Wakuu,
Kunuka harufu mbaya (kikwapa) ni ugonjwa au uchafu? Kuna dawa?
Kuna hii hali ambayo mtu ananuka kikwapa wakati wa kula tunda (wakati mwingine aaaah yuko safiii tu). Je inatokana na nini? Na nini kifanyike ili kuzuia hali hiyo?
Wakuu,
Kunuka harufu mbaya (kikwapa) ni ugonjwa au uchafu? Kuna dawa?
Kuna hii hali ambayo mtu ananuka kikwapa wakati wa kula tunda (wakati mwingine aaaah yuko safiii tu). Je inatokana na nini? Na nini kifanyike ili kuzuia hali hiyo?
Last edited by Asked for a BAN; 7th December 2009 at 18:54.
Kikwapa si ugonjwa mkuu! Inaitwa kikwapa kwa sababu ni harufu kali, tena isiyopendeza. Lakini kwa kweli ni harufu ya kuzaliwa nayo mtu, ni harufu ya mwili, au tuseme ya ngozi ya mtu. kila mtu ana harufu yake. Kuna watu wana harufu kali sana, na wengine wana harufu za wastani, nk. Sasa huyu mwenye harufu kali sana ndo huwa tunasema ana kikwapa. Yeye hata aoge namna gani harufu hiyo haitoki kwa sababu ni harufu ya mwili/ngozi/maumbile. Kumbe inabaki palepale tu. Ndo mana wanaojijua wana hiyo hali wanajitahidi kwa usafi na marashi ili kupunguza makali.
Kwa wale kina mimi wasiojijali au hawana uwezo basi harufu hiyo inakuwa kali kweli. Na mbaya zaidi mtu awe mchafu hajijali basi ndo hivo tena. Ananuka kwelikweli. Cha maana tuvumiliane kwamba tuko tofauti. Pili, tusaidiane kushauriana ili kuboreshana pale tunapokutana na wenye kikwapa. Mpe ushauri, mwambie afanyeje, atumie marashi gani, nk. Kwa hili wanawake ni mabingwa kuliko wanaume.
God writes straight with crooked lines.
Mkuu kuna njia nyepesi za kuzuwia hiyo hali miaka ya nyuma baadhi ya sehemu wazazi na kina dada walikuwa wanatumia kitu kitwacho PODA kuweka katika kwapa zao hapo husikii harufu ,kama kuna mtu unafanya nae kazi tafuta njia siku ya Basidei yake Mpe za wadi ya kopo la Poda.,mwambie unapenda hiyo msichana akiweka kwapani kuliko kuweka pafum .
Mshauri awe ananyoa kila nywele zinapoota kwapani akioga na kusafisha kwapa, afanye hivi akate ndimu au limao katikati halafu apake chumvi kidogo na asugue kwapani, aache kama dakika 5 hivi halafu asuuze kwapa na maji, njia hii itasaidia kiasi au kuondoa kabis harufu!
mshauri pia awe anatumia deodorant.
If u can't stand for something , u will fall for anything !
[QUOTE=Maria Roza;853035]Mshauri awe ananyoa kila nywele zinapoota kwapani akioga na kusafisha kwapa, afanye hivi akate ndimu au limao katikati halafu apake chumvi kidogo na asugue kwapani, aache kama dakika 5 hivi halafu asuuze kwapa na maji, njia hii itasaidia kiasi au kuondoa kabis harufu!
mshauri pia awe anatumia deodorant.
Natia (naweka) nyogeza ndani ya ushauri wako
There are SO MANY ways to treat excessive or persistent armpit odor. Have no fear.
This article is going to give you to the treatments that will significantly decrease if not completely eliminate your armpit odor.
So, let's get right to it and make your persistent armpit odor history.
Lime Juice
Believe it or not, a remedy as simple as Lime Juice yields fantastic results. It's also incredibly easy to apply this treatment. Just divide a key lime (not so ripe) and then rub each half on your armpits.
