Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Lugha gani itumike kufundisha katika taasisi zetu za elimu: Kiswahili au Kiingereza?

    View Poll Results: Lugha gani inafaa itumike sekondari kwa maslahi ya taifa?

    Voters
    68. You may not vote on this poll
    • Kiswahili

      33 48.53%
    • Kiingereza

      35 51.47%
    Multiple Choice Poll.
    Report Post
    Page 1 of 5 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 88
    1. #1
      Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 3,917
      Rep Power : 6962
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      35

      Default Lugha gani itumike kufundisha katika taasisi zetu za elimu: Kiswahili au Kiingereza?

      Wajemeni, kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala nchini mwetu kuhusu lugha ya kufundishia. Hali ilivyo sasa ni kuwa, watoto wanajifunza kwa lugha ya Kiswahili hadi darasa la Saba. Baada ya hapo, lugha inayotumika katika ngazi ya sekondari hadi chuo kikuu ni Kiingereza. Hata hivyo, ukweli ni kwamba vijana wengi wanaomaliza katika taasisi zetu za elimu kuanzia sekondari hadi chuo kikuu hawakimudu kiingereza kama lugha ya mawasiliano. Lakini ni kweli pia kuwa kama lugha ya kitaaluma, kwa kuangalia kigezo cha kufaulu katika mitihani, vijana wetu hawana tatizo kubwa na lugha ya Kiingereza maana wanafaulu tu vizuri tena siku hizi wanafaulu kwa kiwango cha juu zaidi kuliko zile enzi sisi tukisoma.

      Matatizo ya vijana wetu kutokumudu Kiingereza kama lugha ya mawasiliano yameletekeza baadhi ya watu hasa wanazuoni kupendekeza kuwa tutumie lugha ya Kiswahili katika kufundisha hadi chuo kikuu.

      Kwa maoni yangu, kwa kuachana na kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika taasisi zetu tutawanyima fursa kabisa watanzania angalau kujua kiingereza cha kuombea maji. Ningependekeza kuwa Lugha ya Kiingereza iendelee kuwa lugha ya kufundishia, lakini tuanze mapema zaidi katia ngazi ya shule ya msingi. Ifikapo katika ngazi ya sekondari, tuwe na aina mbili za mitaala, moja unaotumia Kiswahili na mwingine Kiingereza. Wazazi na wanafunzi wapewe uhuru wa kuchagua kuendelea na masomo kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza. wale wanaamua kujifunza kwa Kiingereza wafundishwe sio tu Kiingereza, lakini Kiingereza kizuri!

      Nini maoni yako. Tujadili.
      A Struggle Without Casualties is No Struggle-Steve Biko

    2. Miaka 50

    3. #2
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,041
      Rep Power : 1246
      Likes Received
      16
      Likes Given
      106

      Default

      Mimi nadhani tatizo tulilonalo sio lugha bali ni ufundishaji na mazingira yenyewe ya kufundisha na kujifunza pamoja na mitaala/syllabus ya inayofundishwa.


      Kwa hiyo mpaka tutakapojua kiini cha matatizo hayo na ufumbuzi wake ni nini ndio tuanze kuangali masuala ya lugha ya kufundishia.

      mwanasiasa

      Iwapo kama lugha ya kufundishia ndio tatizo then kuwapa wanafunzi uwezo wa kuchagua wasome kwa englisha au kiswahili ni sawa na kuwaambia wengine wasome na wengine wasisome. Iwapo lugha ndio tatizo basi iwe lazima wote wasome kwa lugha moja.
      KILITIME likes this.

    4. #3
      Kulikoni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2006
      Posts : 434
      Rep Power : 737
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default tusiwe njia panda

      Mwanasiasa

      Nakubaliana nawe kuwa huu ni mjadala muafaka kabisa unaolenga kuangalia mustkabali wa vijana wa taifa letu.

      Nimebahatika kufanya kazi au kwa kusafiri au kwa kuwa stationed sehemu nyingi duniani na nimeshuhudia maeneo yote mawili, i.e. yale mataifa yanayozingatia lugha ya taifa kama medium of instructions across the board na yale mataifa ambayo kwa nafasi yao yanatumia lugha ya kimataifa ie. kifaransa, kireno nk

      I can confidently say kwamba lugha ni njia nzuri sana ya kujifaragua katika uwanja wa dunia kisiasa na kiutamaduni na very beneficial kwa mataifa makubwa ku-exert influence over smaller nations kwa kujaribu kuweka lugha zao kwenye nchi husika.

      Unfortunately Tanzania yetu of which I am mzalendo to the core licha ya kuwa tunajifaharisha na kiswahili lakini mafanikio katika ngazi ya kimataifa kikazi nk hayajawa upande wetu, from the outset hatukuweka mkazo na tulikuwa njia panda.

      Hii kuweka lugha ya kiswahili msingi then secondary kuna kuwa na automatic switch to english imewakanganya wengi matokeo yake yamekuwa kiingereza hatukimudu vyema na kiswahili hatufaidiki.

      Nimekutana na walimu wa kiswahili kutoka kenya sehemu nyingi duniani na ni kenya ndio yenye mkataba hivi sasa wa kufundisha kiswahili nchini Ethiopia, Tanzania kiswahili ni lugha y taifa lakini hapa tumeliwa na ni solely because lugha yetu tumeiweka njia panda, tumeipa half importance!

      Sasa to cut the long story short nadhani tunahitaji kuwa na msimamo thabiti kwamba kiswahili ni lugha ya taifa basi iwe ni kiswahili across the board au kama ni kiingereza basi iwe hivyo right from vidudu.

      Tuna nafasi ya kujifunza lugha zote mbili sambamba, kiswahili home na kizungu as official medium of instruction.

      I prefer kiingereza zaidi kwa vile bado hatujafikia pahala pa kuwa strong enough to export Kiswahili to the world on a mass scale.

