Leo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi hapa katika chuo kikuu cha Dodoma lakini kwa jinsi ambavyo mwenendo wa uchaguzi ulivyokwenda hakika inasikitisha sana, hapa nazungumzia kwenye college ya Social science and humaties
kuanzia katika uundwaji wa tume mambo yalianza kufumuka mara baada ya kugundulika katika tume ya watu kumi wajumbe tisa ni waisram, wapiga kura walitulia na hawakuona tatizo kumbuka tume hii imeundwa na spika Issa mohamed baada ya rais na makamu wa rais kuwa wamefukuzwa chuo tangia mgomo uliopita, mambo hayakuishia hapo wakati wa uchukuaji fomu nafasi ya urais walichukua watu wanne wawili waisramu na wawili wakristo na ubunge watu 56 wakristo 33 waisram 23 tatizo likaja mara baada ya tume kukaa na kuanza kuchambua wagombea katika ngazi ya urais wakristo wote wakatolewa na kubaki waisram 2 na ubunge waisram wote 23 wote wakapita pamoja na wakristo 17 ili kutimiza idadi ya wagombea 40. Mgombea urais bwana Nzamba Nasser aliamua kukata rufaa na bodi ilipokaa na kupitia hoja zake ikaamua kumrudisha na hivyo kutimiza wagombea 3 wa urais lakini cha kushangaza masaa takribani 12 ya uchaguzi kufanyika tume ikamwondoa tena bila hata kutaja sababu yeyote hasira kwa watu ziliongezeka kwani jamaa ndio alikuwa chaguo pekee hivyo kusababisha watu kupiga kura kwa hasira huku wengine wakisusia uchaguzi na wabunge wengine kuamua kujitoa kwenye uchaguzi hasa wa post za ubunge. Mara baada ya kura kuhesabiwa rais bwana Idd Muhammad amepatikana kwa kura 189 dhidi ya mwenzake bwana Zuberi aliyepata kura 81 huku kura zaidi ya 3000 kuharibika kwa watu kuandika kwamba wote hawafai huku zaidi ya 6000 hawakupiga kura kwa madai hawamwoni mtu wa kumpigia kura na wabunge kupatikana wengine kwa kura 10 na wengine hata chini ya hapo
mytake
kwa hali iliyopo udom panatisha kwani ukijaribu tu kuhoji PT 562 inakuja kukuchukua hivyo bora week 3 zilizobaki ziishe haraka tuondoke

Reply With Quote

Follow Us Here