JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

  Report Post
  Results 1 to 14 of 14
  1. MKAKU ED's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 31st January 2012
   Posts : 2
   Rep Power : 0
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013
   UTANGULIZITume ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘Tanzania Commission for Universities-TCU) ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘National Council for Technical Education’ - NACTE) pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher Education Students Loans Board) inapenda kuutarifu umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kupitia mifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”, “Equivalent Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central Admission System’) na utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo:1. MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/131.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry”Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali kabla ya mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu za elimu ya juu (pre-entry programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya kupitia mfumo wa “Mature Age Entry” vinatakiwa kuwasilisha programu hizo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa uhakiki na kupata kibali. Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa muda wa mwaka mmoja. Hali kadhalika kwa upande wa mitihani kupitia mfumo wa mature entry, Tume kwa ushirikiano na Baraza, kwa pamoja wataandaa na kuratibu utaratibu wa mitihani katika vituo maalum kikanda ili vyeti vitakavyotolewa viwe na ulinganifu unaostahili na hatimaye kuweza kutumika katika udahili wa sifa linganishi katika vyuo mbalimbali.Vyuo vinatakiwa kuandaa programu za mifumo ya “Pre-entry” na “Mature Age Entry” na kuziwasilisha Tume na Baraza ili zihakikiwe kwani mwaka wa masomo kwa kusudi hili utaanza mwezi Agosti 2012/2013. Kwa utaratibu huu, watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa kufanya mitihani yao na kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2013/2014.Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13 hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi kwa mfumo wa “Pre-Entry” na “Mature Age Entry”.1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia Mfumo wa Pamoja (Central Admission System)Waombaji watakaopitia mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) wamegawanyika katika makundi manne, ambapo waombaji wa kundi (i), (ii) na (iii) watatambuliwa kama “Direct Applicants” na kundi (iv) watatambuliwa kama “Indirect Applicants”(i) Waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu. (ii) Waliohitimu mafunzo ya diploma ya elimu ya ufundi (NTA level 6) kutoka vyuo vinavyotambulika na NACTE miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu;(iii) Waliohitimu mafunzo ya Diploma ya Ualimu (kutoka vyuo vinavyotambulika) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.(iv) Waombaji ambao sio wa moja kwa moja (Indirect Applicants) ni wote waliohitimu kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6) na Diploma ya Ualimu katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita (kuanzia 2009 kurudi nyuma).1.2 Waombaji Watakaowasilisha Maombi yao Moja kwa Moja VyuoniWaombaji watakaowasilisha maombi kupitia vyuo husika ni wenye sifa linganishi (Equivalent Qualifications) yaani wenye vyeti vya Astashahada na Diploma ambazo hazitambuliwi moja kwa moja na NACTE. Ili kukamilisha udahili, wanashauriwa kuwasiliana na NACTE ili vyeti vyao vitambuliwe na kusajiliwa kabla udahili haujaanza. Vyuo vinavyofundisha programu mbalimbali katika ngazi ya Astashahada na Diploma ambavyo havina usajili wa NACTE/NECTA vinatakiwa kuwasilisha matokeo ya wanafunzi wao NACTE haraka iwezekanavyo ili matokeo hayo yaweze kutumika katika utambuzi wa vyeti vya wanafunzi husika.2. MUDA WA UDAHILI KWA MAKUNDI MBALIMBALIMuda wa maombi wa kuwasilisha maombi ya udahili kwenye CAS umegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:(i) Kundi la Kwanza (1 Aprili mpaka 30 Aprili 2012)Waombaji wote waliomaliza kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6), na Diploma ya Ualimu kuanziamwaka2011 kurudi nyuma wataanza kuomba udahili kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30 Aprili 2012. (ii) Kundi la Pili Waombaji wote watakaomaliza kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi na Diploma ya Ualimu mwaka 2012 wataanza kuomba udahili baada ya matokeo yao ya mitihani kutangazwa na vyombo husika. Hakuna mwanafunzi atakayesajiliwa kwa kutumia matokeo ya muda (provisional or expected results).(iii) Kundi la Tatu Waombaji wote ambao ni raia wa Tanzania waliosoma nje ya nchi au wenye vyeti ambavyo si vya mfumo wa elimu ya Tanzania (mfano: Cambridge, Bacclaureate, n.k). Waombaji wa kundi hili wanashauriwa kuomba udahili mara matokeo yao yatakapotangazwa na watatakiwa kupeleka vyeti vyao Baraza la Taifa la Mitihani (“National Examinations Council of Tanzania – NECTA”) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education - NACTE) kwa ajili ya kulinganisha alama zao za matokeo au kupata ithibati kabla ya kuanza kuomba udahili. Hakuna wanafunzi watakaodahiliwa kwa matokeo ya muda.3. UTARATIBU WA MIKOPOBodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mamlaka iliyopewa kisheria itatoa mwongozo na utaratibu wa utoaji wa mikopo mwezi Februari 2012. Miongozo hii itachapishwa katika vyombo vya habari na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu nchini na Ofisi za Posta na kwa Wakuu wa Elimu kila wilaya. Maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2011/2012 yataanza kupokelewa ifikapo mwezi Machi 2012 na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Juni 2012. Utaratibu huu utahusu waombaji wote wapya na wale walioko masomoni katika vyuo vya elimu ya juu.4. HITIMISHOTunapenda kuwajulisha waombaji wote kuzingatia muda wao wa udahili kama ulivyoainishwa katika tangazo hili. Muda ukiisha hawataweza kuomba hadi mwaka wa masomo 2013/2014. Pia waombaji wote wanashauriwa kufuata taratibu za mikopo kam zitakazotolewa na Bodi ya Mikopo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika swala hiliMaelezo zaidi na ufafanuzi kuhusu udahili na mikopo wa 2012/13 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:Tume ya Vyuo Vikuu; www.tcu.go.tzBaraza la taifa la elimu ya ufundi; www.nacte.go.tzBodi ya Mikopo ya Elimu ya Elimu ya Juu; www.heslb.go.tz