If your underarm skin lightens a bit after a few days of this treatment, don't worry. The citric acid may have this side effect. Let your underarms air dry afterwards. You really want the citric acid to soak into your underarm pores.
Also, beware that if you get the lime juice on your clothes, it can discolor them. That's why it's so important to let your arms airdry before you Stay away from this armpit odor treatment if you have cuts or are prone to rashes from overdrying.
Alum
Alum is a very effective armpit odor treatment. Think of it as a concentrated, crystal form of deodorant (aluminum chloride). Along with taming armpit odor, it actually stops your armpits from getting sweaty in the first place.
Manufacturers have developed deodorants from alum but some swear that using the raw crystal form is just as good as the deodorants which are more expensive. You can pick Alum up at most pharmacies.
You can rub Alum crystal directly into your armpits after drying from a bath or shower. Just be careful when you apply Alum. Occasionally it can have jagged edges and irritate the skin. Try to pick out smooth at the pharmacy.
Vinegar
Applying malt vinegar or Apple Cider Vinegar on the armpits at night as part is another awesome armpit odor treatment. Do this after drying off from a shower. Make sure to allow the vinegar to air dry. In the morning, you can apply your regular deodorant as you normally would.
Much like the lime treatment, the acidity in the vinegar will neutralize the bacteria that clings to your body's Apocrine glands. These three treatments work well - there's no doubt. However, the ultimate armpit odor prevention simply revolves around sweating LESS.
naona umewahi, dawa ni kuweka ndimu hata kama una harufu basi inaondoka na wala haina kuweka deodorant, tena kabisa hakuna kuweka hiyo odorant kwani mtu mwenye hali hiyo ngozi yake itaungua ukiweka hiyo odorant
Pia bicarbonate of soda works wonders....after a shower una apply under your armpits kama powder and you will feel fresh for the whole day........no need for deodorants...
[quote=Sonara;853066] kwa vile huyo mtu anamjua ni vizuri angechukua huu ushauri hapo juu aka print.alafu chukua makaratasi yako mengine weka hii copy ya ushauri juu alafu jifanye umesahau kwenye meza yake au popote pale ambapo yeye ndio ataziona na kukurudushia.akiziona lazima atasoma tu hio copy ya juu na hapo ndio ujumbe utakuwa umemfikia.
"Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger
Mi ni bachelor na mwanzoni nilijifanya mgumu nipike mwenyewe msosi kwa raha zangu.
After a month uzalendo ukanishinda nkaanza kununua ma-junky foods, nikaona haifai hii.
Nikatafta mschana awe ananipikia. Msichana huyu ana hili tatizo la kutoa harufu kali. Hakai kwangu basi mornii akija harufu nyumba nzima.
Nilipanga nimuambie ila napata kigugumizi. Girl friend wangu angekua mtu wa kumuambia ila kwa msimamo wake anaona kwa kua yeye pale kwangu anakuja mara moja kwa mwezi yaan kwa nadra sana anaona ataingilia mambo ya pale kwangu akimuambia. Mimi mwenyewe mwanzoni nimepanga nimnunulie dudorant ila nkawa najishtukia asijeakaona huyu kaka anantaka taratib taratib nini.
Nimependa michango yenu hasa wa ARSN WENGA. Othawaiz kama kuna wazo lingine nawakarbisha.
"Smile though your heart is aching"...Me says
na wengine wanasema kuosha hilo kwapa na maji ya ukoko wa ugali pia inasaidia maana yake ukipika ugali then ukiloweka sufuria yale maji yake unaoshea kwapa lao ila sijui nni kwa muda gani inasaidia kuondoa hiyo harufu kali. ila ushauri wa kutumia ndimu uliotolea hapo juu ni mzuri sana na isitoshe ndimu/limao ni dawa ya vitu vingi hata fungus.
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.
