Jukwaa la Elimu (Education Forum)Educational discussions in here... If you have some College/School materials and you wanna give them to your fellows pls do that favour to them. Let them get educated here! Become a Member to enjoy more stuffs
Kwa wale Ilborins Mnakumbuka hii Misamiati jamani?
KITEI = Kipunga Iva Tule Elimu Inatungoja (Wali)
CHUI = CHUkua chako Iboru (Ugali aka Bondo)
SUMU = Haya yalikuwa Makande
Half Life = Jina Maarufu la kiporo hasa cha SUMU au KIETI ( tulikuwa tunachanganya na Uji)
Umenyeni = Kijiji around Ilboru
Baghdad = Hii siikumbuki mwenye kukumbuka anikumbushie
Golgota = Huu ni Ukumbi juu ya Maktaba ambapo ndipo NECTA inafanyika
Mtego = Chandarua
KUKU = Kalale Upitwe Kama Umesimama ( Usingizi)
Twiga = Sikumbuki
Kufufuka = Kuamka Ucku wa Manane
Bafu Kubwa = Eneo Chini ya Daraja ambako Vijana hupenda kwenda Kuoga
Chief = Mwalimu katili kabisa na mpenda sifa Losujaki ,sijui sasa hivi yuko wapi
Kite = Alikuwa headmaster , Kitemango
Enabo = Enaboishi, hii ni shule Fulani ambayo walikuwa hawaivi na Ngarenaro,totoz zilikuwa
zinagombania Ilborians
Samahani msinishambuliee natoka nje kidogo. Hivi mliwezaje kusoma bila mademu? Yaani wanaume watupu?
We sajo nani kakwambia kuwa tulisoma bila "mademu"??? Mademu walikuwepo ila hawakuwa wanafunzi wa Ilboru. Tofauti ya Ilboru na Mkwawa ni kwamba Ilboru imezungukwa na shule kibao za mchanganyiko. Na iko proximal to city centre ambapo kuna shule kibao za day na boarding.
__________________
"To whom much is given, much is expected"
Baghdad ni ile sehemu ambayo jamaa walikuwa wanakwenda kupata ganja na fegi kupunguza stress zao za masomo. Remember Mtui, Masaki , Medukenya, Kimasia,Machakura, Mama Mutabuzi, Boi, Quaressi,Lolo, Kweka, Chifu and Blanca and many more. Kwa madenti Carlos Mwaibula, Elisante Stanley, Jose James, Victor Maleko, Steven Alfred/ Ras. Rajabu Masale Kaka Zanda,Bandama,Omneni Laiser , Freddy Lowasa Olais Mwing'ori jamaa alikuwa vice prefect alikuwa mnoko sio mchezo. Kipindi hicho wasukuma walikuwa na magovi jamaa mmoja alikuwa na pesa akajitolea kuwatahiri. Namkumbusha mshikaji analikumbuka KATARA? Shule yangu Ilboru inasifika sana popote ninapoenda inasifika sana (Wimbo wa shule) Naishia hapa kwa leo...
Unakumbuka mikate ya "sunkista" pale kwa Loning'o? hv mama tonii bado anapika pilau kule chini? nasikia Shembilu alivuta je ni kweli? Kishuu na Geree bado wapo?
Shembilu aka Mswahili (RIP), Mgaya (RIP)
Kaka umenikumbusha kwa Loning'o, ha ha haaaaa Clasa areaaaa,
We sajo nani kakwambia kuwa tulisoma bila "mademu"??? Mademu walikuwepo ila hawakuwa wanafunzi wa Ilboru. Tofauti ya Ilboru na Mkwawa ni kwamba Ilboru imezungukwa na shule kibao za mchanganyiko. Na iko proximal to city centre ambapo kuna shule kibao za day na boarding.
Kuna kipindi fulani walipelekwa pale mabinti wawili mmoja alikua ana asili ya kiarabu, watoto wa watu walikua wanatongozwa mpaka wakifika kwao wako hoi.
kule kwa bwashee, kishuu, mama natry, mikate ya boflo (Loning'o) na visu (dinning hall)........ duh si mchezo..... na mambo ya Bino Road, MZC (Mzee Zidisha Chui)......... lecture theater, sick bay, tololwa.......... ha ha haaaa....... that was looooong loooooooong time ago!!! Mwalimu Juma (RIP), Mutabuzi (RIP).........
wazee wa gongo, ganja na mbege (kwa bwashee), nyagi na safari & pilsner export (Loning'o).......
lile one ten la blue lilikuwaga STG.......
....hawana lolote hawa mbele ya Umbwe.....tumewakimbiza kutoka weruweru, kibosho mpaka wameishia kwa wamenye wenzao Enaboishu duh!!!
Mti safi, where is Lobilo wajameni...alikua legend wa unoko (equivalent wa Macha kwa Ilboru)..Savimbi? Mzee Kirama? Ile flamboyante tree kati ya form four na dh? Kupiga dipu? Kule 'Cambridge'? Seiya aka jogoo? Swai aka domain?
Quote:
Umbwe walevi wa mbege tu....hawana mpango wowote!, enzi zetu tuliwaputa Machame Girls, Zoo na Ashira Girls! LOL, wakabaki kulialia tu...
Mbege tuliita Nnya..karibia na Mto Umbwe kulikua na kalbu moja spesho wa wanafunzi (mwalimu akijifanya kwenda pale anapewa mbege yenye maji), lakini kitabu kama kawa.
Quote:
Acha maneno bana...Mti safi tumewatesa sana nyie mpaka mkakimbia Weru Weru. Mkaanza kugombea watoto wa O'Level wa Machame Girls na competition yenu.. Lyamungo Sec.
Caught in between Mkuu...I did both (Umbwe/Ilboru)!
Sweet sweet memories
Mmenikumbusha mbali sana. Mzulu na hotuba zake za two hours kwa form five and form ones kuwaeleza namna Ilboru ilivyo na kupata three is as good as kufeli. Mikate ya kwa Loning'o.... ukimuuliza mikate shs ngapi, anakuambia "..bia mbili" meaning mia mbili.
Machakura was the great, funny? guy i have ever met. I remember in one of the school baraza iliposemwa kwamba the only means of communication was in English, na ilipofika zamu yake kama kawaida yake kutoa matangazo he started with ...Aroo, after this exercise..." maneno yakamwishia na kicheko kilichofuata toka kwa wanafunzi kilitosha kuvunja baraza kabisa.
That school song:
Shule yangu Ilboru inasifika sana
Popote ninapokwenda inasifika sana
Kwa elimu (sijui na nini) inasifika sana
Shule yangu nakupenda...
Enzi za Mr. Msaki (Headmaster) kama tulivyo muita an object in the box, kwenye ile ofisi yake ambayo ilikuwa kama in hang vile...
Mambo ya half life, mbona ilikuwa raha? 94-96 kulikuwa na a crazy young man PCM anaitwa Frank, the guy was funny... Oh Ilboru!!!
Wakati wa kampeni za uchaguzi jamaa akawa anahutubia wananchi pale uwanja wa kanisani alisema "Ekenywa na Sekondari, oyeee" Jamaa wa Ekenywa wakawa offended kwa kuwa nao walikuwa ni secondary.