JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

  Report Post
  Page 1 of 2 12 LastLast
  Results 1 to 20 of 24
  1. Lyimo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th March 2006
   Posts : 3,798
   Rep Power : 26587
   Likes Received
   1979
   Likes Given
   825

   Default Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Nimestushwa na taarifa ya serikali kutaka kujenga chuo kikuu kingine cha Kilimo katika mkoa wa Katavi, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira la leo. Sababu ya mstuko huo ni hali mbaya ya vyuo vyetu vya kilimo vilivyopo ambayo vinashindwa kijikidhi na kutoa huduma stahiki kutokana na bajeti finyu inayopokea kutoka serikalini. Chuo kikuu kilichopo (SUA) bado kinahitaji kujitanua na hakijajitosheleza wataalamu, hivyo ni heri serikali ingeongeza nguvu kwenye chuo hicho kama inajali zaidi wakulima. Kwa miaka ya karibuni sasa kumekuwa na mfumuko wa vyuo vikuu Tanzania jambo lililopelekea hata kushusha viwango vya kuingia kwenye vyuo hivyo, jambo ambalo lilibarikiwa na Tume ya vyuo Vikuu (TCU). Mfumuko huu utasababisha kutozalisha wataalamu waendeshaji/ watendaji wenye ngazi ya Diploma na Cerificates ambao ni wanahitajika sana kutokana na mahitaji ya Taifa. Bado wataalamu wa Kilimo hawatoshelezi Kata zote nchini, licha kimfumo kila kijiji kinahitaji bwana shamba na bwana mifugo ambao vijiji vingi sana hawana, hivyo hata kupata maelekezo/ushauri wa kitaalamu haiwezekani. Sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kina katika kuwekeza kwenye mahitaji ya wataalamu wa kilimo nchini.

   Vyuo vya Kilimo na Utafiti vya serikali ninavyovikumbuka kwa uchache, (wachangiaji mtanisaidia kuongezea vingine vingi):
   - Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) – Morogoro;
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Uyole – Mbeya
   - Chuo cha maendeleo ya Mifugo Tengeru (LITI-Tengeru) – Arusha
   - Tengeru Horticultural Reasearch and Trainning (HORTI).- Arusha
   - Chuo cha kilimo na Utafiti Kilombero (KATRIN) – Morogoro
   - Chuo cha Kilimo taaluma ya umwagiliaji Igurusi - Mbeya
   - Chuo cha kilimo na Utafiti Ilonga (MATI – Ilonga) – Morogoro
   - Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro (KATC) - Kilimanjaro
   - Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Mlingo
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Morogoro (LITI – Morogoro) – Morogoro
   - Chuo Cha Utafiti wa Kilimo Cha Ukiriguru
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Buhuri (LITI – Buhuri) – Tanga
   - Chuo cha Maendeleo ya Kilimo Inyala – Mbeya
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) – Arusha
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Mpwapwa (LITI – Mpwapwa) - Mpwapwa
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele – Mtwara
   - Chuo cha utafiti wa Kilimo Tumbi – Kibaha
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Mlingano – Tanga
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Tumbe – Tabora
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa magonjwa ya wanyama (ADRI) – DSM
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Madaba - Songea