Msisitizie pamoja na haya, kuoga at least mara mbili kwa siku na asirudie nguo. Challenge yangu mimi ni rafiki yangu (coaligue) mwanaume, ana mke mrembo kweli na tunafahamiana. Lakini jamaa ananuka kikwapa kweli na anavaa nguo chafu. Nashindwa nimuambieje. kumfumbia naona kama itakuwa uswahili flani? Ushauri tafadhali...
I can be changed by what happens to me. But I refuse to be reduced by it-Maya Angelou
laaahaula lakwata ukistaajabu ya musa.......................... .............sasa gonjwa gani tena hilooooooooooooo
Jino kwa Jino
Jamani naombeni msaada kwenye hili suala kutoa harufu makwapani. Nina uhakika kwamba, hakuna mtu miongoni mwetu, ambaye ameishafikia balehe, na hajawahi kukumbwa na tatizo hili la kunuka KIKWAPA. Wengi wetu tunakabiliana na hali hiyo kwa kutumia DEODORANTS za aina mbalimbali na PODA kwa wakina dada. Lakini maelfu, hususani kwa huko nyumbani, aidha kwa sababu ya hali ngumu ya maisha au kutokuwa aware na hali hii au kwamba kuna vitu unavyoweza kutumia ili kukabiliana na hali hii, basi suala hili limepuuzwa.
Mpaka miezi miwili iliyopita, nilikuwa nafanya kazi kwenye NGO moja hapa Ughaibuni, ambayo inayojishughulisha na kuwa-integrate the newly arrived immigrants katika mambo ya Lugha (English/French), local culture, na Employment. Hivi karibuni tulipokea wageni kadhaa kutoka Zimbabwe na Congo, na ambao baada ya kuwakaribisha na kuwaonyesha sehemu mbalimbali za kupata huduma (Hospital, School, na Metro Transportation), tuliwapeleka sehemu mbalimbali ili kuanza ajira. Sasa, katika kufuatilia maendeleo yao huko makazini, hakukuwa na malalamiko kuhusu utendaji wao wa kazi. Malalamiko makubwa kutoka kwa ma-supervisors wao ni kwamba baadhi ya hawa jamaa wanatoa harufu kali sana (Kikwapa), haswa wakati wa kupiga boksi. Wakatuomba tuwashauri hawa jamaa wawe WANAOGA kila siku. Nimejaribu kuwafahamisha hawa jamaa kwamba hawa wageni wanaoga kila siku, isipokuwa hawajazoea kutumia Deodorant. Supervisors’ hawaamini kwamba mtu anayeoga kila siku atakuwa ananuka kikwapa kiasi hicho.
Kivumbi kilichonipata ni kwamba, nilipowashauri hawa jamaa kuhusu tatizo hili na kuhusu matumizi ya Deodorants, baadhi yao hawakufurahishwa na ushauri wangu. Moja wao (kutoka Congo- Kinshasa) kanishutumu kwamba nimeishabadilika kimaadili kwa kuiga tabia za wazungu!!!
Sasa swali ni je, ni kweli kwamba Waafrika peke yao ndio wenye kunuka KIKWAPA? Pili, utamshauri vipi mtu kuhusu suala personal kama hili? Na mwisho kabisa, je dada zetu wanadeal vipi na hali kama hii katika mahusioano yao? Haswa tukizingatia kwamba mke au rafiki lazima anajuwa kilema cha mume au boyfriend wake. Je, wakina dada wanawaambia ukweli waume na marafiki zao ili kukabiliana na hili TATIZO? Nasita kutumia neno AIBU kwa sababu nafahamu kwamba kuna baadhi ya jamii na makabila ambayo yanatumia zaidi harufu zao (Olfaction) kuliko kuona au kugusa katika maisha yao ya kawaida. Lakini nimeishashuhudia mara kadhaa Wazungu na makabila mengine wakiwanyanyasa watu weusi kwa sababu ya tatizo la KIKWAPA. Msemo kwamba “WAAFRIKA WANANUKA” ndio imekuwa joke kwenye sehemu nyingi za kazi.
