JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: MKUKUTA Phase I: Maoni yako

  Report Post
  Page 1 of 6 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 102
  1. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default MKUKUTA Phase I: Maoni yako

   It is interesting to note that any situation analysis of Tanzania starts with the sentence " Tanzania is the poorest country South of Sahara....Tanzania remains one of the poorest countries in the world, with many of its people living below the World Bank poverty line....,

   THIS IS NOT A VERY PLEASING STATE OF THINGS.

   Our country has since independence adopted policies geared towards poverty reduction and eradication. Tanzania has been thinking globally also in the quest for solutions to end poverty and misery to its people. Tanzania attended the Millennium Summit - the largest gathering of world leaders in history, which was held in September 2000.In this meeting the UN Millennium Declaration, (famously known as MDGs) were adopted, committing countries to a new global partnership to reduce extreme poverty and setting out a series of time-bound targets, with a deadline of 2015.At the local level, Tanzania adopted MKUKUTA - the National Strategy on growth and Eradication of poverty– as a national modality for operationalising the MDGs, encompassing the MDG targets in three clusters– growth, social well-being and governance . Even before that Tanzania had in place Vision 2025, which sets very interesting targets – halving poverty come 2015, which is just around the corner and total eradication of poverty come 2025. MDG:1 which is on Eradicating Extreme Hunger and Poverty,target is halving, between 1990 and 2015, the proportion of people whose income is less than $1 a day.

   The issue is how serious are we in achieving the set targets as per Vision 2025 and the MDG based MKUKUTA?

   Considering the current financial crisis and the economic down turn, pathetic state of governance where billions are being lost through graft, can we say that we are on track? 2015 is only 5 years away. Assuming that all was ok, ( financial crisis is a recent development)would we have still achieved the MKUKUTA/MDGs targets come 2015?

   Phase I ends by July 2010, tuma maoni kwenda [email protected]
   Last edited by WomanOfSubstance; 6th April 2009 at 13:48.
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle
  2. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,809
   Rep Power : 272909924
   Likes Received
   11033
   Likes Given
   17657

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By WomenofSubstanc View Post
   It interesting to note that any situation analysis of Tanzania starts with the sentence " Tanzania is the poorest country South of Sahara....Tanzania remains one of the poorest countries in the world, with many of its people living below the World Bank poverty line....,
   THIS IS NOT A VERY PLEASING STATE OF THINGS.
   WoS, leo umenichekesha sana. Umesahau kuwa hata Matonya na wenzake huanza hivi..."Saidia masikini!!!

   Our country has since independence adopted policies geared towards poverty reduction and eradication. Tanzania has been thinking globally also in the quest for solutions to end poverty and misery to its people. Tanzania attended the Millennium Summit - the largest gathering of world leaders in history, which was held in September 2000.In this meeting the UN Millennium Declaration, (famously known as MDGs) were adopted, committing countries to a new global partnership to reduce extreme poverty and setting out a series of time-bound targets, with a deadline of 2015.At the local level, Tanzania adopted MKUKUTA - the National Strategy on growth and Eradication of poverty– as a national modality for operationalising the MDGs, encompassing the MDG targets in three clusters– growth, social well-being and governance . Even before that Tanzania had in place Vision 2025, which sets very interesting targets – halving poverty by come 2015, which is just around the corner and total eradication of poverty come 2025. MDG:1 which is on Eradicating Extreme Hunger and Poverty. Target is halving, between 1990 and 2015, the proportion of people whose income is less than $1 a day.
   Mama, hizi ni drama tu, za cut and paste!! Hakuna hata mtu mmoja katika nchi hii na hata hao waliondaa hizo documents anayejua utakelezaji wake utafanyikaje. Ila ni kasuku wazuri tu wa kunukuu vipengee vya hayo machapisho ya kisanii. Ningefurahi sana kama tungekuwa na mpango kama ile ya kijeshi. Hapo ingekuwa poa sana kwani ni lazima kwenda mbele au kuondoa majeshi na kumkimbia adui. Ila hii ya sasa inatia kichefu chefu. Mbele hatuendi wala nyuma haturudi, tunabaki tunacheka cheka na kutokwa mate kama mataahira!!

   The issue is how serious are we in achieving the set targets as per Vision 2025 and the MDG based MKUKUTA?
   Kama ilani ya chama tawala haitekelezeki unategemea nini? Mimi naona tumejikalia tu, tunagojea kusukumwa kama gari lililokwama kwenye matope. Tuombe Mungu tupate mtu wa kutusukuma!!

   Considering the current financial crisis and the economic down turn, pathetic state of governance where billions are being lost through graft, can we say that we are on track? 2015 is only 5 years away. Assuming that all was ok, ( financial crisis is a recent development)would we have still achieved the MKUKUTA/MDGs targets come 2015?
   Kwa maoni yangu mambo yanaenda vizuri tu! Mamilionia feki wanaongezeka kwa michezo ya kuigiza na ufisadi (EPA, Radar, ndege ya rais, minara pacha n.k) na pato la wastani la Watanzania litakuwa limeongezeka tu! JK lazima amalizie kazi yake nzuri aliyoipokea toka kwa Ben. Wewe unaonaje?

  3. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Dark City View Post
   Kwa maoni yangu mambo yanaenda vizuri tu! Mamilionia feki wanaongezeka kwa michezo ya kuigiza na ufisadi (EPA, Radar, ndege ya rais, minara pacha n.k) na pato la wastani la Watanzania litakuwa limeongezeka tu! JK lazima amalizie kazi yake nzuri aliyoaipokea toka kwa Ben. Wewe unaonaje?
   I like your comments comrade!

   You could be right.

   Nadhani some of the global commitments zinafanywa na viongozi wetu kama namna ya ku conform ili kunufaika na misaada na siyo kufanya kweli! Ukiangalia kiasi cha ufadhili nchi yetu inachopata kama namna ya kutekeleza hayo malengo ya milenia na pia kutengezea MKUKUTA na michakato yake, utaona kuna wanaofaidika na hiyo michakato.

   Kila kukicha ni seminar kuhusu MKUKUTA, MDGS - mara warsha za wadau maana hiyo michakato ni highly consultative na participatory.