   Vyuo hivi vingeweza kutumika vizuri kufundisha wataalamu na hata wakulima ili kuweza kuendesha kilimo chenye tija. Tukumbuke kuwa, wananchi wengi maskini Tanzania ni wakulima, hivyo tukiacha hivi vyuo vijiendeshe kibiashara kama vyuo vya uhasibu ama IT ambavyo wahitimu wake ni rahisi kuajiriwa mijini. Vilevile mazingira bora ya watumishi wa vijijini yanahitajika ili kuwavutia wataalamu kufanya kazi vijijini. Kama serikali haitaweka kipaumbele kwenye kuboresha miundombinu vijijini na kuelimisha wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija ni dhahiri kuwa wimbi la vijana kukimbilia mijini halitakoma. Serikali ilitakiwa kuvisaidia kwa hali na mali vyuo hivi vilivyotawanyika nchi nzima japo vina wataalamu wachache bado. Sioni mantiki ya kukimbilia Kujenga chuo kikuu cha Kilimo Katavi wakati wahadhiri/watafiti hawapo wa kutosha nchini (SUA haijajitosheleza bado). Vilevile kwa Tanzania ya leo bado ni ndoto kuwa na mabwana shama wenye taaluma ya degree, hivyo ni vema tukaweka mkazo kwanza kwenye hivi vyuo vya diploma na certificate. Wakati utafika ambapo tutakuwa na hitaji la vyuo vikuu baada ya kujitosheleza kwenye hii ngazi ya kati kimahitaji. Swala la Chuo kikuu Katavi ni la haraka mno na linaonekana lina maslahi kisiasa zaidi kuliko kutoa huduma ya elimu, ushauri na utafiti kwa wananchi.
   "Wisdom is not a product of schooling, but of the lifelong attempt to acquire it"

  2. Ms Judith's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th December 2010
   Posts : 2,570
   Rep Power : 1106
   Likes Received
   884
   Likes Given
   604

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   si unajua sera zetu za sasa ni kuwa na institutions za kikata? hopefully, kitakuwa chuo kingine cha kata!
   Mtu awaye yote asiyempenda BWANA, na awe amelaaniwa. MARAN ATHA!!!
   (1 Wakorintho 16:22)

  3. Gurudumu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th February 2008
   Posts : 2,355
   Rep Power : 1192
   Likes Received
   250
   Likes Given
   104

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Pale wananchi watakapokuwa na nguvu ya kuamua pesa zao zitumike kufanya nini ndipo tutakapoachana na bajeti zinazofuata kuwapendezesha na kuwapa utukufu wanasiasa. Possibly kitaitwa Mtoto wa Mkulima University

  4. chetuntu's Avatar
   R I P Array
   Join Date : 10th January 2011
   Location : Paediatrique ward
   Posts : 955
   Rep Power : 747
   Likes Received
   101
   Likes Given
   90

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Ipo kisiasa zaidi.

  5. Nyambala's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th October 2007
   Location : Tahiti
   Posts : 4,495
   Rep Power : 1668
   Likes Received
   1098
   Likes Given
   971

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Hi kile cha JK Nyerere Agricultural university - Musoma kilichoahidiwa na jk wakati wa kampeni kiliishia wapi?

  6. meddie's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2010
   Posts : 385
   Rep Power : 648
   Likes Received
   83
   Likes Given
   8

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   hapa nchini fani yenye wasomi wengi kuliko zote na PH kibao ni kilimo!!! lakini ebu nambie ....

  7. Sooth's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2009
   Posts : 1,284
   Rep Power : 3463047
   Likes Received
   585
   Likes Given
   286

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Quote By lyimo View Post
   Nimestushwa na taarifa ya serikali kutaka kujenga chuo kikuu kingine cha Kilimo katika mkoa wa Katavi, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira la leo. Sababu ya mstuko huo ni hali mbaya ya vyuo vyetu vya kilimo vilivyopo ambayo vinashindwa kijikidhi na kutoa huduma stahiki kutokana na bajeti finyu inayopokea kutoka serikalini. Chuo kikuu kilichopo (SUA) bado kinahitaji kujitanua na hakijajitosheleza wataalamu, hivyo ni heri serikali ingeongeza nguvu kwenye chuo hicho kama inajali zaidi wakulima. Kwa miaka ya karibuni sasa kumekuwa na mfumuko wa vyuo vikuu Tanzania jambo lililopelekea hata kushusha viwango vya kuingia kwenye vyuo hivyo, jambo ambalo lilibarikiwa na Tume ya vyuo Vikuu (TCU). Mfumuko huu utasababisha kutozalisha wataalamu waendeshaji/ watendaji wenye ngazi ya Diploma na Cerificates ambao ni wanahitajika sana kutokana na mahitaji ya Taifa. Bado wataalamu wa Kilimo hawatoshelezi Kata zote nchini, licha kimfumo kila kijiji kinahitaji bwana shamba na bwana mifugo ambao vijiji vingi sana hawana, hivyo hata kupata maelekezo/ushauri wa kitaalamu haiwezekani. Sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kina katika kuwekeza kwenye mahitaji ya wataalamu wa kilimo nchini.