      Sikubaliani na hoja ya kuwa na options kwani hiyo ni unwanted compromise ambayo itaturejesha kule kule kwenye msingi kiswahili, secondary kiingereza!

      Sambamba na hayo naomba niongeze kwamba the way the world is going two things will make our young graduate stand out from the crowd:


      1. Multi Skills
      2. Multi Lingual

      Meaning kwamba the more skills you have the better regardless how small, mfano a graduate with a driving license ni more employable katika private sector kuliko the one without, similarly mtu mwenye kujua lugha zaidi ya moja anaajirika kirahisi kuliko mwenye uchache wa lugha.

      Imagine vijana wakiibuka toka chuoni wakiwa ni graduate wenye kujua accounts and law na kuongea kiingereza na kifaransa au kijerumani na kiarabu...

      Huu utaratibu wa lugha ndio jambo muhimu kulisimamia kwa sasa na ni vizuri kuwa sasa tunaanzisha idara ya kiswahili chuo cha dodoma ili kuweza kukiuza kiswahili na baadae lugha nyingine hazina budi kuanzishwa...

      Mungu ibariki tanzania..
      If you want to judge a leader, look at the organization ten years later.
      Kyoma is offlinestyle="display:none;visibility:hidden;" data-cfsrc="template/JamiV1/default/misc/progress.gif" alt="" /> Reply With Quote

    5. #4
      Kyoma's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd June 2006
      Location : Mfugwa Mbwa
      Posts : 125
      Rep Power : 689
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Mzee Mwanasiasa, Heshima yako Baba!

      Niliwahi kusoma mahala kwamba “kujua Kiingereza sio kujua au kuwa mtaalamu katika eneo lako la kazi”. Ingawa hii dhana ina utata, lakini hakuna ubishi kuwa kujua kiingereza sio sifa ya ubora. Kama zilivyo lugha nyingine, Kinyamwezi, Kihaya, au kisukuma, Kiingereza ni chombo cha mawasiliano kwa wanajamii. Ikiwa Kiingereza ni lugha yako ya kwanza (mother tongue), au jamii uishimo ndio lugha inayotumika, huna budi kukiongea na kukiandika bila matatizo yoyote hata kama sio kwa ufasaha. Kwa mantiki hiyo, haimaanishi wewe ni bora au mtaalamu wa fani yoyote.

      Hata hivyo, nadhalia ya kudhani kwamba lugha na fani ya mtu vinaweza kutenganishwa inahitaji uchanganuzi kidogo. Lugha ya fani yako ni sharti uijue. Aghlabu, mojawapo ya muhimili mkubwa katika fani ya Uandishi wa habari ni umahiri wa kumiliki lugha. Kama wewe ni mwandishi wa habari, na Kiingereza ndio lugha ya mawasiliano katika jamii yako, yakupasa kukiongea na kukiandika kwa ufasaha. Haipendezi kuona mwandishi wa habari wa gazeti la kiingereza amebeba bango la msisitizo kuwa hajuhi kiingereza lakini anaijua fani yake.

      Ingawa ubora wa vielelezo vya ushaidi na uelewa wa sheria katika jamii husika ni nyenzo muhimu kwa Mwanasheria, pia, uwezo wa kumiliki lugha ya mawasiliano kwa maandishi au kujieleza ni nguzo kubwa katika fani ya Sheria. Mwanasheria anajua ni wakati gani atumie lugha ya mafumbo na ni wakati gani atumie lugha inayoeleweka ili kumnusuru mteja wake. Mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Mwansheria, Wazee wa Mahakama, na Mahakimu yana athari zaidi ya kumtumia mkalimani. Lugha ni rafiki mkubwa wa mwansheria. Kama Kingereza ndio lugha ya mawasiliano ndani ya jamii husika, ni vema kutokuitenganisha na fani ya Sheria.

      Historia ya mwanadamu, na maendeleo ya jamii aishimo, vina mahusiano ya moja kwa moja na matumizi ya lugha kama chombo cha mawasiliano baina ya wanajamii. Watu wa mataifa kama ya China, Ujerumani, Urusi, Uajemi, Japan, Marekani, na mengine mengi, wanatumia lugha zao kama chombo cha mawasiliano, na ndizo hizohizo wanazotumia kupata utaalamu katika fani zao.

      Binafsi, sidhani kama mjadala wa matumizi ya Kiingereza ndani ya mfumo wetu wa Elimu unapewa uzito unaostahili. Si vema kuendelea kuukwepa mjadala huu, kwa sababu Kiingereza ndio lugha ya mawasiliano itumikayo kutupatia utaalamu katika fani zetu. Kuna nyenzo mbili za kutilia maanani. Mosi, Utaalamu katika fani yoyote, na pili, Lugha, ambacho ni chombo kinachotumika kuingiza huo utaalamu kwenye ubongo wa mtu.

      Kwa mfano, Mchina anajifunza utaalamu katika fani yoyote ile ambao haujuhi, kwa kurahisishiwa na lugha yake ya msingi ambayo ni Kichina, ambayo tayari imeimarika ndani ya Ubongo wake. Si haba kumkuta Mchina mahala ambapo lugha ya mawasiliano sio Kichina bali ni Kiingereza kama ilivyo Marekani, akitafuta neno la kiingereza kwa dakika kumi au ziadi kuelezea ujuzi anaoujua tayari kwa lugha yake.


      Kinyume, Sisi watanzania tunajifunza vitu vyote viwili ambavyo ni vigeni kwetu kwa wakati mmoja. Tunatakiwa kuelewa Utaalamu ambao ni kitu kipya. Hata Kiingereza ambacho ni chombo kinachotumika kuingiza utaalamu huo katika bongo zetu, ni Lugha mpya, yaani sio Lugha yetu ya kwanza na wala si Lugha yetu ya Msingi.