Things in Perspective:
Suala la kutoa harufu (yoyote) linaweza kuangaliwa katika sehemu kuu mbili au tatu muhimu: 1. Power 2. Classs, 3. Racism kama inavyoelezwa na Ruth Finnegan (2007):
“Odour is a peculiarly emotive basis for social inclusion and exclusion, often invoked by powerful groups to both distinguish and stigmatised those they classify as inferior or alien” (Finnegan 2007).
Mfano:-England wakati wa Industrial Revolution; the Bourgeoisie class waliwashutumu the Proletariat class kwa kutoa harufu mbaya.
-Britons walipokuwa wanaitawala India waliwashutumu Wahindi kwa harufu mbaya.
Racism/Discrimination: Nchini Marekani, haswa wakati wa UTUMWA, wakati wa Civil Rights Movement na mpaka leo wanawashutumu Wamarekani weusi kwa kutoa harufu mbaya.
-German (Third Reich) iliwashutumu European Jews kwamba wanatoa harufu mbaya, pengine kuliko binadamu yoyote yule Duniani.
-Wakati huohuo kuna baadhi ya makabila au jamii ambazo hutumia harufu katika maisha yao ya kila siku. Kwa mfano, The Desana- Amazon Rain Forest, the Umeda- Papua New Guinea, na the Dassanetch- Ethiopia. Kwa tamaduni za haya makabila; harufu ya kila kitu ni muhimu kuliko kuona (Smell outdistance sight).
Huo ni unyanyapaa tu wa wazungu. Mbona waafrika ni wasafi kuwazidi hao wazungu ambao wanaweza kumaliza hata wiki bila kugusa maji. Kwao mapafymu tu. Mnuko unatumiwa kama silaha ya dharau, ubaguzi, nk kama ulivyoitoa hapo juu. Si kweli kwamba waafrika wote wana kikwapa, japo yawezekana wachache wakawa wachafu.
God writes straight with crooked lines.
Tena asikuambie mtu....Hakuna mtu anaeyenuka kama hawa weupe.....wavivu kuoga na wanajipulizia sana manukato na sometymz unakuta yeye mwenyewe ananuka na kisha anajipulizia manukato murua (Harufu nzuri + Mbaya = ............) Unyanyapaa usio na msingi.....
Get Rich or Die Tryn......
Mh jamani hii kweli haitokani na imani kuwa njemba haitakiwi kunukia? Hili lalamiko ni la kawaida sana. Nimeliskia mara nyingi nilipokuwa USA.
Nadhani kwa miaka ya nyuma watu hawakupenda kunukia nukia, nafahamu watu ambao hata kuogea sabuni kama lux ana Rexona walikuwa wanaona ni marashi ati sabuni ya mwanaume ni lifebouy.
Naomba msamaha kama nimekosea, lakini ni kweli atu wa umri fulani walikuwa hawapendi kutumia deodorant. Vijana wetu siku hizi wanajitahidi.
...tukubali kukosoana.
Unaposhauriwa harufu ya mwili wako ni kero kwa wenzako, fanya jitihada kusawazisha hitilafu hiyo. Kunuka mdomo, kikwapa, na hata sehemu za siri sio sifa... ni karaha. Haijalishi wewe ni Muafrika, Mzungu au mhindi. Personal Hygiene ni muhimu.
Huenda wenyewe tunastahmiliana kutokana na ugumu wa hali za maisha, lakini harufu mbaya haimpendezi kila mmoja wetu, iwe ni Tanzania au hata huko ugenini. Jifikirie umo kwenye taxi yenye kiyoyozi halafu dereva ananuka kikwapa!
Tujitahidini jamani...
#Dunia ni yako :Chaguo ni lako.
Follow Us Here