   Vyuo vya Kilimo na Utafiti vya serikali ninavyovikumbuka kwa uchache, (wachangiaji mtanisaidia kuongezea vingine vingi):
   - Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) – Morogoro;
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Uyole – Mbeya
   - Chuo cha maendeleo ya Mifugo Tengeru (LITI-Tengeru) – Arusha
   - Tengeru Horticultural Reasearch and Trainning (HORTI).- Arusha
   - Chuo cha kilimo na Utafiti Kilombero (KATRIN) – Morogoro
   - Chuo cha Kilimo taaluma ya umwagiliaji Igurusi - Mbeya
   - Chuo cha kilimo na Utafiti Ilonga (MATI – Ilonga) – Morogoro
   - Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro (KATC) - Kilimanjaro
   - Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Mlingo
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Morogoro (LITI – Morogoro) – Morogoro
   - Chuo Cha Utafiti wa Kilimo Cha Ukiriguru
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Buhuri (LITI – Buhuri) – Tanga
   - Chuo cha Maendeleo ya Kilimo Inyala – Mbeya
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) – Arusha
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Mpwapwa (LITI – Mpwapwa) - Mpwapwa
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele – Mtwara
   - Chuo cha utafiti wa Kilimo Tumbi – Kibaha
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Mlingano – Tanga
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Tumbe – Tabora
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa magonjwa ya wanyama (ADRI) – DSM
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Madaba - Songea

   Vyuo hivi vingeweza kutumika vizuri kufundisha wataalamu na hata wakulima ili kuweza kuendesha kilimo chenye tija. Tukumbuke kuwa, wananchi wengi maskini Tanzania ni wakulima, hivyo tukiacha hivi vyuo vijiendeshe kibiashara kama vyuo vya uhasibu ama IT ambavyo wahitimu wake ni rahisi kuajiriwa mijini. Vilevile mazingira bora ya watumishi wa vijijini yanahitajika ili kuwavutia wataalamu kufanya kazi vijijini. Kama serikali haitaweka kipaumbele kwenye kuboresha miundombinu vijijini na kuelimisha wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija ni dhahiri kuwa wimbi la vijana kukimbilia mijini halitakoma. Serikali ilitakiwa kuvisaidia kwa hali na mali vyuo hivi vilivyotawanyika nchi nzima japo vina wataalamu wachache bado. Sioni mantiki ya kukimbilia Kujenga chuo kikuu cha Kilimo Katavi wakati wahadhiri/watafiti hawapo wa kutosha nchini (SUA haijajitosheleza bado). Vilevile kwa Tanzania ya leo bado ni ndoto kuwa na mabwana shama wenye taaluma ya degree, hivyo ni vema tukaweka mkazo kwanza kwenye hivi vyuo vya diploma na certificate. Wakati utafika ambapo tutakuwa na hitaji la vyuo vikuu baada ya kujitosheleza kwenye hii ngazi ya kati kimahitaji. Swala la Chuo kikuu Katavi ni la haraka mno na linaonekana lina maslahi kisiasa zaidi kuliko kutoa huduma ya elimu, ushauri na utafiti kwa wananchi.
   Mi naona huu ni uamuzi wa kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Hivi kweli tuna tatizo la wataalamu wa kilimo? Serikali haijui adha wanayopata wanafunzi wa SUA ktk soko la ajira?Kuna wanafunzi wengi wa SUA wako ktk mabenki na wengine ni waalimu wanafundisha shule za sekondari kwa leseni. Na wengine wapo tu mtaani, hii ina maana serikali inasomesha nguvukazi ambayo haitumiki ipasavyo. Serikali inapaswa kufanya utafiti kwanza kabla ya kuanzisha vyuo vikuu mbali mbali huku ikiviacha vingine yatima (kifedha). Kuna faida gani ya kuwa na vyuo vingi vilivyojaa maTA (ambao nao kimsingi ni wanafunzi), badala ya kuwa na vichache vyenye ubora wa miundombinu na wabobezi? Kupeleka Chuo Kikuu cha Kilimo Katavi ni kumfurahisha Ndugu Pinda kwa kuwa anapenda kulima.
   "Iko siku haki itashinda na hiyo ndio siku utakapojua tofauti ya kuvua chupi na kuvua samaki."-Mohammed Ali-KTN.