      Tukiondoa kasumba ya kupima fukuto la joto la Dar es Salaam, na kuvitumia vipimo kama kigezo cha uwakilishi wa joto la nchi nzima, tutakubaliana kwamba, asilimia kubwa ya watanzania, lugha zao za kwanza si Kiswahili wala Kiingereza bali ni zile za asilia. Njia ya kufikiri na kutafakari, mawazo, ubunifu, majina ya vitu, hadithi, simulizi, utamaduni, na vitu vingine vinavotumika kukuza ubongo wa mtoto toka azaliwe mpaka umri wa kwenda shule, vinapokewa na mtoto kwa lugha ya kichaga, kisukuma, kiehe, Kimakonde, Kizalamo, na lugha nyingine za asili.

      Mara mtoto anapoanza shule, mambo yote yanabadilika ghafla na sasa lugha ya msingi inakuwa Kiswahili. Lugha inayojenga msingi wa kuingiza utaalamu katika ubongo wa mtoto wa Kitanzania inaanza kuwa Kiswahili, ambayo si mpya, bali haitumiki majumbani mwa familia nyingi za Kitanzania. Huu ndio unakuwa msingi wa fani ya mtoto. Habari njema ni kwamba ubongo wa mtoto mdogo, una sifa na umaridadi wa kuzinasa lugha zote zinazokatiza mbele yake, na kuziongea bila matatizo yoyote. Habari mbaya ni kuwa uwezo wa mtoto kuzinasa lugha unafifia kadili umri wake unavyozidi kukua. Umri wa kuanza shule kwa watanzania walio wengi unakinzana na umaridadi wa kuzinasa lugha.

      Kadili mtoto anavyopanda kimadarasa, ndivyo uwezo wa kuelewa lugha mpya unavyozidi kufifia, na ndivyo anavyozidi kujiimalisha katika lugha ya msingi. Sifa ya lugha ni matumizi yake. Ili uweze kuimiliki lugha yoyote ile duniani, yakulazimu kuiongea, kuisoma, na kuiandika. Pamoja na ukweli kuwa ukali wa kunasa lugha unakinzana na umri wa mtu, ubongo wa mtoto anayeanza darasa la kwanza kwa wastani wa umri wa miaka saba, bado ni mchanga, Kwa vyovyote vile, tunaufungua ubongo mchanga na kuupa msingi wa lishe ya lugha ya Kiswahili kwa miaka saba mfululizo mpaka ukomavu wake, yaani anapomaliza darasa la saba akiwa na umri wa miaka 14.

      Lugha ya mawasiliano na kufundishia katika shule za msingi ni Kiswahili. Kiingereza kinafundishwa kama somo, na wala si lugha ya mawasiliano au kufundishia. Kibaya zaidi, shule zetu nyingi za msingi zina baadhi ya Walimu wa somo la kiingereza wanaoamini kwamba hawajuhi Kiingereza, lakini wanazimudu vizuri fani zao. Si haba, kukuta somo la Kiingereza linafundishwa kwa kuchanganywa na Kiswahili. Matamshi ya sentensi kama “past tense ya go ni went” si mageni kwa wanafunzi wa shule zetu za msingi. Kumwagia kidonda tindikali, sasa hivi Lowasa amekuwa mtambo wa butua butua, kwa maana ya kufyatua walimu kama matofali ya mchanga bila kuchanganya na simenti.

      Mtoto anapoingia Sekondari, anakuwa ameweka msingi wa fani yake kwa lugha ya kiswahili. Tunatarajia aanze kuimarika na kuongeza misamiati. Gafla, Kiingereza kinakuwa lugha mpya ya mawasiliano na ya kufundishia. Kiswahili ambacho ni lugha ya msingi, kinafundishwa kama somo. Mkinzano huu wa lugha, na uelewa wa fani zetu, unaleta ugonjwa wa Mkanganyano katika asilimia nzuri ya bongo za sisi watanzania.

      Mabadiliko ya ghafla ya lishe ya lugha kwa ubongo bila kuwa na shibe ya stamina ya lugha ya msingi yanaleta utapia mlo wa akili. Sio bongo zote zinaweza kula kila aina ya lugha kwa wakati wowote bila ya kucheuwa. Kinga ya kucheuwa ni kukalili na sifa moja kubwa ya kukalili ni kutokufikiri au kutokuwa mbunifu. Usahaulifu ni rafiki mkubwa wa haya majinamizi. Yeyote aliyetembelewa na hizi sifa, hata mvua zikamnyeshea na akajificha mpaka darini, ni nadra kumkuta ameelimika, ikizingatiwa kuwa elimu ni kitu kinachobaki kichwani baada ya kusahau yale uliyojifunza.

      Kila nchi duniani ina mfumo wake wa elimu na hakuna mzani unaoweza kutumika kupima uzuri au ubaya wa mfumo wa elimu wa nchi moja kulinganisha na nchi nyingine. Ugumu au urahisi wa maswali, kufaulu au kushindwa kwa waliowengi haviwezi kutumika kama kipimo cha ubora wa elimu. Kipimo cha maana cha mfumo wowote wa elimu duniani, ni jinsi unavyowasaidia watu wake kuyabadili mazingira yao yanayowazunguka. Kama wahitimu wa huo mfumo hawawezi kuyabadili mazingira yao binafsi na ya jamii waishimo, basi mfumo huo haufai.

      Binafsi, sio mshabiki wa kupendelea lugha moja zaidi ya nyingine kati ya Kiswahili na Kiingereza. Pendekezo langu ni kwamba lugha ya msingi iwe ndiyo lugha ya sekondari na vyuo vikuu. Msingi wa nyumba, lazima ufanane na nyumba unayotaka kuijenga. Haiwezekani kuporomosha hekalu la ghorofa 30 katika msingi uliokusudiwa kujenga nyumba ya chumba kimoja na Sebure. Msingi wa mawasiliano unaompa kijana kutoka darasa la kwanza mpaka la saba, lazima uendelezwe katika Sekondari na Vyuoni. Msingi maana yake ni kujenga kitu juu yake; Sekondari unayoijenga lazima ifanane na msingi wenyewe. Kiingereza hakifanani na Kiswahili ambacho ni msingi tunaojengewa.

