JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Mjikumbushe Mzumbe High School

  Report Post
  Page 4 of 4 FirstFirst ... 234
  Results 61 to 67 of 67
  1. Bubu Msemaovyo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th May 2007
   Location : All around the World
   Posts : 3,488
   Rep Power : 4269171
   Likes Received
   2118
   Likes Given
   2578

   Default Mjikumbushe Mzumbe High School

   Bila shaka Wana Mzumbe mpo hapa JF, nimetumwa kuwakumbuka wafuatao John Mongela, James Bwana, Michael Thomas Sebastian Sarota, Hassan Rajab Hassan, Patrick Maleva, Anderson Segereti, David Black, Obed Mwakitalika, Clement Mwashambwa, Kwela Mgaya, Theophil Alexander, Njaule Mdendu, Johnson Jasson, Sollomon Shati, Obed Msenga, Charles Nakembetwa, Gideon Mandesi, Isaac Kassanga, Dereck Kassanga, Deus Changala, Timilai Sheshangali, Shemaghembe Ntulwe, Sainet Katulunga, na wengine wengi sana. Waliosoma pale mmeombwa kuongezea majina ya wale mnaowakumbuka.
   "If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart." Nelson Mandela


  2. tusichoke's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd April 2011
   Posts : 1,255
   Rep Power : 794
   Likes Received
   188
   Likes Given
   8

   Default Re: Mjikumbushe Mzumbe High School

   Nimekumbuka mbali sana,miaka ile ya 91-93 ,yule mpishi shangazi,mr KABARE mwl wa BIOS ,mr NDALU CHEM,MAMA MWIYENGE na usmart wake,Marehem Mkomboti na Mr ABOOD bus.Graduation wakaja DAKAWA ikawa issue kwa KILEI,wale F.6 WA 93 mnakumbuka ugali na mahomeboys(DAGAA KAUZU),Vipi ule mchakamchaka c ulikuwa poa kiafya. Kweli mzumbe vimepita vichwa ,wakowapi RAMADHAN ZONGO,BENO CHELELE, na wengine wengi, NAUNGA MKONO WAZO LA KUWA MZUMBE EX BLOG
   Last edited by tusichoke; 18th May 2011 at 07:27.

  3. Mzumbe88/91's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 17th May 2011
   Posts : 2
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Mjikumbushe Mzumbe High School

   Quote By mimindiokile View Post
   Ni furaha kubwa sana kurudi tena kwa mara ya pili ndani ya Jamii Forums, nilipolala i felt Memory ikianza kupata moto nami pia nimekumbuka baadhi ya majina ya Waalimu na Wanafunzi - Ignatus Nangawe, Wabu Matipuka, James Lugembe "Shoka", Francis Mataula, David Magwila, Erasmus Dennis Buberwa, David Athuman "Mchanifu", Kassim Msami, Rodrick Mpogolo, Emmanuel Mahimbo, Geofrey Mhando, Nuru Ndile, William George, Andrew Wawa, Faustine Mduda, Kigobanya, Obed Kayawaya, Peter Billa, Ekwabi Mijungu, Edson Makallo, Joseph Mathias, Paul Kitaly, Mdenye, Mdede, Lemuel Kilallo, Cretus Peter Mnyanga, Lucas, Christopher Shemahonge, Crystogonius Masusu, Wanini Athuman, Kashenge Kimario, Collins Lutenge, Francis Mbenjile, Mussa Sadock, Zhao Ngesile, Baraka, Zephania "Church Man", Abdallah "Mtoto wa Mzinga - Jeshini", Chalesi "Kinara", Shilinde Nzweke, Enock Ndezi "Bob Ndezi", Simon Pasua, Kigume, Ralph Meela, Nolasco Paul Mbepera, Dotto Andrew, Richard Mshyota, Shukuru Basana, Augustine Karadoga, Lupindilwa Luchagula Mulula, Mjusi, Kumalija Mbingu, Mchome, Gilman Nyamubi, Watson Nsaji Mwakyusa, Hanzen Sanga, Phineas, Kinara Maswaga, James Msalika, Nehemia Kamalango'mbe. Majina mengine yanakuja halafu yanapotea kwani ni miaka mingi sana toka mwaka 1991 ni takribani miaka 19 sasa!.

   Waalimu - Mwl. Mgonde, Mwl. Chimile (RIP), Mwl. Mikapagalo, Mwalimu Ndiva, Kulikuwa pia na Mwalimu asiyeona jina limenitoka, Head Master

   Bagenda, Headmaster Kihawa na Mkewe alikuwa Nesi pale Dispensary.[Headmaster huyu katika zunguka yangu kutafuta mlo alikuwa Wiza Schools - Mbeya ofcourse kama Headmaster, Mwl. Mlelwa mara ya mwisho nilimuona huko Handeni kama Headmaster wa Handeni Secondary
   School. Jamani kuna Mwalimu pia jina limenitoka tuliambiwa alikuwa msanifu wa Wimbo wa Shule - "Shule Yetu Mzumbe yasifika sana........,
   Malezi ya Mzumbe ni Kimilifu ya Kitanzania........, Elimu ya Mzumbe........ nakuendelea, Mwl. Minangi.

