Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

    Report Post
    Page 5 of 19 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 362
    1. #1
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,938
      Rep Power : 1432
      Likes Received
      1509
      Likes Given
      1619

      Default Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Haya matokeo ndiyo hayo yametoka!! Kila kitu hadharani, sasa ukiwa hapa JF ndo mpango nzima!! Manake watu washaanza kuhoji, mi nina hiki au kile nitafanyaje, haya ngoja nitajaribu kuweka mwongozo na alternatively nyingine due to spme perfomances kwa wote, manake naona huku kitaa watu wanadanganyana sana!!

      Hii ni kwa kadri ninavyofahamu mimi, kama kuna marekebisho basi yafuatie:

      => Credit Qualification kwa hali ya kawaaida ni 'C'-Na ili uende Form 5 unahitaji uwe na C 3, hapa ni either umebalance Combination(Comb) au hujabalance. Sasa kama una C 3 na comb hujabalance, hautachaguliwa serikalini bali shule binafsi utaenda kusoma mchepuo utakaofanana na masomo yako.
      [ Mfano: Civ-C, Kisw-C, Geo-C...unaweza fanya HGK ama HGL ama kozi nyingine hata kama english na History una D].

      =>Ukiwa na C 2 na D kadhaa(lets say 4 ya 26), hapa utaweza kwenda Form 5 shule za Private lakini utatakiwa utafute C ya 3 kw kureset wakati upo form 5. Same na C 1 You need to re-sit.

      => Hapa sasa ndipo kwenye utata. Ukiwa na D 3, kiukweli sahau Form 5 kama hauhitaji kurisit, sasa qualification hizi zina option zifuatazo:
      1. Unahitaji kupiga long pass kwa kwenda Chuo kwa ngazi ya Certificates. Duraation ya hii kozi ni 1 year Certificate. Sasa hapa kuna vyuo kadhaa vinavyotoa certificates. Hapa ni D za masomo yoyote yale Basic(sina uhakika kama B/Knwoledge na Islam zinazingatiwa na ndio maana nasema D za Basic Subjects)
      Mfano: Unaweza kufanya Certicates vyuo vya CBE-Mambo ya Biashara, IFM, TIA, Utumishi wa Umma(Public Service) Vyuo vya Kilimo na Ualimunk.
      Nakozi nyingi tu wanatoa kwa certificates..mfano Procurement, Accounts, Public Admistration, Recording, Clearing and Forwarding, Social Development, Secretarial Duties, Education nk.

      => Ukiwa na D 4 upo qualified kufanya ngazi ya certificate kama nilivyoanisha hapo juu.

      => Ukiwa na D 5 sasa hapa wewe umeula!! Hapa unaruhusiwa kabisa kufanya Basic Diploma katika vyuo vyote wanavyotoa Duploma. Kwa mfano vyuo hivyo nilivyovitaja hapa JUU, chukua form yako kwa maringo achana na biashara ya kurisit omba kozi ya diploma, Teana kama una D ya hesabu na English ndo inakuwa rahisi zaidi kuchukuliwa.

      => Kwa wale waliosoma mahesabu kuna vyuo vingine kama DIT(Daar Institute), AIT(Arusha Inst) na Mbeya Tech Msishau kufanya maombi, na kwale waliopiga fresh Biology with minimum of D angalieni option za Nursing ni nzuri sana na katika vyuo vya MATC na COTC.

      Kama kuna marekebisho yanakaribishwa na kama hoja ama daubt basi uwanja ndio huu. Most welcome!!

      UPDATE:

      Quote By structuralist
      Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi wako. Hata hivyo kwa kuwa umetoa nafasi ya kujazia sehemu ambayo labda inamabadiliko yafuatie,nafikiri nijikite kwenye mambo mawili
      1:Mkuu kwa ufahamu wangu,hairuhusiwi tena mtu kuendelea na 4m 5 na wakati huohuo akiwa anarisit. Hii ni kwasababu ili ufanye mtihani wa kidato cha sita lazima uwe umekaa darasani miaka miwili toka umalize kidato cha nne,hivyo basi ukijiunga na 4m 5 huku unarisit hiyo miaka miwili haitatimia.
      2:Hairuhusiwi tena kuunga unga vyeti,mfano mtu alikuwa na c mbili then arisit ili apate moja aunganishe na zile mbili za mwanzo,swala hilo haliwezekani tena. Hii ni kwa sababu ili mtahiniwa aruhusiwe kufanya mtihani kidato cha sita lazima awe amepata angalau crediti 3 O-level kutoka kwenye kikao kimoja ( ie 3 credits in o-level at the same sitting). Hii inamaanisha mtu akiamua kurisit anayakana matokeo yake na anatafuta mengine,na kwa mfano kama mtu alikuwa na c mbili na zilizobaki ni D halafu akarist assume akapata tena C mbili na D nne labda na F moja,hawezi kuanga hayo matokea akadai eti ana C nne kwasababu zimepatikana kwenye vikao tofauti(miaka tofauti). Hata hivyo lazima nikiri kwamba taratibu za kuunga vyeti zilikuwa zinatumika hapo nyuma lakini kwa ufahamu wangu ni kwamba kwa sasa zimefutwa. Kwahiyo kama mtu ana C mbli hawezi kwenda form 5, na akiamua kurisit ajue ni kama anaanza kazi upia. So kama kuna mtu hali hii inamgusa aangalie hayo mambo.

      Last edited by Sizinga; 3rd March 2013 at 13:36.
      Invisible, Kijini, Reena and 42 others like this.
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    2. FemaTV & Radio

    3. #81
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,938
      Rep Power : 1432
      Likes Received
      1509
      Likes Given
      1619

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By ummu kulthum
      Maganga Mkweli;3310200]huyu yuko vizuri anaweza akosoma diploma za aina nyingi sana
      za biashara zote anaweza akapiga yaani (accounting,bba, marketing logistics ,procurement)
      tourism ,hotel management, IT, HIV COUNSELLING, TEACHING(EDUCATION) , MAMBO YA CLINICAL OFFICERS NA NURSING KAMA AMEFANYA POA KWENYE BILOLOGY NA CHEMISTRY...

      take 5 jembee,sasa kuna watu wanasema kwamba diploma huwezi kwenda mpaka uwe umepitia A level au certificate kwa vyuo vyote vya biashara nijulishe rafiki ni kweli?
      Ni kweli, Kwa diploma ni lazima uwe umefanya cert au adv bt ukifanya coz wanaofanya vizuri form 4 wote wanapenda kwenda f5 thats the problem, lakini kwa pass za kawaida ambazo unahitaji kureseat(say C 2 na D 3)..the huyu mtu anaweza kufanya Diploma yoyote ile anayoipenda, so ni uzushi kwamba huwezi fanya diploma directly from f4, otherwise mnage cert 1 year then unaliendeleza kwa diploma
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    4. #82
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,938
      Rep Power : 1432
      Likes Received
      1509
      Likes Given
      1619

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Vilevile kuna Chuo kingine cha kilimo Kanda ya Kusini. Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele S.L.P. 509, Mtwara
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    5. #83
      Tilya18's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 44
      Rep Power : 410
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Kwa kweli nimefarijika sana kuona kwamba wapo baadhi ya Watanzania wenye mioyo ya uzalendo na huruma ya kusaidia wengine.

      Mkuu Sizinga nina mdogo wangu wa kike ambaye amepata div IV ya 26
      Civics D
      Hist D
      Geo D
      Kisw C
      Engl D
      Lit Eng C
      Phy D
      Chem D
      Bio D
      B/Math D

      Na ndoto zake zilikuwa kusomea udaktari. Tangu amepata matokeo kila siku anajifungia ndani na kulia kwani alitazamia kupata div I, kwa sababu zonal exams alipata div II ya 19.

      Je mkuu anaweza akasoma diploma ipi ili akiqualify akasomee huo Udaktari au ni lazima areset?

      Tafadhali sana naombeni msaada wenu ili nimtie moyo mdogo wangu asije akanywa sumu.
      CHONDE WAKUU!

    6. #84
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,938
      Rep Power : 1432
      Likes Received
      1509
      Likes Given
      1619

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Tilya18

      Ok,sorry for ya sista, ni kweli mtu ukitegemea matokeo flani yakaja mengine huwa inakatisha tamaa sana, mi mwenyewe mdogo angu wa kike kapata same like that.

      Ok kama alikuwa na plani ya kusomea udaktari we mtie moyo tu ingawa kwa kweli ningumu na itahitaji njia ndefu kidogo, Ujue msingi wa udaktari ni masomo ya Biology na Chemistry, sasa yeye ana D kwa hayo masomo, udaktari una competition sana.

