JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa

  Report Post
  Page 2 of 2 FirstFirst 12
  Results 21 to 23 of 23
  1. Cotan's Avatar
   Member Array
   Join Date : 11th February 2010
   Posts : 71
   Rep Power : 617
   Likes Received
   4
   Likes Given
   8

   Default Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa

   Ukosefu wa Uaminifu katika Biashara ndiyo tatizo kubwa sana linalo gharimu sana katika biashara, Biashara nyingi sana zimekufa kutokana tatizo hili.

   Uaminifu unamaana kubwa sana ktk nyanja hii, mfano km wewe ni mmiliki wa Duka, Bar, Mgahawa, Genge, Kiosiki, nk. Basi unaajiri watu au mtu kwa ajiri ya kukusaidia katika biashara yako au unamchukua ndugu yako au rafiki yako unamuweka katika biashara. Mnakaa mnakubarina kiwango cha mshahara au manufaa atakayoyapata kutoka kwenye biashara hiyo.Pia mnakubariana namna ya kuendesha kazi yaani kanuni za kuendesha biashara husika..

   Basi na kuhakikishia usipokuwa macho utaibiwa tu, utafilisika tu, watu siku hizi hawaaminiki.usifikirie kwamba kwa vile ni Mke wako, Dada yako,Mdogo wako, Kaka Yako, Mjomba wako, Rafiki yako, au Mlokole mwenzio basi hawezi kukuibia, ndg hilo unajidanganya tu. Weka uzibiti maalumu wa Biashara yako hakikisha kila siku unafanya mahesabu km huwezi kufanya kila siku basi fanya angalau kwa kila wiki au kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu. Usichelewe sana kufanya mahesabu kwani kadiri utakavyo chelewa ndo kadri hasara itakavyokuwa kubwa hatimae biashara itakufa.

   Usifanye biashara kwa mazoea tu, jifunze namna ya kutunza kumbukumbu za biashara yako. Wajasiliamali wengi hawaweki kumbukumbu katika biashara zao hili ni tatizo kubwa sana. Matokeo yake ni kufa kwa biashara au kudumaa kwa biashara, kila mwaka utakuwa unapiga makitaimu uko pale pale tu, au unapanda kidogo tu.

   Unapo weka kumbukumbu za biashara yako inakusaidia wewe kujua namna biashara yako inavyokua au inavyoanguka. Kwa hiyo unakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihihi kwa mda muafaka. Usifanye biashara kwa kuangalia kwa macho tu, bila ya kufanya mahesabu.yaani kuna baadhi ya wafanyabiashara hasa hasa wenye maduka huwa wanaangalia tu jinsi bidhaa ilivyojaa kwenye ngazi za duka au jinsi stoo ilivyojaa basi wanaamini kuwa wanasonga mbele kumbe wapi. Huwezi kujua hasara au faida kabla ya kufanya mahesabu (STOCK TAKING).

   Pia tatizo lingine linalowakabiri wa fanyabiashara ni kuchanganya madeni mfano, wewe unaenda kukopa pesa Bank mathalani unakopa Tsh 4ml na liba ya Tsh 760,000/= jumla umekopa 4, 7600, 000/= lazima pesa hiyo uilipe hiyo sio sadaka, usianze kufanya mambo yaliyoinje na malengo ya mkopo, mfano usiende kulipia karo ya mototo au kununua makochi utafungwa bure.Pia lazima uwe na kikomo cha ukopaji usipende kukopa tu kila mahali mfano, Bank umekopa, kwa John umekopa, kwa Musa umekopa ,kwa IDDI umekopa na kwa Masawe umekopa pia.je utaweza kumeneji madeni yote hayo kwa wakati mmoja?. Matokeo yake ni kukimbia tu.au kufirisiwa utaanza kuishi km digidigi.

   Pia km unaweka bidhaa stoo basi kuwa makini sana kwani wafanyabiashara wengi wanafirisika kutokana na kukosa udhibiti wa mali iliyoko stoo( gharani) hakikisha unakuwa na hesabu kamili ya vitu vilivyoko stoo weka kumbukumbu ya kila kinacho toka na kuingia stoo.usipokuwa makini utafirisika tu, watu wanaibiwa sana kuwa makini.Pia hakikisha vitu vinakaa kwa usalama bila kuharibika .pia usiwe mbali sana na biashara yako, angalau uwepo kila mara kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Usiamini watu tu eti watakufanyia kila kitu hakuna biashara ni wewe mwenyewe.

