ndio chuo kilicholifikisha taifa hapa lilipo.mafisadi wote ni product ya udsm.wahujumu uchumi ni product ya udsm hata maprofessor wenye tamaa ya uongozi wengi ni wa udsm
ndio chuo kilicholifikisha taifa hapa lilipo.mafisadi wote ni product ya udsm.wahujumu uchumi ni product ya udsm hata maprofessor wenye tamaa ya uongozi wengi ni wa udsm
hata wapuuzi kama Magulubaja Chemba!
kingxvi wamekutosa kwenye interview nini? naona umejipanga kuchafua hali ya hewa! tuliza munkari, sasa unashauri nini? chuo kifungwe au..
Most discoveries happened by accident!
moja ya research organisation yakijinga duniani inaitwa REDET makao makuu yake yapo wapi pale?
Not researched! Bye bye
If Life gives you lemon, change it to Lemonade.
Ufisadi ni tabia ya mtu hauhusiani na chuo ulichosoma,kwanza by then ndiyo kilikuwa Chuo kikuu pekee Tanzania so kwa msomi yeyote aliyesomea ndani ya nchi ilikuwa lazima asome pale,chuo kikuu cha pili kilikuja mwaka 1984 tena ilikuwa ni college ya UDSM ndiyo ikapandishwa hadhi kuwa Chuo kikuu cha Sokoine (SUA).
mmh inaonekana mleta hoja aliomba hapo UDSM akapigwa chini ......he he he he
Ndugu yangu mpendwa. Kama kweli wewe ni Mtanzania, nakuomba kwa moyo wangu wote utafute Kitu kingine cha kutukana na kudharau.
Mimi Highlander nimeona vyuo vingi kiasi kwa kuvitembelea, na vichache kukalia viti vyake. Nitaje W(V)its Afrika Kusini, Nairobi University, na vingine nje ya bara letu la Afrika. Sifa ya usomi bado sijaifikia, lakini sifa ya ujuzi wa kuona ninayo--tena sana tu.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja katika Vyuo Vikuu vizuri sana katika Bara letu, na Namshukuru sana Mungu nilipata idhini ya kusoma pale katika miaka ya karibuni. Nimewaambia watoto wangu na marafiki zangu wa karibu nikipelekwa kaburini sasa, baada ya kupitia UDSM naenda kwa amani huko roho yangu itakoenda.
Kule Fillipines walikuwapo mafisadi wawili wakiitwa Marcos. Wale walisona UDSM? Pale Cairo pametokea fisadi mmoja akiitwa HOSNI Mubaarak. Yule alisoma UDSM? Kule Marekani kuna fisadi mmoja akiitwa Oliver North alikamatwa akibwiya hela katika kashfa ile ikajulikana kwa jina la The Iran Contra Affair. Yule alisoma UDSM?
Ufisadi haufundishwi katika Chuo chochote. ukweli ni kwamba roho ya wizi wa mali ya umma au mtu yeyote mwingine ni Mama yako mzazi na baba yako ndio wanaokufundisha utotoni kwa values wanazokuonesha. Wezi wa mali ya umma katika Tanzania wametokana na cultural traits za nchi, kuanzia nyumbani, jinsi ileile wezi katika nchi nyingine walivyolelewa na culture--hasa makuzi--kutokuogopa mali ya umma. Blame the culture; not UDSM. Unataka kuniambia wahitimu wote wa Sokoine, IRDP, Mzumbe, kile chuo cha mashushushu wezi kule Kigamboni, IFM na vingine hawamo katika wezi wa mali ya umma katika nchi hii? Inawezekana kabisa wewe ni mtu mwenye bifu fulani na UDSM. Pengine ulishindwa kukidhi vigezi wakakutolea nje na sasa unatafuta kuchafua chuo kwa chuki zako binafsi.
Nimepita pale nikakuta slogan moja naipenda sana: ELIMU KWANZA! Jitahidi popote ulipo jisomee upate grade nzuri watakupokea tu--Kama si katika digrii ya kwanza, kamia kuingia katika ngazi ya Uzamili, au Uzamivu.
Sema Moyoni mwako, Elimu Kwanza utapokelewa.
Hoja za kitoto..mimi nimesoma Mzumbe University, isipokuwa hoja kama hizi ni utoto na kukosa kazi.
"Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
"Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"
Follow Us Here