  2. Mr.creative's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th August 2011
   Posts : 492
   Rep Power : 624
   Likes Received
   72
   Likes Given
   9

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   thank you very much for the info. be blessed

  3. Mzee Dogo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th November 2010
   Location : Kwetonge
   Posts : 295
   Rep Power : 623
   Likes Received
   55
   Likes Given
   33

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Barikiwa sana mkuu...
   Too much fear creates slavery!

   Kenyan proverb

  4. #4
   kinya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th February 2009
   Posts : 456
   Rep Power : 745
   Likes Received
   47
   Likes Given
   9

   Default

   mkuu huu uzi ni muhimu na umesaidia wengi barikiwa GT..

  5. Msafiri Kasian's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th September 2011
   Posts : 1,541
   Rep Power : 829
   Likes Received
   181
   Likes Given
   133

   Default

   Quote By MKAKU ED View Post

   Asante sana!

  6. Nyakageni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2011
   Posts : 12,309
   Rep Power : 71520191
   Likes Received
   2287
   Likes Given
   1068

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   mkuu ahsante sana

  7. Mamilioni's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 16th January 2012
   Posts : 9
   Rep Power : 504
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Thanx alot

  8. matumbo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th July 2011
   Posts : 6,900
   Rep Power : 0
   Likes Received
   3490
   Likes Given
   1545

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Ngoja niwastue wadau waje wachek.

  9. nyamemba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd November 2011
   Posts : 491
   Rep Power : 611
   Likes Received
   91
   Likes Given
   203

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   thanx kaka

  10. SHIEKA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th December 2011
   Location : Moshi
   Posts : 6,929
   Rep Power : 429498321
   Likes Received
   3000
   Likes Given
   2504

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Hii ndo raha iletwayo na wana JF. Wanakuandalia chakula na kukiweka mezani. Hii habari nalikuwa naisubiri sana. Asante sana mleta thread!
   "Bora Sumu Ya Panya Kuliko CCM" - Bango la wananchi wa Tunduru
   Bora Kipindupindu Kuliko CCM Kuendelea Kutawala - Bango la wananchi Mtowambu

  11. Binti Sayuni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2009
   Location : MWILINI
   Posts : 341
   Rep Power : 721
   Likes Received
   32
   Likes Given
   80

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Ubarikiwe sana

  12. NIMEKIMBIA CCM's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 4th October 2011
   Posts : 193
   Rep Power : 556
   Likes Received
   25
   Likes Given
   0

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Hiv kw nn wameandka mwaka 2011/2012 bada ya kuandka wa2 wote walopo vyuön?

  13. BILLY2TRY's Avatar
   Member Array
   Join Date : 3rd December 2008
   Posts : 51
   Rep Power : 675
   Likes Received
   3
   Likes Given
   4

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Thanx!!

  14. Alexism's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th August 2011
   Location : Iringa Municipal TZ
   Posts : 1,123
   Rep Power : 753
   Likes Received
   162
   Likes Given
   18

   Default Re: Udahili vyuo vikuu 2012/2013, tcu yahabarisha

   Wakora waitu.

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...