   Mwisho wa siku matokeo ni vigumu kuyapata hasa kwa wale walengwa - wananchi waishio chini ya hiyo $1 kwa siku.Anayepokea posho za warsha si mwanakijiji wala mlalahoi wa mjini bali ni technocrats wa mijini wenye mishahara yao, wenye vibiashara vyao wanavyofanya baada ya saa kazi n.k.

   Ukiupunguza umaskini by half hata warsha na seminar zitapungua. Ukiufuta umaskini kabisa basi tena utakuwa umefanya baadhi ya watu ( donors, consultants etc) kukosa kazi.
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  4. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,809
   Rep Power : 272909924
   Likes Received
   11033
   Likes Given
   17657

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Haswa WoS, hapo ndo kwenyewe. Kuna mtu aliwahi kusema kwamba jamani msitokomeze Malaria kwa sababu nitosa kazi. Kwamba taasisi yao huko Ujerumani imeajiri karibia watu 1000, wote wanashughulika na malaria. Malaria ikiisha, taasisi itafungwa na watu hao wote watajikuta mtaani hawana kibarua.

   Lakini jamani tuache utani. Semina zinalipa saaaaana! Per diem kwa boss ni 85,000 kwa siku. Akipata semina hata kwa siku 20 tu kwa mwezi, hiyo ni 1.7m. Mshahara utagusa wa nini? Na wakati mwingine zinapandana 2 au tatu na mshiko unakombwa tu! Jamani kama kuna mtu anataka kutangaza kazi kwa ajili watu wanaopenda kuhudhuria semina naomba mnistue. Ni dili la kufa mtu!

  5. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Dark City View Post
   Haswa WoS, hapo ndo kwenyewe. Kuna mtu aliwahi kusema kwamba jamani msitokomeze Malaria kwa sababu nitosa kazi. Kwamba taasisi yao huko Ujerumani imeajiri karibia watu 1000, wote wanashughulika na malaria. Malaria ikiisha, taasisi itafungwa na watu hao wote watajikuta mtaani hawana kibarua.

   Lakini jamani tuache utani. Semina zinalipa saaaaana! Per diem kwa boss ni 85,000 kwa siku. Akipata semina hata kwa siku 20 tu kwa mwezi, hiyo ni 1.7m. Mshahara utagusa wa nini? Na wakati mwingine zinapandana 2 au tatu na mshiko unakombwa tu! Jamani kama kuna mtu anataka kutangaza kazi kwa ajili watu wanaopenda kuhudhuria semina naomba mnistue. Ni dili la kufa mtu!

   Kaa mkao wa kula mtu wangu maana mialiko iko kedekede!
   On a serious note, poverty is a huge opportunity for the rich.It is an industry by itself.If we unpack the MDG and MKUKUTA, we will be opening a pandoras box maana humo ndani kuna mambo ya Malaria, HIV Aids, gender, environment, governance and democracy etc etc etc......kila eneo hapo lina mizengwe yake...
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle
  6. Nyauba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th July 2008
   Posts : 1,110
   Rep Power : 908
   Likes Received
   74
   Likes Given
   61

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Mkuu heshima kwa taarifa muhimu kimaendeleo.

   tatizo letu kubwaa kufikia hayo malengo ni uwezo wa kiuongozi kwa maana ya watu makini na wenye forward thinking approach.

   hapa najumuisha viongozi (wanasiasa na watendaji wote) pamoja na jamii husika katika kuhoji vipaumbele vya taifa lao na utekelezaji wake.

   ni jambo la kusikitisha kwamba serikalini viongozi wenye uelewa wa maana ya MKUKUTA leave alone mapungufu yake ni wachache sanaaa na the rest wanaizungumzia tuu kama hadithi hata work plan hawawezi kuandaa kuendana na maeneo yao achilia mbali ufuatiliaji.

   nchi hii lazima tuwe na focus ya kuwa na rasilimali watu (human capital) kwani ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi. hatuwezi kujivunia maliasili na rasilimali nyingine kama ardhi kubwaaaa yenye rutuba bila kuwa na ujasiri wa kuzifanyia kazi kwa maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla.

   silika yetu ya UVIVU wa kupenda kusimamiwa zaidi katika utendaji bila kuwa na minimum supervision from personal level to national level ni kikwazo kikubwa kufikia maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla.

   kutwa nzima tunapiga kelele kuhusu mafisadi na upuuzi wake bila kujadili kwa mapana uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja na umuhimu wa kujenga tabia ya uwajibikaji wa tija na ufaanisiii... afterall ufisadi uliopo chanzo chake ni utawala uliochokaaa wa CCM unaotumia kama mbinu ya kuendelea kutawalaa..

   tuna mambo mengi ya kuyajadili kwa mapana as our common interest and avoid our accasional difference to frustrate the REAL PROBLEMS WE HAVE AS A NATION.

   mkukuta utekelezaji wake utaendelea kuwa wa kusuasua na matokeo yake kukosa kasi ya kufaa kwa sababu tuu kama taifa hatupendi kutoa changamoto ya uwajibikajiii...

   natoa rai tena tujadili kwa MAPANA UKOSEFU WETU WA KUTOKUWAJIBIKA KWA VIWANGO STAHILI VYA KUFIKIA MAENDELEO.

   PAMOJA NA UTAJIRI WOTE WA ASILI TULIO NAO TUMEKOSA RASILIMALI WATU KUGEUZA KUWA UTAJIRI NA HATIMAYE KUSONGA MBELE KIUCHUMIII.

  7. Masanja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st August 2007
   Location : Benaco
   Posts : 1,915
   Rep Power : 1122
   Likes Received
   576
   Likes Given
   94

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   WoS, This is an interesting topic. I have always thought about it..ila nakosa jibu..perhaps tujadili what we think..

   Nadhani kwa hili la MDGs we are dead wrong. Umasikini utazidi kuongezeka na wala hiyo halina ubishi. Ukiangalia statistics za bongo, tangu mwaka 2005 mpaka mwaka jana december watu million tatu waliingia kwenye ufukara wa kutupwa (absolute poverty joining another twelve million). Hivyo ni dhahiri kwamba we are regressing baada ya kusonga mbele. Na I am sure ni zaidi ya hapo. Viongozi wetu hawana uwezo wa kufikiri tena! we have outsourced everything including our ability to think to western countries (and now China!). Hakuna kiongozi tena anayefanya kazi kwa common good. Its everybody for himself and God for us all. Na sisi wananchi kwa sababu ya njaa, umasikini na ujinga..tumeamua kwamba umasikini ni kazi ya Mungu! Mungu akipenda tutafanikiwa!