      Nakumbuka kuwa miongoni mwa makusudio ya kutumia lugha ya Kiswahili katika shule za msingi yalikuwa kuhakikisha tunaimalika katika lugha iliyotukomboa, na kuondoa makombo yaliyosalia vichwani mwetu baada ya kumung'oa mkoloni. Pia, kuiunganisha jamii yetu, kwani maneno mengi ya Kiswahili yanatumika katika lugha zetu za asili. Suala lingine ambalo ilibidi liende sambamba na makusudio hayo, lakini halikutiliwa maanani, ni kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya ukombozi wa fikra, ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuneemesha hali za watanzania.

      Mojawapo ya kasumba alizotuachia mkoloni ni kumwabudu pamoja na mambo yake yote. Kitu chochote kizuri mpaka sasa kinaitwa cha kizungu. Lugha ya Kiingereza tukawaachia wasomi wetu wachache waliobahatika kuchaguliwa kuendelea na elimu ya juu. Kwa kufanya hivyo, lugha ya Kiswahili imebaki na sura ya kuiunganisha jamii, na tukategemea lugha ya Kiingereza ichukue nafasi ya kuleta ukombozi wa fikra na kuiendeleza jamii. Binafsi, nafikiri jukumu la kuleta ukombozi wa fikra linawahusu wanajamii wote. Ni vema uwepo uelewa wa lugha ya mawasiliano baina ya wataalamu (waandisi), mafundi wa kati (technicians), na wanajamii waliowengi ambao hawana ujuzi wowote. Kiingereza kimekosa nafasi miongoni mwa haya matabaka.

      Ukiacha wazee wetu ambao walisoma shule za msingi na sekondari zilizofundisha kiingereza, au walifunzwa na walimu wanoongea kiingereza bila matatizo yoyote, na matokeo yake wamejaliwa kuongea na kuandika lugha zote mbili kwa ufasaha yaani Kiswahili na kiingereza. Wahitimu waliowengi ambao hasa ni matokeo ya mfumo huu wa sasa ni msalaba kwa jamii. Idadi ya watu wanaotaka kutenganisha lugha na taaluma inaongezeka kwa kasi kubwa. Mfumo wetu unaendelea kuzaa vijana wa kisasa, wasioweza kuandika kwa ufasaha au kuongea sio tu kiingereza peke yake, bali hata Kiswahili.

      Bahati mbaya, kipindi hiki cha mageuzi katika jamii yetu kinahitaji waandishi kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Tumefungua milango; tunatoka nje ya nchi na wageni wanaingia nchini kwetu kwa kasi. Nani atawaandikia wanajamii wetu dhamiri iliyofichika ya hawa wageni? Nani ataweka katika kumbukumbu tamaduni zetu ili wageni wasiziharibu tena? Na nani atawaandikia wajukuu zetu uhalisi wa maisha ya huku ughaibuni?

      Historia ya mwanadamu inatuhasa kuwa tunasoma ili kujitegemea kifikra, kuwa wabunifu na la mihimu hasa ni kuyabadili mazingira yetu. Zamani Watanzania tulikuwa na majigambo kuwa elimu yetu ni bora kulinganisha na nchi nyingi duniani. Walioamini hivyo, sasa wanaachwa kwenye mataa. Mienendo ya makampuni ya kigeni siyo ya kufurahisha na haileti matumaini kwa jamii yetu. Hawa wageni wanakataa wasomi wetu eti kwa sababu hawajuhi lugha waliopatia usomi wao yaani kiingereza. Mkapa aliwahi kuulizwa akiwa Raisi wa nchi lakini majibu yake yalionyesha kuwa tatizo hili bado halina ufumbuzi. Kinyume na imani yetu ya zamani, makampuni ya kigeni yanaonekana kuvutiwa na watu waliosomea nje kuliko wale waliomaliza pale nyumbani.

      Mmomonyoko wa uwezo wa kufikiri katika tabaka la wasomi ndani ya jamii yetu ni mwanzo wa kusambalatika kwa jamii nzima. Kidogo kidogo tunaanza kupoteza hata utamaduni wetu kwa sababu ya udhaifu na ubabaishaji katika lugha zetu. Wahenga wa kihaya walisema kuwa "Olwaita embwa lugibanza enyindo" tafsiri isiyorasmi ni kuwa “kifo cha mbwa huanzia puani”. Ugonjwa wa mkanganyano wa ubongo umeenea katika sehemu nyeti za ujenzi wa jamii yetu. Hapa namaanisha kwenye vyombo vya habari, taasisi mbalimbali za serikali na watu binafsi, baraza la mawaziri, bungeni, mashuleni na sehemu nyingine. Ugonjwa wetu huu umeshika mahala pabaya, yaani sehemu ya ubongo.

      Ni sisi wagonjwa peke yake wa mfumo huu tunaoweza kuondoa aibu na kusimama kidete, ili mfumo mzima ufanyiwe ukarabati. Tuondoe kasumba vichwani mwetu za kudhania kuwa tukisema hatujuhi kiingereza basi hatutaitwa wasomi. Tutoke nyuma ya mapazia ya ubabaishaji na tutoe ushuhuda wa hali halisi zinazotusibu. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kunusuru kizazi kijacho. Tutakaa na kuchanga bongo ili tujue tatizo hasa ni nini.

