Mwanasheria na muuza nyama
Mwanasheria alikua na mbwa wake.Siku moja mbwa aliingia Buchani akaiba nyama na kukimbia.
Muuza nyama akamfuata Mwanasheria. "Mbwa wako akiingia buchani kwangu nakuiba nyama, Je napaswa kukudai malipo?"
Mwanasheria: "Ndio"
Muuza nyama: Ok nakudai 12,000/=
Mwanasheria akamlipa Muuza nyama.
Baada ya siku kama nne hivi muuza nyama alikuta bahasha buchani kwake,alipoifungua ilikua karatasi imetoka kwa Mwanasheria imeandikwa "45,000/=, ada ya kumwona Mwanasheria (Consultation Fee)"
"Serikali inayowashwa wananchi tu ndo wakunaji"
Follow Us Here