   Kitu kingine, sisi waafrika wa kujilaumu ni sisi wenyewe, we have willingly become compradors of the rich at the expense of our people. Wazungu wameshatujua namna ya kula na sisi. Ndo maana katika dunia nzima ukiangalia..sehemu ambako misaada haifanyi kazi ni Africa. anzia na Germany Marshal Fund..US ilitoa hela nyingi sana kusaidia uchumi wa Europe baada ya WW2, leo matokeo tunayaona. Hata eastern Europe ni juzi juzi tuu..lakini we see the progress they are making. Kifupi leo hata ungesema uweke stimulus package ya Obama ya 100 Billions in Africa, I can bet myself. Haitasaidia lolote katika mustakabali wetu. kWA SABABU HATUJUI VIPAUMBELE VYETU!

   Swala la MDG I always say it is a minimalist approach ya western countries kuonekana kwamba they are doing something for this black continent. In reality ni upuuzi mtupu. Hivi niwaulize: Mnajua kwamba Nyerere alianzisha MDGs miaka kibao iliyopita? Nyerere alijua umuhimu wa afya ya mama na mtoto, elimu ya msingi, kupunguza umasikini, availability and accessibility ya tertiary education etc..zamani sana.Ndo maana ulikuta zahanati almost kila kijiji, mabomba ya maji, shule etc... Ndo maana wengi tulifaidika na hii miradi ya mwalimu in the 1970s and 80s mpaka alipoingia ruksa... Leo MDGs ni cut and paste ya what Nyerere did those years. Guess what happened? ni hawa hawa WB na IMF waliokuja na kumpiga mkwara mzee wa watu kwamba huwezi toa elimu wala huduma za jamii bure..wakatishia kukata misaada. We all know what happened next. Leo tunaambiwa tuwapeleke shule watoto wetu wapate elimu..lakini viongozi kama akina Nyerere walilijua hilo mapema! LAKINI KWA SABABU HAIKUWA IDEAS ZA WAZUNGU NA MASHIRIKA YAO..NDO WAKATUNYIMA PESA. NA SIJUI ITATUCHUKUA NINI MPAKA KUFIKIA LITERACY LEVEL YA KIPINDI CHA MWALIMU! TALK OF MDGs!

   Kifupi we have willingly and collectively become stupid as a continent. Tumeshindwa kujua kwamba kamwe hatuwezi kuendelea kama taifa au bara bila kushughulisha bongo zetu. Haiwezekani mtu wa New York au PARIS ajue matatizo yako kuliko wewe unayeyaishi Kibondo au Bwasi.... NEVER! Unafikiria kwa nini miradi ya kuondoa umasikini haifanikiwi katika Africa? Ni Kwa sababu haiwahusishi wadau wa kubwa wa hii sector ambao NDO MASIKINI wenyewe!!

   To me, way forward ni kuwa na mawazo yetu wenyewe tukajua priorities zetu. This nonsense of MDGs ni ujinga ambao we are just wasting our time! Jiulize leo ukienda vijijini hata Kasulu utakuta matank ya maji ya miaka ya 70! Ambayo leo hayana maji...huoni kwamba Nyerere alijua umuhimu wa maji safi na yanayopatikana kwa urahisi kwa wananchi? leo ndo tunapigia MDGs kelele kwa sababu wametoa ideas wengine.

   Afrika needs to think outside the box. Hizi longo longo za Mkukuta, sijui nini..tutazidi kupiga marktime kwenye umasikini tuu..kwa sababu wanaoleta hii miradi na ideas..hawajui matatizo yetu na kibaya sisi tunaoyajua..tunaogopa kuwa wawazi..maana na sisi tunafaidika na hizo warsha..kama mkubwa mmoja alivyosema hapo juu..Its just pathetic and sad when I think of my continent.

   UN ni shirika zuri..lakini haliwezi kutuletea ideas za maana..tuwaache wasaidie wakimbizi wetu makambini. Maendeleo ni jukumu letu. Harafu Mkapa anaenda kumleta mtaalamu De Soto kutoka Peru...aje kutufundisha namna ya kuondokana na umasikini? Hivi waafrika tulirogwa na nani? Duh!

   Mtu wa kuondoa umasikini Tanzania ni Maskini Mwenyewe. Period.
   Silaha ya maskini ni elimu.

  8. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,809
   Rep Power : 272909924
   Likes Received
   11033
   Likes Given
   17657

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By WomenofSubstanc View Post
   Kaa mkao wa kula mtu wangu maana mialiko iko kedekede!
   On a serious note, poverty is a huge opportunity for the rich.It is an industry by itself.If we unpack the MDG and MKUKUTA, we will be opening a pandoras box maana humo ndani kuna mambo ya Malaria, HIV Aids, gender, environment, governance and democracy etc etc etc......kila eneo hapo lina mizengwe yake...
   Mhhh, naona mambo yanakwenda yakiongezeka. Hebu ni-PM tuongee zaidi. Hapa tunaweza kuonekana tunazama kwenye ufisadi hivi. Ila ukweli ni kuwa umasikini wetu ni dili i.e kufa kufaana. It's very sad but that is the truth!

  9. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Masanja View Post
   WoS, This is an interesting topic. I have always thought about it..ila nakosa jibu..perhaps tujadili what we think..

   .....Hakuna kiongozi tena anayefanya kazi kwa common good. Its everybody for himself and God for us all. Na sisi wananchi kwa sababu ya njaa, umasikini na ujinga..tumeamua kwamba umasikini ni kazi ya Mungu! Mungu akipenda tutafanikiwa!

   Kitu kingine, sisi waafrika wa kujilaumu ni sisi wenyewe, we have willingly become compradors of the rich at the expense of our people. ..................
   ..... Kifupi leo hata ungesema uweke stimulus package ya Obama ya 100 Billions in Africa, I can bet myself. Haitasaidia lolote katika mustakabali wetu. kWA SABABU HATUJUI VIPAUMBELE VYETU!

   Swala la MDG I always say it is a minimalist approach ya western countries

   ............LAKINI KWA SABABU HAIKUWA IDEAS ZA WAZUNGU NA MASHIRIKA YAO..NDO WAKATUNYIMA PESA. NA SIJUI ITATUCHUKUA NINI MPAKA KUFIKIA LITERACY LEVEL YA KIPINDI CHA MWALIMU! TALK OF MDGs!

