanataaluma ambao watasaidia kwa kiasi kikubwa kufundisha na kufunya chuo kuendelea kuongeza idadi ya wanafunzi, " aliongeza.

      Kwa upande wa wanafunzi, walisema wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na viongozi wa chuo kwa kubadili mfumo ambao ulikuwa ukiwabana, hivyo mfumo huo mpya utatoa nafasi kwa kila mwanafunzi kufanya mtihani kwa nafasi.

      Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Happy Mbile, alisema mfumo wa awali haukuwa mzuri kwasababu wanafunzi wengi hawakuweza kuonyesha uwezo wao, kwakukosa mda wa kufanya majaribio wenyewe, kulingana na kazi nyingi hasa kwa wale wanaofanya kazi maofisini.
      Last edited by Ngongo; 31st August 2009 at 15:49. Reason: Spelling error


    2. #2
      Shaycas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th February 2009
      Location : Arusha
      Posts : 663
      Rep Power : 659
      Likes Received
      26
      Likes Given
      2

      Default Re: Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

      Wanauwezo wa kupokea na kuhudumia wanafunzi wangapi kwa ufanisi mzuri wakati wanafanya haya?Je inasaidia vp kuondoa uwezekano wa mtahiniwa kufanyiwa mtihani na mwenzake?
      Be YOURSELF

    3. #3
      Nanu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th May 2009
      Posts : 1,211
      Rep Power : 758
      Likes Received
      38
      Likes Given
      77

      Default Re: Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

      It is always good to have a look back and make continual improvement. I applaude OUT for that!!!! Keep up guys. Nasikia siku hizi kuna masters ya mwaka mmoja Mzumbe-Dar Campus (coursework & dissertation within one year, halafu ni evening classes).
      Peace is meaningless if nothing is right. Do it and Do It Right or Not at All.
      Swallowing His Own Words has never Killed the Politician!

    4. #4
      Kagoma's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st May 2009
      Posts : 28
      Rep Power : 518
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

      CHUO kikuu Huria Tanzania kimebadili mfumo wa utoaji majaribio kutoka mara tano kwa mwaka hadi mara mbili, ili kuongeza ufanisi na ubora wa kukuza uwezo wa wanafunzi katika kufaulu mitihani.


      Hata hivyo, alifafanua kwamba bajeti ya fedha iliyotolewa na serikali mwaka huu ni ndogo haiwezi kukidhi mahitaji yote ya chuo hivyo bado wanaendelea kufanya jitihada za kuweza kupata fedha za kutosha ili kuboresha elimu ya juu katika chuo hicho.


      Kwa mtazamo wangu Chuo kimepunguza majaribio from 5 to 2 times because of Budget constraints and NOT to improve! Kimefulishwa na serikali ikabidi wa ji adjust!



    5. #5
      Sipo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th July 2008
      Location : SIPAJUI
      Posts : 2,167
      Rep Power : 989
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default Re: Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

      Kwa mtazamo wangu naona uongozi wa chuo umefanya jambo zuri sana
      Hii itasadia kumpa mwanaffunzi muda mzuri wa kujisomea na kufaulu vizuri
      Lakini pia itatoa nafasi ya Lecturers kusahihisha kwa umakini na nafasi mitihani hiyo na sio kulipua kama wanavyofanya sasa hivi
      "Ficha Upumbavu wako, husifiche hekima yako'' Invisible


    Similar Topics

    1. Mgomo unanukia chuo kikuu huria
      By MADORO in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 4
      Last Post: 19th December 2011, 17:10
    2. Masikini Chuo Kikuu Huria (TZ) - Open University of Tanzania (OUT)
      By Rangi 2 in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 7
      Last Post: 27th March 2011, 09:04
    3. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
      By Magobe T in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 1
      Last Post: 25th August 2009, 18:37
    4. Huduma mbaya za chuo kikuu huria cha tanzania
      By UniqueTanganyika in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 1
      Last Post: 26th January 2009, 20:31
    5. Wizara kudhamini walimu 1,500 Chuo Kikuu Huria
      By Kuntakinte in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 2nd June 2007, 10:56

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...