   Mganga wa Shule - Jina lake lilikuwa Maganga? Sikumbuki vizuri.

   Tulikuwa na Gazeti la Wanafunzi wakora kule ****** - shule ambapo Waandishi na Wachoraji Mahiri walikuwa wanatoa habari nyeti na motomoto kuhusiana na matukio mbalimbali yaliokuwa yakitokea pale shuleni. Katika safari ya maisha kuna wengi ambao tayari wametangulia mbele ya Haki:
   1. Raphael Mwatwinza.
   2. Conrad Dustan Mnywambele "Sauti ya Kamachumu".
   3. Nijimbele Gideon.
   4. George Sindani.
   5. Lusimba Midaba.
   Naambiwa list ni ndefu sana hivyo kwa yeyote mwenye jipya atumuvuzishie - Zuri au Baya.

   Msamiati: Mavuzi - Mboga ya Kabichi, Hunde - akina dada wale wanaofanana na baba zao, walikuwa wanagombaniwa sana pale ka mpira wa
   kona, Mchanifu - Msanii, Anasa - Maandazi ya mke wa Mwl. Omari [alikuwa Kocha pia] nimewahi kumuona huko Pangani, Mharibifu - msamiati huu ulikuja baada ya mfanyakazi mmoja wa pale shule kuoa mdada ambaye alikuwa hawalingani kiumri hivyo watundu wakaja na usemi huu kuwa ni mharibifu, Killer Kala - Rangi inayoua [Msamiati huu uliletwa na watu wenye msimamo mkali kuhusiana na dada zenu hao kutupeleka kasi hata tuliwahi kama sikukumbuki vizuri tulicheza Bull Dance once na baadae tulifanya partneship na wanafunzi wa Kwilo],
   Mbu Jazz Band - Nadhani mwakumbuka wale Mbu pale na Cerebral Malaria [Joining Instructions ilikuwa na phrase tata - Net ni muhimu lakini sio lazima au Net ni lazima lakini sio muhimu, sikumbuki vizuri. Dikodiko - Siku za Jumamosi vijana walikuwa wanakarabati vyakula kwa majiko ya umeme mabwenini, kwa kuchanga na kununua kuku IDM almradi Chakula siku ile kilikuwa kinaleta raha esp. Mirambo Village.

   Nisiyoyasahau:
   1. Dispensary haikuwa na dawa na mganga naye alikuwa na mambo mengi, kama kawaida wanafunzi tulikuwa na tabia ya kuunga Azimio la Arusha kwenda Mzinga Hospital tena kwa kutoroka siku ya Jumamosi bahati mbaya kufika Hospitali badala ya kupata huduma na kurudi shule Daktari aligoma kabisa kuniruhusu kwakuwa hali haikuwa nzuri, Kimbembe kilikuwa kwa mwenzangu ambaye ndie alinisindikiza atawaambia vipi utawala wa shule, kuna mwanafunzi amelazwa?!.

   2. Baada ya pitapita ya Promosheni ya Waalimu pale shule, nadhani baada ya Bagenda kuondoka. Mwl. Chimile (RIP) alipata U-Second Master, sasa wakati ule tayari tulikuwa tunakaribia sana kufanya mithihani, kila mtu alikuwa na excuse zake kutokwenda Assembly mie nikiwa mmoja wao, Si mwakumbuka net zilikuwa lazima zitundikwe juu. Kuna jamaa ule mtego wa Mbu ulishapoteza dira, ilikuwa nyeupe lakini hakuwa akiitendea haki ilibadilika ikawa ndio chaka la wakwepa Assembly ukiireremsha hakuna aliekuwa akikuona basi hilo ndilo lilikuwa chaka langu mpaka muda wa kuingia darasani. Nadhani Mwl. Chimile (RIP) alikuwa anafuatilia kwa karibu sana kwani siku ile nilikamatwa kama Saddam pale pangoni. Nilikuwa bize naendelea kupata shule nadhani alikaa kama dk. 5 mimi nilikuwa simuoni. Alifunua Net akasema nenda Assembly nikapiga Magoti mpaka muda wa Assembly umeisha, Nikaingia Darasani that was it hakuwahi kuniuliza wala kupata Adhabu zaidi ya ile ambayo ilikuwa hardly 10 Minutes.