      Kwanini tusifanye kama Cameroon ambao wanatumia lugha zote mbili bila matatizo. Kuna shule za kifaransa peke yake kuanzia msingi mpaka vyuoni na kuna shule za Kiingereza peke yake kuanzia msingi mpaka vyuoni? Au mfumo wa aina hii utaligawa taifa? Basi tuwaige majirani zetu wa Kenya kwa kufundisha Kiingereza shule za msingi na sekondari, na Kiswahili kibaki kutumika majumbani na mitaani. Je, kwa kufanya hivyo tutaibua ukabila? Kwa nini tusiwe na mfumo wetu wa kipekee wa kufundisha Kiswahili toka msingi mpaka vyuoni. Inawezekana pia kukihalalisha Kiswahili peke yake, tukawa tumejifunga kitanzi na kijiwekea mipaka ya mawasiliano na baadae tukashindwa kupumua kwa sababu ya umasikini wetu, na uduni wa teknolojia yetu. Inawezekana pia kuwa mfumo wa sasa unafaa labda tatizo ni sisi wenyewe! Hatuwezi kufikia majibu kirahisi zaidi ya kuchanga bongo kwa pamoja.
      DASA likes this.

    6. #5
      Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 3,917
      Rep Power : 6962
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      35

      Default

      Kulikoni na Kyoma: Hayo ni madarasa mazito. Naendelea kuyasoma, nitarudi.

    7. Study Abroad

    8. #6
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,041
      Rep Power : 1246
      Likes Received
      16
      Likes Given
      106

      Default

      Kulikoni

      Nakubaliana na wewe kuwa na skills ya lugha zaidi ya moja ni msingi mzui wa mbeleni. Hilo umeainisha vizuri lakini tena umetuchanganya kwa kusema iwe lugha moja kuanzia vidudu mpaka vyuoni. Kama wewe na wanabodi wengine wanapendelea English then ndio tunakubaliana kuwa Kiswahili tunakiua kabisa maana nani atayekuwa tayari kujifunza kwa ufasaha lugha ambayo haina ofisi..??


      Nimebahatika kufanya kazi au kwa kusafiri au kwa kuwa stationed sehemu nyingi duniani na nimeshuhudia maeneo yote mawili, i.e. yale mataifa yanayozingatia lugha ya taifa kama medium of instructions across the board na yale mataifa ambayo kwa nafasi yao yanatumia lugha ya kimataifa ie. kifaransa, kireno nk

      Umesahau kutumabia iwapo huko ulikopita Lugha za Kitaifa zimeleta hasara yoyote kulinganisha na zile za kimataifa. Pia, sijui kama ulipata kufika India au China utupatie mfano maana najua wao hawatumii english kuanzia vidudu lakini uwakilishi wao katika anga za dunia tunaujua.

      Mimi sikubaliani na huu utaratibu wa kusema itumike english au kiswahili accross kuanzia vidudu kwa sababu hatuna USHAHIDI wa kuthibitisha kuwa lugha ndio inatuangusha kwenye maendeleo yetu ya kielimu.

      Unless mniambie kwa nini nahitaji kuelewa vingine.

    9. #7
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,041
      Rep Power : 1246
      Likes Received
      16
      Likes Given
      106

      Default Mnaongea lugha bure..!!

      Quote By Kyoma
      Mzee Mwanasiasa, Heshima yako Baba!
      Kwanini tusifanye kama Cameroon ambao wanatumia lugha zote mbili bila matatizo. Kuna shule za kifaransa peke yake kuanzia msingi mpaka vyuoni na kuna shule za Kiingereza peke yake kuanzia msingi mpaka vyuoni? Au mfumo wa aina hii utaligawa taifa? Basi tuwaige majirani zetu wa Kenya kwa kufundisha Kiingereza shule za msingi na sekondari, na Kiswahili kibaki kutumika majumbani na mitaani. Je, kwa kufanya hivyo tutaibua ukabila? Kwa nini tusiwe na mfumo wetu wa kipekee wa kufundisha Kiswahili toka msingi mpaka vyuoni. Inawezekana pia kukihalalisha Kiswahili peke yake, tukawa tumejifunga kitanzi na kijiwekea mipaka ya mawasiliano na baadae tukashindwa kupumua kwa sababu ya umasikini wetu, na uduni wa teknolojia yetu. Inawezekana pia kuwa mfumo wa sasa unafaa labda tatizo ni sisi wenyewe! Hatuwezi kufikia majibu kirahisi zaidi ya kuchanga bongo kwa pamoja.

      Kyoma chukua kumi mzee. Katika watu ambao nimekutana nao ambao sio wavivu wa kufikiri wewe ni mmoja wapo.

      Makala yako imenikuna katika sehemu mbalimbali, nilipofikia hapo mwisho ndipo nikapumua na kusema huenda pengine sio peke yangu ninayedhani lugha sio tatizo.

      Katika pita pita zangu hapa na pale nimegundua kwamba uwezo wa kujua lugha na kujua namna ya kuitumia vizuri hiyo lugha ni vitu viwili tofauti.

    10. #8
      Kulikoni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2006
      Posts : 434
      Rep Power : 737
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Mfumo ninaopendekeza mimi ni ule nilioukuta India kwamba kihindi ni informal national language lakini mashuleni maofisini na kadhalika ni kiingereza tu, as a result utaona kuna wataalam wengi sana wa fani mbali mbali katika wa kihindi duniani.

      Lugha yao ya kihindi haijaathirika infact professionals wote huacha kiingereza wakiondoka kwenye u-ofisho ili waweze kudumisha utamaduni wao, kwa hiyo Mheshimiwa Yebo Yebo utaona kwamba we as a nation hatutolose kwa vile tumeaccept kiingereza as national language officially.

      Jamani lazima tukubali katika world stage nafasi yetu ni washiriki kwa sasa sio waamuzi hivyo tukiforce kukubali kiswahili itakuwa ni kujimaliza katika ulimwengu huu wa utandawazi.

      Naamini kiswahili kina nafasi ya kukua zaidi lakini kwa sasa kiingereza kitaongeza sana maendeleo ya taifa letu na hususan vijana, kihindi ni market on its own in terms of bollywood nk lakini kiswahili hakina level hiyo ingawa haimaniishi kwamba lazima tukifanye ndio medium of instruction ili kifikie hadhi hiyo!


