Habarini wana jf wote:

Wana jf ninataka kujiajiri kwenye secta ya madini lakini hasa kwenye dhahabu na hata aina nyingine ya madini ya vito...

Kwa sasa siyajui maeneo wanapouza,hivyo ninaomba ushauri wenu kwa walio na ufaham na hata waliofanya na wanaoendelea kufanya shughuli hizi.Ninaomba ushauri katika mambo yafuatayo:

1:changamoto za biashara yenyewe
2:sehemu ninapoweza kupata madini hayo na aina yenyewe
3:usalama wa eneo unaloshauri nifike
4:Upatikanaji wa usafiri na barabara
5:maeneo yenye madini ambayo bado hayajamilikishwa ili ikiwezekana ninunue eneo na kuwa na machimbo yangu
na mengineyo unaweza ongeza

Aliye na taarifa sahihi tunaweza wasiliana kwa kuni-pm,nitawashukuru kwa ushauri mzuri mtakaonipa