      Sasa mpe moyo kwa kumpa hizi option, ajitahidi kuchukua form za Nursing au College za Clinical Officers huko ajitahidi sana na akifanya vizuri kwa ngazi ya diploma then atakuwa kwenye good position ya kufanya MD/udaktari. Clinical officers kwa nchi yetu ni sawa na daktari coz anafanya kazi kwenye vituo vya afya ambavyo vinatoa huduma masaa 24, anagawa dawa kwa wagonjwa, anachoma sindano, anatoa ushauri na mambo mengine mengi.

      Simshauri arudie pepa(reseat) kwani kufaulu Bios na Chem kwa Private Candidate ni ngumu sana. So hope nimeeleweka.
      Mamndenyi likes this.
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    7. #85
      Tilya18's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 44
      Rep Power : 410
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Sizinga

      Asante sana mkuu kwa ushauri wako, sasa naanza kuona mwanga wa namna ya kumsaidia.
      May Jah prosper you!
      Sizinga and Maganga Mkweli like this.

    8. Miaka 50

    9. #86
      Tilya18's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 44
      Rep Power : 410
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Kwa upande wa pili kuna mtoto wa baba yangu mdogo, yeye alikuwa private candidate na ktk masomo yake alipata Div III ya 19;
      Civ - C
      Hist - A
      Geo - B
      Kisw - D
      Engl - B
      Lit Eng - B
      B/Math - F

      Je! Mkuu huyu dogo anaweza kusoma HGE? Maana anapenda sana kusoma Economics. Kama hawezi, Je, kuna uwezekano wa yeye kusoma Comb nyingine halafu akifika university asome hiyo economics au una mshauri asome comb gani?

    10. #87
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,938
      Rep Power : 1432
      Likes Received
      1509
      Likes Given
      1619

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Tilya18
      Asante sana mkuu kwa ushauri wako, sasa naanza kuona mwanga wa namna ya kumsaidia.
      May Jah prosper you!
      Be blessed
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    11. #88
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,938
      Rep Power : 1432
      Likes Received
      1509
      Likes Given
      1619

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Tilya18
      Kwa upande wa pili kuna mtoto wa baba yangu mdogo, yeye alikuwa private candidate na ktk masomo yake alipata Div III ya 19;
      Civ - C
      Hist - A
      Geo - B
      Kisw - D
      Engl - B
      Lit Eng - B
      B/Math - F

      Je! Mkuu huyu dogo anaweza kusoma HGE? Maana anapenda sana kusoma Economics. Kama hawezi, Je, kuna uwezekano wa yeye kusoma Comb nyingine halafu akifika university asome hiyo economics au una mshauri asome comb gani?
      Hahaaaaa, safi sana!! Kapasua sana huyu dogo...kama kajaza HGE as first choice, mbaie ale bata tu atapelekwa shule nzuri sana by government, kwa ufupi huyo kafaulu sana Hist na Geography, so ondoa wasi asianze complication zozote, atasoma tu economics ingawa inahitaji hesabu kiaina, kwani wewe wasiwasi wako upo wapi hasa?
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    12. #89

      Ooh sorry kumbe ni Private candidate..mwache akasome HGE, akakutane na Economics huko mbele.
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    13. #90
      Tilya18's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 44
      Rep Power : 410
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Sizinga
      Hahaaaaa, safi sana!! Kapasua sana huyu dogo...kama kajaza HGE as first choice, mbaie ale bata tu atapelekwa shule nzuri sana by government, kwa ufupi huyo kafaulu sana Hist na Geography, so ondoa wasi asianze complication zozote, atasoma tu economics ingawa inahitaji hesabu kiaina, kwani wewe wasiwasi wako upo wapi hasa?

      Taarifa ambazo tumekuwa tukizipata huku mtaani wanasema ni lazima awe na D ya hesabu ili aweze kufanya mtihani wa kidato cha VI sasa sijui kama ni kweli?

    14. #91
      Maganga Mkweli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th July 2009
      Posts : 1,216
      Rep Power : 745
      Likes Received
      394
      Likes Given
      1002

