Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Serikali yaunda tume ya vyuo vikuu • Itachunguza utata wa mikopo ya wanafunzi

    <
    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,737
      Rep Power : 12927
      Likes Received
      4439
      Likes Given
      7465

      Default Serikali yaunda tume ya vyuo vikuu • Itachunguza utata wa mikopo ya wanafunzi

      Serikali yaunda tume ya vyuo vikuu
      • Itachunguza utata wa mikopo ya wanafunzi

      na Happiness Mtweve, Dodoma


      RAIS Jakaya Kikwete ameunda tume ya wataalamu 11, kufanya mapitio ya mfumo wa uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kuundwa kwa tume hiyo kulitangazwa jana mjini hapa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
      Waziri Mkuu alisema lengo la tume hiyo ni kutaka kuimarisha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini.
      Alieleza kuwa tume hiyo itafanya kazi kwa miezi miwili kuanzia Febeuari 14 mwaka huu na itatakiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi Aprili 15.
      Alisema tume hiyo itaongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Profesa Makenya Maboko.
      Wajumbe ni Masoud Mohamed Haji ambaye ni Ofisa Mahusiano wa Kimataifa, Dk. Eliawony Kristosia Meena, mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu cha Tumaini Arusha na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Zanzibar.
      Wengine ni Paul Daniel Magwiza, Naibu Katibu Tume ya vyuo vikuu, Sarah Baharamoka, Mkurugenzi Msaidizi Uandishi Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Penina Mlama, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa tawi la Tanzania la taasisi inayopigania elimu kwa wanawake.
      Pinda aliwataja wajumbe wengine wa tume hiyo kuwa ni Deo Mbasa Daud ambaye ni ofisa taaluma wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Kassim Almasi Umba, ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro na Anderson Mlabwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mikopo Benki ya CRDB.
      Wengine ni ni Profesa Wilbert Abel Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Rosemary Rulabuka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania.
      Alieleza kuwa tume hiyo itateua Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwa wajumbe ambapo Sekretarieti ya Tume hiyo itatokana na wajumbe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)na Ikulu.
      Alifafanua kuwa hadidu za rejea za tume ni pamoja na kuchambua kwa kina sheria namba tisa ya mwaka 2004 iliyounda Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kanuni zake ili kubainisha vifungu vinavyohitaji marekebisho kulingana na hali halisi ya utoaji wa mikopo.
      Alisema hadidu nyingine za rejea ni kuangalia upya vigezo na sifa zinazozingatiwa katika utoaji wa mkopo endapo vinakidhi haja na mahitaji halisi ya waombaji na taifa kulingana na makusudio ya kuundwa kwa bodi.
      Nyingine ni kuangalia kwa kina muundo wa bodi na ufanisi wake katika utoaji na urejeshwaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa mapendekezo na kuchunguza kiini cha malalamiko na mahusiano yasiyoridhisha kati ya bodi na wanafunzi, bodi na Taasisi ya Elimu ya Juu na kati ya bodi na Wizara ya Elimu na kutoa mapendekezo ya namna ya kurejesha mahusiano mazuri.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. Miaka 50

    3. #2
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,737
      Rep Power : 12927
      Likes Received
      4439
      Likes Given
      7465

      Default Re: Serikali yaunda tume ya vyuo vikuu • Itachunguza utata wa mikopo ya wanafunzi

      JK anaunda tume kuchunguza mambo ambayo majibu yake sote tunayafahamu.........kuwa fedha kwa wananfunzi hazitoshi............na pili serikali kupitia hazina ndiyo chanzo cha kuchelkewesha fedha kupelekwa kwenye tume.......................... ........sasa hii tume ya JK kama siyo kupoteza pesa zetu bure ni nini haswa?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    4. RukaaJuu Final

    Similar Topics

    1. Utaratibu wa mikopo vyuo vikuu kugombanisha familia za wasiojiweza
      By oba in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 23rd September 2011, 11:10
    2. Replies: 26
      Last Post: 1st September 2011, 23:59
    3. Wanafunzi Wavamia Tume ya Vyuo Vikuu - TCU
      By SuperNgekewa in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 2
      Last Post: 29th September 2010, 18:12
    4. Wanafunzi Wavamia Tume ya Vyuo Vikuu - TCU
      By SuperNgekewa in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 2
      Last Post: 29th September 2010, 14:57
    5. Serikali yaunda Tume kuchunguza Ufisadi Tanesco
      By BelindaJacob in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 25
      Last Post: 29th July 2009, 21:41

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...