      Next time nitajadili namna mataifa mengine ya afrika yalivyosonga mbele kwa kukubali lugha zao zichukue back seat na nafasi ya diaspora katika mjadala huu...
      If you want to judge a leader, look at the organization ten years later.

    11. #9
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,488
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16316
      Likes Given
      8395

      Default

      Binafsi nadhani tutenganisha mambo mawili. Lugha ya kufundishia na ujuzi wa lugha ya pili.

      Kwa mtazamo wangu lugha ya Kiswahili iwe ni lugha ya kufundishia kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu. Kwa maana hiyo ni lazima kwanza tujibu swali kubwa lifuatalo, je lugha hiyo inajitosheleza kimisamiati inayoweza kuelezea mawazo, dhana, na nadharia mbalimbali za kitaaluma, kisomi, au kifani? Je Kiswahili kinaweza kufafanua mawazo ya Quantum Physics, nadharia mpya za Biology, dhana za hisabati n.k.

      Jibu langu kwa maswali hayo yote ni kuwa Ndiyo!! Kiswahili ni lugha ambayo inajitosheleza kufundishia somo lolote na kama lugha nyingine pale ambapo maneno au mawazo ya fani fulani siyo asilia katika lugha ya Kiswahili basi wataalamu wa lugha (Taasisi ya Kukuza Kiswahili) wanaamua kukopa na kwetu sisi tunaangalia Kiarabu kwanza halafu tunaangalia na lugha nyingine. Hivyo ni lazima tuelewe kuwa Kiswahili siyo tu kinaweza kuwa lugha inayotumika mitaani lakini inaweza kuwa na misamiati rasmi ya kisomi. Hivyo Kiswahili ni lugha ambayo ina uwezo wa kutumika kufundishia masomo YOTE hadi Chuo Kikuu!!!! Faida yake, ni wanafunzi kuhangaika na tatizo moja tu nalo ni misamiati ya kisomi na nadharia za kitaaluma na siyo tatizo la kuelewa matumizi ya lugha fulani kwanza.

      Kiingereza hata hivyo bado itakuwa ni lugha ya pili ambayo mtu lazima nayo aimudu anapofikia kiwango fulani cha taaluma na aimudu siyo kujua kusoma na kuandika tu bali kuelewa nadharia na mawazo katika lugha hiyo. Hivyo licha ya kuwa lugha ya kufundishia itakuwa Kiswahili, msomi wa Tanzania bado atakuwa anaifahamu lugha ya Kiingereza vizuri. Hivi ndivyo wanavyofanya Uchina, Ujapani, Skandinavia n.k Haina maana tukiamua kujifunza kwa Kiswahili basi Kiingereza kinawekwa pembeni. Mtu hahitimu ngazi za juu za masomo hadi afaulu lugha ya Kiingereza pia!!

      Nimeshawahi kuona TV ambapo wataalamu wa Kichina wanaelezea masuala mbalimabali ya Kisomi kwa kutumia Kichina wakati mtafsiri anatumia Kiingereza kutuelewesha sisi wengine. Hebu fikiria uone mtaalum wa Kitanzania anazungumza kwa lugha ya Kiswahili huku anatafsiriwa kwa lugha nyingine!!

      Tukianza kutumia Kiswahili kufundishia tutafungua mlango mpya kabisa wa uwezo wa kufikiri, kuelewa na kujieleza ambao Watanzania wengi wanajikuta wamefungiwa!! Na pia tutaondoa kasumba ya "ubora" wa wale wanaotumia Kiingereza kama ujiko wa kujionesha wao ni wasomi!!
      mose, Roulette and Dotworld like this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    12. Dua
      #10
      Dua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2006
      Posts : 3,534
      Rep Power : 1364
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default

      Elimu kwa mawazo yangu ifundishwe kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndio wenzetu wanaita mother tongue ili ieleweke vizuri na kiingereza kifundishwe kama lugha nyingine.

      Kitu cha kuzingatia ni kuwa na walimu wazuri katika nyanja zote, i.e. Kiswahili fasaha kutumika na Kiingereza fasaha. Tatizo kubwa ambalo Tanzania tunalo ni lile la kuona kwamba kama unaweza kuongea kiingereza basi wewe umesoma kitu ambacho sio kweli. Tujivunie lugha yetu na tuachane na kasumba ya kukumbatia kiingereza. Asilimia kubwa ya Watanzania waongeaji kiswahili kizuri.

      TUNATAKIWA KUFANYA MAREKEBISHO MACHACHE ILI KUONDOA KASUMBA HII AMBAYO INAWANYIMA WANANCHI AJIRA NA KUWAKUMBATIA WAGENI.
      Dua la kuku halimpati mwewe

    13. #11
      Kulikoni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2006
      Posts : 434
      Rep Power : 737
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Mzee Mwanakijiji:

      Umetoa hoja nzuri sana na kwa kiasi kikubwa nakubaliana na the whole issue in totality ie kuwa na lugha moja across the board, kuwa kiswahili kina uwezo wa kutoa msamiati nk [ingawa hii honestly sio issue saaana], lakini lugha ninayozungumzia mimi ni KIINGEREZA ACROSS THE BOARD.

      Lakini katika kujadili hili tuzingatie yafuatayo:

      1. Wengi wanaotoa mifano wanazungumzia CHINA, tusisahau kuwa China ina watu bilioni moja na ushee wale wanaweza kuwa closed market in their own country bila kuhitaji msaada wala kushirikiana na nchi nyingine [hii ilikuwa ndio theory ya MAO!], Kiswahili on the other hand kina wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni mia moja na ushee!


      2. China ni super power [refer to theory yangu ya kujifaragua in my earlier submission],sisi ni washiriki tu katika world stage hence hatuna nafasi kubwa ya kuweza kutamba na kiswahili chetu.

