Udaku mtupu, Umbea Orijino, Yaani bora usisome.

Niliwahi kusikia siku moja mh makufuli amejiuzulu.

Pale magogoni kabla hujakamata wizara kuna mfumo ulioanzishwa na mchonga meno ambapo unasaini kwanza barua yako ya kujiuzulu isiyokuwa na tarehe kabla ya kuanza kazi. Kwa hiyo hata Kalowa hakujiuzulu bali aliambiwa tu na mtunza barua, ''Mh Kalowa, umejiuzulu rasmi tarehe...''

Sasa najiuliza Makufuli alijiuzulu vipi? Maana mtunza barua ndiye anayejua kama umejiuzulu au la.

Au alimwambia mtunza barua ''Mh JK nakuomba tafadhali andika tarehe ya leo''?

Halafu Mh JK akamjibu '' sitaki, toka hapa''?

Pale kopi orijino ni moja tu inayotambulika. Hata kina Kalamaji, muunga hii na hebu mchenge ni humo humo tu.

Kalowa nae alituzuga tu bungeni hakuandika chochote, barua ilipigwa tarehe tu, kushinei.