   Kifupi we have willingly and collectively become stupid as a continent.

   To me, way forward ni kuwa na mawazo yetu wenyewe tukajua priorities zetu. This nonsense of MDGs ni ujinga ambao we are just wasting our time!

   Afrika needs to think outside the box. Hizi longo longo za Mkukuta, sijui nini..tutazidi kupiga marktime kwenye umasikini tuu..kwa sababu wanaoleta hii miradi na ideas..hawajui matatizo yetu na kibaya sisi tunaoyajua..tunaogopa kuwa wawazi..maana na sisi tunafaidika na hizo warsha..kama mkubwa mmoja alivyosema hapo juu..Its just pathetic and sad when I think of my continent.

   UN ni shirika zuri..lakini haliwezi kutuletea ideas za maana..tuwaache wasaidie wakimbizi wetu makambini. Maendeleo ni jukumu letu. Harafu Mkapa anaenda kumleta mtaalamu De Soto kutoka Peru...aje kutufundisha namna ya kuondokana na umasikini? Hivi waafrika tulirogwa na nani? Duh!

   Mtu wa kuondoa umasikini Tanzania ni Maskini Mwenyewe. Period.
   Mkuu,
   I salute you... umesummarise vizuri sana hii agenda ya AID Effectiveness,
   Na kama ulivyosema ni kama vile he who pays the piper, calls the tune.Fedha ni zao, wao ndio wanataka kutuamulia vitumike vipi na kwa kitu gani...THE IDEA HAS TO COME FROM THEM...but do we have to take it?

   Umezungumzia pia enzi za Nyerere na siasa zake ikiwa ni pamoja na kutoa huduma muhimu bila ya gharama...pamoja na kuwa hiyo ilikuwa hatua nzuri, unafikiri ingeweza kuwa sustainable? Structural Adjustment Programmes of the 1980s kwa kiasi kikubwa ziliharibu mafanikio tuliyokwisha yapata hasa katika elimu, afya, life-expectancy, na kiwango cha watu wanaojua kusoma na kuandika .Lakini pia tujiulize hali ilivyokua inaenda, who would have met the costs in the long run..as a short term measure naikubali.

   Umemtaja DE SOTTO NA prescription zake- nadhani ni muujiza kutegemea mtu wa nje kutuondolea umaskini.Wakati professor Issa shivji anastaafu kufundisha UDSM alitoa hotuba yake ambayo ilichambua sana hili suala la AID KATIKA MTIZAMO WA NEO-LIBERALISM na nafasi ya wanasheria. Tukumbuke kuwa De Sotto approach yake ni kurasmisha rasilimali za wanyonge ili ziweze kutumika katika kujikwamua na umaskini kama vile hizo rasilimali ukizisajili zitaleta muujiza na kuufuta umaskini kama mwalimu afutavyo ubao baada ya kuandika na chaki!

   De Sotto anaona kuwa wanyonge wamekalia dead capital which needs rescusitation. Shivji alisema "we hire a De Soto to tell us that we are too stupid to recognise ‘the mystery of capital’ and understand ‘why capitalism triumphs in the West and fails everywhere else’.

   We are sitting on trillions of dollars of ‘dead capital’. We have to breath legal life into these ‘dead’ assets and lo! behold, we’ll all be as capitalist as the West.

   The question is who would have the trillions of dollars at the end of the process, and who would be dead?
   Mkuu, na wengine wenye interest kujadili hii mada, tujiulize hivi pamoja na kila tulicho nacho ni kwanini tunazidi kudidimia kwenye umaskini uliokithiri hivi despite all measures taken so far and resources that we have.
   Last edited by WomanOfSubstance; 6th April 2009 at 16:35.
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  10. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Dark City View Post
   Mhhh, naona mambo yanakwenda yakiongezeka. Hebu ni-PM tuongee zaidi. Hapa tunaweza kuonekana tunazama kwenye ufisadi hivi. Ila ukweli ni kuwa umasikini wetu ni dili i.e kufa kufaana. It's very sad but that is the truth!
   Hebu kwanza tujadili bayana hii ishu kwa mapana yake ndipo tuwe na bilateral discussion thru PM.
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  11. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,809
   Rep Power : 272909924
   Likes Received
   11033
   Likes Given
   17657

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Masanja View Post
   WoS, This is an interesting topic. I have always thought about it..ila nakosa jibu..perhaps tujadili what we think..

   Viongozi wetu hawana uwezo wa kufikiri tena! we have outsourced everything including our ability to think to western countries (and now China!). Hakuna kiongozi tena anayefanya kazi kwa common good. Its everybody for himself and God for us all. Na sisi wananchi kwa sababu ya njaa, umasikini na ujinga..tumeamua kwamba umasikini ni kazi ya Mungu! Mungu akipenda tutafanikiwa!
   Mkuu, huwezi kufikiri kama hujui tatizo ni nini, na chanzo chake ni nini. Sasa kama Mkuu wa kaya hajui chanzo cha matatizo ya kaya yake na hasa umasikini unategemea nini? Mbaya zaidi mambo hayo yanatokea kwenye kaya ambayo kila kitu kinamtegemea mkuu huyo. Ukijaribu kuleta kilimi limi unaishia pabaya. We are doomed!

   Kitu kingine, sisi waafrika wa kujilaumu ni sisi wenyewe, we have willingly become compradors of the rich at the expense of our people. Wazungu wameshatujua namna ya kula na sisi. Ndo maana katika dunia nzima

   Kifupi we have willingly and collectively become stupid as a continent. Tumeshindwa kujua kwamba kamwe hatuwezi kuendelea kama taifa au bara bila kushughulisha bongo zetu. Haiwezekani mtu wa New York au PARIS ajue matatizo yako kuliko wewe unayeyaishi Kibondo au Bwasi.... NEVER! Unafikiria kwa nini miradi ya kuondoa umasikini haifanikiwi katika Africa? Ni Kwa sababu haiwahusishi wadau wa kubwa wa hii sector ambao NDO MASIKINI wenyewe!!
   Kama umewahi kwenda wa Sangoma basi unaweza kujua yaliyotukuta. Sangoma akishakwambia kuwa mchawi wako ni mama yako mzazi wakati unajua si kweli na ukaamini unategemea nini? Kesho anakwambia kamchinje mwanao upate utajiri unakimbilia kunoa kisu! Ukishakabidhi kichwa chako kwa mtu ujue yamekukuta. Sina hakina tunatokaje hapo lakini tumezama kwenye maji ya kina kirefu.