   3. Mnakumbuka enzi za Disco kule Kilei na hata Mzumbe kulikuwa na Madaraja ukumbini from First Class mpaka Third Class huko watu ni muziki kwa kwenda mbele yaani washika mchuma [un-mademu] na mademu kutudanganya majina wengine walikuwa wanapewa majina ya mabasi. Walahi ufisadi ulianza zamani, na visiting day watu wanapeleka mikate na siku hiyo unapiga mswaki sana, nywele unapiga cut iliyokwenda shule si mnawakumbuka vinyozi maarufu. Pale Morogoro kulikuwa na jamaa alikuwa anawatia watu joto kuhusu watoto wa killer Colour - Alex Mikate, Mnamkumbuka.

   4. Je, Siku za kazi shambani na Club's day na Prep ya mchana baada ya mlo, Si waalimu wakali walikuwa wanapita kuangalia wanaopiga stori na kulala mchana. Hivyo solution ilikuwa kupanda na kujificha juu ya dari. Kuna jamaa aliteremka nalo, jina silikumbuki vizuri ndio ukawa mchezo huo umepungua.

   5. Kuiba machungwa ya shule na kuficha kwenye Ma-locker au viazi na kuchemsha kwa Heater Mwitu [Spring za Vitanda]

   6. Uzamiaji wa msosi Mzumbe, Unaoga na kuvaa koti pamoja na kijiko. Kwanini Koti?, Lilikuwa linajenga personality. Ole wako ushtukiwe na
   walinzi watakufukuza kama mwizi na kijiko chako mkononi. Tabia hii ilipungua watu wakawa wanakula kwa Ma-poti wao [Home boy] mabwenini pale chuoni.

   7. Vita vya kujikomboa kutoka kuvaa Kaptura za kaki hadi kuvaa Suruali nyeusi.

   8. Mgomo baridi wa chakula ambacho hakikuwa kizuri especially madondo lakini jamaa zetu wengine wakatusaliti walizidiwa na njaa ikabidi wale tu, nadhani mnawakumbuka.

   9. Michezo na vijana wa mazimbu - wapigania uhuru.

   10. Siku ambayo vijana walikula doria usiku mzima baada ya kutembelewa na Kina dada wa Msalato Girls. Mnaikumbuka hiyo?. Walilala Mirambo Village Dorm. #4 or #3. Ikaleta manungu'niko kwa dada zetu wa Kilakala.

   11. Siku ya Nyali na Nyama au siku ya ugali na kabichi - {Siku ya kabichi ilikuwa siku ngumu sana na haswa kama huna jinsi ya kukarakachua miundo mbinu ili upate mbadala]

   12. Siku ya Jumamosi ilikuwa ni kama siku ambayo unajikomboa, kwani baada ya shughuli ya usafi na ukaguzi na matangazo ya hapa na pale,
   unakuwa huru ukisubiri misosi ya mitaani au unaenda kubadilisha mkaango mjini au pale mwanzo wa lami ya kupaka kuja chuoni IDM ukila miwa. Jioni unawahi Roll Call halafu wasubiria wali tena ukivuta hisia ya Kideo cha Mwl. Myenge. Wengine watafuata Uzo "gongo" Changalawe. Watu wa dini watakuwa wakisali na kuimba. Almradi Jmosi ilikuwa inasaidia sana kutoa msongo.

   Na zile trip za Tangeni zilisaidia sana kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii, usafi bila viboko.

   Ya kukumbuka ni mengi sana i hope wengine watasaidia kuleta raha ya zamani.

   Natarajia kusikia mengi kutoka pembe mbalimbazi za dunia hii.

   Naomba kuwasilisha.

   NB: HuXiang umenena itakuwa ni kitu cha maana kuwa na wavuti dedicated kwa Wazumbe [Alumni].

   Brother Mimindiokile umenikumbusha sana Kijiji cha MIRAMBO hasa bweni namba 3. Church man, Karadoga, Shukuru, Clemence Mwashambwa na wengi uliowataja nilikuwa nakaa nao katika bweni hilo. Huenda nikawa nafit ktk utambulisho wako wa Mtoto wa Mzinga Jeshini...............Kuna muungwana amemtaja brother Ndezi, Bob Ndezi, nasikitika kusema kuwa nilimkuta home kwao Igunga, anaonekana kutatizika na matatizo ya ufahamu kwa sasa, nilimsababhi na kumkumbusha kuhusu Mzumbe lakini hatukua ktk frequence moja. Jamaa wa pembeni wakasema anasumbuka na matatizo ya akili. Mungu amsaidie apone. Yako mengi ya kukumbuka kuhusu MZUMBE. Wazo la kuwa na Alumni ni zuri sana, litatuunganisha na kutoa mchango wa kuisaidia shule kwa namna moja ama nyingine.
   Mungu ibariki Mzumbe

