Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Taarifa kutoka kwa wanafunzi nchini algeria.........

    Report Post
    Results 1 to 7 of 7
    1. #1
      mzee wa njaa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2011
      Posts : 1,340
      Rep Power : 669
      Likes Received
      194
      Likes Given
      107

      Default Taarifa kutoka kwa wanafunzi nchini algeria.........

      Sisi ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza tunaosoma nchini Algeria kutoka Tanzania,tumeamua kutuma taarifaa hizi katika vyombo vya habari kuhusu bodi ya mikopo yaani kuhusu utumaji wa pesa kwetu sisi
      YALIYOMO
      · Ahadi za kutuma pesa
      · Utumaji wa akaunti
      · Maisha tunayoishi sasa
      · Utumaji wa pesa usiokamilika
      · Madeni
      · Jitihada za viongozi
      · Matatizo




      Ø AHADI ZA KUTUMA PESA
      Tarehe 8 /10/2011 tulipokuwa tunajiandaa na safari ya kuja nchini Algeria tulikabidhiwa asilimia 50 ya mkopo na kuhaidiwa kwamba tutamaliziwa asilimia 50 iliyobaka baada ya miezi sita mara baada ya kuwatumia akaunti zetu
      Ø UTUMAJI WA AKAUNTI
      Ufunguaji wa akaunti ulikamilika 4 /4/2012 na kutumwa katika wizara ya elimu na bodi ya mikopo.Tangu kutumwa kwa akaunti hizo tulitegemea kwamba pesa zingetumwa mara baada ya wiki mbili lakini mpaka sasa tarehe 4/6 /2012 pesa hazijatumwa na ni takribani miezi miwili
      Ø MAISHA TUNAYOISHI
      Kutokana na kutokuwa na pesa tunaishi maisha magumu mpaka tunalazimika kukopa kwa kaka zetu na watu wamataifa mengine kwa kiasi tofauti wengine ni euro 500 na kuendelea kuwaahidi kwamba tutawalipa mwezi wa tano mwanzoni na mpaka sasa bado hatujalipa madeni hayo na watu wanatishiwa kupelekwa polisi
      Ø MADENI
      Watu walilazimika kukopa pesa kwa sababu zifuatazo
      v Gharama za chakula
      v Gharama za usafiri
      v Malazi
      v Matibabu
      v Stationary
      v Mawasiliano
      Na vitu vyote hivyo ni ghali sana katika nchi ya Ageria na tunaishi kwa mashaka kwa sababu ya kudaiwa madeni na hatuwezi kukopoa tena kwa sababu hatuaminiwi tena
      Ø JITIHADA ZA VIONGOZI
      Tangu kutumwa kwa akaunti hakukuwa na taarifa zozote viongozi wa chama cha wanafunzi wanaosoma Algeria (ATSA)Walifanya mawasiliano na viongozi wa bodi ya mikopo na kupewa taarifa zisizo rasmi mpaka mwezi wa tano, na baadae waliahidi kutuma pesa katikati ya mwezi wa tano lakini hazikuweza kutumwa mpaka tarehe 27/5/2012 ,ndipo tulipopata taarifa kwamba pesa zitatumwa tarehe 1 /6/2012 Lakini hazikutumwa mpaka leo hii
      Ø MATATIZO
      v Watu hatuna pesa na tulizokopa zimeisha
      v Tunadaiwa na hatuwezi kukopa tena
      v Tunaweza kupelekwa polisi kwa kutolipa madeni
      v Kuna wagonjwa na hatuna pesa za kuwaudumia kwa matibabu
      v Dada zetu wapo katika mazingira magumu kiasi kwamba wakati wowote wanaweza kufanya maamuzi na mambo tofauti na yaliyowaleta huku
      v Tumefikia hatua mpaka ya kuuza mali zetu kwa bei ya HASARA.
      v Tuna msongo mkubwa wa mawazo ambao umesababisha kutokuelewa masomo
      UTUMAJI WA PESA USIOKAMILIKA.
      · 8/10/2011, Bodi ya mikopo ilitupatia pesa kwa mafungu mafungu na kusababisha wengine kuja baada ya mwezi 1.Tuna wasiwasi ya kuwa jambo hili litajirudia tena kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara.mfano 2011 Tumekuja makundi 3 pasipo sababu za msingi.
      · Tunaomba uhakika ya kuwa wote tutatumiwa pesa haraka sana.Jumla tupo wanafunzi 56 wa mwaka wa kifaransa nchini ALGERIA.