   To me, way forward ni kuwa na mawazo yetu wenyewe tukajua priorities zetu. This nonsense of MDGs ni ujinga ambao we are just wasting our time! Jiulize leo ukienda vijijini hata Kasulu utakuta matank ya maji ya miaka ya 70! Ambayo leo hayana maji...huoni kwamba Nyerere alijua umuhimu wa maji safi na yanayopatikana kwa urahisi kwa wananchi? leo ndo tunapigia MDGs kelele kwa sababu wametoa ideas wengine.

   Afrika needs to think outside the box. Hizi longo longo za Mkukuta, sijui nini..tutazidi kupiga marktime kwenye umasikini tuu..kwa sababu wanaoleta hii miradi na ideas..hawajui matatizo yetu na kibaya sisi tunaoyajua..tunaogopa kuwa wawazi..maana na sisi tunafaidika na hizo warsha..kama mkubwa mmoja alivyosema hapo juu..Its just pathetic and sad when I think of my continent.

   Mtu wa kuondoa umasikini Tanzania ni Maskini Mwenyewe. Period.
   Mimi nadhani kufikiri hatuwezi kukutegemea kama njia ya kubadilisha mawazo na mwelekeo wetu kwa sasa, ikizingatiwa tuliowategemea na sisi wenyewe tumefikia ukomo wa kufikiri. Tunahitaji kichaa mmoja aje na operation ya kusafisha kizazi hiki cha nyoka. Yaani kwanza atuchape hata viboko ili tufanye kazi kwa bidii kwa lengo la kujenga nchi yetu. Pili awatokomeze mafisadi hata ikibidi kutumia njia za kijeshi. Na mwisho atutie adabu (discipline) ya kuheshimu mali ya umma na kutafuta utukufu wa kutumikia umma badala ya matumbo yetu. Bila hivyo tutaendelea kucheka cheka tu!

  12. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Dark City View Post
   Mkuu, huwezi kufikiri kama hujui tatizo ni nini, na chanzo chake ni nini. Sasa kama Mkuu wa kaya hajui chanzo cha matatizo ya kaya yake na hasa umasikini unategemea nini? Mbaya zaidi mambo hayo yanatokea kwenye kaya ambayo kila kitu kinamtegemea mkuu huyo. Ukijaribu kuleta kilimi limi unaishia pabaya. We are doomed!

   Kama umewahi kwenda wa Sangoma basi unaweza kujua yaliyotukuta. Sangoma akishakwambia kuwa mchawi wako ni mama yako mzazi wakati unajua si kweli na ukaamini unategemea nini? Kesho anakwambia kamchinje mwanao upate utajiri unakimbilia kunoa kisu! Ukishakabidhi kichwa chako kwa mtu ujue yamekukuta. Sina hakina tunatokaje hapo lakini tumezama kwenye maji ya kina kirefu.

   Mimi nadhani kufikiri hatuwezi kukutegemea kama njia ya kubadilisha mawazo na mwelekeo wetu kwa sasa, ikizingatiwa tuliowategemea na sisi wenyewe tumefikia ukomo wa kufikiri. Tunahitaji kichaa mmoja aje na operation ya kusafisha kizazi hiki cha nyoka. Yaani kwanza atuchape hata viboko ili tufanye kazi kwa bidii kwa lengo la kujenga nchi yetu. Pili awatokomeze mafisadi hata ikibidi kutumia njia za kijeshi. Na mwisho atutie adabu (discipline) ya kuheshimu mali ya umma na kutafuta utukufu wa kutumikia umma badala ya matumbo yetu. Bila hivyo tutaendelea kucheka cheka tu!
   Nchi ni yetu wote lakini inakuwa kama kuna wenye nchi na wapangaji!

   Huwa najiuliza, hao wenzetu walioendelea ni nini hasa kiliwasukuma hadi wakafikia huko waliko? Je ni hali ya hewa yenye changamoto ( winter - baridi kali lazima kichwa kichangamke ujue kipindi hicho utaishije -chakula, mavazi stahiki, malazi, etc, summer nayo si hali ya hewa nzuri sana maana wakati mwingine joto huweza kufanya mtu akose raha etc), je ni uzalendo tu ? je ni fursa zilizokuwepo kuwafanya waliothubutu kutoka wakaweza kwenda kufanya uharamia na kupora waliolala ( siye ambao bado tunasuasua hadi leo), na je huo uharamia ulitupumbaza kama bangi hadi leo bado hatujaamka? na je wale "waliopigania uhuru" wetu walipoonja utamu wa kutawala, nao wakatuteka nyara na kutufanya watumwa wao na ndiyo maana hadi leo hata tuone kuna ufisadi tunabaki kujadili na kusikitika tu bila kujua la kufanya? Hali hii itaendelea hadi lini?

   Nimekumbuka kidogo historia ya Ufaransa na mapinduzi yake, Mfalme Louis wa 16 na mkewe Marie Antoinette walivyokuwa wamejisahau katika kula maraha wakati wananchi wanateseka hawa hata mkate ( basic food) na ni hasira hiyo iliyowafanya wananchi wainuke na kupambana na hawa mafisadi.

   Nakumbuka pia Urusi na akina Czar Nicolas wa 2 na mapinduzi ya 1917 yaliyopelekea mabadiliko makubwa; nakumbuka pia Ceaucescu wa Rumania na mkewe Ellena na walivyofikishwa tamati ya maisha yao mwaka 1989 baada ya kuwatesa wananchi na kuwafanya waishi katika umaskini ilhali wao wakiishi kifahari.Lakini ninapokumbuka zama hizo, simaanishi kuwa tunahitaji kuondoa waliopo kwa njia za mapinduzi maana hii si njia muafaka sana.Siku hizi kuna democrasia ( both liberal and illiberal) yenye kuwaachia wananchi waamue wanamtaka nani through the ballot box.Sasa ballot box hiyo ambayo tunaitumia siku zote, ni kwa vipi itatuletea viongozi bora watakaoweza kutufikisha panapostahili kwa maana ya maendelea kwa wananchi wote na si kufaidika kwa wachache tu.