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Tilya18
      Taarifa ambazo tumekuwa tukizipata huku mtaani wanasema ni lazima awe na D ya hesabu ili aweze kufanya mtihani wa kidato cha VI sasa sijui kama ni kweli?
      hapana kitu kama hicho ndugu yangu nijuavyo mimi sifa kubwa ya kwenda a-level yaani form six nikuwa na C TATU (3) kwenye matokeo yako ya kidato cha nne kwenye yale masomo saba ya lazima au kwenye yale ya mchepuo kama (physics ,chemistry (michepuo ya sayansi)commerce na bookingg(mchepuo wa biashara) au agriculture kwenye shule za michepuo ya kilimo) credit sizisokuwa na nguvu ni za masomo ya dini kama (bible knowledge na islamic knowledge)
      mtu anaye soma combination kama HGE hesabu haikimbii A-LEVEL kwani anakutana na kitu inaitwa BAM yaani basic applied mathematics na ili aweze kupata course nzuri za biashara(bcom,baf,bba nk) kwenye vyuo vikuu lazima awe amefaulu hili somo au awe na D ya mathematics ya O-LEVEL(FORM 4)
      UZURI WA KUFAULU HESABU(MATHS) FORM 4 utakusaidia wakati wakuchagua course nyingi wakati wakuomba vyuo maana nyingi zinataka walau uwe na D ya mathematics o-level kama mojawapo ya sifa za kupata hiyo course naamini nimejaribu kukuelewesha
      angalizo:na kama unataka kupata selection ya serikali itagemea na uchaguzi wako wa combination na shule alizoomba kwa combi husika maana kuna CUT-OFF POINT kwenye kila shule kutegemea na mahitaji shule, uwezo shule husika ufaulu wa mwanafunzi kiwango cha ujumla cha ufaulu kwa mwaka husika cha nchi ..
      nawasilisha
      Last edited by Maganga Mkweli; 13th February 2012 at 10:35.
      Sizinga likes this.
      LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...
      MHANDISI WA MFUMO WA UMEME /POWER SYSTEM ENGINEER -ANY ELECTRICAL ENGINEERING ISSUE YOU CAN CONSULT ME..

    15. #92
      Edwine Suarez's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 371
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Brother mie kuna jembe langu lina PCB but imesimama ki_hivi DDC vip kuhusu huyu ana four ya 27 na result lake ni_civ D, chem D, geo D, eng F , kisw D, math F,phy D, hist D and bios C..,nifahamishe kuhusu hapo..
      Sizinga likes this.

    16. #93
      Maganga Mkweli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th July 2009
      Posts : 1,216
      Rep Power : 745
      Likes Received
      394
      Likes Given
      1002

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      nina ushauri hasa kwa wazazi na walezi wadogo zetu hawa waliomaliza kidato cha nne na ambao wamejitahidi kupata alama za kwenda kidato cha tano
      endapo mwanao au nduguyo amefaulu shule ya serikali tizama ni mchepuo gani anaenda kusoma na shule gani kapata usikurupuke kumuhamisha bila kufanya japo katafiti kadogo kwa shule nyingi za serikali ni hali si hali yaani zote ni panzi na nzige hazichekani sana kutokana na uhaba wa vitendea kazi na walimu ukiacha shule chache sana ambazo huwa zinafanya vizuri kwa hiyo walimu huwa wanapata motisha ya kufanya kazi na si nyingi kihivyo.. sasa basi suala tuition kwa mwanafunzi kabla hajaenda form five kwa haka kwa mwezi ni lazima kubali au kataa kama una uwezo mpeleke tu ,ununuzi wa vitabu ni lazima kubali kataa ,pocket money yake kwa ajili ya tution atakapo kuwa shule ni lazima maana atakutana uhaba walimu kwa hiyo lazima atafute njia mbadala ambayo ni tution
      jambo jingine chagua shule ambayo unaweza kuwasiliana naye kirahisi au anaweza kupata resourse kwa ajili ya kusoma kirahisi(vitin na vitabu)hapa kama unataka kumuahamisha
      elimu ya A-LEVEL ni kipindi kifupi na syllabus yake ni kubwa sana kwa hiyo ajitahidi sana kusoma na kumaliza syllabus mapema iwezekano
      usomaji wa vitabu kuongeza maarifa sio kung'ang'ania past pepa tu na vitin
      wale ambao mnechaguliwa shule za michepuo ya sayansi za A-LEVEL(pcm,pcb,cbg,cbn,cb,pgm) huku kunachangamoto nyingi sana kunahitaji kujituma kwa hali ya juu na kuwa na moyo binafsi maana huku ndio kwenye matatizo sana hasa ya walimu na vifaa vya practicals
      Sizinga and Mamndenyi like this.
      LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...
      MHANDISI WA MFUMO WA UMEME /POWER SYSTEM ENGINEER -ANY ELECTRICAL ENGINEERING ISSUE YOU CAN CONSULT ME..