  4. Aine's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st November 2010
   Location : Tz
   Posts : 1,616
   Rep Power : 850
   Likes Received
   473
   Likes Given
   1132

   Default Re: Mjikumbushe Mzumbe High School

   Quote By Yo Yo View Post
   Well well man wangu.......ma TO nawaona ovyoo sana kazi hawajui material hamna kichwani i could say that walikuwa wanakariri as Wibonele(nimem miss Wibo) alivyowalikishia pepa......Nani asiyejua mzumbe wanapewa pepa(maswali) kabla ya mtihani.Kuna To mmoja nilienda nae sehemu fulani alikimbia akarudi Bongo kwenye elimu ya kukariri.
   Kwenye red and his wife are no more in this world!!!!!!!!!

  5. ded2010's Avatar
   Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 10
   Rep Power : 544
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Mjikumbushe Mzumbe High School

   mmenikumbusha mbali sana mimimnilikuwa mzumbe kwa miaka sita 1995-2000 nilikuwa mkwawa namba nne namkumbuka mwalimu minja alitutandika darasa zima form one A kisa kumkumbushia muda wa kipindi chake cha english ulikuwa bado; tunawakumbuka enzi hizo mwalimu mkumbo ,bitwale, T.D.K. MSUKAhead master,mwasha marehemu wibonele, kabale(mganda) wazumbe wengi ni madaktari,mainjinia na wahasibu,tuache chuki binafsi kama ulishindwa kuachieve ulipokuwa mzumbe usitake kuwaaminisha watu kama wazumbe walikuwa wanpewa paper,katika darasa letu la PCB tulikuwa 25 ishirini wote tulikwenda muhimbili,2 walikwenda abrod na wawili walikwenda mlimani kuchukua bicom

  6. 3D.'s Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th September 2010
   Location : DSM, Tanzania
   Posts : 1,025
   Rep Power : 778
   Likes Received
   262
   Likes Given
   1465

   Default Re: Mjikumbushe Mzumbe High School

   Quote By Vitendo View Post
   Minja bado yupo.
   Sapila,Mtawajibu,Malale,Mtesig wa wamepata Kuwa Head Master kwenye shule za Kata.
   Matekele yuko Mzumbe University anapigisha vijana elimu.
   Sapila du nimemmiss. Minja anawakumbuka almost wanafunzi wote aliowafundisha. Those days. Those days!!


  7. FUKO LA DHIKI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th May 2011
   Posts : 409
   Rep Power : 619
   Likes Received
   84
   Likes Given
   172

   Default Re: Mjikumbushe Mzumbe High School

   jamani mimi nawakumbuka GREYSON NYANTAMBA,LUSEKELO KIBONA,BENJAMIN AMOS,ASAJILE JOHN,JOSIAH NOMBO,DANIEL NGONDYA,KWAME etc
   ''Work Smart,not Hard''


  8. Kim Adiel's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 14th January 2013
   Posts : 1
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Bubu Msemaovyo View Post
   Bila shaka Wana Mzumbe mpo hapa JF, nimetumwa kuwakumbuka wafuatao John Mongela, James Bwana, Michael Thomas Sebastian Sarota, Hassan Rajab Hassan, Patrick Maleva, Anderson Segereti, David Black, Obed Mwakitalika, Clement Mwashambwa, Kwela Mgaya, Theophil Alexander, Njaule Mdendu, Johnson Jasson, Sollomon Shati, Obed Msenga, Charles Nakembetwa, Gideon Mandesi, Isaac Kassanga, Dereck Kassanga, Deus Changala, Timilai Sheshangali, Shemaghembe Ntulwe, Sainet Katulunga, na wengine wengi sana. Waliosoma pale mmeombwa kuongezea majina ya wale mnaowakumbuka.
   Wengine ni Yohana Punguja, Mathew Maziku, Fikiri Charles, Batandika Mtaganya, Nkuba, Paul Daud.


  Page 4 of 4 FirstFirst ... 234

  Similar Topics

  1. Mkwawa High School mpo?
   By Kitia in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 137
   Last Post: 11th January 2014, 15:00
  2. Tanzania tele-high school
   By SolarPower in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 0
   Last Post: 2nd June 2011, 17:30
  3. Mkwawa high school: Singo hii inakukumbusha nini?
   By NewDawnTz in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 26
   Last Post: 21st May 2011, 00:41
  4. High School Sweethearts
   By n00b in forum Jokes/Utani + Udaku/Gossips
   Replies: 3
   Last Post: 23rd September 2008, 10:42
  5. Kenya to scrap high school fees
   By Icadon in forum International Forum
   Replies: 4
   Last Post: 2nd May 2007, 14:24

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...