   Fikiria huu mjadala wa Dr Slaa aliouanzisha kuhusu mishahara na maslahi ya wabunge. Hivi kweli kama wawakilishi wa wananchi wao hawana njaa , watawakumbuka wale wenye njaa waliowachagua?

   Tutaona jinsi kutakavyokuwa na kupigana vikumbo uchaguzi ujao na jinsi rushwa itakavyotumika ilimradi tu mtu aningie bungeni akajinafasi.

   Lakini mwisho wa siku tutabakia kama kawaida kulalama tu na life will go on kwa wale waliobahatika tena kuingia madarakani.I see no hope for change in the near future labda miaka 1000 ijayo!
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  13. Masanja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st August 2007
   Location : Benaco
   Posts : 1,915
   Rep Power : 1122
   Likes Received
   576
   Likes Given
   94

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Dark City na WoS,

   kusema kwamba Zile programme za Mwalimu miaka ya sabini na themanini hazikuwa sustainable, nadhani tunaingia kwenye ule ule mtego wa wakubwa hawa wa magharibi. Kwani how will you sustain hizi MDGs za leo? pesa iko wapi? Are we better off today than we were in those days? Ukianza na Mkukuta sijui Mkurabita just name them..yote hii miradi inategemea pesa za wafadhili. Kifupi wakiondoka hata hiyo miradi itakufa natural death. Sasa basi ni kutomtendea haki Mwalimu aliyeona umuhimu wa hizi MDGs mapema akaamua kutumia raslimali za taifa na kukopa kusudi watu wake wasome. Tunavyoongea hapa, hata elimu ya kipindi cha mwalimu ilikuwa tofauti na elimu ya leo "leo inaitwa Voda fasta". Ndo maana leo mzazi unahangaika kumpeleka mwanao kwenye "academy" siyo shule za sikinde tulizosoma sisi..why? you know the answer!

   Kwamba wenzetu walisukumwa na nini kupata maendeleo..nadhani sisi kama ambavyo nimeelezea mara nyingi...we tend to think poverty is predistined matter. KAMA ALIVYOELEZEA Dark City hapo juu. Sisi tumekumbatia rushwa, uzembe just name them..Hatujajua kwamba collectively we have a duty to liberate ourself from poverty. Bado kuna watanzania wenzetu wanaamini kwamba viongozi watawaondolea umasikini. Hiyo ni ndoto. Wenzetu likija swala la maslahi ya umma..ni social contract. Kila mtu ni muhusika. Ukichaguliwa ukafanya uzembe...watakumwaga chini na utaishia jela. Ask Korea au Thailand! You see? Harafu angalia wananchi sisi Africa...

   WoS na Dark City Iam sure nyinyi mmekaa au mmetembelea nje, hivi niambieni..mbona waafrika wakifika huko wanakuwa na adabu? jiulize..ukinywa bia hata moja US au Europe unaogopa kuendesha gari by all means! Huyo huyo mtu akija Dar..atakaa Rose Garden anywe bia hata kumi...na aendeshe gari! Why? wenzetu ukivunja sheria kuna consequences, kwetu ukivunja sheria-it depends on whom you know! Mifano ni mingi.

   Kabla ya kulilia maendeleo tunahitaji kuaddress vitu basic sana wala siyo vikubwa. Mfano rushwa ni tatizo kubwa ulimwenguni..lakini tofauti ni kwamba Maddof yuko jela na Lowassa au Rostam anapeta ingawa wote wameiba kwa Ponzi scheme albeit differently!

   Narudia kusema: Jukumu la kuondoa umasikini ni la masikini wenyewe in this case waafrika.

   Africa siyo tuu kubadili mawazo..bali pia Tunahitaji kujua wajibu wetu wa kiraia. Sasa kama tunasubiri "tupewe" elimu ya uraia. Mpaka tunapewa tutakuwa tumeshateketea kwa njaa, magonjwa na umasikini.
   Silaha ya maskini ni elimu.

  14. Dark City's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2008
   Location : Roaming
   Posts : 15,809
   Rep Power : 272909924
   Likes Received
   11033
   Likes Given
   17657

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By WomenofSubstanc View Post
   Nimekumbuka kidogo historia ya Ufaransa na mapinduzi yake, Mfalme Louis wa 16 na mkewe Marie Antoinette walivyokuwa wamejisahau katika kula maraha wakati wananchi wanateseka hawa hata mkate ( basic food) na ni hasira hiyo iliyowafanya wananchi wainuke na kupambana na hawa mafisadi.Nakumbuka pia Urusi na akina Czar Nicolas wa 2 na mapinduzi ya 1917yaliyopelekea mabadiliko makubwa; nakumbuka pia Ceaucescu wa Rumania na mkewe Ellena na walivyofikishwa tamati ya maisha yao mwaka 1989 baada ya kuwatesa wananchi na kuwafanya waishi katika umaskini ilhali wao wakiishi kifahari.
   Katika hayo yote uliyosema hapo juu, wananchi waliteseka sana na pia wakajua wanateseka. Inawezekana sisi bado hatujateseka kiasi cha kutosha!

   Lakini ninapokumbuka zama hizo, simaanishi kuwa tunahitaji kuondoa waliopo kwa njia za mapinduzi maana hii si njia muafaka sana.Siku hizi kuna democrasia ( both liberal and illiberal) yenye kuwaachia wananchi waamue wanamtaka nani through the ballot box.Sasa ballot box hiyo ambayo tunaitumia siku zote, ni kwa vipi itatuletea viongozi bora watakaoweza kutufikisha panapostahili kwa maana ya maendelea kwa wananchi wote na si kufaidika kwa wachache tu
   .

   Kama sanduku la kura litabaki kuwa mazingaombwe tufanye nini? Kwani Madagascar wanaishi sayari nyingine? Lazima kuna njia ya kuachana na mazoea na mateso. Labda hatujampata Musa wetu.