    17. #94
      Maganga Mkweli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th July 2009
      Posts : 1,216
      Rep Power : 745
      Likes Received
      394
      Likes Given
      1002

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Edwine Suarez
      Brother mie kuna jembe langu lina PCB but imesimama ki_hivi DDC vip kuhusu huyu ana four ya 27 na result lake ni_civ D, chem D, geo D, eng F , kisw D, math F,phy D, hist D and bios C..,nifahamishe kuhusu hapo..
      kiukweli huyu kama anataka kusoma A-LEVEL haiwezekani kwani ana credit moja tu yaani BIOLOGY =C na ili uwe na sifa za kusoma A-LEVEL ni lazima uwe na C TATU(3) ..LAZIMA areseat huyu hana ujanja ndio aende form five .. ila sasa kama wadau wengi walivyoshauri na maudhui ya thread hii ya ni kusaidia wale ambao hakufanya vizuri kwenye matokeo yao kuna njia mbadala ambazo zimetolewa na wadau hapo juu
      sasa cha msingi tunge jua yeye anataka kureseat au kuchangua hizi njia mbadala (za kupitia chuo ) halafu tunaweza kuongezea nini cha kufanya
      Sizinga likes this.
      LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...
      MHANDISI WA MFUMO WA UMEME /POWER SYSTEM ENGINEER -ANY ELECTRICAL ENGINEERING ISSUE YOU CAN CONSULT ME..

    18. #95
      Tilya18's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 44
      Rep Power : 410
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Maganga Mkweli
      hapana kitu kama hicho ndugu yangu nijuavyo mimi sifa kubwa ya kwenda a-level yaani form six nikuwa na C TATU (3) kwenye matokeo yako ya kidato cha nne kwenye yale masomo saba ya lazima au kwenye yale ya mchepuo kama (physics ,chemistry (michepuo ya sayansi)commerce na bookingg(mchepuo wa biashara) au agriculture kwenye shule za michepuo ya kilimo) credit sizisokuwa na nguvu ni za masomo ya dini kama (bible knowledge na islamic knowledge)
      mtu anaye soma combination kama HGE hesabu haikimbii A-LEVEL kwani anakutana na kitu inaitwa BAM yaani basic applied mathematics na ili aweze kupata course nzuri za biashara(bcom,baf,bba nk) kwenye vyuo vikuu lazima awe amefaulu hili somo au awe na D ya mathematics ya O-LEVEL(FORM 4)
      UZURI WA KUFAULU HESABU(MATHS) FORM 4 utakusaidia wakati wakuchagua course nyingi wakati wakuomba vyuo maana nyingi zinataka walau uwe na D ya mathematics o-level kama mojawapo ya sifa za kupata hiyo course naamini nimejaribu kukuelewesha
      angalizo:na kama unataka kupata selection ya serikali itagemea na uchaguzi wako wa combination na shule alizoomba kwa combi husika maana kuna CUT-OFF POINT kwenye kila shule kutegemea na mahitaji shule, uwezo shule husika ufaulu wa mwanafunzi kiwango cha ujumla cha ufaulu kwa mwaka husika cha nchi ..
      nawasilisha

      Hivyo kwa ushauri wako mkuu ni bora dogo arudie hesabu ili aondoe hiyo F ili aweze kupata option nyingi university!

    19. #96
      Edwine Suarez's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 371
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Jamaa anasema nia yake toka akiwa form one ni kujiunga na vyuo vya elim mbalimbali..

    20. #97
      Maganga Mkweli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th July 2009
      Posts : 1,216
      Rep Power : 745
      Likes Received
      394
      Likes Given
      1002

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Tilya18
      Hivyo kwa ushauri wako mkuu ni bora dogo arudie hesabu ili aondoe hiyo F ili aweze kupata option nyingi university!
      Kwa upande wa pili kuna mtoto wa baba yangu mdogo, yeye alikuwa private candidate na ktk masomo yake alipata Div III ya 19;
      Civ - C
      Hist - A
      Geo - B
      Kisw - D
      Engl - B
      Lit Eng - B
      B/Math - F

      Je! Mkuu huyu dogo anaweza kusoma HGE? Maana anapenda sana kusoma Economics. Kama hawezi, Je, kuna uwezekano wa yeye kusoma Comb nyingine halafu akifika university asome hiyo economics au una mshauri asome comb gani?

