Jukwaa la Elimu (Education Forum)Educational discussions in here... If you have some College/School materials and you wanna give them to your fellows pls do that favour to them. Let them get educated here! Become a Member to enjoy more stuffs
Kwa wale Ilborins Mnakumbuka hii Misamiati jamani?
KITEI = Kipunga Iva Tule Elimu Inatungoja (Wali)
CHUI = CHUkua chako Iboru (Ugali aka Bondo)
SUMU = Haya yalikuwa Makande
Half Life = Jina Maarufu la kiporo hasa cha SUMU au KIETI ( tulikuwa tunachanganya na Uji)
Umenyeni = Kijiji around Ilboru
Baghdad = Hii siikumbuki mwenye kukumbuka anikumbushie
Golgota = Huu ni Ukumbi juu ya Maktaba ambapo ndipo NECTA inafanyika
Mtego = Chandarua
KUKU = Kalale Upitwe Kama Umesimama ( Usingizi)
Twiga = Sikumbuki
Kufufuka = Kuamka Ucku wa Manane
Bafu Kubwa = Eneo Chini ya Daraja ambako Vijana hupenda kwenda Kuoga
Chief = Mwalimu katili kabisa na mpenda sifa Losujaki ,sijui sasa hivi yuko wapi
Kite = Alikuwa headmaster , Kitemango
Enabo = Enaboishi, hii ni shule Fulani ambayo walikuwa hawaivi na Ngarenaro,totoz zilikuwa
zinagombania Ilborians
Ilboru ni Ilboru tuu. Mimi ni wa Enzi za Bino. Japo alikuwa mkali kupindukia lakini dicipline yake imesaidia kujunga tabaka la mafakio kwa walipitia mikononi mwake. Nakumbuka sana bweni langu Oldonyo as an A-Level sikufua nguo zaidi za ndani. Form one from were proud not to let big brothers do the wash. Ilikuwa ni Ilboru ya heshima mbele. Akina siye tuliyeripoti pale toka Tambaza, Tambaza kweli, mbona tuliyookea hapo.
Disco la KB na Weruweru limesaidia baadhi yetu wa enzi hizo kuna watu zaidi ya 10 walijipatia wenzi wao wa maisha na kengele kanisani zimelia.
Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wenzetu waliotangulia akiwemo Jamaa aliyeitwa Rundiyaeli Masawe wa Boma Ng'ombe na Ujerummani.
Jamani Ilboru ile inatukumbusha mbali wee acha tuu.
Baghdad ni ile sehemu ambayo jamaa walikuwa wanakwenda kupata ganja na fegi kupunguza stress zao za masomo. Remember Mtui, Masaki , Medukenya, Kimasia,Machakura, Mama Mutabuzi, Boi, Quaressi,Lolo, Kweka, Chifu and Blanca and many more. Kwa madenti Carlos Mwaibula, Elisante Stanley, Jose James, Victor Maleko, Steven Alfred/Ras. Rajabu Masale Kaka Zanda,Bandama,Omneni Laiser , Freddy Lowasa Olais Mwing'ori jamaa alikuwa vice prefect alikuwa mnoko sio mchezo. Kipindi hicho wasukuma walikuwa na magovi jamaa mmoja alikuwa na pesa akajitolea kuwatahiri. Namkumbusha mshikaji analikumbuka KATARA? Shule yangu Ilboru inasifika sana popote ninapoenda inasifika sana (Wimbo wa shule) Naishia hapa kwa leo...
Huyo jamaa kwenye bold best wangu sana! alinipokea nilipoingia pale form V, mara ya mwisho nilikutana nae Jersey City in late 90's.
Dah eeebana we noma!! huo mlango wa kwanza hapo nyuma ya jamaa ktk hiyo picha ni room one ya Kilimanjaro.....niliishi humo mwaka mzima wakati nipo form VI!! Umenikumbusha mbali sana mazee....siku ya mwisho, tulichinja mbusi na washkaji kuiga room kwa nyama choma!!
Ab-Tichaz, naona Rungwe kwa mbaali na pia pembeni ni yale mabweni ya form six (form seven) Assembly hall, naiona chapel nayo inajitokeza kiaina mwihsoni kule kwenye miti na nini!! dah mzee imekuwa more than 16 years sijapita viwanja pale..... big up mate nice clip mkuu....
Karibu sana niko mbioni na nitaongeza zengine pindi ninapomaliza kazi hapa.
Subiri.
Dah eeebana we noma!! huo mlango wa kwanza hapo nyuma ya jamaa ktk hiyo picha ni room one ya Kilimanjaro.....niliishi humo mwaka mzima wakati nipo form VI!! Umenikumbusha mbali sana mazee....siku ya mwisho, tulichinja mbusi na washkaji kuiga room kwa nyama choma!!
Asante sana....room hiyo kuna memories nyingine sana, kuna mshkaji alivuta kabla hatuja maliza, watu kushindwa kupanda ngazi tokana na tungi jingi wakati wa wkend na vituko vya "kapteni Rume" na kikopo chake cha kuchukulia ng'ande.....!!
duh, asante sana...naona bweni langu la mwanzo Hanang picha ya juu! chini hapo picha ya tatu naona darasa langu form V PCB enzi hizo...sijui bado ni darasa au?? Katara....LOL.
Asante sana....room hiyo kuna memories nyingine sana, kuna mshkaji alivuta kabla hatuja maliza, watu kushindwa kupanda ngazi tokana na tungi jingi wakati wa wkend na vituko vya "kapteni Rume" na kikopo chake cha kuchukulia ng'ande.....!!
Kumbe dogo ulianza zamani eeeh? Sasa kuwa mwangalifu dogo maana huko unakoelekea ni kwenye alcoholism....
Sweet memories... Katara, hilo school bus kumbe bado lipo? Viva Ilboru and Viva Ilborians. Hiyo picha ya kwanza na ya pili kama vile zile siku za usafi??? Najaribu kukumbuka kwa mbali. Hawa jamaa walio mbele ya Katara wananikumbusha mbali sana, mmojawapo kama vile chalii angu Olais, but that was long time ago (96s). Ile picha nyingine iliyoonyesha Chapel inachomoza kwa mbali, inanikumbusha vipindi vya UKWATA kila jioni na ibada za Jumapili ambazo tulikuwa tunahudumiwa na a certain confused old man, at least we called him "Clergy".