| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 502
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Lugha ninayojua ni "akifanya hivyo atakiona cha mtemakuni". Ninaelewa ni kama tishio au onyo: akifanya kitu kisicho halali ataona matokeo yake yaani atapata adhabu.
Mtemakuni (pia: mtema-kuni au mtema kuni) ni mtu anayepasua miti kuwa kuni. Kwa hiyo ana kazi nzitonzito pia ni watu wenye nguvu ya kimwili. Maana neno "kutema" hupatikana kwa maana mawili moja ni "kutema mate" mengine ni "kupasua kitu" kama ubao, miwa n.k. Sina uhakika juu ya asili ya usemi lakini nimeielewa hivyo: Hawa watemakuni ni watu wenye nguvu wanajua kuadhibu. Ukitaka kuiba kwao utaona jinsi gani wanavyoweza kujitetea. - au labda pia: Watemakuni ni watu wanaoishi katika mazingira magumu msituni wakifanya kazi hii nzito heri usijaribu kucheza nao... Sijui wenzangu wanaonaje? |
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Nashukuru sana ndugu yangu, si haba, iatabidi niende BAKITA pia kujiridhisha.
Hapa inaoneka wengi wetu huwa tuna tumia misemo tusiyojua asili yake!
__________________
Heri kupendwa na mwenye akili mmoja, kuliko kupendwa wapumbavu maelfu! |
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
BAKITA unataka kuuliza namna gani? Je wanao ukurasa mtandaoni unapoandika maswali?
|
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Ntakwenda mzimamzima ofisini kwao, ninashida sana na hii kitu ndugu yangu nina kazi nayo. Sidhani kama watakosa ufafanuzi juu ya msemo huu. Kama unakingine cha kunisaidia, sema ndugu yangu.
__________________
Heri kupendwa na mwenye akili mmoja, kuliko kupendwa wapumbavu maelfu! |
|
#6
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Mzizi wa Mbuyu nimekupata mkuu ngoja nichangie kidogo; Mimi hili nilipata simulizi toka kwa jamaa mmoja wa Kenya ambae anasema kuna mwalimu aliwasimulia shule ya msingi juu ya kisa cha mtema kuni. Hiyo hadithi inasema hivi:
Siku moja jamaa mtema (mkata) kuni alienda porini kukata kuni. Sasa akakuta mti mkubwa umeanguka na umekauka vizuri, ambao wenyeji wanaupenda sana kwa kutumia kwa vile kuni zake hazitoi moshi n.k. Sasa huyo mtema kuni akaanza kukata kuni na kurundika mzigo mkubwa tu. Jua lilipozidi kuwa kali jamaa akavua nguo akabaki uchi (hakutarajia mtu kutokea maeneo hayo kwa vile ni mbali na makazi ya watu) huku akiendelea na kupasua kuni toka kwenye lile gogo. Ikatokea jamaa akawa amechoka na pia jua kali, kwa hivyo akaamua kukaa juu ya lile gogo kupumzika. Sasa lile gogo lilikuwa lina ufa (kutokana na kutanuka kwa jua kali), kwa hivyo nyanya zikawa zimening'inia kwenye huo ufa. Baada ya kitambo kirefu kupita, jua nalo likawa linazama; kwa hivyo jamaa akaamua kunyanyuka ili ajitayarishe kuondoka. Sasa kumbe lile gogo lilikuwa limeshaanza ku-contract (kusinyaa); kwa hiyo nyanya zikashindwa kutoka. Jamaa wakati anakukuruka, huku contraction ya gogo inaendelea taratibu; jamaa akajikuta immediate options zimekauka kwa vile hakuweza kujinasua na shoka lilikuwa mbali hivyo hawezi kuzikata nyanya ili atoke. So, jamaa ndio akafia pale juu ya gogo baada ya mateso ya muda mrefu, kwani hata kelele alizopiga hazikuweza kusikika kijijini ambako palikuwa mbali. Kwa hivyo, ndugu, jamaa na marafiki walipomtafuta ndio wakamkuta jamaa amejifia juu ya gogo na nyanya zimenasa ndani ya gogo....! Kwa hivyo ikaonekana ni mateso makubwa mno mtu anayoweza kuyapata, so watu wakawa wanafanya reference kwamba ukifanya jambo baya/ukaidi n.k then utakiona cha mtema kuni Poa mkuu nipe thanks....
__________________
It's been long since I've lost all fears and concerns. I don't worry, I calculate Last edited by Kwetunikwetu; 17th June 2009 at 10:36 PM.. Reason: Rephrasing |
|
#7
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mtemakuni hakika ni mpasuaji au mkataji wa kuni kama wengine walivyosema. Hadithi ya mkatakuni wengine wanasema wakati akikata kuni alikosea mahesabu (umakini)shoka likatua kwenye mguu likampasua na kumjeruhi sana. Kwa hiyo, kukiona cha mtemakuni ina maana ya kujiingiza kwenye shida ya kujitakia, ni kukosa umakini katika kutenda jambo ambapo baadaye mtu anakuja kujuta kutokana na shida atakayoipata. Kumbe, ni msemo wa onyo, wa kumtaka mtu awe mwangalifu ili mabaya yasimkute. Ni msemo unaotaka seriousness ya mtu katika kutenda ili kujiepusha na matokeo mabaya.
|
|
#8
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Bonge la elimu hii, tumeelimika wengi!
|
|
#9
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Poa, lakini kweli pia ntakwenda BAKITA, nikipata muda kuchunguza jambo hili.
__________________
Heri kupendwa na mwenye akili mmoja, kuliko kupendwa wapumbavu maelfu! |
|
#10
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Mi huwa nafahamu simulizi tofauti kuhusu ''kukiona cha mtemakuni'', sikuwahi kusikia pia hizo zilipoelezwa hapo juu.
Niliambiwa kuwa mtema kuni ni mtu anaekata kuni na alieenda kukata kuni porini na alipokuwa anataka kuzifunga kuni pamoja akawa anatafuta kamba, na bila kujua akamgusa nyoka akidhani ni kamba ili afungie kuni, loooo! kilichofuata ni mapambano... kwa hiyo hicho ndo kilikuwa ''cha mtemakuni'' nilichokifahamu. It is so intresting kuwa kuna simulizi tofauti tofauti kuhusiana na msemo uleule. Na nafikiri mambo kama haya yangehifadhiwa vizuri (yangekuwa well documented) ingesaidia kwa vizazi vijavyo hasa ukizingatia kiswahili kinakua sana sasa hivi ktk nch nyingi za Afrika.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 01:34 AM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||