  8. babayah67's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th March 2008
   Location : Makasuku
   Posts : 485
   Rep Power : 802
   Likes Received
   66
   Likes Given
   9

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Ahhh kaka hujui sera ya serikali ya awamu ya nne chini ya JK??? Basi ni kujenga chuo kikuu katika kila majimbo ya uchaguzi wanayotoka viongozi wakuu wa serikali. Ilianza University ya Bagamoyo kwa JK, haya sasa inakuja university jimboni kwa Mtoto wa mkulima, usishangae ukisikia kikifuatia jimboni kwa Ghalibu bilali au kwa Makinda!!!

  9. DUNIANGUMU JR's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th April 2011
   Posts : 43
   Rep Power : 549
   Likes Received
   14
   Likes Given
   6

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   kila kiongozi CCM anakilmbilia kuwekeza kwao, hii rushwa mamboleo! huoni shule ya msingi kujengwa na wachina?
   Ni Nyerere tu hakufanikiwa kufanya hivyo.

  10. jambotemuv's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th February 2008
   Posts : 187
   Rep Power : 745
   Likes Received
   26
   Likes Given
   3

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Quote By lyimo View Post
   Nimestushwa na taarifa ya serikali kutaka kujenga chuo kikuu kingine cha Kilimo katika mkoa wa Katavi, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Majira la leo. Sababu ya mstuko huo ni hali mbaya ya vyuo vyetu vya kilimo vilivyopo ambayo vinashindwa kijikidhi na kutoa huduma stahiki kutokana na bajeti finyu inayopokea kutoka serikalini. Chuo kikuu kilichopo (SUA) bado kinahitaji kujitanua na hakijajitosheleza wataalamu, hivyo ni heri serikali ingeongeza nguvu kwenye chuo hicho kama inajali zaidi wakulima. Kwa miaka ya karibuni sasa kumekuwa na mfumuko wa vyuo vikuu Tanzania jambo lililopelekea hata kushusha viwango vya kuingia kwenye vyuo hivyo, jambo ambalo lilibarikiwa na Tume ya vyuo Vikuu (TCU). Mfumuko huu utasababisha kutozalisha wataalamu waendeshaji/ watendaji wenye ngazi ya Diploma na Cerificates ambao ni wanahitajika sana kutokana na mahitaji ya Taifa. Bado wataalamu wa Kilimo hawatoshelezi Kata zote nchini, licha kimfumo kila kijiji kinahitaji bwana shamba na bwana mifugo ambao vijiji vingi sana hawana, hivyo hata kupata maelekezo/ushauri wa kitaalamu haiwezekani. Sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kina katika kuwekeza kwenye mahitaji ya wataalamu wa kilimo nchini.

