Re: Oral exminations at college/university level

By
mkamap
Mkuu Heshima yako
Mie pia na mtazamo kama wako na nimejaribu pia kushuhudia wezentu wanavyoendeleza mambo yao na kuendelea Na nikajaribu kubainisha kuhusu Elimu ya Vyuo vyetu ilivyo tofauti na vyuo vilivyomakini vitoavyo elimu bora ma CONSECUTIVES wa UDSM wakanipinga wakasema vyuo vikuu ni UNIVERSE wakapigiana makofi na elimu yetu inaendelea kua duni.
Nikaandika mfumo wetu wa Elimu unahitaji marekebisho watu wakaa kimya wakapuuzia .
Nikaandika kuishutumu UDSM na nikaifungamanisha na kudoda kwa uchumi wetu ma CONSECUTIVE kama kawaida wakapinga wachache tukakubaliana ktk hilo rejea topic hiyo.
Mwisho nami nasisitiza kua UFISADI/RUSHWA/mikataba mibovu Ni matokeo yakutukua na wasomi.Wasomi ni wale walioelimika wakawa waelewa Wengi tunaowaita wasomi ni wa kwenye makaratasi tu.HAkika msomi hawezi kuwa fisadi ,msomi hawezi kuingia mikataba ya kuiuza jamii yake katu.
Huku kutokua na wasomi ndiko kunakopelekea uchumi wetu kudumaa ilihiali tunakilasababu yakuwa matajiri.
Watu utakuta wanapiga kelele ooh CCM OOh CHADEMA,ooh CUF hakika hivi vyama havina ubavu wowote wakukuletea uchumi bora ,vyama ni kama moshi ELIMU ni MOTO ,sasa basi ukitaka kuzima moshi hunabudi kuzima kwanza motto,lakini ukikuta watu wanahangaika kuzuia moshi bila kuzima moto jua watu hao hawajaelimika.
Uchumi wetu hauleweki/mafisadi wamezidi/mikataba ya ulaghai imejaa hii ni kutokana hawajaelimika.Na njia ulizopendekeza ni sahihi kabisa kama chazo cha mchkato wa kurudisha Elimu iliyosahihi nahatimaye UCHUMI BORA. Ma consecutive kubalini kunamatatizo makubwa ktk elimu ya juu ya tz na kubalini mfumo uliopo sasa hauna tija unahitaji mabadiriko ya haraka.
Ndugu yangu kama ulikuwa unategemea jibu au mchango wewote ule kuhusu mambo yanayohitaji kutumia akili basi humu ktk jf utakuwa mkiwa siku zote... humu ukitaka upate washabiki na wachangiaji hoja wengi basi anzisha hoja kama "afrika imelaaniwa", "hii inatokea afrika tuu", "waafrika wabinafsi", "waafrika hawana akili ukilinganisha na watu wengine" n.k na ukitaka wakushabikie hasa basi uongezee na kuandika kwa lugha ya KIINGEREZA basi hapo mtajibishana mpka kukuche lkni kama unaandika mambo yenye AKILI na ya MAANA kama hayo uliyoorodhesha hapo juu hupati mtu na ndio maana unaona hii hoja imechangiwa mara tano tuu... hii inaonyesha ni jinsi gani uwezo wa kiakili wa watu wengi humu ulivyokuwa mdogo, kwa mfano mimi huwaga nawauliza humu kila siku kuna haja ya mtu kuandika hoja yeyote ile kiingereza wakati sisi wote humu lugha yetu ya kwanza ni KISWAHILI? sipati jibu...
sasa kurudi ktk hoja yako ninakubaliana na wewe 100% kuhusu chimbuko la matatizo yetu yoote yanayotukabili nchini mwetu nayo ni UBORA WA ELIMU YETU na hiyo inaanzia chini kabisa na sio chuo kikuu tuu, ni bado hatujaweza kuweka msingi imara ktk elimu yetu ya chini kwa maana nyingine mfumo wetu hautuandaii vyema kuweza "kuelimika" kutumia msemo wako, vyema na kuweza kufanikiwa na masomo ya chuo kikuu... kwa mfano ktk maisha yangu yoote nchini mwetu sijawahi kusikia hata siku moja serikali ikiongelea urekebishwaji na uboresishwaji wa mitaala ya shule za msingi sekondari, mfumo uliopo ndio ule ule alioacha mkoloni... kuna mambo mengi hapa kwa mfano ukweli ni kwamba ktk nchi yetu lugha ambayo inatumiwa na kueleweka bila matatizo yeyote na watu wetu ni KISWAHILI sasa ni kwa nini mtoto afundishwe masomo yote kiingereza?? mimi nikichukulia uzoefu wangu shule ya msingi tulifundishwa kila kitu kiswahili, baada ya hapo nikabahatika kusoma tabora boys ambayo ilikua inajulikana kama shule maalumu kwa watu wenye vipaji maalaumu, na kule kila kitu kikabadilika ghafla na kuwa kiingereza na ukweli ni kwamba mimi pamoja na wenzangu tulipata shida sana na tukawa hatuelewi mwalimu anachosema kwa hiyo tukawa tuna buruzwa tuu na miaka inakwenda.. swali langu ni kwamba Je ni kwa nini mtu anashindwa kuliona hilo?? hauwezi ukafanikiwa ktk masomo yako vizuri kama hata lugha unayofundishiwa hauilewi vizuri...
Na hii inajionyesha ktk mambo mengi nchini mwetu sasa ukija kwenye mikataba ni kwa nini mkataba uandikwe kiingereza? kwa nini usitafsiriwe? Je hauoni kwamba kama mkataba ungeandikwa kwa lugha yetu yule aneusoma labda ingeongeza uelevu wake na kisha labda ingesaidia kiasi fulani?
kwa hiyo mambo ni mengi na yote chanzo chake ni kimoja nacho ni kuutambua na kuukubali UKWELI nakisha baada ya hapo kuanza kuufanyia kazi, na mimi nafikiri kwanza kabisa tukubali kwamba sisi kiingereza sio lugha yetu hivyo basi haiwezekani kama mtu amezaliwa na kukulia tz kuweza kukimudu vizuri kiingereza kiasi cha kuweza kuelewa vizuri kinachoongelewa darasani au kwenye vitabu (mtanzania wa kawaida ni yule anaeshi magomeni au sinza au temeke)...
na baada hapo basi mimi nina imani mambo yataanza kwenda vizuri, napenda ukumbuke pia kwamba nchi ni ya pekee ktk mengi ktk dunia hii, sisi ni wa pekee, matatizo makubwa ambayo jamii zingine zinakabiliana nayo sisis hatuna.. hata nchi zilizoendelea mimi nafikiri pia wbado wana matatizo makubwa ya kutatua kuliko sisi.. kwa hiyo tunaweza kutatua matatizo yetu haraka sana ikama watu kama wewe na mimi na baadhi ya wengine hatutachoka kufanya kile ambacho tumejaliwa kuwa nacho nacho uwezo wa kuuona ukweli....
Ni rahisi sana Kwa ngamia kupenya kwenye Tundu Lisu la Sindano kuliko Kiongozi Bora kupatikana kwa njia ya Kupiga Kura Tanzania!
Follow Us Here