   Fikiria huu mjadala wa Dr Slaa aliouanzisha kuhusu mishahara na maslahi ya wabunge.Hivi kweli kama wawakilishi wa wananchi wao hawana njaa , watawakumbuka wale wenye njaa waliowachagua? Tutaona jinsi kutakavyokuwa na kupigana vikumbo uchaguzi ujao na jinsi rushwa itakavyotumika ilimradi tu mtu aningie bungeni akajinafasi.Lakini mwisho wa siku tutabakia kama kawaida kulalama tu na life will go on kwa wale waliobahatika tena kuingia madarakani.I see no hope for change in the near future labda miaka 1000 ijayo!
   Siwezi kuchangaa kitu. Ukienda kwenye sherehe ya kunguru basi na wewe ni kunguru! Kama ni hivyo basi hakuna lolote la kutegemea zaidi ya kunguru kumaliza mbegu zetu kabla hata hazijaota!!

  15. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Dark City View Post
   Katika hayo yote uliyosema hapo juu, wananchi waliteseka sana na pia wakajua wanateseka. Inawezekana sisi bado hatujateseka kiasi cha kutosha!

   Kama sanduku la kura litabaki kuwa mazingaombwe tufanye nini? Kwani Madagascar wanaishi sayari nyingine? Lazima kuna njia ya kuachana na mazoea na mateso. Labda hatujampata Musa wetu.

   Siwezi kuchangaa kitu. Ukienda kwenye sherehe ya kunguru basi na wewe ni kunguru! Kama ni hivyo basi hakuna lolote la kutegemea zaidi ya kunguru kumaliza mbegu zetu kabla hata hazijaota!!
   Tutesekeje tena? kama sasa kuna watu baadhi ya mikoa wana njaa.Kuna watu wanaishi chini ya dola 1 kwa siku.Kuna watu wanakufa kila siku kwa kukosa shilingi elfu 2, 3 , 4 za kumwona daktari watibiwe.Kuna akina mama wajawazito wanakufa kila siku kwa kuishiwa damu.Wengine wanakufa kwakukosa huduma ya kuzalishwa na mkunga.Kuna watoto wanakufa wakiwa hawajafikisha miaka 5 na hii si haki.Kuna mamilioni ya watoto hawaendi shule kwa sababu mbalimbali.Kuna mamilioni hawana maji safi na salama.Hii ni kwa uchache - extremes.Bado kuna ishu kama mishahara midogo isiyotosheleza, kutokulipwa mishahara kwa wakati, Mgao wa umeme kufuatia mipango mibovu n.k.

   Tusubiri mateso gani tena? Labda moto wa jehanamu!
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  16. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Quote By Masanja View Post
   Dark City na WoS,

   WoS na Dark City Iam sure nyinyi mmekaa au mmetembelea nje, hivi niambieni..mbona waafrika wakifika huko wanakuwa na adabu? jiulize..ukinywa bia hata moja US au Europe unaogopa kuendesha gari by all means! Huyo huyo mtu akija Dar..atakaa Rose Garden anywe bia hata kumi...na aendeshe gari! Why? wenzetu ukivunja sheria kuna consequences, kwetu ukivunja sheria-it depends on whom you know! Mifano ni mingi.

   Kabla ya kulilia maendeleo tunahitaji kuaddress vitu basic sana wala siyo vikubwa. Mfano rushwa ni tatizo kubwa ulimwenguni..lakini tofauti ni kwamba Maddof yuko jela na Lowassa au Rostam anapeta ingawa wote wameiba kwa Ponzi scheme albeit differently!

   Narudia kusema: Jukumu la kuondoa umasikini ni la masikini wenyewe in this case waafrika.

   Africa siyo tuu kubadili mawazo..bali pia Tunahitaji kujua wajibu wetu wa kiraia. Sasa kama tunasubiri "tupewe" elimu ya uraia. Mpaka tunapewa tutakuwa tumeshateketea kwa njaa, magonjwa na umasikini.
   Naanza kwakusema kuwa signature yako imenifanya niwaze mengi.Sasa siye tunachezea kipi kati ya hizo nyeti mbili??Hii methali nadhani ina ujumbe mzito kwetu watz.
   Haya turudi kwenye mada.Kweli kabisa watz wakiwa nje wana nidhamu kama ulivyosema maana when in Rome, do what the Romans do.Na inawezekana.Unajua nimeshangazwa na kitu kimoja.Mkoani Kilimanjaro - Moshi nadhani ndiyo the cleanest town in the whole of Tanzania.Jiulize kwanini.Kuna by-laws to keep the town clean.Kuna askari kila mahali tena without uniform, ukionekana unatupa hata kichungi cha sigara utapigwa fine papo hapo na hutapata hata fursa kuhonga.Ukipark gari yako bila kuzingatia utaratibu ni fine ya 50,000/- hapohapo na hakuna negotiation.Matokeo Yake hata watz kutoka mikoa mingine wakienda Moshi wanakuwa na nidhamu ya usafi.Linganisha na Dar the so called capital city ( Dodoma ishu tuache kwanza) nadhani ndiyo kitovu cha uchafu na kama unataka kujifunza culture ya uchafu basi nadhani ni sehemu nzuri for such TOUR! Kama kitu kidogo kama hiki kimewezekana Moshi, kwanini kisiwezekane kwingine? Nadhani ni kukosa ile political will na commitment tu.
   Swali - Why is there no political will and commitment katika mambo mbalimbali ?
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  17. Masanja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st August 2007
   Location : Benaco
   Posts : 1,915
   Rep Power : 1122
   Likes Received
   576
   Likes Given
   94

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   WoS you nailed it.

   SASA CHUKULIA HUO MFANO MDOGO WA KILIMANJARO NA USAFI. UTAKUTA KWAMBA HAWA JAMAA HATA MAMBO MENGINE YA MAENDELEO WAKO MBELE KULIKO WATANZANIA WENGINE! I STAND TO BE CORRECTED.

   Kwa sababu kama ukijifunza ku-appreciate vitu vidogo vidogo kama hivi..automatically hata vile vikubwa utakuta unavi-appreciate (Yesu ana akili sana--si alisema usipokuwa mwaminifu katika madogo hata makubwa huyawezi?)...so its the same! Kuna jamaa alinitonya kwamba..JK ni worst katika kuheshimu mda na appointments... Akiwa na kikao saa tano, mida yake ni tano na nusu.....NDEGE INAWEZA KUKAA AIRPORT HATA MASAA MAWILI IKIMSUBIRI! Well, he is a President. But you get the bigger picture..

