Jamani nilipokuwa mdogo hii ndo ilikuwa hobby yangu maana kwa umbo langu dogo sikuweza kupigana ila ukinikosea kidogo..nitakupa neno utakaa kimya mwenyewe!
Najikumbushia tu...(usinichukie...)
Unataka matani.. Nyani Ngabu, una bichwa kubwa mpaka shuleni ulikuwa unaitwa Headboy! twende twende..
fidel 80, wewe umekonda mpaka ukisimama kwenye ukuta unakaa kama crack...
:Mzee mwanakijiji demu wako amekonda mpaka akivaa t-shirt ya bluu anafanana na sim card ya tiGO.. Asprin unamashavu kama mimba ya panya..
Na wewe TUKUTUKU uso kama shamba la matuta...
Unataka unataka..
Mwangalie kwanza, wewe Bigirita yaani wewe ni mbaya mpaka hutumia lotion inayoitwa 'why bother!'..teh teh..
Zak wewe ni mweusi mpaka ukirushiwa jiwe linarudi kuitisha tochi...
PS: On a light touch...


Reply With Quote

Follow Us Here