   Vyuo vya Kilimo na Utafiti vya serikali ninavyovikumbuka kwa uchache, (wachangiaji mtanisaidia kuongezea vingine vingi):
   - Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) – Morogoro;
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Uyole – Mbeya
   - Chuo cha maendeleo ya Mifugo Tengeru (LITI-Tengeru) – Arusha
   - Tengeru Horticultural Reasearch and Trainning (HORTI).- Arusha
   - Chuo cha kilimo na Utafiti Kilombero (KATRIN) – Morogoro
   - Chuo cha Kilimo taaluma ya umwagiliaji Igurusi - Mbeya
   - Chuo cha kilimo na Utafiti Ilonga (MATI – Ilonga) – Morogoro
   - Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro (KATC) - Kilimanjaro
   - Chuo cha Mafunzo ya Kilimo cha Mlingo
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Morogoro (LITI – Morogoro) – Morogoro
   - Chuo Cha Utafiti wa Kilimo Cha Ukiriguru
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Buhuri (LITI – Buhuri) – Tanga
   - Chuo cha Maendeleo ya Kilimo Inyala – Mbeya
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) – Arusha
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Mpwapwa (LITI – Mpwapwa) - Mpwapwa
   - Chuo cha Utafiti wa Kilimo cha Naliendele – Mtwara
   - Chuo cha utafiti wa Kilimo Tumbi – Kibaha
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Mlingano – Tanga
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa Kilimo cha Tumbe – Tabora
   - Chuo cha Mafunzo ya Utafiti wa magonjwa ya wanyama (ADRI) – DSM
   - Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Madaba - Songea

   Vyuo hivi vingeweza kutumika vizuri kufundisha wataalamu na hata wakulima ili kuweza kuendesha kilimo chenye tija. Tukumbuke kuwa, wananchi wengi maskini Tanzania ni wakulima, hivyo tukiacha hivi vyuo vijiendeshe kibiashara kama vyuo vya uhasibu ama IT ambavyo wahitimu wake ni rahisi kuajiriwa mijini. Vilevile mazingira bora ya watumishi wa vijijini yanahitajika ili kuwavutia wataalamu kufanya kazi vijijini. Kama serikali haitaweka kipaumbele kwenye kuboresha miundombinu vijijini na kuelimisha wakulima ili waweze kufanya kilimo chenye tija ni dhahiri kuwa wimbi la vijana kukimbilia mijini halitakoma. Serikali ilitakiwa kuvisaidia kwa hali na mali vyuo hivi vilivyotawanyika nchi nzima japo vina wataalamu wachache bado. Sioni mantiki ya kukimbilia Kujenga chuo kikuu cha Kilimo Katavi wakati wahadhiri/watafiti hawapo wa kutosha nchini (SUA haijajitosheleza bado). Vilevile kwa Tanzania ya leo bado ni ndoto kuwa na mabwana shama wenye taaluma ya degree, hivyo ni vema tukaweka mkazo kwanza kwenye hivi vyuo vya diploma na certificate. Wakati utafika ambapo tutakuwa na hitaji la vyuo vikuu baada ya kujitosheleza kwenye hii ngazi ya kati kimahitaji. Swala la Chuo kikuu Katavi ni la haraka mno na linaonekana lina maslahi kisiasa zaidi kuliko kutoa huduma ya elimu, ushauri na utafiti kwa wananchi.
   Nadhani cha Tabora ni TUMBI- siyo TUMBE. Kulikuwepo pia cha MARUKU - Kagera na kipo cha Minazi pwani sijui wakiitaje.