   Mfano, mama Migiro juzi alipokuwa kwenye Summit ya AU Egypt alipiga mkwara sana viongozi wa Africa "this is the moment of truth" katika kudeal na Mugabe. LAKINI huyo huyo mama alipokuwa Foreign Minister wetu..kamwe asingeweza kutamka hayo maneno. Infact alipo kuwa foreign alipoulizwa mtizamo wa TANZANIA kuhusu Irani..alisema "Iran has a right to develop peaceful neuclear and TANZANIA supports her" Unaona? Comapare na Obama alivyokuwa Senator alissuport mauaji ya Waarmenia yaliyofanya na waturkish 1915 kuitwa Genocide. Jana akiwa rais aliulizwa tena akiwa Turkey..hizi answer was clear "I havent changed my stand about the resoultion I supported in the Congress"..ndo akaendelea na blah blah za kidiplomacia..

   Why do I tell you this? sisi waafrika kuanzia kwa viongozi wetu hatuna msimamo..kifupi we are intelligent people and capable of doing good. LAKINI kwa sababu kwetu kila kitu ni opportunism bila merit..ndo tunajikuta hapa tulipo...So we go back...bila utawala wa sheria, where we merit and competence are cerebrated..we can hardly go anywhere..You wonder kiongozi mwenye uhakika wa decent pension..kwa nini aibe?? Labda unajibu wewe..
   Silaha ya maskini ni elimu.

  18. MzalendoHalisi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th June 2007
   Posts : 4,260
   Rep Power : 1592
   Likes Received
   222
   Likes Given
   536

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Huu mjadala nimeupenda sana!

   Halafu hali hii sii kwa Tz tu jamani ni most of sub-Saharan Africa! Exceptions ni chache sana kama Mauritius and may be Botswana waliodiriki kumpasulia Mugabe kuwa hawamtaki kwa kuwa hajachaguliwa kihalali!

   Uliangalia nchi za Asia na Latine Amerika miaka ya 60 na 70 tulikuwa tu pamoja! Inakuwaje hizi nchi zikatupita kwa kasi ya ajabu hivyo?

   Afrika tuna tatizo mahali may be rooted in our culture ktk kulindana tukifanya mabaya, ukabila n.k

   Kijiji kimoja kule Tanga vijana wanakata na kuiba nyaya za umeme na kuuza Kenya..na watu hapo wanawajua na viongozi pia wanawaficha wasichukuliwe hatua eti afterall umeme unapita tu hapo wengi wa wanavijiji hawana umeme hapo..why walinde umeme usiokuwa na manufaa kwao? Au vijana wanaweka magogo njiani gari lipate ajali ili waibe!

   Sasa collectively, as a society bado tupo nyuma mno..je tuanzie wapi?

   Sheria kwanza?? Kazi kwa fimbo kwanza? Elimu kwanza??

   What is the entry point??

   MKUKUTA sidhani kama ni jawabu la haya matatizo yetu..there is too wide gap kati ya what is in the documents and the reality in the ground!
   Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!

  19. WomanOfSubstance's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th May 2008
   Posts : 5,480
   Rep Power : 85964256
   Likes Received
   794
   Likes Given
   721

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Talking of decent pension,

   Mkuu Masanja nimekumbuka kitu:

   Ukiangalia wazee wa enzi za Mwl,Nyerere walikokuwa watendaji wakuu kama makatibu wakuu hata mawaziri pension zao was nothing to write home about- mere peanuts! Ulikuja utawala wa awamu ya tatu - viongozi wakajiongezea mishahara, marupurupu na wakajiwekea mafao ya kutosha kama si ya kufa mtu! Niambie- hao wanaotuhumiwa na Ufisadi ni wa awamu ipi?
   Nadhani it is more than kuwa na pension nzuri au hata mishahara mikubwa.

   I think kuna kitu kinaitwa institutional or organisational culture.Nadhani taasis nyingi za serikali zimeshajenga ka utamaduni ka umimi, ubinfasi. Na ndiyo maana hakuna kutosheka kwa lolote hata wapewe nini bado uroho na ufisadi vitakuwepo.

   Tizama taasisi za kimataifa au sekta binafsi. Kwanza kuna codes of conduct ambapo rushwa however small na misconducts nyingine zitakufukuzisha kazi mara moja na ni non-negotiable.Pili, mtu anaridhika na kile anachopata na anafurahia kazi yake. Tatu, kuna mikataba ambayo ni performance based .You dont deliver you are flushed out like garbage.

   Sasa mafisadi kwanza wana ajira ambazo ni permanent and pensionable hakuna kujali kuhusu performance. I'm not sure how the OPRAS is doing as a performance measurement tool maana watu wanapeta tu hata pale unaona kabisa hakuna ufanisi.

   Nadhani kama ingetokea, kukawa na kubadili mfumo mzima wa kiutendaji basi tungepunguza baadhi ya matatizo yaliyopo kwenye mfumo.

   THE PROBLEM IS SYSTEMIC MKUU!
   Educating the mind without educating the heart is no education at all.... Aristotle  20. Masanja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st August 2007
   Location : Benaco
   Posts : 1,915
   Rep Power : 1122
   Likes Received
   576
   Likes Given
   94

   Default Re: MDG-based MKUKUTA and Poverty Reduction strategies and reality in Tanzania

   Mama sasa tufanye nini?

   Ndo hapo tunahitaji akina MUSA wa kutuvusha bahari ya Shamu! Sasa kama Musa hajui tuelekee wapi? sisi tunaomfuata ni dhahiri tutapotea.

   SASA BASI itahitajika wale wenye kujua pa kuelekea kwenye kundi la Musa..wamwambie...kwamba ..mzee unakotupeleka siko!

   Nani wa kumwambia hivyo Musa? ni mimi na wewe!
   Silaha ya maskini ni elimu.

  Page 1 of 6 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Toa maoni yako.
   By Webville in forum Tech, Gadgets & Science Forum
   Replies: 0
   Last Post: 8th July 2011, 17:50
  2. Replies: 0
   Last Post: 29th April 2011, 17:37
  3. Toa maoni yako juu ya picha hii
   By PingPong in forum Jamii Photos
   Replies: 7
   Last Post: 17th May 2010, 21:10
  4. Replies: 2
   Last Post: 16th April 2010, 18:39
  5. Toa maoni yako
   By Mtu Mzima in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 8
   Last Post: 17th November 2007, 00:15

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...