      MADHARA YATAKAYO TUPATA KAMA HATUTOPATA PESA MPAKA 8/6/2012
      · TUTAKOSA CHAKULA.
      · TUTAKOSA MALAZI.
      · TUTAKOSA USAFIRI.
      · TUTAKOSA VIFAA VYA KIMASOMO&MITIHANI.
      · TUNAWEZA KUPELEKWA POLISI KWA SABABU TUNADAIWA PESA NYINGI NA MUDA TULIOAHIDI KULIPA MADENI HAYO UMESHAPITA ZAIDI YA MWEZI MMOJA.
      · TUTAKOSA HUDUMA YA MAWASILIANO.
      · HATUTOAMINIWA TENA KWA SABABU HESLB WAMESABABISHA TUVUNJIWE UAMINIFU.
      · DADA ZETU KUFANYA KINYUME NA KILICHOWALETA ALGERIA ILI KUPATA PESA.
      · WIZI WA MALI ZA WATU WATU ILI KUPATA PESA.
      Hayo ni baadhi tuu.Je serekali ilituleta kwa ajili ya hayo?


      MAPENDEKEZO YETU
      · Vyoombo vya habari mtusaidie kuanzia sasa mpaka tutakapopata pesa zetu haraka sana.
      · Vyombo vya habari mtusaidie jambo hili mpaka kufika mwisho.
      · Hatuhitaji kudanganjwa na BODI YA MIKOPO kwa sababu kabla hatujaja WALITUNDANGANYA na mpaka sasa wanatudanganya.
      · PESA tunataka tutumiwe watu wote 56 na asiwepo hata mmoja wetu atakayecheleweshewa.
      · Tunaomba vyombo vya habari vitupatie taarifa za KWELI kila wakati ili tujue&tuwe na nguvu.
      Nakala kwa:
      Bodi ya mikopo Tanzania
      Wizara ya elimu Tanzania
      Ofisi ya waziri mkuu Tanzania
      MAWASILIANO YETU
      [email protected], Tel +213551867346
      [email protected]

    2. Miaka 50

    3. #2
      MJIMPYA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2011
      Posts : 326
      Rep Power : 478
      Likes Received
      125
      Likes Given
      63

      Default Re: Taarifa kutoka kwa wanafunzi nchini algeria.........

      Hawa hata mpangilio wa barua ni tatizo,
      Vijana hata kama ni haki yenu jifunzeni jinsi ya kuandika barua yenye staha na hoja,

      Nawatakia heri ombi lenu lipate majibu haraka.


    4. #3
      mzee wa njaa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2011
      Posts : 1,340
      Rep Power : 669
      Likes Received
      194
      Likes Given
      107

      Default Re: Taarifa kutoka kwa wanafunzi nchini algeria.........

      Quote By MJIMPYA
      Hawa hata mpangilio wa barua ni tatizo,
      Vijana hata kama ni haki yenu jifunzeni jinsi ya kuandika barua yenye staha na hoja,

      Nawatakia heri ombi lenu lipate majibu haraka.

      Issue sio barua ila matatizo yao. Kwani hawajaeleweka?

    5. #4
      Sting's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd June 2011
      Location : Mafichoni
      Posts : 671
      Rep Power : 534
      Likes Received
      131
      Likes Given
      45

      Default

      Quote By MJIMPYA
      Hawa hata mpangilio wa barua ni tatizo,
      Vijana hata kama ni haki yenu jifunzeni jinsi ya kuandika barua yenye staha na hoja,

      Nawatakia heri ombi lenu lipate majibu haraka.
      Hujaelewa kwani???
      Barua imeeleza kila kitu kwa kirefu, ulitaka iweje???

    6. #5
      Billie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th August 2011
      Posts : 1,741
      Rep Power : 802
      Likes Received
      444
      Likes Given
      186

      Default

      Quote By Sir. Burn
      Hujaelewa kwani???
      Barua imeeleza kila kitu kwa kirefu, ulitaka iweje???
      Inaelekea alitaka ianze na neno YAHUSU:BOOM LETU SISI HUKU TWAFA akute na neno kili of kwani wametuma ije kusahishwa huku wameshasema wana msongo wa mawazo wee umeng'ang'ania mpango wa barua kwani ni tatizo gani halijaeleweka hapo juu.Anyway mi ndo maana niligoma kwenda huko hayo ndo madhara ya sera mbovu za nchi yetu haswa kwenye sector nyeti kama hii(elimu)

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      usernom's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 6th June 2012
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Taarifa kutoka kwa wanafunzi nchini algeria.........

      He! hii haikua barua, hii ni taarifa hata ingekua ni two lines. vp kama wewe mjimpya ungekua na mtoto kule ungeongea hayo? nadhani ulipaswa kwanza kuwaonea huruma wako ugenini na kuwatia moyo. Lets be wise.

    9. #7
      The_Emperor's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2012
      Posts : 472
      Rep Power : 455
      Likes Received
      41
      Likes Given
      0

      Default Re: Taarifa kutoka kwa wanafunzi nchini algeria.........

      Kila lenye mwanzo halikosi mwisho[/QUOTE]

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...