  11. pichuwanyi's Avatar
   Member Array
   Join Date : 13th January 2011
   Posts : 21
   Rep Power : 559
   Likes Received
   4
   Likes Given
   0

   Default

   Lyimo umesema vyema, katika harakati za serikali za kuongeza wataalam wa kilimo na mifugo (maafisa ugani) imekua ikiwasomesha kwenye vyuo vyake vya MATI na LITI, na wanahitimu huwapangia kazi ktk halmashauri zake, tatizo linakuja pale hao wataalam wanapokwenda kwenye maeneo ya kazi wanakutana na mazingira magumu ya kazi, maslahi mabovu, hakuna vitendea kazi, sasa anawezaje kugawa utaalamu alioupata kwa hao watanzani wenzetu ili kilimo na ufugaji viweze kumsaidia mkulima huyu ambaye Pinda anapigia kelele, w

  12. Katavi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st August 2009
   Location : Lyamba Lya Mfipa
   Posts : 31,878
   Rep Power : 271424181
   Likes Received
   5828
   Likes Given
   3414

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Kuna wale waliosomeshwa kwa mtindo wao wa zimamoto katika vyuo vya MATI na LITI, bado wapo mtaani ajira hakuna!

  13. Maimai's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 1st November 2010
   Posts : 174
   Rep Power : 600
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Gurudumu View Post
   Pale wananchi watakapokuwa na nguvu ya kuamua pesa zao zitumike kufanya nini ndipo tutakapoachana na bajeti zinazofuata kuwapendezesha na kuwapa utukufu wanasiasa. Possibly kitaitwa Mtoto wa Mkulima University
   .......:...... True mkuu kwani umestukiaje kwamba son of a poor dad anashadadia kupata umaarufu wa milele...MKP UNIVERITY OF AGRICULTURE... P.O BOX 00000 MPANDA RUKWA... JIWE LA MSINGI LILIWEKWA MWAKA 2012 NA WAZIRI..........BW MKP....TU du mizengo bwana... Shabaabi kweli kweli wa umaarufu wakati mafisadi wamemweka kwapani anapelekwa kama bajaza..

  14. Edward Teller's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st November 2010
   Location : Area 51
   Posts : 3,633
   Rep Power : 1292
   Likes Received
   613
   Likes Given
   692

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Click image for larger version. 

Name:	pinda et al.JPG 
Views:	22 
Size:	249.7 KB 
ID:	27904
   Waziri mkuu akizungumza na viongozi wa mfuko wa Dr David Livingstone Academy Ltd-mara baada ya kikao cha kujadili uanzishwaji wa chuo kikuu cha katavi
   Binafsi naona kuliko wangeanzisha chuo kipya-ni bora wangeboresha hiv vilivyopo sasa hivi
   “Talk slowly but think quickly”

  15. Bulesi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2008
   Posts : 5,953
   Rep Power : 32129417
   Likes Received
   1272
   Likes Given
   191

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Have you noticed one thing; kila waziri mkuu anapoingia madarakani ajenda yake ni kwanza ni kutengeneza mkoa mpya huko kwao anakotoka. Sumaye kabla ya kumaliza ngwe yake alitengeneza mkoa wa Manyara na sasa Pinda nae ametemgeneza mkoa wa Katavi na sasa anataka kupeleka chuo kikuu cha kilimo!! Is there any economic justification for a poor country like Tanzania to embark on such uncalled for projects? Huo wote ni kuonesha ubinafsi kwa hawa viongozi.

  16. Mahesabu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th January 2008
   Location : manzese
   Posts : 4,078
   Rep Power : 1659
   Likes Received
   565
   Likes Given
   5929

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   badala ya kupongeza hatua nzuri tunaponda.....MIMI NAPONGEZA TENA VYUO VINGI ZAIDI VIANZISHWE ILI PIA KUJIJENGA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO TUTAKAZOKUTANA NAZO NA KUZITATUA
   BILA RUSHWA..HAKI HAIPATIKANI....TOA RUSHWA UPATE HAKI.....(?)
   RUSHWA NA TANZANIA DAM-DAM.....!
   TAASISI IPI RUSHWA KWAO MWIKO?
   NASEMA KWA KUWA YAMENIKUTA......!

