Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

    Report Post
    Results 1 to 9 of 9
    1. #1
      kilimasera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2009
      Posts : 3,036
      Rep Power : 1097
      Likes Received
      182
      Likes Given
      245

      Default Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      Wanaume wote raia wa kigeni watakaotaka kuwaoa wanawake wa nchini Tajikistan watalazimika kuzifungua waleti zao na kuwanunulia nyumba wake zao kabla ya ndoa kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo leo.
      Kuanzia leo mwanaume yeyote ambaye si raia wa Tajikistan ambayo zamani ilikuwa sehemu ya Urusi, atalazimika kumnunulia nyumba mwanamke anayetaka kumuoa kama sharti kubwa la kwanza kabla ya harusi.

      Hiyo ni kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa leo na bunge la nchi hiyo ambapo sharti kubwa lingine lililopitishwa ni kwamba mwanaume atalazimika kukaa mwaka mmoja nchini humo kabla ya kupewa kibali cha kuruhusiwa kuoa.

      Watunga sheria wa Tajikistan wamesema kuwa sheria hiyo mpya itasaidia kuwalinda wanawake wanaotelekezwa na waume zao raia wa kigeni.

      "Baada ya ndoa kuvunjika, majukumu ya kuwalea watoto huangukia kwa mama na serikali", alisema mwakilishi wa rais bungeni, Dzhumakhon Davlatov.

      Davlatov aliongeza kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza idadi ya wanaume watakaowatekeleza wake na watoto wao.

      Wanaume wengi toka Afghanistan na Iran, ndio wanaoongoza kwa kuoa wanawake wa Tajikistan ingawa katika miezi ya karibuni kumekuwa na ongezeko la wanaume wengi toka nchi za barani ulaya, Marekani na Japan wanaooa wanawake wa Tajikistan.

      Tajikistan ni nchi maskini iliyokuwa miongoni mwa nchi zilizounda Umoja wa Sovieti na uchumi wake umetetereka tangu mwaka 1990 kutokana na matatizo ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    2. Miaka 50

    3. #2
      St. Paka Mweusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2010
      Location : Ukune,
      Posts : 5,289
      Rep Power : 1691
      Likes Received
      1564
      Likes Given
      3289

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      Sheria hii ilitakiwa kuwepo hapa kwetu Tanzania,na ingesaidia sana wale wadada walioachiwa vichotara vya kitaliano kuanzia Isaka,Kagongwa,Kahama,Masumbwe , Ushirombo na kuendelea mpaka Ngara.
      UKICHOKA KUFANYA SIRI,FUMANIWA TU YAISHE . By Simon Kitururu.

    4. #3
      MUREFU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2010
      Location : BUNJU
      Posts : 1,142
      Rep Power : 666
      Likes Received
      65
      Likes Given
      2

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      hii ya ukwel yan kwa lugha nyngne marufuku mgen kama mackin kuoa yan dah safi

    5. #4
      Inkoskaz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Location : URT
      Posts : 4,396
      Rep Power : 7348
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      1088

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      kwa bonngo vin'gast wote watataka kuolewa na foreigners tu hata kama vibabubabu
      Thinking is the hardest work there is,which is probably the reason why so few engage in it!!

    6. #5
      tzjamani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th October 2010
      Posts : 999
      Rep Power : 645
      Likes Received
      25
      Likes Given
      96

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      Duh hii kali.

      Wachina nasikia huko singida na tabora amefanya mambo. Serikali ichangamkie dili ili watoto wapate matunzo.
      The more anger towards the past you carry in your heart, the less capable you are of loving in the present- Barbara De Angelis

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,575
      Rep Power : 16764
      Likes Received
      2481
      Likes Given
      1845

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      Hii imetulia!

    9. #7
      hmethod's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2008
      Posts : 1,737
      Rep Power : 931
      Likes Received
      116
      Likes Given
      131

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      Hata hapa tz hii sheria ipo ila kwa kificho. Dada zetu wajanja wanaitumia sana!
      Salus Populi Suprema Lex Esto

      Salva Veritate

    10. #8
      kilimasera's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2009
      Posts : 3,036
      Rep Power : 1097
      Likes Received
      182
      Likes Given
      245

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      Quote By hmethod
      Hata hapa tz hii sheria ipo ila kwa kificho. Dada zetu wajanja wanaitumia sana!
      wanaangalia mawe kama huna mawe unakosa mke!

    11. #9
      B'REAL's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2010
      Location : streat
      Posts : 1,206
      Rep Power : 676
      Likes Received
      196
      Likes Given
      82

      Default Re: Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba

      hii ingekuwaa bongo ingekuwaa poaa sanaa,tushaa chokaa kulea ma uncle ma point 5 banaaa

    Similar Topics

    1. Tabia za ukoo zinahusika ukitaka kuoa au kuolewa?
      By Galileo Galilei in forum JF Chit-Chat
      Replies: 6
      Last Post: 25th September 2011, 12:21
    2. Mwanamke wa kuoa
      By dmasoko in forum Love Connect
      Replies: 16
      Last Post: 6th September 2011, 13:08
    3. Ukitaka kumtongoza mwanamke wa kijapani......
      By nyengo in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 7
      Last Post: 2nd June 2011, 19:09
    4. Ukitaka kuniteka nipe Mwanamke mwenye sifa hizi.
      By Liverpool in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 42
      Last Post: 28th December 2010, 19:30

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...