Jukwaa la Elimu (Education Forum)Educational discussions in here... If you have some College/School materials and you wanna give them to your fellows pls do that favour to them. Let them get educated here! Become a Member to enjoy more stuffs
Kwa wale Ilborins Mnakumbuka hii Misamiati jamani?
KITEI = Kipunga Iva Tule Elimu Inatungoja (Wali)
CHUI = CHUkua chako Iboru (Ugali aka Bondo)
SUMU = Haya yalikuwa Makande
Half Life = Jina Maarufu la kiporo hasa cha SUMU au KIETI ( tulikuwa tunachanganya na Uji)
Umenyeni = Kijiji around Ilboru
Baghdad = Hii siikumbuki mwenye kukumbuka anikumbushie
Golgota = Huu ni Ukumbi juu ya Maktaba ambapo ndipo NECTA inafanyika
Mtego = Chandarua
KUKU = Kalale Upitwe Kama Umesimama ( Usingizi)
Twiga = Sikumbuki
Kufufuka = Kuamka Ucku wa Manane
Bafu Kubwa = Eneo Chini ya Daraja ambako Vijana hupenda kwenda Kuoga
Chief = Mwalimu katili kabisa na mpenda sifa Losujaki ,sijui sasa hivi yuko wapi
Kite = Alikuwa headmaster , Kitemango
Enabo = Enaboishi, hii ni shule Fulani ambayo walikuwa hawaivi na Ngarenaro,totoz zilikuwa
zinagombania Ilborians
mumezungumzia ilboru mumenikumbusha mbali sana na mimi nilikuwa shule ya jirani pale Ekenywa nimepiga mwaka pale,si vumbi hilo kupandisha kutoka mjini,nilitokea Enaboishu baada ya kupewa suspesion ndo nikapiga mwaka pale kumalizia o'lever,mwaka 98.MTM ulikua mwaka gani ilbori?maana hata ile disco tushatembeleana sana michezo.ilikuwa ni shule yenye vipaji maalum ilboru
Tabu, mambo ya discipline master Mshanga nini? ndo yaliyokufanya ukatimkia Ekenywa!!! Nani aliyesoma Enaboishu hasiyemjua Mshanga na ubabe wake!!!
Hakika mmenikumbusha mbali sana hapa ILBORU. mimi nilipita pale 1985 -87 form five na six HGL. nilipangiwa kukaa bweni la hanang lakini mimi nilikaa MERU.
Nilikuwa mwenyekiti wa waislamu na mwenyekiti wa ulinzi
Nimewakumbuka sana waalimu wangu Kwanza BINO( Head master) Mzava ( maarufu kama Mapambano), Medukenya (Mzuru) mwl wangu Mzava Kapombe, Mwl Mushi (Mke wa capt), Mwl Jumaa (Bwana kaka) na wengine wengi.
naukumbuka kwa mbali sana wimbo wa shule especially wakati wa MZEE BANGO.
Shule yangu Ilboru inasifika sana.
Popote ninapokenda Inasifika sana.
Kwa usafi na ......, Inasifika sana,
Walimu wafanyakazi, wasifika sana.
......
...
Shule yangu nakupeenda.
Hakika hii ilikuwa ni shule best katika Tanzania. jamani nipeni habari za waalimu hawa BINO, KAPOMBE na Mwl JUMA wapo. naomba mawasiliano nao.
duh, nimekumbuka kina Blanka Shao, Moikan, Kimaro na yule wa konyagi pale kwa Loning'o (Johnson) alikuwa anafundisha kiswahili miaka ya mwisho ya 80, nimemsahau jina (is it Kimasiha??)....
Kuna mzee wa Mh, ndio bwana mzee (RIP, Juma) etc.....
duh, nimekumbuka kina Blanka Shao, Moikan, Kimaro na yule wa konyagi pale kwa Loning'o (Johnson) alikuwa anafundisha kiswahili miaka ya mwisho ya 80, nimemsahau jina (is it Kimasiha??)....
Kuna mzee wa Mh, ndio bwana mzee (RIP, Juma) etc.....
Duh kweli imekuwa zamani...
Aisee kuna jamaa mmoja alikuwa anaitwa Chacha Horombe, yuko wapi?