  17. Liwolo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 13
   Rep Power : 545
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Si unajua tena mwamba ngoma kamba kwake,KATAVI juzi mkoa leo University Agriculture

  18. Bulesi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th May 2008
   Posts : 5,953
   Rep Power : 32129417
   Likes Received
   1272
   Likes Given
   191

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Quote By Mahesabu View Post
   badala ya kupongeza hatua nzuri tunaponda.....MIMI NAPONGEZA TENA VYUO VINGI ZAIDI VIANZISHWE ILI PIA KUJIJENGA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO TUTAKAZOKUTANA NAZO NA KUZITATUA

   Tunachotaka ni kuwa na vyuo vyenye ubora na sio idadi; pale tutakapoweza kuvihudumia hivi tulivyokuwanavyo kwa kiwango cha kuridhisha hakuna ubaya kuongeza vingine vipya.

  19. mduwa's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 14th December 2007
   Posts : 3
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Angry Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   It is sickening to note that in the year 2011 there are still so many ignorant Tanzanians who have no clue what the meaning of higher education is. What escaped the narrow-minded who decried the idea of addition of a prestigious university to Tanzania in general and to Katavi in particular is the concept behind it.

   A university is more than issuance of degrees. Degrees are more than what gives individuals licence to work in airconditioned offices in big cities like Dar es salaam. Show me a degree holder (in anything) who doesn't have anything to do, you will be showing me an ignorant buffoon who has wasted public funds in creating nothing more than a useless robot of self.

   Higher education is supposed to open your mind to a higher level of thinking, higher level of reasoning, it is supposed to make you more inquisitive, more imaginative,definitely self-sufficient and forward looking. It is extremely idiotic to surmise that if you have a degree then you have to have an office job. If that is your thinking, then I am not surprised that there so many ignorant

   Tanzanians who are quite contended to clean other peoples toilets in UK, America, etc rather than go back to their villages and do real respectable work. Looking at another aspect, the original author of this despicable blog (and those who supported it) is the fact that this person hails from a place where there are 5 or more institutions of higher education.

   The whole of Western Corridor has no such luxury! Therefore, you don't need standard 7 education to figure out why an institution of higher education is so invaluable to this part of grossly marginalised world. Remember,Tanzania has massive land which is yet to be exploited commercially.

   In the next 25 years we will need to produce in excess of 50,000 agriculturists annually to be anywhere near meeting the shortage of people with suffient skills to make use of our land. And if the idea of starting such an expensive university is politically motivated, so what?

   And who gives a toss? What is important in the end is getting something useful for once. After all, is that not why we have politicians? Any politician who leaves a legacy of something as important as a university should be praised by all even if you never had a chance to get no more than primary education yourself.

  20. Rwamuhuru's Avatar
   Member Array
   Join Date : 22nd December 2010
   Location : Karatu, Arusha
   Posts : 50
   Rep Power : 569
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Chuo kikuu kipya cha kilimo Katavi, ni haraka mno

   Looking for something to say 2015.........no priorities these days, its just a matter of "what something physical and attractive" watakachotudanganya nacho kwenye next election
   "Whoever corrects a mocker invites insult; whoever rebuke a wicked man incurs abuse"

  Page 1 of 2 12 LastLast

  Similar Topics

  1. Jakaya Kikwete kuanzisha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Julius Nyerere
   By Nyambala in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 24
   Last Post: 20th December 2014, 06:31
  2. Chuo kikuu cha katavi kuanzishwa, cha Butiama kiko wapi?
   By tatanyengo in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 4
   Last Post: 20th April 2011, 14:36
  3. Chuo Kikuu kipya kuiinua Tabora
   By Rutashubanyuma in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
   Replies: 5
   Last Post: 10th February 2011, 23:34
  4. Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Wavumbua Kifaa kipya
   By kayundi2 in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
   Replies: 11
   Last Post: 27th May 2010, 09:07
  5. Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar
   By Kimeo in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 51
   Last Post: 8th July 2009, 11:24

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...