   Usitafute mchawi kwenye Biashara yako elewa kuwa Mchawi ni wewe MWENYEWE wala USITAFUTE MGANGA WA BIASHARA YAKO ELEWA KUWA MGANGA NI WEWE MWENYEWE. Ninasema hivi kwa sababu ya baadhi ya wafanyabiashara kupenda sana mambo ya ushirikina wakiamini kwamba bila ya kwenda kwa mganga mambo hayawezi kwenda veme hii ni imani mbaya sana wengi imewakwamisha wengi wameangamia pia wameangamiza ndugu zao kwa ujinga huu.

   Hakuna mganga anaejua dawa ya biashara hakuna bali kuna mazingaombwe tu, na kulishwa imani mbovu. Km huyo mganga anajua dawa ya utajiri kwa nini yeye awe masikini au kwanini watoto wake wawe masikini.mnadanganyika bure tu, hakuna miujiza katika biashara usidanganyike.Dawa ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa Mkalimu kwa wateja na kujitaidi kuweka kumbukumbu za biashara vizuri. Pia kujitaidi kuwa muaminifu ukikopa kumbuka kulipa usipokuwa muaminifu watu hawatakuamini elewa kuwa biashara ni uaminifu.Pia weka malengo ya biashara yako.

   ASANTENI.

  2. Belyo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 13th April 2010
   Posts : 13
   Rep Power : 596
   Likes Received
   3
   Likes Given
   0

   Default Re: Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa

   Asante kwa somo hilo. Hata hivyo ningependa kufahamu jinsi gani naweza kuchagua biashara ya kufanya

  3. Tindikali's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th March 2010
   Posts : 276
   Rep Power : 652
   Likes Received
   5
   Likes Given
   0

   Default Re: Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa

   Quote By Cotan View Post

   Umejuaje?

   Una mamlaka gani ya kutupa somo la biashara, wewe ni nani, umefanya utafiti gani, umesomea nini, umefanya nini na unafanya nini sasa hivi.

   Unaoposema "wengi wamepoteza mali kutokana na mikopo blah.. blah..." lete takwimu, umejuaje, una mamlaka gani kwenye fani husika?

  4. MeinKempf's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th June 2013
   Location : Hamburg, Germany.
   Posts : 6,989
   Rep Power : 171802601
   Likes Received
   2514
   Likes Given
   1796

   Default Re: Kama wewe ni mjasiliamali soma hapa

   Quote By Tindikali View Post
   Umejuaje?

   Una mamlaka gani ya kutupa somo la biashara, wewe ni nani, umefanya utafiti gani, umesomea nini, umefanya nini na unafanya nini sasa hivi.

   Unaoposema "wengi wamepoteza mali kutokana na mikopo blah.. blah..." lete takwimu, umejuaje, una mamlaka gani kwenye fani husika?
   Nina wasi wasi na uwezo wa IQ yako coz nahisi yaweza kuwa kama ya funza dume.
   Immature Love says "I Love U Bcoz I need U BUT Mature love says "I need U Bcoz I Love U".

  Page 2 of 2 FirstFirst 12

  Similar Topics

  1. Kama mwanaume kikojozi unakosa mchumba soma hapa plz.
   By Mtaftaji in forum Love Connect
   Replies: 25
   Last Post: 29th November 2011, 02:25
  2. Kama hupati Jamiiforums and mitandao mingine ya kijamii kama youtube soma hapa
   By kasimba123 in forum Tech, Gadgets & Science Forum
   Replies: 4
   Last Post: 3rd July 2011, 01:14
  3. Kwa babu Ambi kama sio ushirikina......! Soma hapa
   By Dopas in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 0
   Last Post: 8th April 2011, 18:21
  4. Lunyungu umefanya nini tena wewe ?????? soma hapa
   By KadaMpinzani in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 9
   Last Post: 12th October 2007, 00:17

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...