      SIYO LAZIMA SANA MAANA KAMA ATAENDA HGE LAZIMA ATASOMA BAM(BASIC APPLID MATHEMATICS) AMBAYO NAYO NI MSAADA MKUBWA ILA KAMA ANAENDA KUSOMA HGL,HKL ,HGK,KLF NA MICHEPUO MINGINE YA ARTS ISIYO HITAJI MATHS ASOME TU A-LEVEL NA CHUO ATAPATA TU AKIFAULU BILA SHIDA KWENYE COURSE AMBAZO HAZIITAJI MTU UWE UMEFANYA VIZURI HESABU KAMA MUDA UPO WA YEYE KURUDIA NI VYEMA... ILA KWA VINGINEVYO VIGEZO VYA KUSOMA FORM ANAVYO BILA SHIDA KABISAAAAAAAA NA ONDOA SHAKA
      KWA HGE HIYO BAM(BASIC APPLIED MATHS ) INA MSAADA SANA MBELE
      Sizinga likes this.
      LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...
      MHANDISI WA MFUMO WA UMEME /POWER SYSTEM ENGINEER -ANY ELECTRICAL ENGINEERING ISSUE YOU CAN CONSULT ME..

    21. #98
      Maganga Mkweli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th July 2009
      Posts : 1,216
      Rep Power : 745
      Likes Received
      394
      Likes Given
      1002

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By edwine suarez
      jamaa anasema nia yake toka akiwa form one ni kujiunga na vyuo vya elim mbalimbali..
      vyuo vya elimu kwa maana kuwa mwalimu au vyuo vya elimu vya juu ?
      kama anataka kuwa mwalimu ana qualify kusoma grade a BILA SHIDA YEYOTE
      kama anatakusoma vyuo vingine anaweza pia akapata jaribu kupitia toka mwanzo hii thread utaona kuna option nyingi za vyuo vya kati mtu anaweza kujiunga kutegemea na sifa alizonazo
      LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...
      MHANDISI WA MFUMO WA UMEME /POWER SYSTEM ENGINEER -ANY ELECTRICAL ENGINEERING ISSUE YOU CAN CONSULT ME..

    22. #99
      Tilya18's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 44
      Rep Power : 410
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Sizinga

      Ok,sorry for ya sista, ni kweli mtu ukitegemea matokeo flani yakaja mengine huwa inakatisha tamaa sana, mi mwenyewe mdogo angu wa kike kapata same like that.

      Ok kama alikuwa na plani ya kusomea udaktari we mtie moyo tu ingawa kwa kweli ningumu na itahitaji njia ndefu kidogo, Ujue msingi wa udaktari ni masomo ya Biology na Chemistry, sasa yeye ana D kwa hayo masomo, udaktari una competition sana.

      Sasa mpe moyo kwa kumpa hizi option, ajitahidi kuchukua form za Nursing au College za Clinical Officers huko ajitahidi sana na akifanya vizuri kwa ngazi ya diploma then atakuwa kwenye good position ya kufanya MD/udaktari. Clinical officers kwa nchi yetu ni sawa na daktari coz anafanya kazi kwenye vituo vya afya ambavyo vinatoa huduma masaa 24, anagawa dawa kwa wagonjwa, anachoma sindano, anatoa ushauri na mambo mengine mengi.

      Simshauri arudie pepa(reseat) kwani kufaulu Bios na Chem kwa Private Candidate ni ngumu sana. So hope nimeeleweka.

      Mkuu naomba uniorodheshee baadhi ya vyu vinavyo toa Diploma ya Clinical officers vilivyopo ktk mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pamoja na addresses za vyuo hivyo.
      TAFADHALI NAOMBA MNISAIDIE!

    23. #100
      Maganga Mkweli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th July 2009
      Posts : 1,216
      Rep Power : 745
      Likes Received
      394
      Likes Given
      1002

      Default Re: Form 4 na wengine..Angalieni hapa!!

      Quote By Tilya18
      Mkuu naomba uniorodheshee baadhi ya vyu vinavyo toa Diploma ya Clinical officers vilivyopo ktk mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pamoja na addresses za vyuo hivyo.
      TAFADHALI NAOMBA MNISAIDIE!
      http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ml#post3310175
      NAOMBA FUATA HII LINK NI POST #69 YA HII THREAD INAWEZA KUKUPA JIBU
      LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...
      MHANDISI WA MFUMO WA UMEME /POWER SYSTEM ENGINEER -ANY ELECTRICAL ENGINEERING ISSUE YOU CAN CONSULT ME..

    Page 5 of 19 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...