Jukwaa la Elimu (Education Forum)Educational discussions in here... If you have some College/School materials and you wanna give them to your fellows pls do that favour to them. Let them get educated here! Become a Member to enjoy more stuffs
Ninajua kunawadau wengi sana ambao katika maisha yao watakuwa wamepitia pale Pugu Secondary School kama wanafunzi, wafanyakazi, wakazi etc. Wadau hawa sasahivi wametawanyika sehemu mbalimbali ya nchi yetu na duniani kote.
Mimi binafsi ni mojawapo ya watu waliopitia pale kama dent wa high school...(form 5 to 6), ningependa tujikumbushe mambo mbalimbali kuhusu shule ile ambayo ina historia ndefu sana kwa Taifa letu. Ni shule ambayo viongozi wetu mbalimbali walishapitia pale kama wanafunzi au walimu kama vile Mwal. Nyerere, Mkapa (kama sikosei) na wengine wengi tu.
Kwa kuanza kabisa mimi nakumbuka wakati tukisoma pale, maji yalikuwa upatikanaji wake wa shida sana, kulikuwa na wadudu wa malaria na tryphoid sana, kulikuwa na Fungus acha kabisa....yaani tulikuwa tunakamatwa na fungus kiasi cha kushindwa kutembea au kutembea as if one has STDs.....jamaa mtaani mpaka wakawa wanatuita FUNGUS BOYS Mabafu halikuwa haba sana na machafu...so option ilikuwa kwenda kuogea kule mtoni tulikuwa tunakuita POND....hence tukawa tunaitwa POND BOYS.....!
Anything you remember here?
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Hivi pale Baghdad siku hizi vipi, bado wauza mafuta na wapiga ndumu wapo?
Wale masela nilipita pale last year sikuwaona......kilichokuwa kinawaweka pale ilikuwa pia dili za kupakia mchango kule mtoni upande wa kushoto ukiwa unapanda skonga......!
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
nimefurahi sana kusikia baghdad!!!!! niliacha kiatu pale masela waliomba hela ya ndumu na mimi nikawa hata 100 ya kupanda gari za chanika sina, pia kwa wale waliokuwepo till 2000 wanakumbuka jamaa mmoja alikua anaitwa Mabagala? anakukimbiza hata ukiwa uchi.

Pale Bagdad washkaji walishanichukuliaga madikodiko....niliDROP kwenda street kufuata maji ya kunywa....maza mmoja kanifungia madikodiko....kufika pale washkaji wakamind kabidi niwaachie...kabakia najilamba vidole tu!
Umenikumbusha mabags....ha!ha!ha!...huya jamaa alikuwa navituko sana...eti akiwakuta mmelala wawili kitanda kimoja anaomba cheti cha ndoa....ha!ha! mibangi ilikuwa inamsumbua sana!
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Unawakumbuka walimu wafuatao?Mabagara,Wajimira,Nzoi,Msungu(marehemu),S econdmaster Swai(marehemu),Headmaster Mtera,Mama Mukuru,Mzee Mukuru,Makono(marehemu),Teti,Mkwiche,Grace Chuma,Mamiro,Mama Mtera,Mbulanya,Godfrey Wasiwasi,Kaunda(mwalimu wa michezo 1984-1988),Mzava,Chamuriro,Mugyabuso(marehemu),Bakari Mbonde(Ex-Rufiji Mp)n.k Orodha yao ni wengi sana,waliotangulia mbele ya haki Mungu awaweke mahari panapostaili, aaaammmmmmiiiiiiiiiinnnn.
The Following User Says Thank You to Amosam For This Useful Post:
Kila asubuhi mkondo mmoja lazima kuchota maji ya kupikia kila mwanafunzi ndoo sita kutoka Pondi,na jioni darasa lingine nalo huchukua nafasi.Kweli tunahaki ya kupata maisha tuliyonayo,Pugu wee acha tuuuuu.
The Following User Says Thank You to Amosam For This Useful Post:
Unawakumbuka walimu wafuatao?Mabagara,Wajimira,Nzoi,Msungu(marehemu),S econdmaster Swai(marehemu),Headmaster Mtera,Mama Mukuru,Mzee Mukuru,Makono(marehemu),Teti,Mkwiche,Grace Chuma,Mamiro,Mama Mtera,Mbulanya,Godfrey Wasiwasi,Kaunda(mwalimu wa michezo 1984-1988),Mzava,Chamuriro,Mugyabuso(marehemu),Bakari Mbonde(Ex-Rufiji Mp)n.k Orodha yao ni wengi sana,waliotangulia mbele ya haki Mungu awaweke mahari panapostaili, aaaammmmmmiiiiiiiiiinnnn.
Hapo kny bold sio Juma wasiwasi....mzee wa midevu na mtaalam wa Lugha na ushairi.....nywele zake alikuwa anapaka black....! Du hao marehemu hata sikuwa nimesikia habari hizo isipokuwa Msungu (RIP).....!
Kuna mwingine alikuwa anitwa Juma....huyu alikuwa anadeal na misosi.....ha!ha!ha! mtaalam wa mambo ya MNAZI....kazi kwelikweli!....Hujalipa ada....no Kidishi cha msosi!
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Aksante kwa kutukumbusa mambo ya DOCEBIT VOS OMNIA,Naomba wadau wa kilatini watukumbushe maana yake,Kilichonifurahisha mbali na kukosa maji ni Muhogo wa mzee wa shamba na sitantasahau siku ambayo mzee wa shamba alimcheza ngoma mwanae,Mchiriku mpaka asubuhi ilikuwa raha sana na kitu kingine ni siku ambayo Mkuu wa shule alikuja Morning assemble na kutangaza namna hii ninanukuu.""Nimeenda wizarani,hamna pesa na shule inafungwa kuanzia leo sababu hakuna chakula"" Ilikuwa may katikati tukalrudi nyumbani na na shule ikafunguliwa July mwishoni.
Ilikuwa shida sana.
Aksante kwa kutukumbusa mambo ya DOCEBIT VOS OMNIA,
PONDUS DEUS MEUM.....unalikumbuka na hili?
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Juma Wasiwasi vipi yupo? mara ya mwisho nilisikia alikuwa anasoma Open University or UDSM. Jamaa alikuwa na misemo ya kutukana, aliniboa pale alipochukua TV ya shule akaweka nyumbani kwake.....watu walipiga kelele lakini jamaa wapi harudishi.....kelele zilipofika mbinguni akaona noma akairudisha
__________________ It's been long since I've lost all fears and concerns. I don't worry, I calculate