Matokeo ya Kidato cha Pili 2012, Shule zakosa wanafunzi wa kidato cha TATU 2013!
Kuna taarifa kutoka kwa wasahihishaji wa mtihani wa kidato cha pili wa mwaka 2012 kuwa HALI NI MBAYA SANA na kuna shule huenda zikakosa kabisa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tatu kwa mwaka 2013! Taarifa zinaeleza kuwa wakati wastani wa kufaulu ni Alama 30, shule kwa Kanda ya Kusini-Lindi na Mtwara wanafunzi wake wameshindwa kabisa kufikisha wastani huo na wengi wao wameishia wastani wa 10 hadi 15! Ikumbukwe kuwa kuanzia mwaka 2012 wanafunzi watakaoshindwa kufikisha wastani wa alama 30 hatawaruhisiwa kuendelea kidato cha tatu bali watatakiwa kukariri kidato cha pili! Matokea ni mabaya sana, lakini swali la kujiuliza ni kuwa TATIZO LIKO WAPI?
tusubiri tena watu kuruhusiwa kuingia kidato cha tatu kwa wastani wa 15 na waziri kujinasibu kwamba kiwango cha ufaulu kimepanda. Aibu kubwa hii mwisho wake ni kuwalipa mishahara mizuri walimu. Otherwise kila mwaka kiwango cha ufaulu kitazidi kushuka.
Tulidai kuwa shule zitakosa wanafunzi sasa mbona ufaulu umeongezeka kwa asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka jana. Kweli nimeamini Watu wa wizara ya elimu hawana haya, wakati wa usahihishaji yale masifuri baadhi ya vituo aliyekuwa na alma nyingi anapata chini ya 10 sasa kama wanatakiwa wewe na wastani wa 30 ulifikaje? Ama kweli hapa ni mserereko kila kitu
Follow Us Here