      Yes Mwanakijiji huwa ni raha kusikia kiswahili katika tv za magharibi na mara zote inapokuwa ni case, aidha watoto au mama yao au mimi tunaitana kusikiliza ingawa kina english voiceovers lakini tujiulize namna china inavyoplay a big role duniani na nafasi yetu ndio utaona kwamba kiswahili bado hakijawa nafasi ya kudominate the centre ground...


      Siamini kwangu mimi ni utumwa kuiweka lugha ya asili kwenye back seat, tuna lugha kadhaa za makabila zimechukua back seat licha ya kuwa wasomi wengi ni fluent, tuna radio kadhaa siku hizi tungeweza kupromote lugha kama yetu ya nshomire lakini ndio hivyo tumeamua kuziweka benchi for the same reason.


      Sisi katika international circles tunaamini katika utandawazi ambapo ukiangalia tuna nafasi nzuri ya kutoa watalaam wengi sana kwa kupromote kiswahili, mfano mzuri tu KENYA si wanatumia kiingereza zaidi na tunaona matunda yao!

      Sisi bado kwa hakika na kiswahili kimetuunganisha sana na kadhalika na hili ni thanks to Mwalimu ila kwa sasa kimaendeleo we have to change our mindset.

      Kupenda lugha ya nje sio utumwa bali ni kubadilika kivitendo, haya ndio mabadiliko tunayohitajia.

      Kwa lugha ya kimataifa as official medium of instruction na kiswahili as our traditional language tutafika....
      Last edited by Kulikoni; 13th April 2007 at 17:27.
      If you want to judge a leader, look at the organization ten years later.

    14. #12
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,488
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16316
      Likes Given
      8395

      Default

      Kulikoni, kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia kunarahisisha mambo kadhaa moja wapo na kubwa ni kurahisisha kueleweka kwa mawazo na dhana za kitaaluma ukiondoa ukuta wa lugha. Wengi wa watoto wetu wanaanza na lugha za makabila yao, halafu Kiswahili halafu Kiingereza. Ni sawa sawa na sehemu wanakofundisha Kifaransa kwa Kiingereza wakiwafundisha Watanzania..

      Kuna msomi mmoja ameamua kufundisha Kifaransa moja kwa moja kwenda Kiswahili badala ya kupitia Kiingereza na amekuwa na mafanikio makubwa zaidi.

      Nikupe mfano: Maelezo ya nadharia ya Fizikia ya Kuantum

      Quantum physics is a branch of science that deals with discrete, indivisible units of energy called quanta as described by the Quantum Theory. There are five main ideas represented in Quantum Theory:

      Energy is not continuous, but comes in small but discrete units. 1
      The elementary particles behave both like particles and like waves. 2
      The movement of these particles is inherently random. 3
      It is physically impossible to know both the position and the momentum of a particle at the same time. The more precisely one is known, the less precise the measurement of the other is.4
      The atomic world is nothing like the world we live in. 5

      Tafsiri ya Kiswahili:

      Fizikia ya Kuantumi ni tawi la sayansi linalohusiana na kujifunza juu ya chembe ndogo ndogo zaidi za nishati zijulikano kwa jina la Quanta kama inavyofafanuliwa katika nadharia ya Kuantum (Quantum Theory). Kuna mawazo makubwa matano yanayohusiana na nadharia mpya ya sayansi ya fizikia ya Kuantum. Nayo:

      a. Nishati siyo kitu kinachokuja kwa mtiririko unaoendelea bali huja kwa vipande vidogo vidogo zaidi visivyoonekana
      b. Vipande hivi vidogo vina tabia ya chembe (particle) na mawimbi (wave)
      c. Kuhamahama kwa chembe chembe hizi ni kwa kutokufuata mpangilio
      d. Ni vigumu kwa kuangalia au kupima kisayansi kuweza kujua mahali chembe ilipo au mwendo wake, kwani ukijua kimojawapo kati ya hivyo viwili ndivyo ilivyongumu kufahamu hicho kingine. Yaani ukijua chembe ilipo (mahali) ni vigumu kujua ina mwendo gani
      e. Ulimwengu wa kiatomiki huongozwa na sheria ambazo ni tofauti sana na sheria tunazoongozwa nazo katika ulimwengu wa vitu vikubwa. Hivyo ni ulimwengu tofauti sana.

      Je, katika maelezo hayo mawili ya kiingereza na Kiswahili nikimpelekea mtoto wa shule ya sekondari ni yapi anaweza kuelewa zaidi. Of course, ambaye anaimudu lugha ya Kiingereza maelezo ya kwanza hayana ugumu wowote na anaweza kuona makosa katika maelezo yangu ya Kiswahili. Lakini kwa mtu anayejua Kiswahili, ni ugumu gani atauona katika maelezo ya Kiswahili?
      Roulette and Dotworld like this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    15. #13
      Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 3,917
      Rep Power : 6962
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      35

      Default

      Mzee Mwanakijiji: Tusisahau kuwa hata hio lugha ya kiswahili wengi wetu hatukuzaliwa nacho. Mimi kwa mfano, hadi naanza darasa la kwanza nilikuwa sijui Kiswahili zaidi ya maneno machache kama baba na mama. Nilipofika shule tulikuwa tunavalishwa vipande fulani shingoni pindi uongeapo lugha ya nyumbani na baadaye kupewa adhabu hadi tukakijua kiswahili. Hadi leo nikienda nyumbani na mke wangu ambaye ni kabila lingine, mimi huwa mkalimani wa Kiswahili kwa mke wangu.

      Kwa hiyo sio kweli kwamba Kiswahili kipo kwenye DNA zetu, tulijifunza kwenye mazingira. Kumbe basi hata kiingereza kikiwekewa mazingira mazuri tunaweza kujifunza tukakijua vizuri. NImepata kutembelea nchi za Zambia, Malawi na Zimbabwe ambao wanatumia Kiingereza kama lugha ya Taifa na kufundisha, hawa bwana hadi wana misamiati ya baadhi ya miti kwa mfano kwa lugha yao.

      Na kwa nini all the time huwa tunatoa mifano ya nchi zilezile na hasa China. Kwa nini pia tusiangalie nchi za Kiafrika ambazo mazingira yao yanfanana zaidi na ya kwetu. kwa mfano, kwa nini hatujiulizi kwa nini wenzetu wa Ghana, Nigeria, na hata Kenya na Uganda wanajiamii zaidi katika nyanja za kimataifa kuliko sisi? Ni wazi kuwa hapa language factor inaingia.

      Watanzania tufike mahala tuache kujidanganya kuwa Kiswahili ni lugha inayojitosheleza. Inajitosheleza kwa kazi zetu za umachinga, lakini kama tunataka kuingia kikamilifu katika mapambano ya utandawazi basi tutakiitaji sana Kiingereza, tena Kiingereza kizuri sio hichi tulicho nacho cha kuokoteza.


      Tukumbuke maneno ya mwalimu: "English is the Kiswahili of the world"!
      DASA likes this.
      A Struggle Without Casualties is No Struggle-Steve Biko

    16. #14
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,488
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16316
      Likes Given
      8395

      Default

      mwanasiasa, mfano wako huo wa Waghana, Wanigeria, na Wakenya.. ni mzuri lakini angalia kama kiingereza kimeweza kuwaunganisha kuwa watu wamoja. Nadhani Kiswahili kinaweza kabisa kutumika kutimiza malengo hayo mawili, kuwa lugha ya kufundishia na lugha ya kuzungumza. Huku Kiingereza nacho kikiwekewa mkazo wa hali juu. Tatizo je ni lazima tuchagua kimoja kati ya hivyo viwili, je twaweza kupata vyote viwili?
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    17. #15
      Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Posts : 1,725
      Rep Power : 1021
      Likes Received
      54
      Likes Given
      6

      Default

      Lugha ni mama wa ufahamu wa kila jambo kwa undani.Sasa kama tunataka tuendelee ktk Fani nyingi ktk Nchi yetu Matumizi ya Lugha mama Lazima yapewe kipau mbele ktk ufundishaji taaluma mbali mbali kwani Tafiti nyingi zimebaini kwamba Nchi nyingi wanazotumia Lugha zao mama ktk kufundishia taaluma mbali mbali zimefanikiwa zaidi ktk uzalishaji wa watalaamu Bora na si Bora wataalamu.

    18. #16
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,041
      Rep Power : 1246
      Likes Received
      16
      Likes Given
      106

      Default

      Quote By mwanasiasa
      Sasa nasema wakati mwingine, matatizo yetu ni makubwa kuliko yanavyoonekana nje. Kuna shida kwenye mfumo wa elimu. Elimu tunayoipata katika mfumo wetu ni elimu inayozalisha woga na comformist wa ajabu sana. Ndio maana hata maprofesa wetu wanaishia kutoa vitisho badala hoja za kiprofesa! Tuna shida kubwa sana, Mungu tu ndio anayejua!

      Mwanasiasa,

      Nimeona nichukue maneno yako maana yanaendana na huu mjadala kuhusu lugha ya kufundishia Tanzania. Mimi nasema kasoro zipo kwenye mfumo mzima wa elimu...lugha ni kitu kimojawapo na pengine kidogo sana maana vijana wameonyesha wanaweza kukabiliana nalo.

      Huu mfumo wa elimu ya woga, kutegemea kuajiriwa, kukubali yaishe, aliye juu mngoje chini...huu ndio bomu na tena ni sumu kali sana kwenye akili za vizazi vijavyo.

    19. #17
      Mlaleo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2011
      Location : Ndani ya Yai
      Posts : 665
      Rep Power : 517
      Likes Received
      95
      Likes Given
      61

      Default Re: Lugha gani itumike kufundisha katika taasisi zetu za elimu: Kiswahili au Kiingereza?

      Kiswahili hakina issue watu hawakielewi darasani hata mitihani ya darasa la Saba wanafail ni wengi mno Bora english tu ndio iwe lugha ya darasani kiswahili kinachanganya tu watu
      They Said we are young and we don't know..We won't found out till we grow Baby i got you

    20. #18
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,163
      Rep Power : 31372
      Likes Received
      9572
      Likes Given
      683

      Default Re: Lugha gani itumike kufundisha katika taasisi zetu za elimu: Kiswahili au Kiingereza?

      Kyoma uko wapi kaka? Namiss sana nondo zako.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    21. #19
      Vakwavwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th May 2009
      Posts : 486
      Rep Power : 607
      Likes Received
      79
      Likes Given
      111

      Default degree za kiswahili ziwe na majina ya kiswahili

      Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha kiswahili kupitia redio one,watalaamu wa lugha waliobobea bado walikuwa wanatumia makina ya kiingreza kuzitaja kama vile master of arts in Kiswahili,hatuwezi kusema shahada ya umahili katika kiswahili? Napendekeza hata cheti kiandikwe hivyo.

    22. #20
      Adrian Stepp's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2011
      Posts : 1,573
      Rep Power : 713
      Likes Received
      438
      Likes Given
      2560

      Default Re: degree za kiswahili ziwe na majina ya kiswahili

      Quote By Vakwavwe
      Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha kiswahili kupitia redio one,watalaamu wa lugha waliobobea bado walikuwa wanatumia makina ya kiingreza kuzitaja kama vile master of arts in Kiswahili,hatuwezi kusema shahada ya umahili katika kiswahili? Napendekeza hata cheti kiandikwe hivyo.

      eti eeeh

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 5 123 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Je lugha bora ya utoa elimu ni kiingereza ama kiswahili
      By BUMIJA in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 6
      Last Post: 21st October 2011, 19:42
    2. Replies: 24
      Last Post: 11th October 2011, 11:01
    3. Replies: 146
      Last Post: 14th April 2011, 12:02
    4. Replies: 5
      Last Post: 9th June 2009, 01:48
    5. Replies: 15
      Last Post: 25th May 2009, 14:09

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...